Simulizi: Sasha Mlinzi wa Nafsi - 1

Simulizi: Sasha Mlinzi wa Nafsi - 1

SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya............36
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Wakati huo Tesha na Felix waliendelea kutazamana, hali hiyo ikidumu kwa zaidi ya sekunde 60 kila mmoja akiwa haamini anachokiona.

SASA ENDELEA...
Mwisho Brandina akatoa ishara fulani akiwataka wenzake waendelee na safari yeye akabaki amesimama pale pale.

"Tesha... Tesha..." Felix aliita wakati huo akibebwa msobe msobe kupelekwaa kwenye gari ya polisi.
Wakati huo Tesha akawa anapiga hatua ndefu ndefu kumfuata huku akiliita jina la mpenzi wake Felix, lakini alipofika usawa wa Inspekta Brandina akamshika mkono kumzuia.

"What's real going on Brandina?" Aliuliza Tesha akimtazama Brandina kwa macho makali.

"Relax Tesha..."

"Nirelax kitu gani na sielewi kinachoendelea Afande"

"Ndio maana nasema relax nikuelezee?"

"Okay nambie basi"

"Mpenzi wako anatuhuma nzito za utekaji, ikiwemo tukio la kutekwa kwa David juzi. Tumemkamata kwa ajili ya mahojiano zaidi pengine kupitia yeye tutafahamu ni wapi alipo David, Dayana pamoja na watu wengine wengi. Tesha tunaomba ushirikiano wako pia, tutakuhitaji kwa ajili ya ushahidi, wewe umekuwa karibu na Felix lakini pia ulikuwa shuhuda wa tukio la juzi pale mgahawani, asante tutaonana" Brandina alieleza na mwisho akaondoka.
Tesha alibaki amesimama huku mwili wake wote ukiwa umeshikwa na ganzi ya ghafula. Taarifa alizopewa na Inspekta Brandina zilimshtua na kumtisha mno. Inakuwaje mpenzi wake Felix ahusishwe na tuhuma nzito kiasi hiki. Na mbaya zaidi miongoni mwa watu waliotekwa ni kijana David ambaye tayari alishaanza kuingia taratibu kwenye moyo wa Tesha.

Tesha alikosa nguvu taratibu miguu yake ikalegea akajikuta anakaa chini pasipo kupenda.

"No hawezi kuwa Felix, sio yeye, Felix hawezi kumteka mtu" Tesha alijisemea mwenyewe huku akijitahidi kusimama tena.

[emoji294][emoji294][emoji294]

MTWARA...
Mkoa wa mtwara wilaya mpya ya Masasi katika kijiji kimoja kiitwacho Nagaga, wakati huu Kijiji hiki kilikuwa kwenye majanga makubwa mno.
Ni mara baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku tatu mfululizo, wakati wanakijiji wa Nagaga wakichukulia jambo hilo kama hali ya kawaida mara ghafula mambo yanabadilika na kujikuta wanakumbwa na mafuriko makubwa. Maji yalikuwa yakiporomoka kwa wingi kutokea milimani na kukifunika kijiji hicho ambacho kilikuwa eneo la bondeni huku kikiwa kimezunguukwa na milima karibu pande zote.

Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo maji yalizidi kuongezeka na kuwapa wakati mgumu wanakijiji wa Nagaga ambao walianza kuhangaika kujiokoa wenyewe na mali zao. Lakini baadae wakagundua kuwa maisha yao yalikuwa na umuhimu zaidi kuliko mali zao kwani maji yalikuwa yakiongezeka kwa kasi sana kutokea milimani, kulikuwa na kila dalili kwamba kama wataendelea kupambana kuokoa mali zao basi watajikuta wanaingia hatarini na pengine hata kupoteza maisha.
Hali ilikuwa ni tete zaidi kwa wanawake, wazee na watoto pamoja na wale ambao walikuwa hawaelewi lolote kuhusu kuogelea.

Ni wachache sana ambao walifanikiwa kukimbilia milimani na wengine wakafanikiwa kutoka hadi nje kabisa ya kijiji hicho lakini wengi wao walibaki kijijini wakapanda juu ya miti na wengine juu ya nyumba zao wakiamini pengine hali ingekuwa shwari baada ya muda mfupi maji yatapungua. La hasha, haikuwa hivyo, ingawa mvua ilikata lakini maji yaliendelea kuongezeka muda hadi muda na sasa tayari baadhi ya nyumba zilianza kubomoka.

Sasa ikawa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akawa anahangaika kutetea maisha yake. Hakuna aliyemkumbuka mke, mume, mtoto au mzazi, kila mmoja alikuwa akihangaika kwa nafasi yake kujiokoa mwenyewe. Muda huo tayari watu walianza kupoteza maisha mmoja baada ya mwingine. Hali ilitisha mno.

Taarifa hizi za mafuriko katika kijiji cha Nagaga zilisambaa kwa kasi sana, kikosi cha uokoaji kutoka mtwara mjini kilianza safari kwa haraka sana kuelekea eneo la tukio. Kulikuwa na umbali mrefu kutoka mtwara mjini hadi kufika kijiji cha Nagaga sawa na kilometa 201, ambayo itawachukua karibu masaa matatu hadi manne kufika.

Hakukuwa na helikopta ya dharula usafiri ambao pengine ungerahisisha zoezi la uokoaji badala yake zilitumika gari za kawaida kabisa.

Licha ya kuwepo kwa mapungufu hayo makubwa lakini tayari wasamalia wema kutoka vijiji vya jirani walifika eneo la tukio kujaribu kufanya uokoaji kwa kadri watakavyoweza. Wapo ambao pia walifika kwa ajili ya kutazama tu huku wengine wakidiriki kuchukua picha na video kwa kutumia simu zao kisha kuzituma mtandaoni.

Taratibu za uokoaji ziliendelea huku vijana machachali wakipambana kwa hali na mali kufanya zoezi hilo muhimu la uokoaji.

"Nyie kuna mtu kulee.... Yule kuleee..."

"Ooh! jamani maskini hajui hata kuogelea..."

Zilikuwa ni sauti za mashuhuda eneo la tukio wakipiga kelele mara baada ya kumuona mtu mmoja kwa mbali sana akipambana kuokoa maisha yake lakini tayari alishachoka na sasa akawa anazama na kuibuka.

Watu walizidi kupiga kelele lakini hakuna aliyethubutu kwenda, hata wale vijana waliojipa jukumu la uokoaji nao pia waliogopa. Mtu huyo alikuwa mbali sana kutoka pale walipo na mbaya zaidi alikuwa karibu kabisa na sehemu ambayo kulikuwa na poromoko moja kubwa la maji yaendayo kwa kasi sana.

"Atakufa jamani yule mwanamke..."

"Maskini anazamaaa..."

"Ooh! Yule kaibuka tena yule kuleee onenii....."

Dada mmoja ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kurekodi kwa kutumia simu janja yake alisikika akipiga kelele kuliko wengine wote.

Kufumba na kufumbua mara kuna kijana mmoja alikimbia kwa kasi akaruka na kujitosa majini kisha akaanza kupiga mbizi kumfuata yule mwanamke.

Hili lilikuwa ni tukio lililowaacha watu wote vinywa wazi, kitendo cha kijana yule kujitosa ilikuwa ni sawa na kubeti maisha yake yaani kufa au kupona.

"Feiiiii....Feisaaaaaal, rudi mwanangu achana naye huyo utakufa" Vijana wenzake walisikika wakipiga kelele kumuonya mwenzao arudi lakini Feisal hakujali akazidi kupiga mbizi kusonga mbele.
Naam, mwanaume huyu alikuwa ni Feisal yule tunayemfahamu tangu utoto wake yaani Feisal kaka yake David. Wakati ndugu na jamaa zake wakiamini amekufa miaka mingi iliyopita kumbe Feisal alikuwa hai kwa sasa akiishi mkoa wa Mtwara wilayani Masasi. Haikujulikana hasa ni nini kilitokea hapa katikati mara baada ya Feisal kutumbukia darajani miaka mingi iliyopita, lakini jambo la msingi ni kwamba Feisal yupo hai na sasa anapambana kuyaokoa maisha ya mwanamke mmoja ambaye yuko mbioni kufa majini.

Feisal alikuwa ni mtaalamu mzuri wa kuogelea dakika tatu pekee zilimtosha kupiga mbizi na kumfikia yule mwanamke haraka alimshika na kumuweka mgongoni huku akiendelea kupiga mbizi. Lakini kwa bahati mbaya Feisal ya yule mwanamke walipigwa na wimbi kubwa la maji. Wimbi hilo liliwarusha hadi kule kwenye maji yaliyokuwa yakienda kwa kasi sana. Hakukuwa na namna ya kujizuia, Feisal na yule mwanamke walijikuta wanabebwa na maji yale yaendayo kasi.

Mashuhuda wa tukio hilo walizidi kupiga kelele huku wengine wakishika vichwa vyao kwa masikitiko makubwa wakiamini huo ndio utakuwa ni mwisho wa Feisal.

"Tunafanyaje?"

"Tutafanya nini mwamba mwenyewe kazingua.."

"Daah"

Walisikika baadhi ya vijana washikaji zake Feisal wakijadili. Ni kweli hawakuwa na la kufanya waliishia kumshuhudia Feisal na yule mwanamke wakisombwa na maji na mwisho wakapotea kwenye upeo wa macho yao.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Unaambiwa haijaisha mpaka ifike mwisho, Jitihada za Feisal hazikuwa zimefika ukomo bado aliendelea kupambana kuogelea huku yule mwanamke akiwa ameng'ang'ania mgongoni.
Kwa bahati iliyo njema Feisal alifanikiwa kushikilia kipande cha gogo ambacho kilimfanya yeye na yule mwanamke wasizame majini. Walibebwa na maji hadi eneo ambalo kulikuwa na hali ya utulivu, maji hayakuwa yakienda kasi sana hivyo ilimpa Feisal mwanya wa kupiga mbizi hadi eneo lisilo na maji mwisho wakafanikiwa kutoka wakiwa ni wazima.

Feisal akiwa amembeba yule mwanamke alimshusha chini nchi kavu kisha na yeye akakaa pembeni yake huku akihema kwa nguvu. Yule mwanamke naye akawa anakohowa kwa nguvu, alikuwa amekunywa maji ya kutosha.

"Uko sawa?" Aliuliza Feisal akimtazama yule mwanamke, lakini ajabu mwanamke huyo akawa anaona aibu kubwa kumtazama Feisal usoni, hata kusema neno asante ilikuwa ni ngumu kwake. Gauni jepesi alilokuwa amelivaa lilikuwa limelowa chapa chapa kiasi cha kuung'ang'ania mwili wake na kumfanya aonekane kama alivyoumbwa na hii ndiyo sababu kubwa iliyomfanya mwanamke huyu kuwa na aibu.

Lakini hili halikumuingia Feisal akilini hata kidogo, suala la mwili wa mwanamke huyo kuchwora na vazi lake halikuwa kipaombele kikubwa zaidi ya wao kunusurika kufa kwenye maji muda mfupi uliopita.
Ziasi
"Khaa wewe... Nakuuliza uko sawa, sasa unamuonea nani aibu?" Alisema Feisal huku akishangazwa na Tabia ya mwanamke huyo, akawa anajifuta maji kichwani kwa mkono wake.

"Unaitwa nani?" Feisal aliuliza tena swali lingine huku akimshika mkono yule mwanamke akimtaka wainuke na kuondoka.

"Sasha"

"Nani?" Feisal aliuliza akiwa hajasikia vizuri

"Naitwa Sasha.." Sauti nyororo ilisikika kutoka kwa yule mwanamke ambaye sasa alisimama. Hapo ndipo Feisal alibaki kinywa wazi mara baada ya kufanikiwa kuiona sura yake. Alikuwa ni mwanamke mwenye sura nzuri isivyo kawaida. Pengine tangu kuzaliwa kwake hakuwahi kukutana na binti mrembo wa kiwango cha Sasha. Naam alikuwa ni Sasha yule yule tunayemfahamu kutoka ISRA. Sasa rasmi binti huyu wa Gu Gamilo alikuwa nje ya ISRA mara baada ya kufukuzwa. Kwa bahati nzuri anajikuta kwenye mikono ya Feisal kaka yake David ambaye inaaminika amekufa miaka mingi iliyopita lakini kumbe yuko hai.

Mwanzo ilikuwa ni David na Dayana, Felix na Tesha na sasa ni Feisal na Sasha.

Je, nini kitafuata?

ITAENDELEA....
 
At least hata vipande vitatu mpaka vitano italeta maana hiki kimoja kimoja na kutuma mwendelezo mpaka wiki ipite inaboa na tunasahau tumeishia wapi.
Badirika SIMULIZI RIWAYA
 
Usiache kufuatilia Simulizi nyingine nzuri ya KIJASUSI MKEKA huu hapa[emoji116]
[emoji116]
 
SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya............37-38
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

Pole kwa kuchelewa kupost...

ILIPOISHIA...
Kwa bahati nzuri Sasha anajikuta kwenye mikono ya Feisal kaka yake David ambaye inaaminika amekufa miaka mingi iliyopita lakini kumbe yuko hai.
Mwanzo ilikuwa ni David na Dayana, Felix na Tesha na sasa ni Feisal na Sasha.

SASA ENDELEA...
Feisal alijisahau kabisa, kwa zaidi ya sekunde 60 akawa anamtazama mwanamke huyo mrembo aliyejitambulisha kwake kwa jina la Sasha

"Nashukuru kwa msaada wako" Mwisho Sasha alitoa shukrani kwa mwanaume huyo baada ya kuona anamtazama sana.

"Aah..hehehe...usijali pole pia kwa majanga yaliyowapata" Alisema Feisal huku akijichekesha.

"Kuna watu wengine wapo kule tumefanikiwa kuwaokoa tunaweza kwenda ukawaangalie pengine unaweza kuwatambua ndugu zako"

"Hapana mimi sina ndugu"

"Kivipi, wewe sio mwenyeji wa hiki kijiji cha Nagaga?"

"Eh! Ndiyo mimi ni mpitaji tu kwa bahati mbaya nikajikuta ni mmoja kati ya wahanga wa haya mafuriko" Sasha alidanganya, hakutaka kuweka wazi habari za yeye kutokea katika mji wa ajabu ISRA.

Feisal alitulia kwa muda akijaribu kuyatafakari maelezo hayo kutoka kwa Sasha kisha akauliza.

"Sawa kwa hiyo wewe nyumbani wapi sasa?"
Sasha alitulia kwa muda huku akiwaza ajibu nini, ukweli hakuwa akifahamu lolote kuhusu miji wala vijiji villivyopo.

"Mimi?"

"Ndiyo wewe unatokea wapi?"

"Aah....ooh! Mungu wangu" Sasha aliongea na mwisho akapiga kelele huku akishikilia kichwa chake kwa mikono yake yote miwili. Hali hii ilimshangaza Feisal akamsogelea.

"Nini shida Sasha?"

"Kichwa, kichwa kinauma sana..?" Sasha aliendelea kuigiza akionekana kama kweli anamaumivu makali ya kichwa.

"Hebu sogea, kaa chini kwanza..." Alisema Feisal huku akimsaidia Sasha kukaa chini.

"Vipi unajisikiaje sasa mmh?"

"Bado, nikijaribu kuvuta kumbukumbu naumia sana, kichwa kinauma. Alafu sikumbuki kitu chochote kaka yangu... Nimepatwa na nini mimi Mungu wangu"

"Hukumbuki, kwamba umepoteza kumbukumbu...?"

"Hebu subiri, ngoja nijaribu tena kukumbuka ilikuwajee....ooh! Mama kichwaaaaaaa... " Sasha alilia tena kwa maumivu makali.

"Okay! Okay! Hebu tulia kwanza, inawezekana kwenye hizi purukushani ndani ya maji kuna mahali utakuwa umejigonga kichwani. Tulia tu usiendelee kujiumiza nina imani baada ya muda mfupi akili itakaa sawa kumbukumbu zako zitarejea" Alisema Feisal na hii ndio ikawa ahueni kwa Sasha kwani kama Feisal angeendelea kumuuliza maswali basi angeweza kubaini kitu cha tofauti kwake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili mara baada ya gari za polisi kuondoka maeneo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere, Haron alichukua simu yake akampigia Kareem kwa mara nyingine tena.

"Hallo Kareem, tayari polisi wameshaondoka na Felix nini kinafuata?"

"Kila kitu kinakwenda vizuri usijali" Alijibu Kareem

"Sasa ni nani atamueleza Felix kuhusu mpango wenu? tayari yupo chini ya ulinzi mkali wa polisi na hajui chochote mpaka sasa"

"Hilo tuachie sisi, ila kuna kazi moja nisaidie"

"Kazi gani Kareem?"

"Unamuona huyo mwanamke nyuma yako..." Alisema Kareem ndipo hapo Haron akageuka nyuma, akakutana na sura ya mwanamke mrembo Tesha ambaye sasa alikuwa anapiga hatua ndefu ndefu kuelekea lilipo gari lake la kifahari.

"Ndiyo nimemuona, namfahamu vizuri ni Tesha mpenzi wa Felix"

"Sawa sasa hakikisha huyo mwanamke hafuati kituo cha polisi, ataharibu mpango wetu, fanya lolote unaloliweza kumzuia. Kuna vijana wapo hapo watakusaidia"
Kareem alitoa maelezo na mwisho wakakubaliana hivyo. Sasa jukumu likabaki kwa Haron kuhakikisha anamzuia Tesha ambaye tayari alishaingia ndani ya gari yake.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baada ya muda mfupi msafara wa gari za polisi zisizopungua nane ulifika kituo cha polisi. Moja kwa moja Felix alishushwa na kuingizwa ndani ya ofisi za upelelezi kwa ajili ya mahojiano.

"Nashukuru sana Jacob kwa msaada wako mkubwa mpaka kufanikisha zoezi la kumkamata huyu mtu" Inspekta Brandina alikuwa akitoa shukrani zake kwa jasusi Jacob. Wakati huo kuna askari alikuwa akimsindikiza Felix kuelekea chumba maalumu cha mahojiano

"Usijali tuko pamoja Inspekta, nafikiri mpaka hapa ulipofikia kazi yako itakuwa rahisi"

"Ni kweli, kwa hiyo unaondoka au bado utakuwa na sisi?"

"Ah! Twende na mimi nataka kusikia majibu ya huyu mtuhumiwa"

Baada ya kusema hivyo Jacob na Brandina waliongozana kwa pamoja kuingia ofisi za upelelezi.

Yule askari aliyemsindikiza Felix kuingia chumba cha mahojiano alimbinya mkono Felix kisha akaongea.

"Nisikilize, naitwa Inspekta Mwampagama mimi ni member wa MG Family pia, kuna maelezo muhimu nimeambiwa nikupe kabla hujaanza mahojiano"

"Ongea nakusikia..." Alisema Felix na hapo yule askari akaanza kumueleza kwa sauti ya chini jinsi mpango mzima wa MG Family ulivyo wakati huo tayari walishafika chumba cha mahojiano.

"Kuna nini Inspekta Mwampagama?" Ilikuwa ni sauti ya Inspekta Brandina akiwa nyuma yao baada ya kuingia ndani ya kile chumba alishangaa kuona askari mwenzake amemuinamia Felix ni kama wanazungumza.

"Aaah!..alikuwa anaomba simu ampigie mwanasheria wake" Mwampagama alidanganya huku akiondoka taratibu lakini alipomfikia Inspekta Brandina alimtenga njiani.

"Sipendi kuingiliana kwenye kazi" Alisema Brandina kwa sauti ya chini ambayo ni wao wawili tu ndio waliisikia. Inspekta Mwampagama akaondoka akiwa na aibu usoni.
Siku zote Brandina alikuwa ni aina ya polisi ambaye amenyooka kwenye mambo yake, hakuwa mtu wa makandokando hata kidogo na hii ndio sababu aliaminiwa na kupewa kesi kubwa kubwa azisimamie.

Alipiga hatua na kukaa kwenye kiti mbele ya Felix, sasa wakawa wanatazama huku katikati yao wakiwa wametenganishwa na meza ndefu ya chuma. Brandina akaiweka kompyuta yake ndogo aliyokujanayo juu ya meza hiyo, sasa wakawa tayari kwa mahojiano.

Nyuma ya Inspekta Brandina kulikuwa na dirisha kubwa lenye kioo. Kioo hicho kiliruhusu mtu aliye nje kuona ndani lakini mtu aliye ndani hawezi kuona nje badala yake hujiona yeye mwenyewe kama ilivyo kioo cha kawaida.

Nyuma ya kioo hicho walisimama polisi wapelelezi waliokuwa wakiifuatilia kesi hiyo ya utekaji nyara pamoja na Jacob Kutoka Idara ya usalama wa Taifa, wakawa wanasikiliza na kutazama kwa makini mahojiano kati ya Inspekta Brandina na Felix.

Kwanza kabisa Inspekta Brandina alichukua simu yake akaitupa mezani karibu na Felix.

"Tumia hiyo.." Alisema Brandina.
Felix akainua uso wake huku akimtazama Brandina kwa macho ya kuuliza.

"Si unataka kumpiga mwanasheria wako?"

"Aah! Okay nimehairisha, haina haja kama kuna maelezo yanahitajika basi nitayatoa mwenyewe"

"Unauhakika?"

"Yes, bila shaka. Naomba niulize haraka haraka kuna mahali nataka kwenda, kwanza kabisa naweza kujua kwa nini niko hapa?" Aliuliza Felix. Brandina alitulia kwa muda kisha akaongea...

"Naitwa Inspekta Brandina ni afisa wa polisi kitengo cha upelelezi kesi za jinai, naweza kujua majina yako yote matatu"

Badala ya kujibu swali, Felix alitoa kitambulisho chake mfukoni akampatia Brandina ambaye alikipokea na kuyasoma majina yote matatu kwenye kitambulisho hicho kisha akainua uso wake akamtazama Felix.

"Lakini nimesikia kuna mtu anakuita kwa jina la Felix pale uwanja wa ndege, hii imekaaje unamajina mangapi na tutumie jina gani?"

"Aah! Ni kweli watu wanapenda kuniita Felix, wengine Fei, na wengine kama unavyoona kwenye kitambulisho hilo ndilo jina langu halisi"

"Inakuwaje wanakuita Felix badala ya jina lako halisi..."
"Ah! Niliamua waniite hivyo mimi mwenyewe baada ya kuhama dini kutoka uislam kuja ukiristo nikapenda waniite Felix, hata mchungaji alishauri hivyo"

"Vipi unaweza kunipa historia yako kwa ufupi ulizaliwa wapi ulisoma wapi, unajishughulisha na nini kwa kifupi tu"

"Afande ulitakiwa kuingia mtandaoni kufuatilia profile yangu hata kabla ya kunikamata na kunileta hapa, mbona kila kitu kinajieleza. Naomba nipate haki yangu ya msingi kama mtu mnaenishikilia tafadhali nataka kujua kwa nini niko hapa?" Felix aliongea kwa kujiamini na mwisho akauliza swali.

Kauli hii ilimbana Inspekta Brandina na maswali yake ya mtego akaona sasa ni wakati wa kwenda moja kwa moja kwenye lengo. Akaifungua kompyuta yake na kuiwasha kisha moja kwa moja akaicheza ile video inayoonyesha tukio la utekaji pale supermarket. Video ambayo ilirekodiwa na kamera za CCTV.

Inspekta Brandina aliigeuza kompyuta yake ili kumpa nafasi Felix atazame. Felix alifanya hivyo akaitazama video hiyo yenye dakika 3 na sekunde 25 mpaka mwisho, kisha akainua uso wake na kumtazama Inspekta Brandina. Ajabu Felix hakuonyesha mshtuko wala hofu ya aina yoyote ile. Hii ilimpa ugumu Brandina ambaye mda wote alikuwa amekaza macho yake kumtazama Felix usoni akitaka kuisoma saikojia yake lakini mpaka video inafika mwisho hakuambulia kitu.

"Imefika mwisho ila sijaelewa kitu afande" Alisema Felix kauli iliyomfanya Brandina ainuke na kuzunguuka upande wa pili akaicheza tena. Ilipofika wakati ule ambao yule mtu anaonekana kuvua helmet yake baada ya zoezi la utekaji Brandina akaisimamisha video hiyo.

"Unamuona huyu mtu hapa ni....eeh!" Brandina aliongea lakini akaonekana kusita. Ipo sababu iliyomfanya asite, video hiyo ilikuwa na tofauti kiasi na video waliyoitazama mwanzo. Yule mtu aliyevua helmet na kuingia kwenye gari hakuwa Felix kama ilivyokuwa mwanzo ajabu ilionekana sura ya mtu tofauti kabisa na Felix.

"Hii inawezekanaje?" Aliwaza Brandina huku akiicheza tena video hiyo kwa mara ya pili na ya tatu tena mara hii akiweka kasi ndogo sana, lakini hali ilikuwa ni ile ile yule mtu hakuwa Felix ila kila kitu kilikuwa sawa kabisa na video waliyoitazama awali isipokuwa sura ya Felix ndiye alionekana mtu mwingine tofauti.

Je , nini kitafuata?

SASHA MLINZI WA NAFSI
Episode ya........38

"Jacob naomba ingia tafadhali" Alisema Brandina.
Ndani ya sekunde chache mlango ulifunguliwa Jacob akaingia. Wakati huo tayari Felix alikuwa anaujua mchezo mzima unaofanywa na kikosi kazi kinachomilikiwa na baba yake Magnus yaani MG Family. Alitulia kama vile hajui kitu akawa anawatazama askari hao wanavyoanza kupapalika, akatabasamu moyoni.

"Kuna shida gani Inspekta?" Aliuliza Jacob akiwa na shauku ya kujua sababu za kuitwa.
Brandina aliisogeza ile kompyuta karibu na Jacob.

"Angalia hiyo clip hadi mwisho"

Haraka Jacob aliicheza kama alivyoelezwa, naye pia alionyesha mshtuko mkubwa mara baada ya kuiona tofauti ile. Aliyevua helmet na kuonekana sura yake si Felix kama ilivyoonyesha awali bali ni mtu mwingine tofauti kabisa.

"Hii imekaaje Inspekta?" Aliuliza Jacob

"Hata mimi sielewi, hebu tutoke nje tuongee kwanza..." Alisema Brandina wakawa wanatoka yeye na jasusi Jacob lakini mara ghafula Felix akapaza sauti kuwaita.

"Kwa hiyo inakuwaje mnaniacha hapa sielewi kitu, si niliwaambia nina haraka. Naomba kwanza mniambie nina kosa gani hadi mnikamate, la sivyo mimi pia nina haki ya kisheria kuwashtaki" Aliongea Felix huku akisimama.

Jacob na Brandina wakatazamana.

"Tunafanyaje, ni kweli ana haki ya kutushtaki kwa sababu hatujamwambia kosa au sababu ya kumshikilia" Jacob alinong'ona. Sasa wakaanza kujadili kwa sauti ya chini wakiwa pale mlangoni

"Sasa tutamwambia nini na umeshaona ile video haionyeshi sura yake?"

"Basi tumuache kwanza aende Inspekta"

"No, Big No, hatuwezi kumuacha aende, kumbuka namna tulivyohangaika hadi kumpata ni zaidi ya miaka miwili. Tukimuacha hapa ndio basi tena Jacob, atapotea"

"Ni sawa lakini tutafanyaje sasa na hatuna kesi ya kumtia hatiani itakayofanya kuendelee kumshikilia"

"Kesi ipo Jacob, tuliona wote ni huyu mtu ndio alikuwepo kwenye video ya CCTV kamera hapo awali iweje sasa hivi useme hana hatia, kitendo cha kubadilishwa kwa hii video ni wazi kuwa tunapambana na watu wakubwa mno waliopo nyuma yake hatuwezi kumuacha aende."

"Basi inabidi tutafute namna ya kuendelea kumshikilia"

"Nimepata wazo Jacob"

"Nambie!"

Brandina alipiga hatua akatembea na kusimama mbele ya Felix, wakatazamana.

"Umesema utatushitaki si ndiyo? Bila shaka kumbe unazijua sheria vizuri. Upo hapa kama mhisiwa wa tuhuma za utekaji, hivyo tuna haki ya kukuhoji kwa masaa manne mfululizo na kama hutobainika kuwa na hatia basi tutakuacha uende ila kama ukikutwa na hatia basi utakuwa na masaa 24 na zaidi mpaka kesi yako itakapoanza kuunguruma mahakamani. Hivi sasa tumetumia dakika 30 pekee bado tuna masaa matatu na nusu ya kuendelea kuwa na wewe hapa kwa hiyo kuwa mtulivu" Alisema Brandina kisha akageuka na kuanza kuondoka. Felix alimtazama mwanamke huyo ambaye alionyesha kumaanisha anachokisema, akajitupa na kukaa kwenye kiti huku akionekana kukerwa mno na maelezo ya Brandina. Felix aliitazama saa yake ya mkononi kisha akajisemea mwenyewe huku akiwa ameuma mdomo wake kwa hasira.

"Masaa manne my foot.."

Brandina alitembea haraka akamfikia jasusi Jacob pale mlangoni.

"Jacob we need to find the original compact disc (CD) right now" (Jacob tunatakiwa kutafuta CD halisi sasa hivi)

"Sure, bila shaka kuna mchezo hapa katikati"

"Haswaa, tuna masaa matatu tu, bila hiyo CD hatutakuwa na haki ya kuendelea kumshikilia Felix hapa kituoni. tupambane ndani ya huu mda kuhakikisha tunapata kitu"

"Sawa basi tugawane majukumu mimi naenda ofisi za idara ya usalama wa Taifa kwa sababu usiku wote CD ilikuwa kule na itakuwa mchezo wa kuibadilisha umefanyika kule, nitafuatilia kwa umakini mazingira ya upotevu, wewe nenda pale supermarket mahali ambapo tukio lilifanyika ninaimani watakuwa na kopi ya tukio kwa sababu ni kamera zao ndio zilirekodi" Jacob alitoa maelezo.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa, walimuacha Felix akiwa chini ya uangalizi mkali wa polisi wakiongozwa na Inspekta Masoud, wao wakaingia ndani ya gari zao kila mmoja akaelekea upande wake, ilikuwa ni lazima wafanye juu chini kuhakikisha wanamtia Felix hatiani ndani ya masaa hayo manne ndipo mambo mengine yafuate.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Dakika 9 zilimtosha Inspekta Brandina kufika MINI supermarket eneo ambalo ndipo ile video inayomhusisha Felix na tukio la utekaji ilirekodiwa na kamera za CCTV nje ya jengo hilo.

Wakati anafika Brandina anakutana na tukio la ajabu ambalo lilimuacha kinywa wazi, MINI Supermarket ilikuwa ikiteketea kwa moto huku mamia ya watu wakiwa wamezunguuka kushuhudia tukio hilo lililotokea katikati ya mji wa Dar es salaam.

Brandina alipaki gari lake hatua kadhaa kutoka eneo la tukio akashuka haraka na kukimbia kwenda kushuhudia maafa hayo. Kwa bahati mbaya hakukumbuka kuuchomoa ufunguo wa gari lake wala kuufunga mlango vizuri alichowaza ni kuwahi MINI supermarket. Mara tu baada ya kutoka kuna muhuni mmoja akafungua mlango wa gari akaingia akawasha na kuondoka nalo taratibu, akapotea.

Brandina alifika na kujiunga na umati wa watu waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kusikitisha. Tayari zimamoto walishafika eneo la tukio na sasa walikuwa wakiifanya kazi yao ipasavyo ingawa walichelewa kwani tayari robo tatu ya jengo hilo ilikuwa imeteketea vibaya kwa moto.

"Felix...Felix...Felix...wewe ni nani hasa.." Aliwaza Inspekta Brandina huku akikunja ngumi kwa hasira. Tayari alikuwa anaamini kwa asilimia zote kuwa Felix ndiye muhusika wa tukio hilo la kuungua kwa MINI supermarket.
Ni kweli njama zote hizi zilikuwa zikifanywa na kikosi hatari cha kigaidi MG Family. Kama utakumbuka Magnus aliwaagiza watu wake wahakikishe Felix anakuwa huru na hivi ndivyo namna uhuru wa Felix ulikuwa ukitafutwa.
Kushambulia na kumtoa Felix kwenye mikono ya polisi lilikuwa ni jambo dogo mno kwa MG Family lakini hili halikuwa agizo la Magnus. Mzee alitaka mwanae awe huru hivyo mpaka sasa tayari MG Family walikuwa wamefanikiwa kwa hatua moja ambayo ni kuupoteza kabisa ushahidi. Wakabadilisha CD, wakachukua ile yenye tukio halisi wakaacha yenye tukio feki iliyotengenezwa kitaalamu sana na mwisho kabisa wanaichoma moto MINI supermarket
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili ndani ya kisiwa ilipo himaya ya Magnus, Katika chumba kimoja alionekana Zungu akiwa amefungwa mikono yake yote miwili kisha kamba hiyo ikafungwa juu ya paa akawa ananing'inia miguu yake ikiwa haijagusa chini. Mwili wake ulikuwa umetapakaa damu karibu kila mahali huku wanaume wawili wenye misuli mikubwa na umbo la miraba minne wakimsindilia ngumi nzito zisizo na hesabu eneo la tumbo na kifua.

Zungu alikuwa akipitia kwenye mateso makubwa mno na hayo yote yalifanyika ili tu aeleze ni vipi ameweza kutoka bondeni hadi kufika kule barabarani. Hili lilikuwa ni agizo la Magnus mwenyewe mara tu baada ya kupata taarifa za mateka huyo aliyefanikiwa kutoka bondeni. Lakini hadi dakika hii Zungu ambaye alikuwa hoi taabani pamoja na mateso makali aliyopitia hakuweza kufungua mdomo wake na kuzungumza ukweli kuhusu ile njia ya pangoni. Aliona ni heri kufa kuliko kueleza ukweli huo ambao ni msaada mkubwa kwa David, Dayana pamoja na mateka wote bondeni.

Baada ya mateso ya muda mrefu taarifa zilimfikia Magnus kuwa mateka hajazungumza chochote hadi sasa. Mwisho Magnus akainuka mwenyewe na sasa akawa anaelekea kwenye chumba cha mateso alipo Zungu. Pembeni yake aliongozana na mpambe wake wa karibu pamoja na walizi kadhaa nyuma yake lakini wale wanawake wanne wenye visahani vinavyotoa moshi hakuwaacha kila anapokwenda.

"Unajua nini Zorrack" Magnus aliongea na mpambe wake wakati wakielekea chumba cha mateso.

"Ndiyo Mkuu nakusikiliza..."

"Napata hisia kuwa tayari Sasha mtoto wa Gu Gamilo yupo nje ya ISRA kwa sasa, inabidi tumtafute haraka tumpate na kumleta hapa. Fanya kila liwezekanalo Sasha apatiakane haraka. Huyu binti ni kete moja muhimu na ya ushindi kwetu"

"Nimekuelewa mkuu..."

"Vizuri taratibu za kumtafuta zianze leo, na huyu kijana ni lazima azungumze ukweli kama mateso makali yameshindwa kuufungua mdomo wake basi nitatumia njia mbadala"

"Njia gani mkuu?"

"Ushawishi, tumpe anachokitaka. Nitacheza na saikolojia yake" Alisema Magnus na tayari walishafika chumba cha mateso, mlango ukafunguliwa wakaingia.

Je nini kitafuata?

ITAENDELEA...

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya...........39 -40

SASA ENDELEA....
[emoji294][emoji294][emoji294]
Upande wa pili mbele ya macho yake Inspekta Brandina anashuhudia supermarket ya MINI ikiteketea kwa moto hii ikiwa ni tafsiri kwamba hakukuwa na namna nyingine ya kupata kopi ya ile video ya ushahidi iliyorekodiwa na kamera za CCTV.

Haraka alichukua simu yake kutoka mfukoni kisha akampigia Jasusi Jacob ili kusikia upande wake kama kuna chochote amekipata.

"Hallo Inspekta" sauti ya Jacob ilisikika simuni.

"Ndiyo Jacob, hali sio nzuri huku. Wameichoma moto ile supermarket hivi ninavyoongea kila kitu kinageuka majivu. Hatuwezi kupata kopi ya ile CD kabisa" Alieleza Brandina.

"Aisee! Hawa watu mbona wako serious sana..."

"Sana tena sana, na sisi tusipokuwa serious watatupiga bao kila mahali, tunatakiwa kuwa hatua moja mbele yao. Tayari wameshatuzidi akili, tutafute maarifa mapya ya kupambana nao"

"Tunafanyaje sasa Inspekta?"

"Hamna kurudi nyuma, Felix ni lazima aendelee kubaki mikononi mwetu Jacob, tutafute sababu yoyote ya kuendelea kumshikilia"

"Nimepata wazo Inspekta"

"Ndiyo nakusikiliza Jacob"

"Nakumbuka wakati nafuatilia mahojiano yako na Felix mwanzoni kabisa kuna kitu niliona si cha kawaida"

"Kipi hicho Jacob?"

"Ni kuhusu jina halisi la Felix, alidai kuwa alibadili jina baada ya kuhama dini. Lakini akaongeza na kusema alishauriwa na mchungaji, vipi kwa muonekano wa Felix jinsi alivyo unaona ni mtu wa dini kweli?"
Brandina alitulia kidogo kisha akajibu...

"No, hawezi kuwa mtu wa dini yule, uko sahihi Jacob. Tunatakiwa tuchimbe zaidi kuhusu historia ya huyu mtu huenda tukapata kitu"

"Yes! sure, kwani tumebakia na muda gani mpaka sasa?"

"Eee! hapa tuna kama masaa mawili na kidogo..."

"Okay basi wacha tuingie kazini wewe pambana huko na mimi nipambane huku ofisini kwetu tunayo mifumo mizuri ya kuweza kutambua historia ya maisha ya nyuma ya kila mtu. Nitafanya mawasiliano na watu wanaoweza kumfahamu kama ikibidi. Nitafuatilia kila kitu kuanzia alipozaliwa shule aliyosoma na kadharika"

"Inawezekana Jacob? Ndani ya huu mda?"

"Bila shaka Inspekta kama mtu ameweza kusafiri hadi Marekani na kapanda hizi hizi ndege zetu basi lazima taarifa zake tutazipata tu..."

"Okay wazo jema"

"Nitajie basi yale majina yaliyopo kwenye kitambulisho chake"

"Sawa anaitwaa..."

"Sorry ngoja kidogo nichukue pen na karatasi....okay nitajie sasa"

"Anaitwa Feisal Ayoub Suleiman"

"Sawa basi baada ya nusu saa tukutane kituoni pale tuunganishe taarifa..hallo... Inspekta...hallo..." Jacob aliita lakini Brandina akawa kimya ghafula, tayari alishafika pale mahali alipoacha gari lake ajabu hakuliona, akawa anaangaza macho yake huku na kule kulitafuta, hakumjali tena jasusi Jacob aliyekuwa akiita simuni.

"... Inspekta??"

"Eeh nakupata Jacob nusu saa nusu saa tukutane" Brandina aliongea haraka haraka kisha akakata simu.

"Ooops! One mistake one goal!! wanaume wa dar pumbavu kweli" Brandina alijisemea mwenyewe huku akiwa ameshika kiuno chake, tayari alishatambua kuwa gari yake imeibiwa.

Pamoja na yote bado mwanadada huyu machachali hakutoka kwenye lengo, alimpigia simu dereva taksi mmoja anayemfahamu na punde alifika na kumchukua wakaondoka. Bado alikuwa kwenye mapambano makubwa kuhakikisha Felix hatoki kwenye mikono yake, tayari alishajua kuna njama za makusudi zinaendelea.

Ni kweli mara baada ya Inspekta Brandina kuondoka maeneo ya MINI supermarket kwa mbali alionekana mwanamke mmoja mrembo akiwa ndani ya gari dogo Nissan, huyu alikuwa ni mtu kutoka kundi la kigaidi MG Family kazi yake kubwa ni kufuatilia nyendo zote za Inspekta Brandina na kutoa taarifa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Nusu saa baadae....
Tayari Inspekta Brandina na jasusi Jacob walikutana kituo cha polisi. Sasa waliungana pia na Inspekta Masoud pamoja na askari wengine watatu, wakawa wanajadili taarifa walizozipata.
Jasusi Jacob ndiye aliyeanza kuzungumza akaeleza akisema...

"Anaitwa Feisal Ayoub Suleiman, mtoto wa kwanza wa marehemu mzee Suleiman. Amezaliwa tarehe 19/9/1992. Mwaka 2008 Feisal akiwa na miaka 16 alikuwa akisoma kidato cha pili shule ya Sekondari Mkwawa Mbeya- chunya. Kwa bahati mbaya wakati akicheza na mdogo wake alipata ajali na kutumbukia darajani ndani ya maji. Hakuna aliyefanikiwa kuupata mwili wake zaidi ya mwili wa baba yake marehemu mzee Suleiman ambaye alijitosa majini kujaribu kumsaidia mwanae lakini alishindwa na kujikuta anapoteza maisha."

"Kwa hiyo Feisal alikufa?" Aliuliza Masoud

"Iko hivyo kila mtu kwenye kijiji chake anaamini Feisal alishakufa lakini hakuna aliyewahi kuthibitisha hilo kwa sababu mwili wake haukuonekana mpaka leo, ni miaka 13 imepita tangu kutokea kwa tukio hilo"

"Kwa hiyo inaweza kuwa Felix ndiyo Feisal mwenyewe?" Aliuliza Brandina

"Hii ndiyo maana yake.. huyu ndiye Feisal mwenyewe hakufa alipona na anaishi mpaka leo huku watu wakiamini alishakufa" askari mmoja alitoa wazo.

"Acha kurahisisha mambo afande Chopa, hapa naona kuna akina Feisal wawili huyu wa utotoni na huyu wa ukubwani tunachotakiwa kuthibitisha ni je huyu ni mtu mmoja au ni watu wawili tofauti. Na kama ni tofauti kwa nini Felix anatumia jina la marehemu Feisal? Lazima hapa atakuwa na kesi ya kujibu, au mnasemaje?" Alieleza Jacob na mwisho akauliza swali

"Ni sawa lakini tutathibitisha vipi sasa, hata picha zake za utotoni hatuna" Aliuliza Inspekta Masoud

"Nimepata hii picha moja tu ni kama passport aliyotumia shuleni wakati akiingia kidato cha kwanza na alikuwa na miaka 15 pekee. Nimetumiwa na mwalimu mkuu Sekondari ya Mkwawa huko chunya" alieleza Jacob

"Hebu subiri kwanza, Inspekta Brandina unakumbuka jina la yule kijana ambaye ametekwa juzi pale mgahawani anaitwa nani ulisema?" Aliuliza Inspekta Masoud

"Woow! Uko smart sana Inspekta, yule kijana ni David, anaitwa David Ayoub Suleiman" alisema Brandina kila mmoja akaguna na kujaribu kuwaza.

"Ni majina tu yanafanana au wanaweza kuwa ndugu? Feisal Ayoub Suleiman, David Ayoub Suleiman.... Kwamba hawa wawili ni ndugu yaani mtu na kaka yake?" Aliuliza Masoud

"Ngoja kwanza..." Alisema Jacob kisha akawa anapiga simu mahali, simu iliita na kupokelewa.

"Hallo Headmaster, ni mimi tena kutoka Idara ya usalama wa Taifa... Ndiyo... samahani naomba nikusumbue tena, ulisema yule kijana Feisal aliyefariki alikuwa na mdogo wake unaweza kukumbuka jina la huyo mdogo wake...eeh ndiyo...nani....sawa... asante sana mzee wangu....." Jacob alimaliza maongezi kisha akakata simu. Wote wakawa makini kumsikiliza atasema nini.

"Mdogo wake Feisal anaitwa David" alisema jasusi Jacob, ilikuwa ni taarifa iliyozidi kumfikilisha kila mmoja.

"Kwa hiyo basi ni kweli David na Feisal ni ndugu...kuna mtu mmoja tunaweza kumtumia kuthibitisha kama kweli Felix huyu ndiyo Feisal mwenyewe" Alisema Inspekta Brandina.

"Ni nani..?"

"Ni Mama David"

"Yupo? Huyo mama yuko wapi?"

"Yupo hapa hapa Dar, acha nitafute mawasiliano yake..." Alisema Inspekta Brandina kisha akatoka nje ya kile chumba.
Wakati wote huo Felix alikuwa ndani ya kile chumba cha mahojiano akisubiri, tayari alishachoka. Akawa anahesabu masaa huku akiamini kabisa hakuna watakachopata, mwisho atatoka, watamuachia huru. Mpango wa MG Family kuhakikisha anakuwa huru ulikuwa umesukwa ki ufundi sana.

Ni kweli kabisa wakati Magnus amefukuzwa ISRA akiwa na mtoto wake mdogo Felix aliyaanza maisha yake kule kisiwani lakini wakati wote Felix alikuwa akimsumbua akitaka kuingia uraiani. Baadae sana Magnus aliwapa jukumu hili MG Family watafute namna ambayo mwanae Felix atatambulika kama Raia wa kawaida nchini. Ndipo hapo MG Family walipoingilia taarifa za mtu aliyewahi kupotea Feisal Ayoub Suleiman wakazibadilisha taarifa hizo zikawa za Felix.
Felix akaingia uraiani akiishi kwa jina la Feisal, vitambulisho vyake na kila kitu vikapewa jina la Feisal. Hii ndiyo sababu hata wakati ule Tesha alipouliza abiria aliyepanda ndege ya BOENG 707 mwenye jina la Felix hakulipata.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili nyumbani kwa Mama David. Bado mama huyu alionekana kuwa kwenye majonzi makubwa tangu siku ya jana alipotembelewa na ugeni wa ghafula pale alipotoka hospitali.

Sasa Mama David alikuwa amekaa varandani nje ya nyumba yake huku akilia kwa kwikwi akisema...

"Mwanangu alishakufa...hawezi kuwa hai...mwanangu Feisal alikufa, mrudisheni Tatu wangu, eeh! Mungu kwa nini unaruhusu nipitie kwenye huu mtihani. Nalazimishwaje kukubali mwanangu anaishi wakati najua ulishamchukua.. Eee Baba nitazame mimi mwanao, ni nini hiki mbona sielewi" Mama David alikuwa akilia na kulalamika.
Siku ya jana alipotembelewa na Husnata kutoka MG Family hali ilikuwa hivi....
[emoji294][emoji294][emoji294]

NYUMBANI KWA MAMA DAVID JANA BAADA YA KUTOKA HOSPITALI...

Kulikuwa na gari tatu za kifahari zimepaki nje ya nyumba yake.

"Karibuni" Alisema Mama David mara baada ya kufika nyumbani kwake, ingawa aliogopa lakini alijikaza na kuongea.

"Asante mama vipi hali yako? Unaendeleaje?" Aliuliza Husnata kauli iliyomshangaza sana Mama David, ni vipi mtu huyo katambua kama yeye anaumwa.

"Asante"

"Tunaweza kukaa na kuzungumza kidogo mama..."

"Sawa tu karibu ndani" Alijibu mama David. Akafungua mlango kisha wakaingia ndani yeye na Husnata pekee, Tatu na wengine wote wakabaki pale nje.

"Nakusikiliza mwanangu"

"Asante mama. Nikulize kitu...hivi utajisikiaje kusikia mwanao anaishi." Alisema Husnata kauli iliyo mshtua sana Mama David, akauliza...

"Mwanangu yupi?"

"Mwanao Feisal, ukisikia kuwa hakufa ule mwaka 2008 yupo hai na anaishi mahali fulani..!!"
Mama David alijisikia vibaya sana kuulizwa swali la namna ile, lilimtonesha kidonda ambacho kilishapona muda mrefu na kubaki kovu. Aliinua uso wake taratibu na kumtazama Madam Husnata kwa macho makali.

"Ulishawahi kuzaa we binti?"

"Mmh?"

"Nauliza una mtoto?"
Madam Husnata akatikisa kichwa kukataa.

"Ndiyo maana, basi nikwambie kitu usichokijua sisi akina mama Mungu ametuumba kwa namna ya ajabu sana tuna muunganiko wa kipekee na wanetu tuliowazaa, kama Feisal angekuwa hai au kungekuwa na dalili za kumpata basi ningepata ishara kabla hata hujaja. Feisal mwanangu alishakufa, nambie unataka nini kwangu nikusaidie" Alisema Mama David maneno ambayo kwa kiasi hayakumfurahisha Madam Husnata akaamua aende kwenye lengo moja kwa moja.

"Sawa mama basi kama ni hivyo kuna taarifa muhimu nataka nikupe, ni kweli mwanao Feisal alishakufa lakini kuna mtu ambaye yupo anaishi kwa jina na taarifa zake. Kwa sasa huyu mtu yupo kwenye matatizo makubwa sana. Itafika wakati polisi watahitaji taarifa zake nyingi kutoka kwako na ikibidi uthibitishe kama mtu huyo ndiye mwanao Feisal au laa. Sisi tupo hapa kwa ajili ya kukuomba ufanye hivyo. Kubali huyu mtu ni mwanao Feisal aliyepotelea majini miaka 13 iliyopita" Alieleza Husnata Mama David akahisi mwili wake unakufa ganzi.

"Binti.." aliita mama David kwa sauti ya upole

"Ndiyo mama nakusikiliza, kuna pesa nyingi sana tumekuandalia kwa ajili ya kazi hii, hili begi linapesa nyingi zitakazo kufanya uuage umaskini"

"Achana na hizo pesa kwanza... Je, unafikiri hakuna namna nyingine ya kuthibitisha kuwa huyo mtu wenu sio mwanangu Feisal? Ni kauli yangu pekee ndio inatosha?"

"Najua kuna namna nyingine, lakini wewe kazi yako ni hiyo tu kubali huyu mtu ni mwanao hayo mengine tuachie sisi"

"Siwezi na naomba uondoke" sasa Mama David alifoka.

"Sawa naondoka tutakupa maelezo nini cha kufanya zaidi subiri simu yetu, hizi pesa baki nazo na ukijaribu kutoa taarifa kokote basi utampoteza mwanao wa pili ambaye ni huyu binti mdogo hapo nje tunaondoka naye. Narudia tena kaa usubiri simu yetu kesho" Alisema Husnata na kuondoka.
Mama David alipojaribu kutoka kumfuata alizuiliwa mlangoni na mwanaume mlinzi mmoja wa Husnata. Alishuhudia kwa macho yake mawili mwanae Tatu akikamatwa na watu hao kisha wakapanda garini na kuondoka kwa kasi. Mama David alilia sana pasipo msaada. Siku hiyo ilikuwa ngumu mno kwake, hakula kunywa wala kulala. Hadi kunapambazuka bado alikuwa katika hali ya huzuni Feisal hayupo, David hayupo na Tatu pia hayupo, mama huyu alipata maumivu yasiyo na mfano. Kwa ajili ya usalama wa mwanae ilimbidi Mama David afanye kama alivyoelezwa akawa kimya na kuugulia kwa ndani huku akisubiri simu tukoka MG Family.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati mama David akiwa pale nje valandani akilia mara simu yake iliita haraka akatazama namba ya mpigaji ilikuwa ni namba ngeni, moja kwa moja akaamini watakuwa ni wale watu waliomteka mwanae Tatu. Akapokea haraka.

"Hallo shikamoo mama, unaongea na Inspekta Brandina kutoka kituo cha polisi tafadhali tunamazungumzo muhimu sana na wewe naweza kujua uko wapi kwa sasa nije kuchukua, ni muhimu sana Mama yangu"
Alisikika Inspekta Brandina simuni lakini kabla Mama David hajajibu lolote mara kuna gari ilifika kwa kasi na kufunga breki kali mbele ya nyumba yake. Kufumba na kufumbua mlango wa gari ukafunguliwa, akashuka mwanadada Husnata akiwa na walinzi wawili nyuma yake.

Je nini kitafuata?

ITAENDELEA...

SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya.........40

Baada ya Mama David kumuona Husnata mwanamke ambaye aliondoka na mwanae Tatu siku ya jana alishtuka na kujikuta anashindwa kuijibu simu ya Inspekta Brandina.

Akiwa katika hali hiyo Husnata ambaye alianza kumsogelea taratibu alimuonyesha ishara kuwa aendelee na mazungumzo kwenye simu ile. Mama David aliielewa ishara hiyo kisha akajibu...

"...nipo nyumbani kwangu kwa sasa..."

"Sawa basi tunakuja sasa hivi kukuchukua Mama" Brandina alizungumza upande wa pili wa simu.

"Unapafahamu nyumbani?"

"Yes! Nimepewa adress, dakika kumi tutakuwa hapa"
Simu ikakatwa.
Mama David aliinuka haraka mara baada ya simu ile kukatwa, sasa akawa anatazamana uso kwa uso na Husnata ambaye alishafika na kusimama mbele yake.

"... mwanangu yuko wapi?" Hili lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa mama David.

"Kuwa mtulivu mama, mtoto wako yuko salama, kama utaifanya kazi yetu ipasavyo nakuhakikishia hatutomgusa hata unywele wake"

"Mnataka nifanye nini sasa?"

"Tuingie ndani kwanza" Alisema Husnata kisha yeye na mama David wakaongozana na kuingia ndani sebuleni.

Baada ya kuingia Husnata alienda moja kwa moja ilipo Televisheni ndogo ya Mama David akaiwasha, akawasha pia na king'amuzi chake aina ya Zuku.

"Hey! Hakuna kifurushi chukua namba ya kadi nunua..." Husnata alimuagiza mmoja kati ya walinzi wake kisha akageuka na kumtazama Mama David ambaye alikuwa akimtazama tu mwanamke huyo asielewe ni nini hasa anafanya.

"Mama David, hii ni picha ya mtu niliyekwambia jana, mtu ambaye anaishi kwa jina la mwanao Feisal. Polisi wanakuja hapa ndani ya muda mfupi kama walivyokupigia simu na kukueleza. Kuna kitu unatakiwa ufanye mara tu watakapofika, hii ni kwa ajili ya usalama wa binti yako. Leo itabidi uwe muigizaji mzuri" Alisema Husnata huku akimkabidhi Mama David picha ya Felix kisha akaanza kumpa maelezo nini cha kufanya. Mama David hakuwa na jinsi, alisikiliza na kukubaliana na kila agizo alilopewa. Alifanya hivi kwa ajili ya usalama wa mwanae mdogo Tatu ambaye mpaka sasa yupo kwenye mikono ya watu hawa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati huo upande wa pili kituo cha polisi, Inspekta Brandina akiwa pamoja na askari wengine wawili waliingia ndani ya gari la polisi na safari kuelekea nyumbani kwa mama David ikaanza. Kama kawaida yule mwanamke ndani ya gari aina ya Nissan kutoka MG Family hakuwa akicheza mbali. Alipowaona tu wakitoka naye akaingia barabarani na gari yake akawa anawafuata nyuma.

Wakati huo Jasusi Jacob pamoja na Inspekta Masoud wao waliingia chumba kile cha mahojiano mahali walipomuacha Felix kwa muda.
Walimkuta kijana huyo amekaa pasipo kuwa na wasiwasi wowote huku miguu yake akiwa ameinyoosha na kuiweka juu ya meza, wala hakujali.

Baada ya Jacob na Masoud kuingia Felix alitazama saa yake ya mkononi, sasa lilisalia lisaa limoja pekee ili yatimie yale masaa manne ambayo ni ya mahojiano kisheria katika ofisi za kipelelezi. Baada ya hapo kama hatokutwa na shitaka lolote basi ni haki yake kuachwa huru.

Masoud na Jacob walizunguuka upande wa pili wa meza na kukaa kwenye viti, wakawa wanatazamana na Felix ambaye aliishusha miguu yake chini.

"Sasa mnaweza kuniambia kwa nini niko hapa ndugu zangu? maana siwaelewi kabisa"

"Usijali.. iko hivi Bwana Felix, tumetilia shaka jina lako unalotumia yaani Feisal Ayoub Suleiman kwamba huenda sio jina lako halisi. Je, unaweza kutuambia japo kwa kifupi historia ya maisha yako kabla hatujaenda hatua inayofuata" Alizungumza Inspekta Masoud.

"Hebu subiri kwanza, sijaelewa mnata kujua kwa nini watu wananiita Felix badala ya Feisal? Mbona nilishamwambia yule askari wa kike tayari!!"

"Hapana hujatuelewa, tunataka utueleze kwa kifupi historia ya maisha yako tangu kuzaliwa kwako mpaka hapa ulipo, kwa kifupi tu halafu mambo mengine yataendelea..."

"Mmm!! Basi sawa, kwa kifupi kama mlivyosema mimi naitwa Feisal Ayoub Suleiman, nimezaliwa Mbeya-chunya na kusoma huko mpaka kidato cha pili, mwaka 2008 nilipata ajali mbaya nikatumbukia majini, sikujitambua hadi siku nne baadae ndipo nilipata fahamu nikajikuta niko jijini mbeya mikononi mwa mtu nisie mfahamu ambaye alitaka kunitumia katika biashara zake ovu. Kwa bahati mbaya pia nilipoteza kumbukumbu zangu baada ya ajali ile sikuwa nakumbuka chochote, hata jina langu tu sikulikumbuka pia. Kwa bahati nzuri niliweza kusaidiwa na mtu mmoja ambaye ndiye amenilea na kunikuza hadi hapa nilipofikia. Nilikaa kwa kipindi kirefu sana ndipo baadae kumbukumbu zangu zilianza kurejea upya taratibu. Mwisho nilirudi nyumbani Chunya kuwatafuta ndugu zangu sikuwapata niliambiwa walihama zamani sana mara baada ya mazishi ya baba yangu, nimehangaika kwa kipindi kirefu mno kuitafuta familia yangu bila mafanikio mpaka sasa tunavyoongea. Huwa naumia sana afande, nimeishi kwenye mazingira ambayo sina hata ndugu mmoja wa damu ninaemjua, nipo mimi kama mimi" Felix alimaliza simulizi yake yenye uongo uliokubuhu. Historia iliyowafanya Inspekta Masoud na Jasusi Jacob watazamane na kushika tama. Ingekuwa ni mechi mpaka sasa tungesema Felix anaongoza mbili bila. Kila kete waliyojaribu kusukuma askari hawa waliambulia patupu. Mwanzo waliamini kama Felix sio Feisal basi angejichanganya mahali katika maelezo yake, la hasha maelezo ya Felix yalijitosheleza mno. Sasa ni mama David pekee ndiye aliyekuwa akitegemewa kwa muda uliobaki.
Huwezi kuamini mpaka dakika hii bado polisi hawa walikuwa hawajazungumza chochote mbele ya Felix kuhusu kesi kubwa ya utekaji. Wangeanzia wapi kueleza? Kwa ushahidi upi? CD yenye ushahidi haipo na hata Felix bado anatengeneza mazingira ya kuwafanya waamini yeye ndiye mmiliki wa jina la Feisal Ayoub Suleiman.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Upande wa pili kule mkoani Mtwara katika kijiji cha Nagaga tayari kikosi cha uokoaji kilishawasili na sasa zoezi la uokoaji kwa wahanga wa janga la mafuriko lilikuwa likienda vizuri.

Feisal ambaye huyu ndiye Feisal halisi kaka yake David, alimchukua Sasha mpaka nyumbani kwake katika kijiji jirani cha Nachingwea wilaya hiyo ya Masasi. Feisal alipanga kumsaidia dada huyo(Sasha) mpaka pale kumbukumbu zake zitakapo rejea. Hakujua kuwa Sasha alikuwa akijitambua vizuri tu lakini aliamua kutumia uongo wa kujifanya kapoteza kumbukumbu ili tu kuficha asili yake kwamba ni mtu wa ajabu kutoka ISRA.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Gari la polisi lilifunga breki kali nje ya nyumba ya Mama David. Inspekta Brandina alikuwa ni wa kwanza kushuka, akawa anapiga hatua ndefu ndefu kuuelekea mlango wa nyumba hiyo ambao ulikuwa wazi, askari wenzake wakawa wanamfuata nyuma. Wakati huo hakukuwa na gari lolote nje ya nyumba ya Mama David, Husnata na wenzake hawakuwepo.

"Hodi hapa, ma...."Alisema Inspekta Brandina lakini mara akasita kuendelea baada ya kumuona mama David akitoka chumbani kwake kwa kasi huku akijifunga kitenge chake, alionekana kuwa na haraka sana.

"Vipi mama uko sawa?" Brandina aliuliza huku akipiga hatua zaidi kuingia ndani.

"Mwanangu jamani mwanangu...." Alisema mama David hali akizunguuka huku na kule mle sebuleni kama anaetafuta kitu. Alionekana kuchanganyikiwa haswa.

"Hebu tulia basi mama, unashida gani? Sisi ni polisi mimi ndio niliongea na wewe kwenye simu muda si mrefu.."

"Ninyi ni polisi? Ooh! Sawa..." Alisema mama David, akaelewa zaidi mara baada ya kuwaona wale askari nyuma ya Inspekta Brandina ambao wao walivalia sare zao za polisi.

".....nimemuona mwanangu kwenye Tv, mmemkamata mwanangu Feisal, ni mwanangu alipotea miaka mingi sana iliyopita. Naomba nipelekeni nikamuone" Alisema Mama David kauli iliyomuacha kinywa wazi Inspekta Brandina. Akageuka na kutazama Tv ni kweli kabisa wakati huo kupitia chaneli ya MMD TV walikuwa wakirusha habari za mwanamitindo maarufu nchini Tesha ambaye alionekana uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere asubuhi ya siku hiyo akiwa katika hali ya huzuni kubwa mara baada ya kushuhudia mwanaume mmoja(Felix) ambaye bado mahusiano yao hayajajulikana akikamatwa na polisi. Katika Tv Tesha alionekana wakati ule akiwa amekaa chini baada ya kuishiwa nguvu eneo la mapokezi alipoambiwa na Inspekta Brandina kuwa Felix anahusika na utekaji wa David na wengine.

Inspekta Brandina aliitazama taarifa hiyo kisha akageuka kumtazama Mama David ambaye aliendelea kusisitiza kuwa wampeleke kituo cha polisi akamuone mwanae Feisal aliyempoteza kwa muda mrefu.

Brandina alijikuta anachoka mwili na akili, hata kabla hajaeleza kilichomfanya kuja kwa mama huyo tayari alikuwa na majibu ya maswali yake yote. Tayari Mama David kamfahamu mwanae hata kabla ya kuulizwa.

"Kwa hiyo kumbe ni kweli Felix ni Feisal... nafanyaje sasa" Aliwaza Brandina huku akikaa Kwenye kiti. Hakujua ni ushahidi gani ambao utamfanya aendelee kumshikilia Felix kwa kesi ile ya utekaji. Ingawa ni kweli kabisa Brandina pamoja na askari wengine waliishuhudia ile video orijino ambayo Felix alionekana dhahiri akiwa miongoni mwa watu waliofanya utekaji pale supermarket ya MINI lakini video hiyo imeibiwa haipo kwenye mikono yao tena. Watamshitaki Felix kwa lipi? Kwa ushahidi gani? Hawawezi hata kupeleka kesi mahakamani bila vielelezo muhimu.

Dakika mbili baadae gari hilo la polisi liliondoka kwa kasi huku mama David akiwa pamoja nao.
Kwa mbali Husnata na watu wake walionekana pembeni ya barabara wakilisindikiza kwa macho gari hilo la polisi.

"Mama ni muigizaji mzuri zaidi hata ya watu wa bongo muvi..." Alisema Husnata huku akitabasamu na kuweka simu yake sikioni.

"Hallo.. tuko kwenye hatua za mwisho endelea kuwafuatilia" Alisema Husnata kisha akakata simu. Alikuwa akiwasiliana na yule dada ndani ya gari la Nissan ambaye kazi yake kubwa ni kumfuatilia Inspekta Brandina.

ITAENDELEA....

Simulizi hii inapatika kwa tsh elfu 1 tu njoo WhatsApp namba 0756862047
 
Asant kingine
 
SASHA MLINZI WA NAFSI
Sehemu ya.........41
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

[emoji294][emoji294][emoji294]
Inspekta Masoud pamoja na jasusi Jacob hawakuwa na jambo tena la kuuliza kwa Felix ambaye tayari alisharuka kila aina ya mtego waliomtegea.
Ilikuwa ni aibu sana kwao kushindwa kumtia Felix hatiani angali wanajua kabisa huyu ni mmoja kati ya wahusika wa matukio ya utekaji na walimshuhudia kwa macho yao katika ile video iliyorekodiwa na kamera za CCTV. Hawakuwa na hata sababu yoyote ya kumuweka Felix kizuizini wakati upelelezi ukiendelea.

Wakiwa katika hali ya ukimya kila mmoja akiumiza kichwa nini cha kufanya mara mlango ulifunguliwa akaingia Inspekta Brandina. Wote walikurupuka kwenye viti wakamfuata Brandina pale mlangoni haraka huku kila mmoja akiwa na uso wenye matumaini.

"Vipi umempata?" Masoud alikuwa ni wa kwanza kuuliza swali. Lakini kwa namna sura ya Brandina ilivyokuwa imepowa hii Ilikuwa ni ishara tosha kuwa mambo huenda sio mazuri.

"Vipi kuna shida Inspekta?" Aliuliza Jasusi Jacob. Brandina hakujibu kitu hadi pale walipotoka nje ya chumba hicho wakimuacha Felix mle ndani.

"Hali si nzuri ndugu zangu! Hata kabla sijafanya kitu tayari Mama David amemtambua Felix kama mtoto wake aliyepotea" alieleza Inspekta Brandina.

"Kivipi? Mbona sijaelewa, kamtambua vipi na bado hajamuona?"

"Kamuona kwenye Tv, kuna channel ilirusha lile tukio la airport wakati tunamkamata Felix, lakini walikuwa wanaripoti hasa tukio la yule Dada mwanamitindo anaitwa Tesha"

"Mmh! Kwa hiyo Mama kamuona Felix kwenye Tv na kamfahamu hapo hapo..."

"Ndiyo wakati nafika ndio naye anajiaanda kutoka aje huku kumuona mwanae"

"Aisee! yuko wapi sasa Mama David?"

"Analetwa..."
Wakati wakizungumza hayo Mama David akiwa ameongozana na askari wawili aliingizwa ndani ya chumba hicho na baadae Brandina akawapa ishara wampeleke moja kwa moja kile chumba cha mahojiano alipo mwanae Feisal (Felix).

Inspekta Brandina, Inspekta Masoud, jasusi Jacob pamoja na wale askari walisogea kwenye kioo wakawa wanawatazama mama na mwana wanaodai wamepotezana kwa zaidi ya miaka 13.

Baada ya Mama David kuingia ndani ya kile chumba uso kwa uso anakutana na Felix ambaye naye alisimama ghafula baada ya kumuona.

"Mamaa...." Felix aliita kwa sauti ya chini. Tayari alikuwa anaujua mchezo wote uliopangwa na MG Family hivyo hakupata shida.

Bila kuzungumza neno mama David alianza kupiga hatua kumfuata Felix naye akafanya hivyo mwisho walikutana katikati wakakumbatiana kwa hisia sana. Laiti kama ungewaona usingeamini kama watu hawa wanaigiza. Mama David anajua kabisa Felix sio mtoto wake huku Felix akitambua kabisa mama huyo si mama yake mzazi, bali ni mchezo tu kwa ajili ya kuwazuga askari.

"Mwanangu..."

"Mamaaa.."

"Uko hai Feisal...!!"

"Ndiyo mama ni mimi, niko hai"

Brandina na askari wengine walikodoa macho kutazama na sasa wakaamini moja kwa moja kuwa ni kweli Mama na mtoto wake wamekuta. Laiti kama kungekuwa na vyeti vinatolewa basi Mama David na Felix wangepewa shahada ya uigizaji.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baadae taratibu zote za Felix kuachiwa huru zilikamilika, hakuwa na kesi ya kujibu. Alimpigia simu msaidizi wake wa karibu Haron ambaye alifika baada ya muda mfupi kuwachukua yeye na mama yake.

Wakati Felix na Mama David wakipiga hatua kuelekea kwenye gari mara Inspekta Brandina aliwatokea kwa mbele, wakasimama.

"Mama tangulia kwenye gari" alisema Felix, Mama David akafanya hivyo.

Sasa Brandina na Felix mtoto wa Magnus wakawa wanatazamana uso kwa uso.

"Kwa nini mnateka watu? Mnawapeleka wapi? Kwa sababu zipi?" Brandina alimuuliza Felix maswali matatu mfululizo.

"Sijakuelewa afande" Felix akajifanya hajui kitu.

"Unanielewa vizuri sana nini namaanisha Felix, Najua kila kilichotokea leo ni mchezo wako wewe na watu wako unaoshirikiana nao ila nataka nikuhakikishie kitu kimoja. Iko hivi, siku si nyingi nitakurudisha hapa na hautokuwa na mahali pa kutokea tena, wewe na watu wako wote mtakuwa na kesi ya kujibu ni wapi ambapo huwa mnawapeleka Raia mnaowateka" Alisema Brandina.

Baada ya kusema hivyo Felix aliachia tabasamu la dharau, akaangaza macho yake huku na kule kisha akapiga hatua akamsogelea Inspekta Brandina na kumnong'oneza sikioni.

"Napenda sana michezo kama hii, ila nina sheria zangu, ukiamua kuanza kucheza na mimi basi hutakiwi kuacha hadi mshindi apatikane, sasa tumeanza rasmi mchezo wetu, Karibu Inspekta Brandina. Nafikiri hata mtoto wako Corinne atafurahia kuwa na mama mpambanaji kama wewe..."
Baada ya kusema hayo Felix aliondoka huku akitembea kwa kujiamini sana. Brandina aligeuka akawa anamsindikiza mtu huyo kwa macho hadi pale alipoingia ndani ya gari na kuondoka. Hakujua ni vipi Felix ameweza kulifahamu jina la mtoto wake wa kike Corrine. Alielewa wazi Felix anajaribu kumtisha.
Felix alizungumza maneno mazito mno yenye fumbo ndani yake lakini Brandina hakuwa na kichwa kizito, alimuelewa vizuri sana.

"Felix, hadi hapa nilipofikia nimepambana na watu wazito na wakubwa kuliko hata wewe, mwisho wa siku wote niliwasweka gerezani. Acha tuone nani atakuwa na mchezo mzuri kati yangu mimi na wewe." Brandina alijisemea mwenyewe na baada ya hapo akapiga hatua kurudi ofisini kwake.

ITAENDELEA...

Weka comment yako hapa chini
 
oya mbona hauko kibiashara hivyo. kuingia huku chenga. na fb pia nimetuma ujumbe toka jana chenga. unazingua sana
 
Back
Top Bottom