1. Wako tayari kukukandamiza hata km huna kosa , hawawezi kukutetea kwa bosi/ mkuu, they are always on management side.
2. Wanapenda kujua habari za wenzao ila zakwao hawataki zijukikane
3. Wanaroho mbaya ya uchoyo
4. Mbali na kingereza, hawako smart sana kama inavyofikiriwa
5. Wanapenda mambo ya kulinganisha hasa mambo ya kimaendeleo.
6. Wakenya wakiume walipata nafasi kidogo ni waxhafu sana kwa dada zetu
7. They like show off, wanapenda kujionesha kua wao wema na wanafanya kazi
Prove me wrong from your work place
Mambo haya huhitaji utulivu na uwezo wa kuchanganua mambo kwa mapana. Mimi nina haya:
1. Si mara ya kwanza mimi kusikia waTz tukiwalaumu waKE kwa mienendo yao. Lakini, kwanini tumekuwa watu wa kulaumu tu, hakuna namna ya kujibu mashambulizi? Ukiona tunabaki kulaumu tuu, ujue kuna shida upande wetu pia. Tusipokubali kujitathmini, au kukiri udhaifu wetu tutabaki hivihivi.
2. Mengi uliyoongea ni tabia za jamii nyingi sema tunazidiana kutokana na mazingira tuliyokulia. Sisi Tz, hatukukaa na mkoloni. Wenzetu waliishi nao, hivyo, uchumi wa kibepari na tabia zao wamezibeba sana(uninafsi, hila, ari ya kufanya kazi n.k). Wakenya wanafahamu maana ya kazi, na wanajua kama huna kazi unakufa au unaishia uchizi. Tz hatupo hivyo, mbongo ni mpole siku anaomba kazi tu, baada ya hapo utajuta kumuajiri. Mbongo hata ofisi au biashara yake binafsi anaifanyia upuuzi. Hatupendi kujifunza zaidi, kile ulichotoka nacho darasani tu ndicho hicho utakufa nacho. So, ile hali ya kupigana na kufanya lolote ili maisha yaende sisi hatuna sana, Wakenya wanalo kwa kiasi fulani.
3. Kutokana na maisha ya kikoloni, maisha magumu, yamewafanya Wakenya kuwa na ujanjaujanja ili waweze kukabiliana na mazingira yao. Kwa kulinganisha, kwao wasomi ni wengi, hawana rasilimali za kutosha kama sisi pia, hivyo, ushindani ni mkubwa sana. Ndiyo maana utaona wanatuzidi maeneo kadhaa japo wengi hawaamini hili ,pengine kwa kutokujua ama kwa uzalendo usio na tija. Tazama sekta ya habari tu, wao tuliwatangulia kuwa na TV binafsi. ITV yetu ni bibi kwa TV nyingi za binafsi za Kenya, lakini, tazama vyombo vya Kenya na TZ. Kama mfuatiliaji utaona tofauti kubwa.
Kiufupi , hizo tabia unaweza kuzitazama kwa ubaya ama uzuri. Sisi tunapowasema hivyo Wakenya, tuna uzuri gani? Sisi ndiyo wachamungu sana? Sisi hatuna majungu? Je, mkaka wa kiTz ndiyo atawaacha salama wadada wa Kikenya akipata fursa? Usishangae, hayo niliyosema hapo juu ndiyo yanaingia hadi huku kwenye relationship. Si ajabu kumuapproach mdada wa Kikikuyu ikawa na tofauti fulani na huyu wa kibongo maana tuna tofautishwa sana na exposure. Hii inaweza kulinganishwa hata hapa Tz, katika mahusiano, kuna wadada wa mikoa /kabila fulani hawapo sawa na wa kabila fulani. Kuna ambao ukiwa nao wanajitambua, hujiloweki tu kirahisi, lazima kuwe na returns. Ndugu,huenda sisi ni hatari zaidi sema tu sababu ya kukosa exposure na uelewa, hatuna ujanjaujanja kama wenzetu. Mkenya anaweza asiwe na ujuzi kiviiile kwa kazi anayoifanya, lakini ile aggressiveness inaweza kumpa kazi na akakubalika kuliko mbongo na PhD yake.
Note
Siwasifii Wakenya, bali ninakerwa na tabia ya kuwalalamikia wakati maisha ya kidunia ni kama Yanga na Simba. Hakuna atakaekuombea heri. Hakuna atakaekuonea huruma. So, turekebishe tabia na mienendo yetu na sisi siku moja tulalamikiwe kwa kuwazidi wengine. Kuwatukana, kuwasema vibaya hakusaidiii lolote zaidi ya kujiangamiza zaidi.
Mjadala ni mpana na hauna jibu moja, itategemea sana mtazamo wa mtu juu ya kibaya na kizuri ni kipi kwake. Haya hapa ni maoni yangu,kadiri ninavyofahamu hali ya mambo.
Good day