Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Utasikia happy birthday baba mtoto wangu, Mungu akutunze wewe ndo ulinifanya niitwe mama kwa mara ya kwanza.
Single mother mna mambo [emoji3]
Si tulikubaliana msitufokee mtuambie taratibu jaman..

Mnatufokea sana 😁punguzen sauti sasa
 
Utasikia happy birthday baba mtoto wangu, Mungu akutunze wewe ndo ulinifanya niitwe mama kwa mara ya kwanza.
Single mother mna mambo [emoji3]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Aaa mimi kuna rafiki yake Dada mmoja alikuwa na jamaa mmoja hivi baadae si akabeba ujauzito jamaa akakimbia.
Alipojifungua akajifungua watoto mapacha 2 tena wakike tupu.

Yule Dada aliangaika nae ustawi wa jamii kudai child support, jamaa alikuwa kaajiriwa Serikalini.
Mwishowe jamaa alihonga maafisa ustawi wa jamii. Na kukana watoto si wake kule kule ustawi wa jamii.

Watu wakamwambia wa ustawi wa jamii kuwa jamaa kahonga pesa hutashida.
Yule dada anaondoka zake. Mama yake alifariki siku nyingi tuu.
Baba yake akamwambia kuwa utakaa hapa hapa home kwa sasa nagalia jinsi ya kuwalea watoto wako.

Yule dada alipata shida mpaka akawa yupo stable kipesa. Kwa sasa watoto wana umri wa miaka 6 anawasomesha shule mzuri tuu ya over 1 miilion per year. Anaishi Kigamboni.

Alimtembelea sister angu siku moja alimpelekea zawadi kibao.

Jamaa nasikia kuna kipindi alikuwa anamtafuta wayamalize, alikuwa anaomba msamaha kwa baby mama. Ila kagoma kabisa na alimblock.

Nafikili jamaa huyu itakuwa ngumu kwenda tena ustawi wa jamii, maana alikana kule kule watoto. Sasa naona itakuwa ngumu kwake.

Nafikiri anaumia sana moyoni jamaa.
Safi sana
 
I’m a single mama…kitu alichokwama mwenzetu ni kuruhusu mawasiliano ya yeye na mzazi mwenzie moja kwa moja.

kuna wakati hata sisi single moms tunazingua big time[emoji18][emoji18].kulingana na huu uzi..single mom ndie aliyeanza kumkaribisha shetani.unatolea wapi ujasiri wa kwenda ustawi wa jamii bila kwenda na mumeo?huo ni upumbavu mzito na hakuna mwanaume yeyote mwenye kupenda Amani ya moyo angevumilia[emoji174][emoji174]

Hivi unakuwaje na mume kabisa ambae amekukubali wewe na mtoto wako wote kuwalea halafu eti from nowhere ***** unakuja kuwasiliana na mzazi mwenzio just namna hiyo[emoji15]
You are very RIGHT. Kwanza mimi huko ustawi nisingeenda kabisa..Ningeblock ukoo mzima .In short sitaki mazoea.
 
Hapo sasa kama alikubali kumuoa akabeba na majukumu ya kulea mtoto. Nimfiche kipi. Kwa kweli kabisa,,binafsi ikitokea mwanaume anamkataa mtoto nalea napambana mwenyewe nije nipate mtu wa kunipa heshima na usingle maza wangu. Hakuna cha sheria ya mtoto,,,wala afisa Ustawi atayetoa hukumu kumchukua mtoto mikononi mwangu.

Binafsi kwenye majukumu yangu tunashirikiana na ustawi kwenye majukumu ya watoto kwa mashauri hayo ya malezi wanaume wanapewa ulezi wa watoto ni wanawake wenyewe ndo wanaamua kwa mapenzi yao. Na hata hao huwa wanashauriwa ni mara mia mtoto alelewe na mama kuliko kwenda kwenye mikono ya mama..

Tena kwa mwanaume ambaye alimtelekeza looooh.
Embu Imagine..
 
Mkuu ukizaa na mwanmake ukamuachia mtoto na unakaa mji mmoja hapa hapa anaolewa hapo hapo mji mmoja .
Utashidwa kujua kweli??

Mtoto kutumia jina la Baba yek ni haki ya mtoto.
Mbona kuna jamii ni Maternal wanatumia majina ya mama zao au mjomba.??

Mimi mtu asiyelea mtoto, Hakuna haja ya mwanangu kutumia jina lake..Mambo yasiwe mengi!!!!

Ni Roho mbaya tu ya badhi ya wanaume, wewe unatelekeza damu yako wakati una uwezo wa kumlea mtoto.Unamwachia mzigo wote mama yake tu?
 
SIngle mama ukitaka kuolewa uchague kukabidhi mtoto kwa baba yake, ama kukata mawasiliano kabisa na baba mtoto na ndugu zake, kiufupi asijue ulipo.

Ila mimi pangechimbika aisee...mtoto asingempata, hata kama huyo mume angeniacha lkn ningebaki na mtoto wangu katika hali yoyote ile.
Kama mimi..Mtoto hatoki kwangu hata alete madefender
 
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa na mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa muda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lakini baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume kwa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuona, kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda minne.

Jamaa hakuwa tayari kuwa nae si unajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpaka kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae dogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule nzuri ya 2 million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake. Na alirudi kipindi sister ana watoto wadogo mapacha aliyezaa na mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto ana haki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.

Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpaka kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.

Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikiri.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, muda wote. So anajikuta muda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.

Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuluhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suluhisho. Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe karudi tena single mother. Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoka shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA, KARIBUNI.
Sister wako mzembe na mjinga

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom