PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0765168293
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA-21
"Nimekukubali wewe ni mwanaume wa shoka, kama kweli ulilipa kisasi hakika ulistahili kufanya hivyo. Lakini uliwezaje kutembeza hiyo dozi katika hicho kijiji? ",alisema Veronica akisindikiza na swali,kwani alisema hivyo baada Zabroni kumsimulia kisa na mkasa kuhusu kifo cha wazazi wake. Zabroni hakuishia hapo,alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba alilipa kisasi. Jambo ambalo lilimfanya Veronica kumsifia kijana huyo,ambapo hakuishia hapo alimuuliza pia ni namna gani aliweza kutembeza dozi katika hicho kijiji.
Zabroni alikaa kimya kidogo huku akionekana kutafakari jambo fulani,Veronica alipoona hiyo hali akamsogolea karibu zaidi kisha akasema "Niambie shujaa wangu,kidume kati ya vidume. Uliwezaje kutembeza kichapo kijijini. Ikumbukwe wewe ni mtu mmoja,sasa iweje upigane na uma? Ama ndio hivyo unanidanganya?..", aliongea Veronica wakati huo sasa mikono yake ikishughulika kuvua nguo ya juu huku akibaki na sindilia. Kifua chake kikawa wazi, ngozi nyororo isiyo na mikwaruzo ilionekana kwenye mwili wake,kiasi kwamba ilimfanya Zabroni kusisimkwa mwili wake baada kutupia jicho upande aliokaa Veronica.
"Niambie basi" ,aliongeza kusema Veronica. Zabroni alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Kiukweli sikuogopa kitu,kile kifo cha wazazi wangu kilinipa shinikizo. Mmoja baada ya mwingine niliuwa. Hasa hasa yule aliyejaribu kunifuatilia kwa niaba ya kunikatisha kile nilicho kipanga. Nilichoma nyumba hovyo pale kijijini wakati huo tayari ninacho cha kujivunia."
"Mmh kitu gani hicho? Alihoji Veronica. Zabroni akajibu huku akianza kwa kicheko "Hirizi,Nilipewa dawa na mzee yule ambaye nilikwambia kwamba baada wazee wangu kufa nikawa naishi kwake. Huyo mzee ni mtu kutoka Nigeria, alinisaidia kunipa hiyo dawa ili niweze kulipa kisasi kwa uhuru zaidi" . Kimya kilitawala kidogo,kimya ambacho kilimstua Zabroni ambapo alimuuliza nini hasa kilicho mfanya akaye kimya,aidha maneno aliyomuambia? "Vero mbona upokimya ama umeogopa maneno yangu? Usiogope bwana hiyo ilikuwa zamani. Kwanza kwa sasa nipo kawaida sana,istoshe wabaya wangu nilishawapiteza Kwahiyo wala usiwaze. Nakupenda sana tena sana Veronica wangu",alisema Zabroni akimwambia Veronica, ndani ya moyo wake Vero aliamini tayari Zabroni hana ujanja kwake. Hivyo kupitia nafasi hiyo alimuuliza "Mmh nitakuaminije? Usije ukaniuwa na mimi humu ndani"
"Kukuuwa? Hapana siwezi bwana hebu acha utani",alijibu Zabroni huku akiyastaajabu maneno aliyoyasema Veronica.
"Kwahiyo unataka kusema kwamba dawa imeshaisha mwilini? ", akijifanya mtu mwenye hofu alimuuliza swali hilo Zabroni.
"Kabisa,hata hivyo yule babu alinambia kwamba ili dawa aliyonipa ili ipoteze nguvu ni pale nitakapo fanya mapenzi, na tangu niachane na yale matukio sijawahi kufanya mapenzi ingawa naaamini kwamba dawa imeshapoteza ubora kwani kitambo sana sijaitumia"
"Mmmh",aliguna Veronica wakati huo moyo wake ukiwa umefura furaha isiyo kifani.
"Ndio hivyo"
"Kwahiyo unataka kusema hujalala na mwanamke?.."
"Niamini Veronica kama mimi nilivyokuamini mpaka nikaweza kukwambia hii siri nzito. Sijawahi kumwambia mtu yoyote ila wewe,ingawa nakusihi usimwambie mtu yoyote. Ingawa wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini naomba hii iwe siri ya watu wawili tu. ", Zabroni alisisitiza.
"Zabroni mpenzi ", kwa sauti ya upole Veronica akamuita Zabroni.
"Naam! Mpenzi Veronica "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio nakupenda sana"
"Sawa nikuulize swali?.."
"Uliza tu upo huru"
"Hivi ikitokea labda nimevujisha hii siri utanifanya nini?..", akastuka Zabroni baada kuulizwa swali hilo,alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Sitikufanya chochote ila nitafurahi kama utaniomba msamaha". Veronica alicheka kidogo halafu akasema "Hapana siwezi kufanya hivyo kwani hata mimi nakupenda sana"
Siku ya tatu ikawa imeishia hivyo,hapo Veronica alibaki kumaliza kazi aliyopewa kwani tayari kile alichokuwa alikitaka amekipata. Ndani ya nafsi yake akajikuta akijisemea "Ama kweli dunia ina mambo. Kwa mwendo huu kamwe wasingemuweza huyu mtu". Upesi akatoa taarifa kwa uongozi "Safi sana Veronica, wewe ni jembe unafaa sana. Sasa nafikiri ng'ombe mzima umeshamaliza bado mkia tu", alijibu kamanda wake mkuu akifurahishwa na hatua nzuri aliyofikia kamanda Veronica ambaye ametwishwa jukumu nzito la kumpeleleza mtukutu Zabroni ili mwisho wa siku atiwe katika mkono wa sheria baada kusumbua kwa kipindi kirefu sana.
Siku ya pili yake ilipo fika,siku ya nne sasa. Asubuhi mapema Zabroni alimuamsha Veronica ili ampe madini ajilie,lakini Veronica muda huo akajifanya kuamka kwa haraka haraka akidai kwamba kachelewa shule. "Baby unajua mimi nikadhani lao mapumziko. Afadhali ulivyoniamsha acha niwahi ingawa leo nitatoka mapema ili nije nicheze na wewe mpaka pale hamu yako utakapo kata. Alisikika akisema hivyo Veronica akimwambia Zabroni ambaye yeye muda huo alimuamsha kwa niaba ya kutaka $$## lakini Vero akawa ameingizia mambo mengine tofauti na aliyo yatarajia Zabroni.
"Subiri atakuja kunielewa atakavyo nipa nafasi lazima aombe mchuzi wa supu",alijisemea Zabroni ndani ya nafsi yake akionekana kumkamia Veronica pindi atakapo mpa penzi lake. Na wakati Zabroni anajisemea hayo,Veronica alikuwa bafuni kuoga. Punde si punde alirejea akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga mpenzi wake akawa ameondoka zake akiwa katika hali ya kujifanya mwanafunzi.
Huko alikokwenda,aliwataarifu police wenzake ili wajisogeze karibu na tukio. Kamanda mkuu Molisy alionekana kutoyaamini maneno ya Veronica,lakini alipowahakikishia mara mbili mbili hatimaye walikubali.
Jioni aliporejea nyumbani alimchukua Zabroni akampeleka moja ya kumbi ya starehe,ambako huko walikula na kunywa. Waliporejea nyumbani kila mmoja alionekana kuwa tayari kwa niaba ya kucheza mechi,mechi ambayo ilikuwa ya malengo kwa Veronica. Walifanya mapenzi,baada ya tendo Zabroni alilala moja kwa moja mpaka asubuhi ambapo alipo amka hakumkuta Veronica. Alistuka sana kwani haikuwa kawaida ya Veronica kuondoka pasipo kumuaga,wakati akiwa ameshikwa na bumbuwazi..mara ghafla kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi mfano wa nyundo inayotua kwenye chuma. Hali hiyo ilimtia wasi wasi Zabroni, akatoka ndani huku akiwa ameshika kichwa chake. Nje alikutana na muhudumu wa mle ndani ya hoteli waliyokuwa wakiishi na Zabroni na Veronica. "Umenionea mdada kapita hapa asubuhi hii?..", akiwa na hofu dhufo lihali Zabroni akamuuliza muhudumu wa mapokezi kuhusu Veronica.
"Ndio ila..",kabla muhudumu huyo hajaendelea kusema,mara ghafla alidakia braza mmoja aliyekuwa amesimama kando. Braza huyo alisema " Si yule dada mzuri? Anaishi humu ndani? Mweupe kidogo!.."
"Ndio huyo huyo",alijibu Zabloni huku akiwa amekunja uso kwa sababu ya maumivu ya kichwa.
"Doh nimemuona kule maeneo ya gulioni ameambatana na jeshi la polisi lakini baadaye wakawa wameachana sasa sijui kaenda wapi?.." alieleza Braza huyo. Ghafla Zabroni akastuka kusikia habari hiyo, woga ulimjaa kwa mshangao akahoji "Polisi?.."
"Mmh sawa nisubirini nakuja hivi punde ",Kwisha kusema hivyo alitimua mbio kurudi kijijini kwa swahiba wake huku akiamini kwamba tayari maji yamezidi unga, Veronica amemuingiza mkenge. Hivyo aliamua kurudi kijijini kwa niaba ya kuchukua hirizi yake aliyopewa na yule mzee Maboso, hirizi ambayo Bruno aliwahi kuitwaa mikononi mwake baada kumchezeshea kichapo Zabroni cha mbwa mwizi lakini mwishowe akaidondosha pasipo kujua ikawa imerudi mikononi mwa Zabroni kwa mara nyingine tena. Kwahiyo dhumuni kuu ni kuchukuwa hirizi hiyo ambayo alikuwa hatembei nayo,ajifunge ili ajitetee kwa jambo lolote litakalo mkabili ingawa uwezo wa kupotea kama awali hakuwa nao tena. Alipofanya mapenzi,nayo ikawa imepotea. Hivyo hirizi hiyo ni kwa niaba ya kuwa na nguvu za ziada za kuweza kupambana hata na watu mia kasoro lisasi aidha panga.
Alipofika nyumbani alizama moja kwa moja chumbani, alikuta mlango upo wazi,huko alimkuta Bukulu akitupa miguu huku na kule wakati huo damu zikivuja tumboni. Akastuka Zabroni, upesii akamvagaa kumuuliza swahiba wake kipi kimemsibu "BUKULU Bukulu nini kimekupata?.." alihoji Zabroni huku akiwa amechuchumaa kumtazama.
"Bru bru...nooo ", alijibu Bukulu kisha akakata roho. Zabroni alizidi kuchanganyikiwa kusikia jina hilo,akajiuliza "Bruno? Inaamana Karudi?..", kabla hajapata jibu alisikia amri ikitoka nje. "Zabroni toka humo ndani kabla hatujafyatua risasi ", akastuka zaidi Zabroni huku kijasho kikimtoka, alitoka ndani. Nje alikuta jeshi la polisi likiwa na siraha zao mbali mbali huku pembeni akionekana Veronica akiwa amevaa kwanda la kipolisi. "Vero? Ni wewe?", kwa TAHARUKI alihoji Zabroni.
"Ndio mimi nilikuwa kikazi Zabroni,hakuna mwamba chini ya jua. Hatimaye umekamatika mshenzi mkubwa wewe",alijibu kwa dharau na kebehi Veronica. Mkuu wa msafara huo uliofika kumkata Zabroni akatoa amri Zabroni akamatwe. Hukumu ikatolewa kuhukumiwa kifungo cha maisha huku akizushishwa kumuua Buruno kwa mikono yake.
*****
Ndio hivyo ilivyokuwa washkaji, ila siwezi kuendelea kuishi jela. Adui yangu kajitokeza mwingine, lazima nikale nae sahani moja vile vile nikammalize na yule dogo aliyemuuwa Swahiba wangu. Alisema Zabroni huku akiwa amezungukwa na kundi la wafungwa,katika gereza la Ukonga jijijini Dar es salaam. Wafungwa hao walikuwa wakisikiliza mkasa wake huo ambao uliwaacha vinywa wazi.
"Kwahiyo utafanye sasa mwamba?.?", alihoji mmoja wa mfungwa aliyekuwepo hapo. Zabroni alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Nitatoroka siku yoyote"
ITAENDELEA..