Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Mzee wa nyuzi zenye maslahi ya taifa skuizi unanifurahisha sana
Mkuu Mnyanyembe wa Mboka , asante, endelea kufurahi.
unajua watakusikiliza lakini kwa maswala ya kitaifa ambayo ni unfavourable kwa CCM upo kimyaaaa kama huoni malalamiko ya watu kuhusu TOZO batili eti kwa sababu tu umeisha lambishwa tayari.
CCM ni mti, una mashina, matawi na mizizi, hivyo mtu huwezi kukata tawi ulilokalia, utaanguka.
Nakwambia hivi Mungu anakuona na atakuonyesha In Shaa Allah kwa double standard zako !!!
Mimi mbona ni good boy!. Sina double standards zozote, ila nakiri kuwa selectively kwenye mada ninazochangia, siwezi kuchangia kila mada!.
Jua kua hiyo sauti uliyojaaliwa hukujipa wewe kama wewe, ulibarikiwa na Mungu sasa unapoidhulumu baraka ya Mungu maana yake unajitafutia laana
Kwanza namshukuru sana Mungu kujijaalia sauti inayosikika!. Kwa miaka yangu 30 ya utangazaji, sauti yangu imesaidia mengi, imesaidia wengi na nimebarikiwa sana kwa hilo.
MAYALLA, MAYALLA, MAYALLA X 3

Kuwa makini na sauti yako unajitafutia laana shauri yako usije sema hatukukwambia hiyo asali ya CCM itakuponza
Asante kwa ushauri, nitauzingatia!.
P
 
Hatujafika huko sisi, ila huyu dogo kazingua Sana......

Ana kiburi Cha kijinga
Na hakuna kitu watamfanya hao polisi 😂😂😂 alichokosea ni kujigamba tu ila kwa kuwa baba yake kashatamka hakuna kitu watafanya.

Simu moja kw RTO aisee afande hawa vijana wako wana shida gani wanataka kutuletea balaa. Mitandaoni kote ni shida tu, hakikisha huyo kijana wetu anaondolewa hapo haraka bwana.

RTO: Hapana shaka kiongozi na hawa ma afande naona wamevuka mipaka sasa nitawapanga Lindi. Kijana nimeshatoa maelekezo aachiwe mara moja mkuu.
 
Ni ngumu mno nakuhakikishia. Yaani mtoto wa bosi hahahah. Yaani hapo Mama mtu akisema tu sitaki mwanangu ateseke hao polisi watakoma. Unakumbuka yule traffic wa Mke wa Dkt Mahiga, unajua kilichomtokea??? Alijuta!
Alijuta,wakati alipongezwa na bilashaka itakua alipandishwa hadi cheo...
 
Njia pekee yakuwafanya polisi wamshughulikie huyu kijana kwa kuvunja sheria, kudhalilisha jeshi letu, kuonea watu, kuikosea heshima serikali nk, NI KWA SIMBACHAWENE KUJIUZURU AU KUWAJIBISHWA.

AKIWA HAYUKO KAZINI polisi wetu watamshughulikia huyu kijana, kitendo cha yeye kuwepo kazini na eti kutoa maagizo ashughulikiwe ni sinema tu.

IMPACT YA YEYE KUJIUZURU AU KUWAJIBISHWA ITALETA HESHIMA KWA NDUGU NA WATOTO WENGINE WA VIONGOZI SIKU ZA USONI LAKINI PIA ITALETA KUJIAMINI KWENYE UTENDAJI WA KAZI KWA WATENDAJI WA SERIKALI.
Wewe unaweza kujiuzulu? Chukulia hilo limekukuta wewe sahizi unaweza kuacha kiti ukafe njaa uraiani ili uwafurahishe mazuzu wa kitanzania😀
 
Ni ngumu mno nakuhakikishia. Yaani mtoto wa bosi hahahah. Yaani hapo Mama mtu akisema tu sitaki mwanangu ateseke hao polisi watakoma. Unakumbuka yule traffic wa Mke wa Dkt Mahiga, unajua kilichomtokea??? Alijuta!
Trafiki alimfanyaje mke wa bosi?
 
Mzumbe sekondari au?

Nakumbuka kulikuwa na dogo wa simbachawene pia, haguswi na mtu pale. Alikuja kuhama.
Watoto wa mawaziri huwa hawasumbuliwi, mi nilisoma na mtoto wa Juma Ngasongwa enzi ile ya Mkapa, mzee wake alikuwa waziri wa viwanda na biashara.
 
Kwenye nchi za wenzetu zinazoheshimu uwajibikaji, this is an embarrassment kwa mzazi!, mwana unleavyo ndivyo akuavyo, Mhe. Simbachawene anawajibika kwa tortuous liability ya malezi ya kijana wake iitwayo vicarious liability ya malezi mabovu ya wazazi, hivyo Baba anapaswa kuwajibika kwa embarrassment iliyosababishwa na makosa ya kijana wake, mzazi anawajibika kwa kosa la mtoto, mume anawajibika kwa kosa la mke, boss anawajibika kwa kosa la mtumishi wake, hata Ali Hassan Mwinyi alipowajibika ile 1976 akiwa Waziri wa mambo ya ndani kwa vifo vya wale mahabusu wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng'wana Ng'hohoboko, Mwinyi did nothing!, mahabusu hao walikufa kufuatia mahojiano na polisi eneo la Kigoto, na waliokolewa na RSO wa Mwanza, na vifo vyao vikamponza Mzee wa watu aliyewaokoa!. Aliyejiuzulu ni Mwinyi na hakuwa na kosa lolote.

UK, US, Canada, Australia na Newsland, Baba, mama, mke na mtoto wa politicians ukifanya kosa lolote la embarrassment and put the public office into disrepute, mfano kukutwa na Wanawake wa barabarani, ukiacha mke, mtoto wako akifanya kituko, you immediately leave the public office!.

P.
Hiki ulichokiandika kinafanya kazi kwenye nchi za kijamaa tu, nchi za kibepari kama Marekani, Uingereza, Finland familia au ndugu wa viongozi wakifanya vituko au makosa wanawajibika wenyewe.
Mfano Trump na familia yake kipindi wapo madarakani walifanya vituko vingi sana, mtoto wa Joe Biden anahusishwa kwenye mambo mengi ya rushwa lakini baba yake mbona hajawajibishwa.
NB: Hayo yalio fanyika mpaka kupelekea mzee Mwinyi kujiuzuru ni makosa ya kiofisi hivyo bosi anawajibika
 
Kwenye nchi za wenzetu zinazoheshimu uwajibikaji, this is an embarrassment kwa mzazi!, mwana unleavyo ndivyo akuavyo, Mhe. Simbachawene anawajibika kwa tortuous liability ya malezi ya kijana wake iitwayo vicarious liability ya malezi mabovu ya wazazi, hivyo Baba anapaswa kuwajibika kwa embarrassment iliyosababishwa na makosa ya kijana wake, mzazi anawajibika kwa kosa la mtoto, mume anawajibika kwa kosa la mke, boss anawajibika kwa kosa la mtumishi wake, hata Ali Hassan Mwinyi alipowajibika ile 1976 akiwa Waziri wa mambo ya ndani kwa vifo vya wale mahabusu wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng'wana Ng'hohoboko, Mwinyi did nothing!, mahabusu hao walikufa kufuatia mahojiano na polisi eneo la Kigoto, na waliokolewa na RSO wa Mwanza, na vifo vyao vikamponza Mzee wa watu aliyewaokoa!. Aliyejiuzulu ni Mwinyi na hakuwa na kosa lolote.

UK, US, Canada, Australia na Newsland, Baba, mama, mke na mtoto wa politicians ukifanya kosa lolote la embarrassment and put the public office into disrepute, mfano kukutwa na Wanawake wa barabarani, ukiacha mke, mtoto wako akifanya kituko, you immediately leave the public office!.

P.
Kwa Tanzania hili haliwezi tokea..!!
 
Uliona zile video za mtoto wa Biden? Na bado Biden Yuko ofisini.

Muda mwingine mzazi unajitahidi Ila watoto hawasikii, hasa hiki kizazi cha hovyo!
kizazi cha nyoka! vijana wetu kichwani logic , jadi , kazi , history kuko empty kumejaa boli Simba na Yanga jezi mpya imetoka ila nzito na manyimbo tu umeachwa kubali , kamserereko nikuoneeee! wanaboa kinoma hawana akili aisee wengine wanatembea michupi michafu nje milegezo wanatia kichefuchefu
 
Huyo kijana ni mtu mzima awajibishwe kwa makosa yake, sio kosa kafanya mtoto basi awajibishwe mzazi wakati mtoto ni mtu mzima na anajua anachokifanya.
 
Kwahaya namengine yanayotokea napatawasiwasi hukotuendako tutakosa hata jeshi makini nasema hivyo kwani naona hatapolice watachukua hatua baada ya mzee wake kusema anatoa kibali ashughulikiwe apate adabu inamaana bila mzee kusema sipati picha
Kabisa mkuu,jeshi limepoteza sifa, linaendeshwa kisiasa na wanasiasa, halina nguvu tena , halifanyi kazi katika mhimili wake...
Ukitaka kuliona hilo ungeona jinsi walivyo respond mpka kijana anaonekana ana power kushinda wao,anadhalirau jeshi hadharani,
km inavyodhaniwa na wengi kuna mchezo umechezeka kiprotokali ili kuficha aibu lakini litakuja kutokea jingine.

Mtazamo tu.
 
Ila kuna baadhi yawatu tuna unafiki sana.
Hapo angelimtetea mwanae bado ungetokwa povu.
Yupo sahihi na katumia busara zaidi.
 
Tunasubiria jumatatu afikishwe mahakamani akifunguliwa mashitaka ya kukashifu jeshi la polisi na kuendesha gari kwa uzembe akiwa amelewa tofauti na hapo ni maigizo kama mengine.
 
Wewe unaweza kujiuzulu? Chukulia hilo limekukuta wewe sahizi unaweza kuacha kiti ukafe njaa uraiani ili uwafurahishe mazuzu wa kitanzania😀

mimi mapema tu ningemwaga wino sio kuwafurahisha watanzania bali kuonyesha uwajibigaji wangu kwa kushindwa responsible kwa malezi ya mtoto mpaka kuchafua image yangu hasa kutumia jina langu kufanya upumbavu wake.

angeishia kulewa tu na kuchukua malaya huko element isingekuwa issue kwangu ni his personal business, kitendo cha kumtaja baba waziri tayari jamii inaamini ndio mafunzo anayopewa au aliyopewa nyumbani, lakini pia itafundisha vijana wetu kujua madhara ya kutumia vyeo vya baba zao kujipatia unafuu wa maisha, kuonea wengine nk.
 
Back
Top Bottom