Sipati ajira, sioni faida ya elimu yangu, naona bora kuuza vyeti

Sipati ajira, sioni faida ya elimu yangu, naona bora kuuza vyeti

Bado muda kidogo utaanza kutafuta mganga mzuri, kuwa makini usikate tamaa, giza linapokuwa totoro. Mwanga upo karibu kutokea
 
Tatizo tumeaminishwa na wazazi au mfumo kuwa usome, upate alama nzuri darasani kisha utapata ajira hiki kitu hakipo tena, kwenye masomo yetu elimu ya ujasiriamali au fedha kama mie ndio ningekuwa muunda sera ingekuwa ya lazima hii itasaidia sana jamii yetu
 
Kichwa cha uzi chahusika, Kwa wale wenye uhitaji wa vyeti mimi ninavyo.
Nitakuuzia vyeti vyote kuanzia sekondar mpaka chuo ili visikusumbue kwenye matumizi yako.

Sifa ya vyeti,
O-level kina masomo 10 hakina F
A-level matatu (comb CBA) hakina F zaidi ya Bam
Degree ya Sua na Post graduate diploma in Education Teaching, chuo St. John.

Bei ya vyeti vyote ni tsh 18,000,000
Tutawasiliana Pm mpaka tuonane nikukabidh mzigo nawe unipe hiyo pesa.
Hii ni baada ya kuona naenda off target na mahitaji ya serikali yangu kwa soko la ajira.
Kwa sasa napatikana Rufiji njoo tufanye biashara.
Nasikitika ulisoma upate A na usipate F
Maana unasema vyeti vyote havina F
Vyeti ulivyonavyo NI makaratasi unamuuzia Nani atoe hela yake akupe wewe?
Elimu uliyoipata iko kwenye kichwa chako sio kwenye hzo karatasi unazoziuza
Hakuna mjinga anaweza kununua makaratasi hate ukiuza kwa laki moja
Have dunia ya Sasa hv Kuna mjinga gani anaweza kununua vyeti?
Nahisi huo ufaulu haikuwa kwa uwezo wako
Mwisho kaa chini ufikirie Cha kufanya Anza hata na biashara yenye mtaji mdogo kabisa itakua taratibu acha kuwaza Mambo ya ajira au biashara zenye mitaji mikubwa
Hakuna maisha rahisi hapa duniani
Sgida ya watu wengine wanawaza alimaliza tu chuo anaajiriwa maisha yanakuwa rahisi
Maisha hayako hvyo
Pambana!!!!
 
Back
Top Bottom