Legacy ya JF imejengwa kutokana na uchambuzi wa kina wa habari zenye utata kama hizi. Haya chini ni maoni yangu kama mmoja ya watu tuliosomea cuba lkn hatukumaliza mafunzo.
Turudi nyuma kwanza, binti alielalamika kudhalilishwa kingono na RC Yahaya alishawahi kuwa na kesi huko nyuma ambayo ilipelekea mpenzi wake kufungwa miaka 30 kwa kosa la kubaka. Lkn na hio kesi ilikua na utata sana kama alivyoandika
Pascal Mayalla
Inaonekana wazazi wake ili kuzuia fedhea ya mtoto wao kutorokea kwa boda waliamua kulazimisha ionekane mtoto wao alibakwa japo kwa maelezo ya mwanzo ya huyo binti alikiri kuwa alienda kwa jamaa yake kwa utashi wake mwenyewe.
Sasa hawa wazazi nahofia walihonga sehemu au walipewa favor sehemu ili kukamilisha lengo lao la kushinda kesi na kumwangia boda mvua ya miaka 30.
Lkn tunajua favor huwa haziendi burebure. Watesi wa RC Yahaya kama zilivyoonesha chats za whatsapp zilizovuja (alizokuwa anazisoma Maulid Kitenge) walimtumia huyu binti kufanikisha lengo lao la kumuumiza. Je haya matukio mawili yanahusiana? Inawezekana waliowapa wazazi wa huyu binti favor miaka ile ndio wamekuja kudai deni na kumtumia tena huyu binti na mzazi wake kufanikisha nia yao ovu.
Yahaya kama ana team yake na anataka kuwajua wabaya wake aanzie kwenye hio kesi ya yule boda alofungwa miaka 30. Waliofanikisha hio hukumu wanawajua wabaya wake kama sio wao wenyewe.
Mwisho wanaume tuwe makini sana na hawa viumbe, huyu binti kaangusha ndoto za watu wawili kwa kumpa mmoja miaka 30 jela na kumchafua mwingine kwa tuhuma ambazo zitamfuata maisha yake yote. Weekend njema.