Sina furaha kwenye ndoa yangu, nahisi nilikurupuka

Sina furaha kwenye ndoa yangu, nahisi nilikurupuka

Tupate burudani kidogo

HODI_NACHA

Lyrics


Hodi wenyewe Nacha ndo nagonga
Namuulizia ndoa hivi nimemkuta au katoka
Ala kumbe yupo mwite namhitaji huku
Naitaka sana ndoa ila tatizo najishuku
Nataka kujua pia nimekuja kukuuliza
Na kama ndoa ni tamu ni kwanini inawaliza?
Ni kwanini inawaumiza bado najiuliza
Na ni kwanini baada ya ndoa majuto hupitiliza
Wanandoa wengi hawana furaha
Na wengi wao mara nyingi tunakutana sana bar
Nakata tamaa jirani kila siku zogo
Na na mbona wanandoa wengi wana nyumba ndogo?
Kipi ni sababu ya wanandoa kugombana?
Kitandani hana kipya kwaiyo hana tena maana?
Aliamua kukuigizia na kuwa kakupenda sana
Au mlikurupuka kipindi cha uchumba nyinyi mkaoana
Inanipa wasi inaniwia vigumu
Kuamini nikioa ndoa yangu inaweza dumu
Mawazo yananikumba nikiwaza kuingia ndoa
Nachohofia ni kuingia ule mlango wa kutoka
Hata maji ya moto kuna muda yanapoa
Hakuna kitu kibaya kama kukosea kuoa
Sorry kwa usumbufu ila nilitaka tu nipime
Nitarudi tena wacha nigonge hodi kwingine

Chorus

I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
Ngoja nigonge mlango wa dini nitatue haya mafumnbo
Nijue kinagaubaga sitaki kufuata mkumbo
Mi sio Isaka, Yakobpo wala Musa mwenye fimbo
Wanafanya kwa faida ya Mungu au faida ya matumbo?
Nijitie mkosi na nijisahau
Na mwisho nikapige goti chini mbele ya madhabahu
Au nijivike ugaidi ukaidi hayawani
Au niwe na busara kama mfalme Suleimani
Mlango nyeti hadi kuingia tu naogopa
Mnanishauri niji Macca au mchungaji wa kuokoka
Nikiingia huku kuna vitu nitavikosa
Starehe za kidunia unadhani wapi nitapata?
Mmenipata? Na nacho ogopa
Ni kumjaribu Mungu kwa kuingia na kutoka
Nimkane kama Petro nimsaliti kama Yudah
Niutangaze ufalme wa Mungu mbele yao nikiwa shuhuda
Niingie kupata pesa 'NO' moto utanichoma
Au niingie kuitangaza injili kila kona
Toa ndugu toa, toa ulichonacho
Ninunue Prado mpya nongeze kipato
Ogopa kuwa Mungu wakati we mwenyewe una Mungu
Siku Mungu akikasirika dunia utaiona chungu
Kuabudiwa kama Mungu na unajua we sio Mungu
Ni kutafuta mchawi nani na unajua mchawi ndugu

Chorus

I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
Kila mlango ni mgumu sioni pakukimbilia
Najiuliza kwanin ni lazima ndani mi kuingia
Kabla sija ghairi nakuna kichwa faster
Nawaza nikagonge labda mlango wa siasa
Naskia ni mchezo mchafu sitaiweza mi ni msafi
Naogopa kulaghai watu mwisho wakipati
Naogopa tega ndoano niwavue hawa samaki
Na mwisho nishibe mimi niwanyime wao haki
Au niingie huenda naeza kuwa bora ka Nyerere
Bora ka Mandela nifikishe nchi mbele
Nikifa nikazikwe kwa shujaa Butiama
Au kaburi langu likazikwe Nyasubi Kahama
Kabla sijaingia kuna vingi niliona
Kura za haki bao la mkono Maradona
Kwa Mungu sasa nitachosema nini?
Ikiwa nilikula nikasaza nikasahau walio chini
Siasa ina makali kama kisu
Nikikumbuka alivyotakaga kuuawa
Nafikiria kutekana nafikiria kuchafuana
Na ndicho naogopa sana
I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
 
Wakuu nakiri kabisa from heart ya kwamba hii ndoa yangu nilikurupuka sana yapata takribani mienzi minne ya ndoa yangu sina hisia ya mapenzi na nahisi kujuta sana kwenye maisha yangu na sina furaha kabisa.

Yaani sina furaha kabisa wakuu yaani najuta kuoa mwanamke wa chop money yaani yeye ni kula tu na kulala na ni mvivu sana na mbaya zaidi kinachoniuma nimetoa mahari nyingi sana lakini binti ni mvivu sna na nahisi majukumu yamenielemea kabisa.

Tafadhali naombeni ushauri wenu wakuu na nataka nimrudishe mazima kwao ili nikeep furaha yangu.

Msinipopoe wakuu
Mkuu habari, Tafadhali sana Mkuu mvumilie Mkeo, Upendo utakuja automatic tu. Bora kuoa mwanamke ambae hajasoma kuliko kuoa mwanamke ambae amesoma. Pambana wewe kama wewe boss. Mkeo mfungulie duka la Mangi.

Huyo do changuo lako.
 
Feminist msimpopoe kwa kua kaoa golikipa. Ndio mwanaume aliyekamilika hawezi kuoa mwanamke mpambanaji. Upambanaji aupambanie huko huko na sio nyumbani. Akiwa nyumbani ni lazima. Nasisitiza NI LAZIMA atii masharti yote ya mume.

Kutii mashart ni lazima,Mimi naona shida sio kutokuwa na kazi ni mvivu ni tabia yake
 
Yeye alikuwa anajua kuwa akiolewa anatakiwa afanye majukumu yepi?
Ikiwa hamkuongea na kupanga majukumu ya kila mwanandoa kabla haujamuoa hana kosa.
Pili ulimuoa ama mlioana? Ikiwa mlioana basi kila mtu ataendelea na mambo yake aliyokuwa akifanya kabla hamjaoana.
 
Kumbadilisha tabia mtu mzima ni jambo gumu sana unless yeye mwenyewe ajitahidi kufifisha tabia zake ili zisikuathiri..

Mungu amtie nguvu tu maana utamrudisha mke kwao kwa ajili ya uvivu na baadae upate huyo mchakarikaji lakini akawa hana adabu na msaliti. Kwa hiyo kama ulivyosema, ni lazma ujue mazuri na madhaifu ya mtu kabla ili ujue kama utaweza kuyabeba au la
Sahihi mkuu.

Kama atapenda atafute kitabu cha "HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE".

Kinaweza kumsaidia kumbadilisha mkewe kwa sbababu muandushi wa kitabu hiko ameelezea mbinu mbalimbali ambazo ukizitukia zinaweza kukusaidia kuwaweza marafiki na kuwashajihisha watu eidha wabadilike au wawe vile unavyotaka wewe.

Sasa namna gani utafanya ili watu wafanye unavyotaka wewe basi mtoa mada asakw hiko kitabu akisome kwa utulivu sana.
 
Sasa wewe si ulisema unaingiza Milion 100 Kwa mwaka?
Ambayo ni sawa na makadirio yafuatayo..
Ambayo ni sawa na Milion 8.4 Kwa mwezi?
Ambayo ni sawa na 1,946,000/- kwa wiki?
Ambayo ni sawa na 278,000/- kwa siku?
Ambayo ni sawa na Tsh 11,590/- kwa saa?
Ambayo ni sawa na makadirio ya Tsh 200 kwa Dakika?

Sasa kilio cha Nini Mkuu,Unatka kumchosha mtoto wa watu wakati pesa Ipo ajiri Watu wafanye kazi nyumban Mke Ni pambo!
😃😃😃😃😃😃😃
 
Tabia sio kilema mrekebishe, japo tatizo hapo nahisi sio tabia Bali ni hisia, huna hisia nae kimapenzi
Hisia sio tatizo.

Miezi minne ni mingi sana kwa mwanaume kumkinai mwanamke unalala nae,unaamka nae.

Cha muhimu ajitahidi kula vizuri na kulala vizuri hamu ya mapenzi itakuja yenyewe tu akishakaa siku kadhaa hajafanya tendo.

Anaweza kukaa siku tatu mpaka 5 ndio akapata hisia za mapenzi hapo anaweza kufanya tendo.

Ila hatakiwi kuwa mpiga punyeto maana itamuondolea hisia na mkewe,anatakiwa awe bize na mishe zake suala la hisia zitakuja tu.

WAnandoa hawawezi kuwa na hisia baina yao kila siku,hakuna binadamu huyo na kama wapo ni wachache sana.

Hisia huja masaa kadhaa baada ya siku kadhaa kupita mnafanya yenu then munaendelea na kujenga familia na uchumi.
 
Wakuu nakiri kabisa from heart ya kwamba hii ndoa yangu nilikurupuka sana yapata takribani mienzi minne ya ndoa yangu sina hisia ya mapenzi na nahisi kujuta sana kwenye maisha yangu na sina furaha kabisa.

Yaani sina furaha kabisa wakuu yaani najuta kuoa mwanamke wa chop money yaani yeye ni kula tu na kulala na ni mvivu sana na mbaya zaidi kinachoniuma nimetoa mahari nyingi sana lakini binti ni mvivu sna na nahisi majukumu yamenielemea kabisa.

Tafadhali naombeni ushauri wenu wakuu na nataka nimrudishe mazima kwao ili nikeep furaha yangu.

Msinipopoe wakuu
Nachokioma hii mada haitusu Aya ni mmbo ya familia zaidi
 
Wakuu nakiri kabisa from heart ya kwamba hii ndoa yangu nilikurupuka sana yapata takribani mienzi minne ya ndoa yangu sina hisia ya mapenzi na nahisi kujuta sana kwenye maisha yangu na sina furaha kabisa.

Yaani sina furaha kabisa wakuu yaani najuta kuoa mwanamke wa chop money yaani yeye ni kula tu na kulala na ni mvivu sana na mbaya zaidi kinachoniuma nimetoa mahari nyingi sana lakini binti ni mvivu sna na nahisi majukumu yamenielemea kabisa.

Tafadhali naombeni ushauri wenu wakuu na nataka nimrudishe mazima kwao ili nikeep furaha yangu.

Msinipopoe wakuu
Tatizo mnangalia sura na shepu lazima liwakute tu... pole mkuu
 
Back
Top Bottom