Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?

Naomba nijikite kwenye sheria kuelezea hoja.
1. Kufanya mapenzi na mtoto yan mtu mwenye umri chini ya miaka 18 hilo ni kosa kisheria.

2. Kufanya na mapenzi na mwanafunzi ni kosa kisheria. Hapa kwenye kufanya mapenzi na mwanafunzi ikibainika umekula mzigo ni ubakaji. Kama hujala mzigo ila unamahusiano naye. Hapa kuna kosa moja ambalo linaweza kuwa kuzorotesha masomo kwa mwanafunzi.

3. Kwa mtumishi wa umma kuwa na skendo kama hiyo inatosha kukuondoa kwenye nafasi yako kupisha uchunguzi.

4. Inawezekana kweli hajaguswa ila inawezekana vipi kufunguliwe kesi ya ulawiti ilihali hajafirwa? Kwa ufaham wangu mpaka mtu afunguliwe kesi kama hiyo lazma pf3 irudishwe na mlengwa na isomwe ili kesi ifunguliwe kulingana na pf3 itakavyojieleza

5. ANGALIZO
Tuwe makini na mazingira hatarishi ambayo yatatunyima utetezi hapo mbeleni. Tuweke mipaka katika kazi na mahusiano. Mbaya wako huwa hakai mbali na hutumia watu wako wa karibu kukuangamiza ama wataangalia udhaifu wako na watautumia kukuangamiza.
 
Watu wengi wanashabikia na kuaminishwa kwamba huyo Mhe. Alifanya hiyi kitu, ila ukitafakari kwa kina sana maelezo ya huyo binti na mazingira utagundua ni siasa za kuchafuana na huyo binti alitumika
Huyo mheshimiwa naye si mpenda chini watu wamepita
Humo humo kwa kutumia udhaifu
Wake inawezekana
Kingine inaelekea huyo dem na mheshimiwa wana mahusiano kitambo sana kama kufukuana mtaro siyo jambo geni

Ova
 
Askari wetu ni wavivu sana, wanauelewa mdogo sana, hawana resources, hawako motivated matokeo yake WATU WENGI WANAKWENDA JELA SANA KIZEMBE.

ukiisikiliza issue ile unajua moja kwa moja ni MCHONGO wakupiga hela ulikuwa kwa jamaa Kwa kutumia Blackmailing style, inaonekana wapo polisi walio involved. Tatizo limetokea issue imeshakuwa viral na watu wengi wameshaiingilia kesi + jamhuri, HAPO MCHONGO UMEKUFA IMEBAKI KESI.
 
Legacy ya JF imejengwa kutokana na uchambuzi wa kina wa habari zenye utata kama hizi. Haya chini ni maoni yangu kama mmoja ya watu tuliosomea cuba lkn hatukumaliza mafunzo.

Turudi nyuma kwanza, binti alielalamika kudhalilishwa kingono na RC Yahaya alishawahi kuwa na kesi huko nyuma ambayo ilipelekea mpenzi wake kufungwa miaka 30 kwa kosa la kubaka. Lkn na hio kesi ilikua na utata sana kama alivyoandika Pascal Mayalla

Inaonekana wazazi wake ili kuzuia fedhea ya mtoto wao kutorokea kwa boda waliamua kulazimisha ionekane mtoto wao alibakwa japo kwa maelezo ya mwanzo ya huyo binti alikiri kuwa alienda kwa jamaa yake kwa utashi wake mwenyewe.

Sasa hawa wazazi nahofia walihonga sehemu au walipewa favor sehemu ili kukamilisha lengo lao la kushinda kesi na kumwangia boda mvua ya miaka 30.

Lkn tunajua favor huwa haziendi burebure. Watesi wa RC Yahaya kama zilivyoonesha chats za whatsapp zilizovuja (alizokuwa anazisoma Maulid Kitenge) walimtumia huyu binti kufanikisha lengo lao la kumuumiza. Je haya matukio mawili yanahusiana? Inawezekana waliowapa wazazi wa huyu binti favor miaka ile ndio wamekuja kudai deni na kumtumia tena huyu binti na mzazi wake kufanikisha nia yao ovu.

Yahaya kama ana team yake na anataka kuwajua wabaya wake aanzie kwenye hio kesi ya yule boda alofungwa miaka 30. Waliofanikisha hio hukumu wanawajua wabaya wake kama sio wao wenyewe.

Mwisho wanaume tuwe makini sana na hawa viumbe, huyu binti kaangusha ndoto za watu wawili kwa kumpa mmoja miaka 30 jela na kumchafua mwingine kwa tuhuma ambazo zitamfuata maisha yake yote. Weekend njema.
Kwanza niweke wazi sitetei upande wowote.

Sasa tuangalie mambo ya msingi.
1. Mkuu! Binti yeyote yule under 18 na yuko shule awe alikutongoza au ulimtongoza, haijalishi ila ukilala nae tu ni umebaka ikiwa proved ulilala nae kimapenzi bila ndoa. Kwa maana hiyo yule wa bodaboda haina uhusiano na kesi hii.​
Japo kwa historia ni kweli inaonekana dada kashazoea kukitembeza na ukinasa lazima uende jela kidogo 😔

2. Ila RC ni kiongozi na mfano wa kuigwa ilitakiwa kwa namna yeyote ile ajiepushe na hayo mambo kama ni kweli alifanya iwe walikubaliana au hawakukubalina. Kulawiti ni kosa kisheria. Kama dada anadai RC alitumia nguvu, binti anakua victim RC ndio mwenye kesi, na kama walikubaliana wote wana kesi ya kujibu.​
Kama ni mchezo wa siasa basi wanajua mapunguvu yake na wameyatumia ila haibadilishi alichokifanya kutokua kosa na kama ni uzushi hicho kitendo hakikufanyika kabisa, hii kesi itaisha mapema tu.
 
Wanabodi

Kiukweli sometimes Jeshi letu la polisi ni michosho sana, katika kufanya uchunguzi, mfano shambulio la Lissu, walishindwa kufanya lolote mpaka leo, Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija hivyo hata hii issue, wanaweza wasiweze kufanya lolote, ila sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kuubaini ukweli.

Simtetei Dr. Yahaya Ismail Nawanda, kwa sababu sijui for sure, nini haswa kilitokea, lakini kwa vile the source ni haka kabinti, TUMSIME MATHIAS NGEMELA, kuna wengi wameguswa na kudhani ni kweli alibakwa, na kuingiliwa kinyume cha maumbile, wakati usikute the reality ni consensual act, kisha binti akashitaki kuwa amebakwa kwa lengo la ku fix Dr. Nawanda!.

Nimesema hivyo, kwasababu, hii sio mara ya kwanza huyu binti kufanya tukio kama hili.

Angalia details za issue hii.

Said Seleman vs Republic (Criminal Appeal 60 of 2020) [2021] TZHC 7055 (11 November 2021)

Issue ilikuwa hivi
  1. Kalianza darasa la 1 kakiwa na miaka 4, hivyo kakamaliza form 4 kakiwa na miaka 16!-Jee ni kweli?
  2. Kati ya tarehe 23 November 2019 hadi 14 December 2019 kakiwa form 4 St. Mary Mpanda, kalitorokea kwa dereva boda boda Saidi Selemani, eneo la Msasani hapo Mpanda mkoa wa Katavi na kuishi nae kinyumba kwa muda wa wiki 3.
  3. Wazazi wake waka ka set kaseme kametekwa na kubakwa, na kweli kakatoa ushahidi wa kutekwa na kubakwa na huyo boda, boda akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela!.
  4. Masikini boda hakuwa na wakili!. Ushahidi pekee kuwa amebakwa, ni uchunguzi wa daktari kuthibitisha amekutwa hana "B"!. Wasichana wangapi wa primari wanaanza mambo?, uwepo wa "B" ndio ushahidi wa kubakwa?.
  5. Ukisoma maelezo ya haka kabinti, kana kiri Boda ni mpenzi wake, na kametoroka nyumbani kwa ridhaa yake, na kakawa kanampa yote!, lakini mahakamani kakasema kametekwa na kamebakwa!. Boda akala kifungo cha miaka 30 jela!.
  6. Usikute hata hili tukio la Mwanza, hakuna ubakaji wowote, kuingiliwa kinyume kwa ridhaa, sio kosa la jinai ila ukishitaki ndipo linageuka ni jinai!.
  7. Kuna uwezekano mkubwa sana Binti alisetiwa, Dr. Nawanda akaingia line kwenye mtego, binti akashitaki kubakwa!.
  8. Baada ya binti kuripoti tukio, akajikuta ni yeye anajiharibia CV yake, akataka kufuta kesi.
  9. Natoa wito kwa Waandishi wa habari wa IJ, wasaidie hili kabla kesi haijafunguliwa, kesi ikifunguliwa, IJ haiwezi kusaidia kitu.
  10. Kwenye issue ya shambulio la Lissu, niliuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?

Paskali
Yaani hujui mtoto wa shule kamahuyo tena chini ya miaka 18 ukilalanae tayari umebaka? Unamtetea bodaboda? Hatakama alikukubalia hicho unachokiita kumpa yote huyo nimtotooo amedanganyika we vipi?? Mwanasheria wawapi wewe...
Unaweka kesi ya Lissu ili ku-win akili zawengi humu,issue yalisu kulikuwa na ubakaji gani acha kutumika wewe!!

Polisi wachunguze hili halina cha uchama,upinzani wala vita vya uchumi vya enzi za jiwe. Kama amefanya ufirauni asionewe huruma hata chembe! Wengi tuu wamefungwa Kwa uchafu wanamna hii kwanini huyu mnamwona spesho sana?!
Jiulize ingekuwa ni mtoto wako au ndugu wa karibu ungeandika haya we mwanasheria wamaajabu!! Acha hizo wewe
 
Kwanza niweke wazi sitetei upande wowote.

Sasa tuangalie mambo ya msingi.
1. Mkuu! Binti yeyote yule under 18 na yuko shule awe alikutongoza au ulimtongoza, haijalishi ila ukilala nae tu ni umebaka ikiwa proved ulilala nae kimapenzi bila ndoa. Kwa maana hiyo yule wa bodaboda haina uhusiano na kesi hii.​
Japo kwa historia ni kweli inaonekana dada kashazoea kukitembeza na ukinasa lazima uende jela kidogo 😔

2. Ila RC ni kiongozi na mfano wa kuigwa ilitakiwa kwa namna yeyote ile ajiepushe na hayo mambo kama ni kweli alifanya iwe walikubaliana au hawakukubalina. Kulawiti ni kosa kisheria. Kama dada anadai RC alitumia nguvu, binti anakua victim RC ndio mwenye kesi, na kama walikubaliana wote wana kesi ya kujibu.​
Kama ni mchezo wa siasa basi wanajua mapunguvu yake na wameyatumia ila haibadilishi alichokifanya kutokua kosa na kama ni uzushi hicho kitendo hakikufanyika kabisa, hii kesi itaisha mapema tu.
Fuatilia ile kesi, yule binti by then inaonekana alikua kavuka 18.

Shida ya kesi za hivi hata akishinda mahakaman bado kwenye jamii hajashinda, yaan ikishaenda tu mainstream tyr jamii inatoa hukumu hata kabla ya mahakama.

Yahaya Jamii ishamuhukum hata ikitoka ikagundulika walikubaliana au hakufanya basi atakosa tu adhabu ya mahakama lkn kwenye jamii, familia yake tyr wameshamuhukumu
 
Legacy ya JF imejengwa kutokana na uchambuzi wa kina wa habari zenye utata kama hizi. Haya chini ni maoni yangu kama mmoja ya watu tuliosomea cuba lkn hatukumaliza mafunzo.

Turudi nyuma kwanza, binti alielalamika kudhalilishwa kingono na RC Yahaya alishawahi kuwa na kesi huko nyuma ambayo ilipelekea mpenzi wake kufungwa miaka 30 kwa kosa la kubaka. Lkn na hio kesi ilikua na utata sana kama alivyoandika Pascal Mayalla

Inaonekana wazazi wake ili kuzuia fedhea ya mtoto wao kutorokea kwa boda waliamua kulazimisha ionekane mtoto wao alibakwa japo kwa maelezo ya mwanzo ya huyo binti alikiri kuwa alienda kwa jamaa yake kwa utashi wake mwenyewe.

Sasa hawa wazazi nahofia walihonga sehemu au walipewa favor sehemu ili kukamilisha lengo lao la kushinda kesi na kumwangia boda mvua ya miaka 30.

Lkn tunajua favor huwa haziendi burebure. Watesi wa RC Yahaya kama zilivyoonesha chats za whatsapp zilizovuja (alizokuwa anazisoma Maulid Kitenge) walimtumia huyu binti kufanikisha lengo lao la kumuumiza. Je haya matukio mawili yanahusiana? Inawezekana waliowapa wazazi wa huyu binti favor miaka ile ndio wamekuja kudai deni na kumtumia tena huyu binti na mzazi wake kufanikisha nia yao ovu.

Yahaya kama ana team yake na anataka kuwajua wabaya wake aanzie kwenye hio kesi ya yule boda alofungwa miaka 30. Waliofanikisha hio hukumu wanawajua wabaya wake kama sio wao wenyewe.

Mwisho wanaume tuwe makini sana na hawa viumbe, huyu binti kaangusha ndoto za watu wawili kwa kumpa mmoja miaka 30 jela na kumchafua mwingine kwa tuhuma ambazo zitamfuata maisha yake yote. Weekend njema.
CCM imemtengenezea Yahaya ajali ya kisiasa
 
Wanabodi

Kiukweli sometimes Jeshi letu la polisi ni michosho sana, katika kufanya uchunguzi, mfano shambulio la Lissu, walishindwa kufanya lolote mpaka leo, Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija hivyo hata hii issue, wanaweza wasiweze kufanya lolote, ila sisi watu wa media, tunaweza kusaidia kuubaini ukweli.

Simtetei Dr. Yahaya Ismail Nawanda, kwa sababu sijui for sure, nini haswa kilitokea, lakini kwa vile the source ni haka kabinti, TUMSIME MATHIAS NGEMELA, kuna wengi wameguswa na kudhani ni kweli alibakwa, na kuingiliwa kinyume cha maumbile, wakati usikute the reality ni consensual act, kisha binti akashitaki kuwa amebakwa kwa lengo la ku fix Dr. Nawanda!.

Nimesema hivyo, kwasababu, hii sio mara ya kwanza huyu binti kufanya tukio kama hili.

Angalia details za issue hii.

Said Seleman vs Republic (Criminal Appeal 60 of 2020) [2021] TZHC 7055 (11 November 2021)

Issue ilikuwa hivi
  1. Kalianza darasa la 1 kakiwa na miaka 4, hivyo kakamaliza form 4 kakiwa na miaka 16!-Jee ni kweli?
  2. Kati ya tarehe 23 November 2019 hadi 14 December 2019 kakiwa form 4 St. Mary Mpanda, kalitorokea kwa dereva boda boda Saidi Selemani, eneo la Msasani hapo Mpanda mkoa wa Katavi na kuishi nae kinyumba kwa muda wa wiki 3.
  3. Wazazi wake waka ka set kaseme kametekwa na kubakwa, na kweli kakatoa ushahidi wa kutekwa na kubakwa na huyo boda, boda akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela!.
  4. Masikini boda hakuwa na wakili!. Ushahidi pekee kuwa amebakwa, ni uchunguzi wa daktari kuthibitisha amekutwa hana "B"!. Wasichana wangapi wa primari wanaanza mambo?, uwepo wa "B" ndio ushahidi wa kubakwa?.
  5. Ukisoma maelezo ya haka kabinti, kana kiri Boda ni mpenzi wake, na kametoroka nyumbani kwa ridhaa yake, na kakawa kanampa yote!, lakini mahakamani kakasema kametekwa na kamebakwa!. Boda akala kifungo cha miaka 30 jela!.
  6. Usikute hata hili tukio la Mwanza, hakuna ubakaji wowote, kuingiliwa kinyume kwa ridhaa, sio kosa la jinai ila ukishitaki ndipo linageuka ni jinai!.
  7. Kuna uwezekano mkubwa sana Binti alisetiwa, Dr. Nawanda akaingia line kwenye mtego, binti akashitaki kubakwa!.
  8. Baada ya binti kuripoti tukio, akajikuta ni yeye anajiharibia CV yake, akataka kufuta kesi.
  9. Natoa wito kwa Waandishi wa habari wa IJ, wasaidie hili kabla kesi haijafunguliwa, kesi ikifunguliwa, IJ haiwezi kusaidia kitu.
  10. Kwenye issue ya shambulio la Lissu, niliuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?

Paskali
Nilisoma humu kuwa wewe ni Wakili. Seriously hujui kuwa kufanya mapenzi na binti under 18 na ni mwanafunzi ni kubaka? Mimi sijui sheria, je sheria inasemaje ukifanya mapenzi na underage girl acha kukaa nae wiki mbili?
Mbona umeandika kishabiki sana kumhukumu binti bila kujua una undermine hata mahakama iliotoa hukumu ya kumfunga huyo bodaboda?
 
Askari wetu ni wavivu sana, wanauelewa mdogo sana, hawana resources, hawako motivated matokeo yake WATU WENGI WANAKWENDA JELA SANA KIZEMBE.

ukiisikiliza issue ile unajua moja kwa moja ni MCHONGO wakupiga hela ulikuwa kwa jamaa Kwa kutumia Blackmailing style, inaonekana wapo polisi walio involved. Tatizo limetokea issue imeshakuwa viral na watu wengi wameshaiingilia kesi + jamhuri, HAPO MCHONGO UMEKUFA IMEBAKI KESI.
Wampime marinda huyo demu

Ova
 
Huu ni unyanyapaaji wa wanawake nashangaa sana kuona na wanawake wenyewe baadhi yao wanashabikia huyu binti kuondelewa haki yake through ‘character assassination’.

Wanawake watanzania wengi kwa tamaa sijui ndio kupenda kuchuna lipo wazi sio siri ila aina maana hiyo iwe sababu ya kubakwa pia.

Binafsi (true story) nakumbuka binamu yangu kabisa kama miaka 10 iliyopita (kipindi hiko akiwa na umri kama huo wa late 40’s) yeye anaishi London. Alikuwa anatupa story ya holiday kuna vibinti vimemlia sana hela yake vitoto hivyo hivyo vya early 20’s na kutoa mzigo havitaki.

Kuna siku akaviita nyumbani kwake akavinywesha pombe yeye mwenyewe sio mnywaji ugonjwa wake ni nyapu tu.

Baada ya kulewa vile vibinti anawashkaji zake manyanya walimpa sigara special akawasha yeye akawa anazuga tu anavuta moshi anatoa, vile vibinti vyenyewe vinavuta wamemaliza kuvuta sigara nusu saa wapo paralytic hawajitambui; akawafanya anavyojua mwenyewe.

Yeye hakuwa anaona kosa la matendo yake, bahati nzuri aliokuwa anatupa story wastaarabu tukamueleza hiyo ni rape asirudie hiyo michezo; akasema hiyo mbinu yeye alipewa na wenyeji.

Hayo mambo wanawake wanafanyiwa sana Tanzania na wengi wanakaa kimya kwa sababu hizi za kuonekana tamaa zao ndio zimewaponza.

Kuna rafiki yangu mwingine yeye ‘what’s up’ video zake ni ngono tu na connections za mastaa. Kuna siku kanitumia video hivyo hivyo binti wa miaka hiyo hiyo early 20’s amelewesha halafu madogo kama watatu wanapokezana.

Ni upumbavu hasa kwa mtoto wa kike kushabikia huyo binti kwa kumuita sijui ni malaya na nini na nini, hiyo ni rape.

Kwanini ampeleke bar kulewa, afanye mambo yake kwenye gari na binti baada ya kutoka hapo aende polisi ku-report.

It’s a rape na matusi kama haya ya kuwaita wanaofanyia hivyo malaya na maneno mengine ya hovyo yanafanya victim wengine wa matukio ya kubakwa wasijitokeze, ujinga zaidi wanawake kushabikia.

Asilimia kubwa ya wanaume wanaomtetea huyo mkuu wa mkoa the only justification na wao ni wabakaji wa kutumia kilevi In my opinion.

Sorry mkuu najaribu kuwaza kwenye angle nyingine, HAKUNA UWEZEKANO MKAKUBALIANA MKAFANYANA NA BAADAYE BINTI AKAKUGEUKA NA KUSEMA UMEMBAKA? na hata ukijitetea ukaonekana unataka kujitetea tu.

Huoni kama Sheria inawafavor Sana wanawake huku ikiwakandamiza wanaume?.

Binti wa zaidi ya miaka 20 anawezaje kufika nyumba ya kulala wageni au ndani ya gari ya mtu usiku akiwa kalewa HALAFU TUSEME KABAKWA hatuoni kama hapa kuna makubaliano na tunaiweka sana jamii ya wanaume Hatarini?

Mfano hapo umezungumzia vibinti vya 20yrs kwenda peke yao nyumbani kwa mwanaume na vikiwa na akili timamu vikanywa pombe na kuingiliwa - KWANINI TUSEME WAMEBAKWA?

Naamini kabisa Sheria hapa inahitaji marekebisho ili pande zote za mwanamke Vs mwanaume ziwe na haki.
Mwanamke ukiwa mazingira tatanishi kama Lodge, Guest house, kwenye gari usiku wa manane under influence ya pombe, nyumbani kwa mwanaume usiku wa maneno, mchana bila uwepo wa watu wengine wa jinsia yako na mwanaume sio ndugu yako HAPO HAKUNA RAPING.
 
Wengi unaosikia wamelawiti ni kusingiziwa.nimewahi kusingiziwa kitu kama hicho,al manusura Nile mvua.sasa hivi nikasikia mtu Kabaka au kalawiti sihitaji kujiweka kwenye dhambi..nafikiria Kuna haja ya kupima sampuli za mbegu zinazobakia baada ya tukio kama zinaoana na za mtuhumiwa kwanza.Wengine wakihisi unaweza kumpa Hela hata milioni kumi anakutengenezea kesi ya magumasi ili ukiingia kwenye kumi na nane ulipe pesa nyingi.baadhi ya watu wanatumia ngono kama sehemu ya kujipatia kipato ,.Unakuta kabinti muda wote kanakuambia beby Nile tigo ,basi kwa ujinga wako unaingia kichwa kichwa na ukishaingia anakuambia nipe kiasi Fulani na usiponipa natangaza kwa watu kuwa umenilawiti.
 
Back
Top Bottom