Anakuwa single kwasababu zake binafsi ila sio za kijamii.....
Okay kuachwa kufukuzwa au kukaa kwenye poisonous relationship hizo sio sababu...,
hakuna sehemu utaenda ukute jamii ya watu civilized na wanaojitambua halafu eti washabikie au waunge mkono mwanamke kuishi maisha yake mwenyewe pekee yake kama jiwe porini.
Nasikitika kusema hujui unalolisema..., Na ni nini maana ya Civilized ? Afrika kwa muda mrefu au kipindi cha Hunters and gathers kulikuwa na mgawanyiko wa kazi Mwanaume kwenda kuwinda na kutafuta na mama kubaki nyumbani kulea na kuangalia watoto...
Unakuta hata Jamii za Kimasai ilikuwa mwanaume akienda kutafuta malisho nyumba ikibaki tupu mwanaume yoyote akija pale anamiliki hiyo nyumba it was necessary sababu mwanamke alihitaji ulinzi wa Mwanaume bila hivyo Jamii ingemtenga na kumuona kama mtu wa ajabu na laana na ingepelekea hatari kwenye maisha yake..., Na mwanaume kwenda kutafuta malisho huende ingechukua hata miaka kabla ya kurudi na aliporudi angekuta mwingine ameshamiliki wala kulikuwa hakuna shida (hio ndio ilifanya Jamii yao iendelee na kuwa na safety kwa watoto, which is the most important issue)... Kuna makabila ilikuwa kaka mtu au mdogo mtu akifa kaka au mdogo wake anarithi mke....; Mama alikuwa ni mama wa nyumbani hana means / haruhusiwi kujishughulisha na kumiliki / kuleta mkate wa kila siku hivyo asingeweza ku-survive bila mwanaume
Mwanamke aliyefiwa na mume wake anaitwa Mjane kwa English ni Widow. Hapa mada inazungumzia Single mothers a.k.a wadangaji. Sasa sijui wewe unachanganya vipi, au haujui tofauti ya matumizi ya neno Single mother na Widow mzee? [emoji848]
Kwamba mjane akifiwa akiendelea kulea watoto peke yake sio single ? au Mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine akapata mwanaume mwingine na wakazaa au wasizae bado ni single mother Au hata hujui unachokiongelea ?
Na wadangaji ni watu gani..., Mwanamke aliyekimbiwa na mtu aliyemzalisha akabaki peke yake kuuza mihogo ili watoto wasife huyo ni mdangaji ? Kwanza binafsi nampa Heko mtu ambaye anaweza hata kuuza utu wake (sio kwa kupenda) bali kwa kukosa alternative ili watoto wake wasife njaa (huyo haitaji kusemwa bali jamii iliyomzunguka iliyomuweka kwenye hio situation ndio ya kulaumu) sio wote wanajiuza wanapenda na wala sio shughuli rahisi ni hatari na wengi wao wamejikuta kwenye hio situation kutokana na circumstances
Kuachwa kuna mawili ni aidha ame underperform kwenye uhusiano au alikubali kusettle na mwanaume ambaye siyo wa hadhi yake jambo ambalo ni very common kwa Single mothers, huwa wanachagua kupuuza red flags makusudi kabisa halafu
Nadhani wewe unadhani unajua haya mambo wakati kwa kweli haujui at least mimi kulinganisha na wewe am Wiser sababu I know that I know nothing hence kuendelea kujifunza kila siku... Mkuu kila situation ni tofauti and every case must be judged differently yaani unasema kabisa kila mtu ana magic fulani ya kujua mahusiano yatakuwaje kesho ? Hakuna perfect marriages kuna uvumilivu wa hali ya juu sababu kuna milima na mabonde na ukipendwa leo haimaanishi kesho utapendwa unaweza ukachokwa na kufanyiwa visa - It takes two to Tango na makosa mara nyingi hayawezi kuwa ya mmoja pekee au sio necessarily ya mwanamke yanaweza kuwa ya Mwanaume....; Na ikifika point of no return kuliko kuona watu wanapigana risasi au kuwekeana sumu ni bora kila mtu akate kona...
yakiwakuta wanaanza tupia lawama upande wa pili while in reality wao ndie wachaguzi. Trust me, mwanamke hazai na mwanaume ambaye hajamchagua yeye kwa hiyari yake awe baba mtoto, labda awekewe kilevi na kubakwa. Ila ukivua chupi mwenyewe jua huyo mwanaume ndie chaguo lake, so lolote litalomkuta na huyo mwanaume sio bahati mbaya wala ajali ni matokeo ya uchaguzi wake, so lawama ni kwake.
Sasa hapo unajipinga mwenyewe kwamba hachagui au kulazimishwa alafu labda kilevi au kubakwa ? kwahio akibakwa au akiwekewa kilevi au akidanganywa alafu akaachwa na akawa mlezi pekee wa watoto huyo ataitwa half single mother ?
Hakuna kitu kama kudanganywa now days, ndio maana unaona watoto wa kiume wamekuwa serious na maamuzi yao na kutokukubali kusettle na wanawake kwanza wasio bikra, pili wana watoto halafu hawajatulia, nani anataka kukaa na vitu vya ajabu ndani?
Speak for yourself Mkuu na ndio nyie ambao huwa tunasikia mmechoma watu visu au kuwapiga risasi sababu mnachodhani kwenye akili zenu does not exist... Huwezi kumiliki binadamu mwanzako..., hususan kama ana choces na options..., sanasana utajitafutia magonjwa na stress za bure Na wewe unachotaka kufanya ni kuondoa hizo choices na options alizonazo (jambo ambalo nakwambia its impossible kwa maisha ya sasa) Na sidhani kama ni better kurudi kwenye dark ages ambapo dada zetu, mama na bibi zetu walikuwa commodities za wanaume kutumia
ingekuwa kupigwa ni serious kama unavyoiweka then hata hapa ninapoishi basi wanawake wote ningeshasikia wanavyopigwa ila you just simply made up a situation. Na hii ndio shida tuliyonayo kwenye jamii ya sasa ku over exaggerate issues na kuzifanya kuwa extreme case.
Kupigwa kumepungua sana angalia historia..., Unajua kwanini sababu kama nilivyokwambia wanawake wana options wana sehemu ya kukimbilia zamani walikuwa hawana hio option na wangekutana na watu wenye fikra kama zako option yao ilikuwa ni kupigwa na kuwa-abused mpaka siku wanaingia kaburini au labda kujiua...
Domestic abuse victims kwa asilimia 90% ni wanaume ila hautajua sababu hakuna media outrage juu ya hilo simply kwasababu wanaume hatuongei, ila emotional abuse inafanywa sana na wanawake na matokeo yake mwanaume akichoshwa anageuka mbogo na kuretaliate na hapo ndipo media zinamulika na kamera zao na kurusha hizo habari inaonekana mwanaume ndie mkorofi na mwenye shida.
Mkuu haya sio mashindano wala sijasema mwanaume hawezi kuwa abused anaweza sana kuwa abused emotionally ila tofauti ni kwamba always amekuwa na option ya kufanya jambo au kumuacha huyo mwanamke au kumfukuza..., jambo ambalo mwanamke alikuwa hana hio option until recently..., sasa hivi hategemei kuletewa chakula mlangoni hategemei mwanaume ili aweze kupata chakula malazi na mavazi (zamani alitegemea yote hayo)..., kwahio hata zamani Bibi zetu wangepata hizo option haya yangetokea then and not now....
Na hakuna direct relation between kudanga na single mother...., Mama mara nyingi kitu cha maana kwake ni watoto wake na ndio maana wengine hawawezi na bora wabaki single kuliko tu kukidhi matakwa yao ya kumpenda fulani basi kuolewa nae bila kwanza kuhakikisha usalama na furaha ya watoto wao (an to me that is a positive and not negative)
Nakushauri uwe na fikra fluid na sio rigid na wala huwezi kugeneralize kila kitu kwa kutumia one explanation..., every case is different