Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0689092982

SEHEMU YA KUMI NA TISA-19

Zabroni na rafiki yake wakuitwa Bukulu walipokuwa njiani wakirudi nyumbani,alimuuliza kipi hasa kilichomfanya yule dada ambaye ni Veronica kumuita ndani ya gari huku akionekana kumwambia jambo fulani. Zabroni alicheka kidogo baada kusikia swali la swahiba wake,na kabla hajamwambia, alisema "Ujue tumesahau kununua mafuta ya kupikia, pia chumvi nayo tumeishiwa ndani". Bukulu alishusha pumzi kwa kasi huku akiwa ameshika kiuno chake kisha akajibu "Basi ningojee hapa hapa nikimbie dukani mara moja nikanunue,hatuwezi kula CHUKU CHUKU ilihali hela tunayo bwana",alijibu huku akifatisha na tabasamu pana lililomfanya Zabroni naye kuachia lake. Baada ya hapo alitumua mbio kufuata hayo mahitaji yao,nyuma nako Zabroni akiwa amejiinamia akifimfikiria yule mwadada Veronica.
"Daah hivi ni kweli mimi Zabroni leo hii napendwa na mrembo kama yule? Kwa kipi hasa,maana sina SWAGA sio mtanashati. Yani nipo nipo tu. Ama kweli nimeamini kupendwa ni nyota tu nasio uvaaji ama muonekano. Hapa ni sawa nimeokota chungwa chini ya mnazi ",kwisha kuwaza hayo alichia tabasamu kwa mara nyingine tena wakati huo huo Bukulu naye tayari alikuwa amerudi ambapo alishangaa sana kumkuta rafiki yake akiachia tabasamu. Kimoyo moyo akajisemea "Sio bure huyu jamaa atakuwa kapewa zawadi na yule binti "
"Zabroni vipi naona utabasamu mwenyewe unatabasamu tu", aliongea Bukulu kwa sauti akimwambia Zabroni, Zabroni aliposikia maneno ya Bukulu alicheka kidogo kisha akajibu "Daah! We acha tu,kiukweli yule msichana nilipo muona mara ya kwanza pale sokoni aliponikanyaga. Moyo wangu ulilia paa,hata maumivu siku yasikia"
"Unamaana gani Zabroni? " Bukulu alihoji.
"Maana yangu ni kwamba,Mungu anajua kuumba kaka. Kusema kweli wakati mungu anamuumba yule msichana alitulia, sio wale ambao aliwaumba akiwa na haraka. Ndio maana utakuta mwanamke anakichogo kama mkono wa bunduki,ukimtazama macho mithili ya nyanya chungu..." , alijibu hivyo Zabroni maneno ambayo yalimfanya Bukulu kuangua kicheko kisha naye akaongezea kusema "Kweli kabisa uyasemayo Zabro,utakuta mwanamke kwanza hajui kutembea. Anatembea upande kama ngadu,sura mbovu mbovu tu halafu maajabu ya watu kama hao mtaani wanalinga. Utasikia mimi nataka mwanaume mwenye gari wakati nyumbani kwao hata baiskeli hawana", alitania Bukulu,hapo sasa ndipo vicheko vilipo sikika huku wakigongeana mikono.
Baaada ya kusema hayo kimya kidogo kilitawala huku wakizipiga hatua kurudi nyumbani kwao,lakini muda mchache baadaye Bukulu alifungua kinywa chake na kisha kusema "Haya sasa niambie yule dada alikuitia nini ndani ya gari"
"Sawa ngoja nikwambie rafiki yangu. Ujue yule dada ni kama anashindwa kuniambia ukweli ila mimi kwa kuwa ni mtalamu wa hayo mambo, nimecheza na hisia zake nimegundua kuwa amenipenda. Na kaniambia kesho niende mjini nikaonane naye", alisema Zabroni, Bukulu alikaa kimya kwa muda wa dakika kadhaa kisha akaongeza kusema.
"Enhee umemjibu nini?.."
"Doh Bukulu,ningemjibu nini sasa zaidi ya nipo tayari? Nimemjibu nipo tayari", alijibu Zabroni huku akionekana kulishangaa swali la Bukulu.
"Sawa lakini sio wewe uliyeniambia unatafuta nauli ya kwenda Dar es salaam kumfuata mpenzi wako Tina?..", alirudia kuhoji Bukulu swali ambalo lilimfanya Zabroni kushusha pumzi kwa kasi na kisha kujibu "Ni kweli lakini Bukulu tambua Dar ni kubwa sana halafu istoshe inawatu wengi. Sawa Tina yupo Dar lakini sijui yupo Dar maeneo gani"
"Kwa maana hiyo Zabroni unataka kumsaliti Tina?.."
"Hapana ila kaa ukijua siku zote mwanaume lijali hakai na mwanamke mmoja",alijibu Zabroni kwa kujiamini kabisa. Bukulu alistaajabu kusikia jibu la rafiki yake. Akataharuki "Nini Zabloni? .."
"Mimi naona tufanye mikakati ya kuandaa chakula tu hayo mengine hata baadaye tutazungumza",alijibu kwa mkato Zabroni.
"Sawa pika mboga mimi nitapika ugali"
Zabroni huku akicheka akajibu "Aaawapi huwezi kunilisha ugali mbichi tena leo"
"Alaah! Umeshau wewe ulipo pika wali bila kuuosha mchele? .."
"Afadhali mimi. Je, wewe uliyetia chimvi nyingi kwenye mboga istoshe mboga yenyewe maharage. Osha ujuavyo lakini chumvi ipo pale pale. Kukosea kupo ila kwa leo sitaki turudie makosa"
Vijana hao wawili walitaniana , hayo yalikuwa ndio maisha yao utani ukichukuwa nafasi kubwa huku Zabroni akiwa ameshatundika daluga la kisasi cha damu alichokuwa akikifanya.
Usiku ulipo ingia,usingizi kwa kijana Zabroni ulionekana kikwazo sana kuja siku hiyo hisia zake zote alizipeleka kwa Veronica. Alijipindua huku na kule kitandani huku akitamani pawahi kukucha ili akaonane naye,lakini mwishowe usingizi ulimpitia. Hiyo tayari ilikuwa saa sita usiku. Kesho yake asubuhi alikuwa wa kwanza kuamka akajianda kwa niaba ya kwenda kuonana na Veronica kama walivyo kubaliana. Alimuaga swahiba wake,lakini kabla hajaondoka Bukulu akamwambia "Mbona mapema hivi Zabloni? Subiri basi hata saa nne ama tano ndio uende",Zabloni akatoka nje akaenda kutazama jua kisha akarudi ndani kumjibu Bukulu "Bukulu saa hizi mpaka kufika mjini muda utakuwa umesonga,Kwahiyo acha niwahi"
"Sawa lakini kuwa makini usione vyaelea!"
"Usijali swahiba"
Zabroni akaondoka zake huku nyuma akimuacha Bukulu akitamani ile bahati ingeangukia mikononi mwake.
********
Hatimae Zabroni anaingia mjini,hiyo tayari ilikuwa yapata saa nne kasoro robo asubuhi. Kijijini na mahali ulipokuwa huo mji mdogo palikuwa na umbali kadhaa hivyo licha ya Zabroni kutoka nyumbani mapema lakini alijikuta akifika muda huo,alitumia masaa takribani matatu kwa mwendo wa kawaida.
Mahala pale pale walipokubaliana kukutana ndipo Zabroni alipokwenda kutulia, ambapo muda sio mrefu Veronica naye alifika. Veronica alifurahi sana kumuona Zabroni, huku Zabroni naye pia akifurahi kumuona Veronica. Baada ya maongezi mawili matatu walikwemda moja kumbi maarufu hapo mjini,wakala chakula cha bei. Na mwisho wa yote Veronica akamwambia Zabroni kwamba ametokea kumpenda tangu mara ya kwanza alipomuona,hivyo angefurahi zaidi endapo kama Zabroni atamkubalia ombi lake. Zabroni aliposikia habari hiyo kutoka kwa Veronica alijifanya kuringa ingawa mwishowe alikubali,kitendo ambacho kiliwafanya wote kutabasamu.
Mahusiano kati ya Veronica na Zabroni yakawa yameanzia hapo,huku kila hatua anayo fikia Veronica aliwataarifu makanda wanzake kwani ikumbukwe Veronica alipewa kazi ya kumkata Zabroni mtukutu aliyefanya mauwaji ya kutisha kipindi cha nyuma. Kwahiyo baada jeshi la polisi kumuwinda bila mafanikio ya kumpata,ndipo wakaamua kutumia nguvu ya mapenzi ambapo walimteua Veronica Afande mrembo aweze kuimaliza hiyo kazi wakiamini kwamba mapenzi yananguvu sana kwenye huu ulimwengu. Kweli hatimaye Veronica anafanikiwa kumtwaa kimapenzi Zabroni,shughuli ikiwa imebakia kumpeleleza kijana huyo ili kujua ni nini hasa kinamfanya apotee katika mazingira yoyote? Pia ili ujanja wake huo utoweke njia gani itumike? Na je, hatomstukia pindi atakapo muuliza hayo maswali?
Maswali hayo yalimuumiza sana kichwa Veronica ila swali ambalo aliliona ni pasua kichwa ni kuhusu pindi pale Zabroni atakapo mstukia na kumuona kuwa hayupo naye kimapenzi zaidi ya kumpeleleza. Siku moja asubuhi mapema Veronica alimpigia simu kamanda mkuu ili amsaidie japo ushauri kuhusiana na hilo swali. Kamamda akamjibu "Mpe mapenzi ya dhati,mfamye awe na furaha wakati wote. Naamini atanogewa na kukuona mtu wa muhimu kwake. Wanaume tukipenda tunakuwa kama mazezeta Kwahiyo nafasi hiyo itumie kumuuliza historia ya maisha yake japo kwa ufupi akisita kukwambia basi mtoe muende kupata kinywaji sehemu nzuri ya utulivu,hapo mmbembeleza kumnywesha pombe. Akilewa yote atasema ", aliongea kamanda mkuu. Veronica aliposikia maelezo ya kamanda wake alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Ahsante sana tutaendelea kuwasiliana"
"Sawa kuwa makini"
Baada ya maongezi aliirudisha simu juu meza halafu akajitupa kitandani. Siku hiyo hakwenda kokote, aliamua kupumzika.
Siku zilisonga..Mapenzi ya Vero na Zabroni nayo yakiendelea kushika kasi. Wiki mbili baadaye zilikatika bila ya wapenzi hao kuonana,hakika kila mmoja alimkumbuka mwenzie hasa hasa Zabroni aliyezama kwenye penzi la Veronica,alitamani sana amtie machoni kwani siku nyingi hawajaonana. Hivyo wakati analitamani hilo suala litokee,mara ghafla Veronica alifika kwenye ghetto lao ambalo aliwakuta vijana Zabroni na Bukulu wakicheza drafti. Walimkaribisha lakini Veronica hakuweza kukaa bali baada ya salamu alimuita faragha Zabroni kisha akamwambia "Mpenzi unajua siku nyingi hatuja onana? Yote ni kwa sababu ya haraka za masomo chuo ndiyo ilinifanya nikawa kimya. Kwahiyo rasmi nimekuja nina hamu na wewe sana sijui hata nisemeje. Chazaidi naomba ujiandae twende mjini ukakae japo siku sita tu tufurahi pamoja istoshe sijawahi kulala na wewe au hujui kama mimi na wewe ni wapenzi?.." alisema Veronica kwa sauti nyororo huku akimfuta futa Zabroni nyuzi za buibui kichwani,kwani alikuwa ameegemea ukuta. Kuta nyingi za nyumba za vijijini zinakuwa na utandu wa buibui.
"Najua kama unanipenda, basi kaa kidogo nijiandae ili twende lakini siku sita tu sizidishi sawa?.."
"Sawa mpenzi wangu",alijibu Veronica huku moyoni akiamini kuwa hizo ndio siku pekee za maangamizi. Siku ambayo Zabroni atakamatwa baada kusumbua sana. Siku za hatari.

KIPI KILITOKEA KATIKA SIKU HIZO? MZEE BABA TUKUTANE SEHEMU IJAYO..
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0765168293

SEHEMU YA ISHIRINI-20

Zabroni alijiandaa haraka haraka,alipokuwa tayari kwa safari alimuaga rafiki yake ambaye ni Bukulu. Bukulu alimtakia kila raheri huku akimtania kwamba ahakikishe anamfyonza mpaka yaliyofichwa. Zabroni alicheka sana akifurahishwa na maneno ya Bukulu, lakini yote kwa yote Zabroni aliondoka zake sambamba na Veronica.
Zabroni alijikuta akisahau masharti ya yule babu kutoka Nigeria, ikumbukwe kipindi Zabroni anajiwekea nia ya kulipa kisasi cha wazazi wake tayari alikuwa nyumbani kwa huyo babu. Kwani hakuwa na sehemu nyingine ya kuishi,nyumba yao iliteketea kwa moto huku wazazi wake wakifia ndani ingawa baba yake alikuwa ameshajinyonga. Hivyo mzee yule kutoka Nigeria alimkabidhi dawa Zabroni ya kumfanya apotee mazingira yoyote,kitu kilicho mplekea Zabroni kulipa kisasi kwa uhuru huku akijivunia hiyo dawa. Na kila aliyejaribu kumfuatilia alipotezwa kama mzee Baluguza mganga nguli,lakini pia Madebe bila kumsahau Bruno. Wote hao walipotezwa kiani yake. Lakini sharti moja ya hiyo dawa aliyopewa Zabroni ni kufanya mapenzi,endapo kama atafanya mapenzi basi dawa hiyo itapotea.
Walifika mjini,hapo sasa ndipo mkakati wa Veronica ulipoanza. Siku ya kwanza Veronica aliitumia kuzurula mjini hapo na Zabroni huku akimpitisha kwenye kumbi mbali mbali za starehe, kumbi za hadhi huku wakila na kunywa kwani bajeti aliyopewa Veronica ilidhihirisha kabisa. Hapo Zabroni akaamini kwamba mke kapata, kiasi kwamba ilimpelekea pole pole kumsahau Tina.
Siku ya pili,siku hiyo Veronica aliitumia kuzungumza na Zabroni kuhusu mahusiano yao ambayo yalionekana kunawili kila kukicha. Kiukweli mtukutu Zabroni alionekana kumpenda sana Veronica ikiwa upande wa Veronica,yeye hakumpenda abadani ingawa usoni alionyesha hisia kwa kwake ila ukweli ukiwa ni kwamba alikuwa kikazi. Ukitaka cha uvunguni sharti uiname ndio msemo aliodumu nao moyoni Veronica, afande aliyekabidhiwa jukumu la kumkamata Zabroni.
Katika ya mgawahawa mmoja ndani ya huo mji mdogo. Mgahawa ulionekana kuwa wa kifahari ,walionekana Veronica na Zabroni wakiwa wameketi huku wakinywa vinywaji. Tabasamu lao lilionyesha kuwa bashasha,vile vile kila muda walikuwa wakigongeana mikono kudhihilisha kwamba zogo walililokuwa wakipiga lilikuwa limenoga.
"Zabroni unajua kwamba wewe ni mwanaume mzuri sana?..na pia namuomba Mungu atujalie tuje tuzae watoto!", alisema Veronica akimwambia Zabfoni. Zabro aliachia tabasamu pana kisha akanywa kinywaji chake kilichokuwa ndani ya grasi halafu akamjibu "Asante sana,vile vile hata mimi naona ni bahati kuwa na mrembo kama wewe. Veronica we mzuri bwana"
"Kweli?.." alihoji Veronica.
"Ndio kwani huamini? "
"Sawa naomba tupendane mpenzi wangu",aliongeza Veronica ambapo waligongeana grasi ishara ya furaha halafu wakanyeshwana. Zabroni akimnywesha Veronica kinywaji chake,ilhali Veronica nae akijibu mapigo. Hakika furaha ilionyesha kutawala eneo hilo,na mwisho wa yote walishikana mikono wakarejea nyumbani kupumzika.
Usiku wa siku hiyo wala wa jana Veronica hakutaka kufanya naue mapenzi Zabtoni ingawa alimuweka katika matamanio,kitendo hicho kilimuumiza sana Zabroni kwani usiku wa jana aliamini kwamba huwenda akapewa kitumbua siku ya kesho ambayo ndio siku hiyo ambayo nayo ilionekana hakuna dalili yoyote ya kupewa ili ajilie vyake.
Sio kwamba Veronica alikuwa hajui jinsi Zabroni anavyoumia,lahasha alifahamu fika ila alifanya hivyo makusudi ili kesho yake amuulize mambo kadhaa wa kadha huku akimuahidi kumpa $$## chake endapo kama atamjibu inavyotakiwa.
Kesho yake asubuhi, siku ya tatu hiyo. Veronica aliamka akaelekea bafuni kuoga huku akimwacha Zabroni kitandani akiwa bado amelala,haikuchukuwa muda mrefu alitoka bafuni akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga Zabroni kuwa anaenda chuo. Utaratibu mzima wa chai pia na chakula cha mchana alimuelekeza muhudumu wa hotel hiyo aliyochukuwa chumba Veronica,akimwambia kwamba ampelekee huduma hizo mtu wake ambaye ni Zabtoni. Zabtoni aliamini moyoni mwake kuwa mpenzi wake Veronica ni mwanafunzi wa chuo,lakini upande wa pili Veronica hakwenda Chuo kama alivyomuaga Zabroni kwani hakuwa mwanafunzi ila plan yake ni kumuacha Zabroni kwa muda ili akirudi ajionyeshe kukasirika,kitu ambacho aliamini lazima Zabroni amuulize nini tatizo pindi atakapo onekana kukasirika. Kupitia nafasi hiyo sasa ndipo aanze kufanya upelelezi.
Wakati Veronica akiamini hayo,upande wa pili Zabroni alikuwa na shauku ya kutaka kuonja penzi la Veronica. Hasa hasa kila alipofikilia umbile la huyo mrembo,mwili wake ulijihisi kusisimka huku moyoni akipania siku hiyo avunje ukimya azungumze kuhusu hisia zake. "Nitamwambiaje?.." alijiuliza Zabroni,akifikiria namna gani atamueleza Veronica juu ya yeye kutaka penzi lake. Kwani siku zote alikaa kimya akidhania kuwa huwenda Veronica akajiongeza akawa amembalikia siku yoyote,lakini sivyo kama alivyo dhania. Kila siku walikula na kutembea baadhi ya kumbi ya starehe kuponda raha,kasoro starehe moja tu ambayo ndiyo hiyo Zabroni alikuwa akiitamani siku yoyote itokee. "Nitajikaza lazima nimwambie,haiwezekani kila siku tunalala kama kaka na dada leo lazima niseleleke naye" alisema Zabroni,akisahau kabisa masharti ya dawa aliyopewa.
Muda ulitaladadi,hatimaye jioni iliwadia. Veronica alipofika chumbani hakusema na Zabroni, alijitupa kitandani huku akiwa amelala kifudi fudi. Zabroni alitaharuki kuona kitendo hicho alichokifanya Veronica, alijiuliza "Nani kamkera? Na mbona sio kawaida yake?..", kabla Zabroni hajapata jibu la hilo swali alilo jiuliza, Veronica akamuuliza "Zabroni unanipenda kweli ama unanizuga?.." Zabroni alistuka kusikia swali hilo la Veronica, akamgeukia kisha akamjibu "Swezi kuchezea hisia zako,nakupenda sana. Kwanini upo hivyo leo,istoshe kitu gani kilicho kufanya unilize hilo swali?..", alijibu Zabroni kwa sauti ya upole huku akimkodolea macho Veronica ambaye muda huo alikuwa amejilaza kitandani akijifanya kukasirika.
"Mimi nahisi hunipendi,laiti kama ungekuwa unanipenda basi ungenipeleka kwa wazazi wako",aliongeza kusema hivyo Veronica,maneno ya mtego kwani alifahamu fika Zabroni hana wazazi. Na chanzo cha mauwaji yaliyokuwa akiyafanya chanzo ni wazazi weke, Kwahiyo alisema hivyo ili kumtega Zabroni. Zabroni kabla hajamjibu Veronica, alishusha pumzi kwa nguvu kisha akasema "Veronica mpenzi, mimi sina wazazi"
"Huna wazazi?..",aling'aka Veronica akijifanya kusituka.
"Ndio walifariki kwa ajari ya moto ",aliongeza kusema Zabroni,hapo Veronica aliamka akamsogelea karibu kisha akasema "Pole sana mpenzi wangu,lakini unaweza kuniambia hiyo ajari ilikuwaje kuwaje? Samahani mimi mkeo naomba uniambie nikae nikijua",alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyomfanya Zabroni kushusha pumzi kwa mara nyingine kabla hajaanza kumsimulia.
Upande wa pili, ndani ya mji huo huo mdogo. Alionekana Bruno akikatiza moja ya mitaa ya sokoni,lakini punde si punde alipotea kimazingara wakati huo huo jeshi la polisi likiambatana na mbwa wao wakionekana kulisambalatisha soko hilo baada kugundua kwamba Bruno yupo mahali hapo. Bruno alikuwa ametoroka kabla siku ya kupandishwa mahakamani kusomewa hukumu haijawadia, nia ya kutoroka ni kutaka kulipa kisasi kwa Zabroni. Ikumbukwe Zabroni alimuuwa kaka yake Bruno ambaye ni Madebe,lakini pia aliwauwa wazazi wake huku akiwa na sura ya Bruno ili Bruno agundulike ndio muuwaji mwishowe ahukumiwe jela,nage Zabro aishi maisha bila kusumbuliwa. Ndivyo alivyo amini Zabroni kwamba Bruno kamwe hatorudia kumsumbua kwani atakuwa jela kwa kesi ya mauwaji aliyomsababishia, na ndio maana hakujali sharti la dawa aliyokuwa nayo, sababu alijuwa kazi kuu alishaikamilisha. Asijue kwamba Bruno karudi uraiani huku anasakwa na jeshi la polisi, naye anamsaka mbaya wake popote pale alipo ili akamilishe lengo lake la kulipa kisasi.

ITAENDELEA
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0765168293

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA-21

"Nimekukubali wewe ni mwanaume wa shoka, kama kweli ulilipa kisasi hakika ulistahili kufanya hivyo. Lakini uliwezaje kutembeza hiyo dozi katika hicho kijiji? ",alisema Veronica akisindikiza na swali,kwani alisema hivyo baada Zabroni kumsimulia kisa na mkasa kuhusu kifo cha wazazi wake. Zabroni hakuishia hapo,alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba alilipa kisasi. Jambo ambalo lilimfanya Veronica kumsifia kijana huyo,ambapo hakuishia hapo alimuuliza pia ni namna gani aliweza kutembeza dozi katika hicho kijiji.
Zabroni alikaa kimya kidogo huku akionekana kutafakari jambo fulani,Veronica alipoona hiyo hali akamsogolea karibu zaidi kisha akasema "Niambie shujaa wangu,kidume kati ya vidume. Uliwezaje kutembeza kichapo kijijini. Ikumbukwe wewe ni mtu mmoja,sasa iweje upigane na uma? Ama ndio hivyo unanidanganya?..", aliongea Veronica wakati huo sasa mikono yake ikishughulika kuvua nguo ya juu huku akibaki na sindilia. Kifua chake kikawa wazi, ngozi nyororo isiyo na mikwaruzo ilionekana kwenye mwili wake,kiasi kwamba ilimfanya Zabroni kusisimkwa mwili wake baada kutupia jicho upande aliokaa Veronica.
"Niambie basi" ,aliongeza kusema Veronica. Zabroni alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Kiukweli sikuogopa kitu,kile kifo cha wazazi wangu kilinipa shinikizo. Mmoja baada ya mwingine niliuwa. Hasa hasa yule aliyejaribu kunifuatilia kwa niaba ya kunikatisha kile nilicho kipanga. Nilichoma nyumba hovyo pale kijijini wakati huo tayari ninacho cha kujivunia."
"Mmh kitu gani hicho? Alihoji Veronica. Zabroni akajibu huku akianza kwa kicheko "Hirizi,Nilipewa dawa na mzee yule ambaye nilikwambia kwamba baada wazee wangu kufa nikawa naishi kwake. Huyo mzee ni mtu kutoka Nigeria, alinisaidia kunipa hiyo dawa ili niweze kulipa kisasi kwa uhuru zaidi" . Kimya kilitawala kidogo,kimya ambacho kilimstua Zabroni ambapo alimuuliza nini hasa kilicho mfanya akaye kimya,aidha maneno aliyomuambia? "Vero mbona upokimya ama umeogopa maneno yangu? Usiogope bwana hiyo ilikuwa zamani. Kwanza kwa sasa nipo kawaida sana,istoshe wabaya wangu nilishawapiteza Kwahiyo wala usiwaze. Nakupenda sana tena sana Veronica wangu",alisema Zabroni akimwambia Veronica, ndani ya moyo wake Vero aliamini tayari Zabroni hana ujanja kwake. Hivyo kupitia nafasi hiyo alimuuliza "Mmh nitakuaminije? Usije ukaniuwa na mimi humu ndani"
"Kukuuwa? Hapana siwezi bwana hebu acha utani",alijibu Zabroni huku akiyastaajabu maneno aliyoyasema Veronica.
"Kwahiyo unataka kusema kwamba dawa imeshaisha mwilini? ", akijifanya mtu mwenye hofu alimuuliza swali hilo Zabroni.
"Kabisa,hata hivyo yule babu alinambia kwamba ili dawa aliyonipa ili ipoteze nguvu ni pale nitakapo fanya mapenzi, na tangu niachane na yale matukio sijawahi kufanya mapenzi ingawa naaamini kwamba dawa imeshapoteza ubora kwani kitambo sana sijaitumia"
"Mmmh",aliguna Veronica wakati huo moyo wake ukiwa umefura furaha isiyo kifani.
"Ndio hivyo"
"Kwahiyo unataka kusema hujalala na mwanamke?.."
"Niamini Veronica kama mimi nilivyokuamini mpaka nikaweza kukwambia hii siri nzito. Sijawahi kumwambia mtu yoyote ila wewe,ingawa nakusihi usimwambie mtu yoyote. Ingawa wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini naomba hii iwe siri ya watu wawili tu. ", Zabroni alisisitiza.
"Zabroni mpenzi ", kwa sauti ya upole Veronica akamuita Zabroni.
"Naam! Mpenzi Veronica "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio nakupenda sana"
"Sawa nikuulize swali?.."
"Uliza tu upo huru"
"Hivi ikitokea labda nimevujisha hii siri utanifanya nini?..", akastuka Zabroni baada kuulizwa swali hilo,alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Sitikufanya chochote ila nitafurahi kama utaniomba msamaha". Veronica alicheka kidogo halafu akasema "Hapana siwezi kufanya hivyo kwani hata mimi nakupenda sana"
Siku ya tatu ikawa imeishia hivyo,hapo Veronica alibaki kumaliza kazi aliyopewa kwani tayari kile alichokuwa alikitaka amekipata. Ndani ya nafsi yake akajikuta akijisemea "Ama kweli dunia ina mambo. Kwa mwendo huu kamwe wasingemuweza huyu mtu". Upesi akatoa taarifa kwa uongozi "Safi sana Veronica, wewe ni jembe unafaa sana. Sasa nafikiri ng'ombe mzima umeshamaliza bado mkia tu", alijibu kamanda wake mkuu akifurahishwa na hatua nzuri aliyofikia kamanda Veronica ambaye ametwishwa jukumu nzito la kumpeleleza mtukutu Zabroni ili mwisho wa siku atiwe katika mkono wa sheria baada kusumbua kwa kipindi kirefu sana.
Siku ya pili yake ilipo fika,siku ya nne sasa. Asubuhi mapema Zabroni alimuamsha Veronica ili ampe madini ajilie,lakini Veronica muda huo akajifanya kuamka kwa haraka haraka akidai kwamba kachelewa shule. "Baby unajua mimi nikadhani lao mapumziko. Afadhali ulivyoniamsha acha niwahi ingawa leo nitatoka mapema ili nije nicheze na wewe mpaka pale hamu yako utakapo kata. Alisikika akisema hivyo Veronica akimwambia Zabroni ambaye yeye muda huo alimuamsha kwa niaba ya kutaka $$## lakini Vero akawa ameingizia mambo mengine tofauti na aliyo yatarajia Zabroni.
"Subiri atakuja kunielewa atakavyo nipa nafasi lazima aombe mchuzi wa supu",alijisemea Zabroni ndani ya nafsi yake akionekana kumkamia Veronica pindi atakapo mpa penzi lake. Na wakati Zabroni anajisemea hayo,Veronica alikuwa bafuni kuoga. Punde si punde alirejea akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga mpenzi wake akawa ameondoka zake akiwa katika hali ya kujifanya mwanafunzi.
Huko alikokwenda,aliwataarifu police wenzake ili wajisogeze karibu na tukio. Kamanda mkuu Molisy alionekana kutoyaamini maneno ya Veronica,lakini alipowahakikishia mara mbili mbili hatimaye walikubali.
Jioni aliporejea nyumbani alimchukua Zabroni akampeleka moja ya kumbi ya starehe,ambako huko walikula na kunywa. Waliporejea nyumbani kila mmoja alionekana kuwa tayari kwa niaba ya kucheza mechi,mechi ambayo ilikuwa ya malengo kwa Veronica. Walifanya mapenzi,baada ya tendo Zabroni alilala moja kwa moja mpaka asubuhi ambapo alipo amka hakumkuta Veronica. Alistuka sana kwani haikuwa kawaida ya Veronica kuondoka pasipo kumuaga,wakati akiwa ameshikwa na bumbuwazi..mara ghafla kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi mfano wa nyundo inayotua kwenye chuma. Hali hiyo ilimtia wasi wasi Zabroni, akatoka ndani huku akiwa ameshika kichwa chake. Nje alikutana na muhudumu wa mle ndani ya hoteli waliyokuwa wakiishi na Zabroni na Veronica. "Umenionea mdada kapita hapa asubuhi hii?..", akiwa na hofu dhufo lihali Zabroni akamuuliza muhudumu wa mapokezi kuhusu Veronica.
"Ndio ila..",kabla muhudumu huyo hajaendelea kusema,mara ghafla alidakia braza mmoja aliyekuwa amesimama kando. Braza huyo alisema " Si yule dada mzuri? Anaishi humu ndani? Mweupe kidogo!.."
"Ndio huyo huyo",alijibu Zabloni huku akiwa amekunja uso kwa sababu ya maumivu ya kichwa.
"Doh nimemuona kule maeneo ya gulioni ameambatana na jeshi la polisi lakini baadaye wakawa wameachana sasa sijui kaenda wapi?.." alieleza Braza huyo. Ghafla Zabroni akastuka kusikia habari hiyo, woga ulimjaa kwa mshangao akahoji "Polisi?.."
"Mmh sawa nisubirini nakuja hivi punde ",Kwisha kusema hivyo alitimua mbio kurudi kijijini kwa swahiba wake huku akiamini kwamba tayari maji yamezidi unga, Veronica amemuingiza mkenge. Hivyo aliamua kurudi kijijini kwa niaba ya kuchukua hirizi yake aliyopewa na yule mzee Maboso, hirizi ambayo Bruno aliwahi kuitwaa mikononi mwake baada kumchezeshea kichapo Zabroni cha mbwa mwizi lakini mwishowe akaidondosha pasipo kujua ikawa imerudi mikononi mwa Zabroni kwa mara nyingine tena. Kwahiyo dhumuni kuu ni kuchukuwa hirizi hiyo ambayo alikuwa hatembei nayo,ajifunge ili ajitetee kwa jambo lolote litakalo mkabili ingawa uwezo wa kupotea kama awali hakuwa nao tena. Alipofanya mapenzi,nayo ikawa imepotea. Hivyo hirizi hiyo ni kwa niaba ya kuwa na nguvu za ziada za kuweza kupambana hata na watu mia kasoro lisasi aidha panga.
Alipofika nyumbani alizama moja kwa moja chumbani, alikuta mlango upo wazi,huko alimkuta Bukulu akitupa miguu huku na kule wakati huo damu zikivuja tumboni. Akastuka Zabroni, upesii akamvagaa kumuuliza swahiba wake kipi kimemsibu "BUKULU Bukulu nini kimekupata?.." alihoji Zabroni huku akiwa amechuchumaa kumtazama.
"Bru bru...nooo ", alijibu Bukulu kisha akakata roho. Zabroni alizidi kuchanganyikiwa kusikia jina hilo,akajiuliza "Bruno? Inaamana Karudi?..", kabla hajapata jibu alisikia amri ikitoka nje. "Zabroni toka humo ndani kabla hatujafyatua risasi ", akastuka zaidi Zabroni huku kijasho kikimtoka, alitoka ndani. Nje alikuta jeshi la polisi likiwa na siraha zao mbali mbali huku pembeni akionekana Veronica akiwa amevaa kwanda la kipolisi. "Vero? Ni wewe?", kwa TAHARUKI alihoji Zabroni.
"Ndio mimi nilikuwa kikazi Zabroni,hakuna mwamba chini ya jua. Hatimaye umekamatika mshenzi mkubwa wewe",alijibu kwa dharau na kebehi Veronica. Mkuu wa msafara huo uliofika kumkata Zabroni akatoa amri Zabroni akamatwe. Hukumu ikatolewa kuhukumiwa kifungo cha maisha huku akizushishwa kumuua Buruno kwa mikono yake.
*****
Ndio hivyo ilivyokuwa washkaji, ila siwezi kuendelea kuishi jela. Adui yangu kajitokeza mwingine, lazima nikale nae sahani moja vile vile nikammalize na yule dogo aliyemuuwa Swahiba wangu. Alisema Zabroni huku akiwa amezungukwa na kundi la wafungwa,katika gereza la Ukonga jijijini Dar es salaam. Wafungwa hao walikuwa wakisikiliza mkasa wake huo ambao uliwaacha vinywa wazi.
"Kwahiyo utafanye sasa mwamba?.?", alihoji mmoja wa mfungwa aliyekuwepo hapo. Zabroni alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Nitatoroka siku yoyote"

ITAENDELEA..
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0765168293

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI-22

Gumzo gerezani,kila sehemu wafungwa walikuwa wakimtazama Zabroni kwa jicho la tatu,yote ikitokana na simulizi fupi aliyowasimulia wafungwa wenzake kisa na mkasa kilicho muingiza jela. Na kitu pekee kilicho mpelelea Zabroni kuogopwa zaidi na wafungwa baadhi,ni kauli aliyoitoa kwamba atatoroka gerezani hapo muda wowote.
Mkasa huo wa kutisha aliosimulia Zabroni, hatimaye ulimfikia kijana mmoja aliyefamika kwa jina Bluyner. Kijana aliyetunikiwa cheo cha nyampala gerezani. Ni kijana ambaye alionekana kujazia mbavu na misuli ya mikono yake,uso wake nao ukiwa mkavu zaidi ya kiatu cha mtemebeza nyegere. Sio kwamba Bluyne hakumfahamu Zabroni,la hasha alimfahamu fika ila Hadithi ya maisha yake hakuifahamu. Hivyo siku hiyo akawa ameambiwa, alistuka sana lakini hakutaka kuamini kama kweli Zabroni anaweza kufanya hayo yote sababu matendo hayo hayaendani na muonekano wake. Kupitia hilo Bluyner akihisi huwenda ufalme wake ndani ya gereza hilo ukifikia tamati kwani kupitia simulizi ile ya Zabroni itawafanya wafungwa kumuogopa na kisha kumzarau yeye,kitu hicho Bluyner hakuta kitokee hata mara moja. "Ipo siku nitamfumua mbele yao ili heshima izidi kubaki kwangu",alijisemea Bluyner baada ya kumtafakari Zabroni kwa muda mrefu.
Siku iliyofuata asubuhi ya mapema,kengere iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka kutoka vyumbani mwao haraka sana wakawahi mstarini kuhesabu namba ilihari huku upande wa pili kijana Bluyner alionekana akitembea chumba baada ya chumba akimsaka Zabroni. Hatimaye alimuona,muda huo Zabroni alikuwa akielekea mstarini. Lakini kabla hajafika,mara ghafla aliguswa bega. Zabro alistuka akasimama akageuka kumtazama mtu aliyemgusa bega akamuona Bluyner kiongozi wao. Kwa sauti ya ngumu iliyojaa utashi wa kibabe Bluyner akamwambia Zabroni "Kijana wewe mzuri sana",aliongea hivyo Bluyner huku akimgusa kidevu Zabroni. Zabri alibaki kumshangaa Bluyner, lakini mwishowe alimshika mkono kisha akamng'atua Kwenye mwili wake halafu akasema "Kwahiyo kama mimi mzuri,inakuhusu nini wewe?..",Bluyner akacheka kwa madaha kisha akajibu "Leo kikombe chako cha uji nakunywa mimi",Hapo Zabroni hakujibu chochote,zaidi aliishia kumsonya kisha akazipiga hatua kuelekea mstarini kuhesabu namba kabla hawajanywa uji na kisha kwenda kulitumikia taifa kwa nguvu. Wakati Zabroni anaondoka zake,huku Bluyner aliishia kucheka ingawa naye alijisogeza mahali hapo japo hakujipanga mstari kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake.
Sauti za kuhesabu namba zilisikika zikipasa,punde si punde zoezi hilo likawa limemalizika ambapo amri ya kupanga mstari kwa niaba ya kupokea uji ilitoka kwa mkuu wa magereza. Wafungwa wote walipanga mstari kisha mmoja baada ya mwingine alipokea kikombe cha uji pamoja na viazi viwili. Hatimaye zamu ya Zabroni ilifika ambapo naye alipewa kikombe cha uji na viazi viwili kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake. Alienda kujiweka kando kabisa na eneo lile la kupokelea uji ili apate kujinafasi ingawa walitangaziwa muda maalumu wa kuhitimisha hilo zoezi la kunywa uji,hivyo Zabroni aliketi chini akaanza na kiazi kabla hajabugia funda la uji. Na baada ya hapo alihitaji kisukumizio ambacho ni uji,kabla hajachukua hicho kikombe ili anywe,mara ghafla akatokea Bluyner akachukuwa uji huo na kisha akaunywa. Alikunywa funda la kwanza akanywa la pili akanywa la tatu,uji wote wa Zabroni akawa ameumaliza hakujali ni wamoto kiasi gani. Zabroni alibaki kumshangaa Bluyner, akajiuliza "Ananitafutia nini mimi? Au anataka ugomvi?", wakati Zabro anajiuliza maswali hayo kichwani mwake,Bluyner akacheka nakisha kusema "Usikasirike kijana mzuri. Ukikasirike utaonekana mbaya na mwishowe utazikosa sifa zako",akamaliza na kicheko Bluyner,papo hapo akachukuwa na kiazi cha pili cha Zabroni halafu akaondoka zake akimuacha Zabroni na kipande kidogo cha kiazi mkononi. Kwahiyo asubuhi hiyo Zabroni akawa ameambulia kiazi kimoja tu. Aliumia sana.
Punde si punde amri ilitoka kuwa umefika muda wa kwenda shambani kulima, gari mbili za wazi zilikuja. Kwa puta ya hali ya juu,wafungwa walipandishwa ndani ya hizo gari. Baada wote kupanda,dereva alilisongesha mpaka kwenye shamba la magereza ambapo napo wakati wa kushuka walikurupushwa huku wakipigwa mateke,kitendo kilicho pelekea kutokea purukushani za hapa na pale.

***********

Kipindi hayo yanatokea gerezani,upande wa pili Bruno baada kumtafuta Zabroni kwa udi na uvumba bila mafanikio ya kumpata hatimaye aliamuwa kutimkia ndani ya jiji la Dar es salaam. Huko alienda kwa niaba ya kujificha kwa sababu kipindi chote hicho alichokuwa akimtafuta Zabroni, naye vile vile alikuwa akitafutwa na serikali kwa kosa la kutoroka rumande kabla hajapandishwa kizimbani. Kwahiyo Bruno alipofika Dar es salaam alibadilisha jina na muonekano wake,ambapo alijiita Mr Rasi. Hakuwa na rasta lakini alijitahidi kuzifuga nywere,zilipokuwa ndefu ndipo akasokota rasta. Na hapo ndipo rasmi kijana Bruno akawa Rasta man,jina ambalo liliendana na muonekano wake. Nitaishije ndani hili jiji? Ndilo swali alilojiuliza kijana Bruno ama Mr Rasi. Kwani baada kujificha kwa kipindi kirefu nje ya kidogo ya Dar akingojea nywere zake zikue zimuweke katika muonekano mwingine ambao utamfanya mtu asimtambue,hatimaye akawa ameingia mjini sasa ambapo hilo ndilo swali alilojiuliza huku akiwa amesimama moja ya eneo ya kinondoni saa za usiku. Muda ambao jiji la Dar es salaam linaonekana kuwa na mishe mishe nyingi utaweza sema mchana ndio usiku na usiku ndio mchana,watu hawalali wanatafuta salali.
Mr Rasi akiwa haelewi jinsi atakavyoishi ndani ya hilo jiji,mara ghafla kando yake alipo simama alionekana binti mmoja wa makamo akingojea daladala. Lakini punde si punde yule binti akasikika akipiga mayowe "Mwizi mwizi mwizii jamani kanikwapulia mkoba wangu",Mr Rasi aliposikia sauti hiyo akatoka kwenye dimbwi la mawazo,akatazama upande ule alio simama huyo binti kisha akautazama ule uma wa watu uliokuwa bize kugombania daladala huku wengine wakiendelea na mambo yao bila kumsaidia dada huyo aliyekuwa akilalama kuibiwa. "Kwanini hawajishughilishi na hili lililotokea?..",alijiuliza Mr Rasi. Papo hapo akapotea kama upepo kumfukuzia yule mwizi, punde si punde akasimama mbele yake. Kibaka alistuka wakati huo huo Bruno ambaye ndio Mr Rasi akamwambia "Dondosha mkoba chini kisha utimue mbio",kauli hiyo ukilinganisha na namna alivyomtokea,ilimuogopesha yule kibaka ambapo alifanya kama alivyo amrishwa kisha akatimua mbio. Mr Rasi akuchukuwa mkoba huo upesi akamkabidhi yule binti huku akimsihi awe makini. Binti alishukuru sana lakini pia alihitaji kumjua jina sababu amemsaudia kwa kiasi kikubwa mno. Ni mgoba ambao ulikuwa na vitu kadhaa vya thamani "Naitwa Mr Rasi",alisema Bruno huku uso wake akiwa ameinamisha chini, kofia aina ya kepu aliyovaa ukiuficha vema uso wake.
"Naitwa Tina, ahsante sana Rasi kwa msaada", alijibu binti huyo. Ni yule Tina mpenzi wa Zabroni,siku hiyo anakutana na mbaya wa mpenzi wake pasipo kujua.
Naam! Siku zilisonga,jina Mr Rasi likiendelea kujizatiti kwa kijana Bruno. Ilihari upande wa pili napo gerezani baada Zabroni kuchoshwa na mnyanyaso kila uchwao kutoka kwa Bluyner,hatimaye siku moja akaamuwa kutangaza pambano. Taarifa hiyo ilipomfikia muhusika mwenyewe kiongozi Bluyner alifurahi sana,kwa maana ndicho alichokuwa akikitafuta kwa muda mrefu. Na wakati Bluyner akifurahia taarifa hiyo, upande wa Zabroni yeye alipania siku hiyo ya pambano ndiyo siku ambayo atakayotumia kutoroka gerezani huku akijanasibu kuwa endapo kama atafanikiwa kurudi uraiani atabadilisha jina hali ya kuwa kimya kimya akiwasaka wabaya wake.

USIKOSE SEHEMU IJAYO..
 
Back
Top Bottom