Okay kuachwa kufukuzwa au kukaa kwenye poisonous relationship hizo sio sababu...,
Nasikitika kusema hujui unalolisema..., Na ni nini maana ya Civilized ? Afrika kwa muda mrefu au kipindi cha Hunters and gathers kulikuwa na mgawanyiko wa kazi Mwanaume kwenda kuwinda na kutafuta na mama kubaki nyumbani kulea na kuangalia watoto...
Unakuta hata Jamii za Kimasai ilikuwa mwanaume akienda kutafuta malisho nyumba ikibaki tupu mwanaume yoyote akija pale anamiliki hiyo nyumba it was necessary sababu mwanamke alihitaji ulinzi wa Mwanaume bila hivyo Jamii ingemtenga na kumuona kama mtu wa ajabu na laana na ingepelekea hatari kwenye maisha yake..., Na mwanaume kwenda kutafuta malisho huende ingechukua hata miaka kabla ya kurudi na aliporudi angekuta mwingine ameshamiliki wala kulikuwa hakuna shida (hio ndio ilifanya Jamii yao iendelee na kuwa na safety kwa watoto, which is the most important issue)... Kuna makabila ilikuwa kaka mtu au mdogo mtu akifa kaka au mdogo wake anarithi mke....; Mama alikuwa ni mama wa nyumbani hana means / haruhusiwi kujishughulisha na kumiliki / kuleta mkate wa kila siku hivyo asingeweza ku-survive bila mwanaume
Kwamba mjane akifiwa akiendelea kulea watoto peke yake sio single ? au Mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine akapata mwanaume mwingine na wakazaa au wasizae bado ni single mother Au hata hujui unachokiongelea ?
Na wadangaji ni watu gani..., Mwanamke aliyekimbiwa na mtu aliyemzalisha akabaki peke yake kuuza mihogo ili watoto wasife huyo ni mdangaji ? Kwanza binafsi nampa Heko mtu ambaye anaweza hata kuuza utu wake (sio kwa kupenda) bali kwa kukosa alternative ili watoto wake wasife njaa (huyo haitaji kusemwa bali jamii iliyomzunguka iliyomuweka kwenye hio situation ndio ya kulaumu) sio wote wanajiuza wanapenda na wala sio shughuli rahisi ni hatari na wengi wao wamejikuta kwenye hio situation kutokana na circumstances
Nadhani wewe unadhani unajua haya mambo wakati kwa kweli haujui at least mimi kulinganisha na wewe am Wiser sababu I know that I know nothing hence kuendelea kujifunza kila siku... Mkuu kila situation ni tofauti and every case must be judged differently yaani unasema kabisa kila mtu ana magic fulani ya kujua mahusiano yatakuwaje kesho ? Hakuna perfect marriages kuna uvumilivu wa hali ya juu sababu kuna milima na mabonde na ukipendwa leo haimaanishi kesho utapendwa unaweza ukachokwa na kufanyiwa visa - It takes two to Tango na makosa mara nyingi hayawezi kuwa ya mmoja pekee au sio necessarily ya mwanamke yanaweza kuwa ya Mwanaume....; Na ikifika point of no return kuliko kuona watu wanapigana risasi au kuwekeana sumu ni bora kila mtu akate kona...
Sasa hapo unajipinga mwenyewe kwamba hachagui au kulazimishwa alafu labda kilevi au kubakwa ? kwahio akibakwa au akiwekewa kilevi au akidanganywa alafu akaachwa na akawa mlezi pekee wa watoto huyo ataitwa half single mother ?
Speak for yourself Mkuu na ndio nyie ambao huwa tunasikia mmechoma watu visu au kuwapiga risasi sababu mnachodhani kwenye akili zenu does not exist... Huwezi kumiliki binadamu mwanzako..., hususan kama ana choces na options..., sanasana utajitafutia magonjwa na stress za bure Na wewe unachotaka kufanya ni kuondoa hizo choices na options alizonazo (jambo ambalo nakwambia its impossible kwa maisha ya sasa) Na sidhani kama ni better kurudi kwenye dark ages ambapo dada zetu, mama na bibi zetu walikuwa commodities za wanaume kutumia
Kupigwa kumepungua sana angalia historia..., Unajua kwanini sababu kama nilivyokwambia wanawake wana options wana sehemu ya kukimbilia zamani walikuwa hawana hio option na wangekutana na watu wenye fikra kama zako option yao ilikuwa ni kupigwa na kuwa-abused mpaka siku wanaingia kaburini au labda kujiua...
Mkuu haya sio mashindano wala sijasema mwanaume hawezi kuwa abused anaweza sana kuwa abused emotionally ila tofauti ni kwamba always amekuwa na option ya kufanya jambo au kumuacha huyo mwanamke au kumfukuza..., jambo ambalo mwanamke alikuwa hana hio option until recently..., sasa hivi hategemei kuletewa chakula mlangoni hategemei mwanaume ili aweze kupata chakula malazi na mavazi (zamani alitegemea yote hayo)..., kwahio hata zamani Bibi zetu wangepata hizo option haya yangetokea then and not now....
Na hakuna direct relation between kudanga na single mother...., Mama mara nyingi kitu cha maana kwake ni watoto wake na ndio maana wengine hawawezi na bora wabaki single kuliko tu kukidhi matakwa yao ya kumpenda fulani basi kuolewa nae bila kwanza kuhakikisha usalama na furaha ya watoto wao (an to me that is a positive and not negative)
Nakushauri uwe na fikra fluid na sio rigid na wala huwezi kugeneralize kila kitu kwa kutumia one explanation..., every case is different