Nashukuru madam Kwa kunishirikisha
Ukweli nawaona Sana,lakini naweza sema hofu Yao na machungu Yao huenda imetokana na uzoefu ambao ima wao wenyewe wamepitia au wameona Kwa wanaume wenzetu waliokutana na kadhia hiyo.
Nina mitazamo miwili juu ya hili Jambo.
Mosi, ni makosa kutoka Kwa wanawake wenyewe ambao wameshindwa kujua sehemu Yao katika jamii au familia,huenda Kwa kupata elimu au muingiliano na dunia kwakuwa imekuwa kijiji sasa hivi basi huenda wamejifunza au kuona jinsi tamaduni nyingine zinavyoishi hivyo kuwafanya nao waige Maisha ya wengine ambao kwao wao ustaarabu wa nafasi ya mwanaume na mwanamke katika jamii haujapewa uzito unaostahili
Pili,tatizo naliona pia Kwa Sisi wanaume wenyewe,nadhani haya mabadiliko ambayo tunayaona Kwa wanawake ambao kila kukicha yanaongezeka Kwa kujitegemea kiuchumi na kielimu yanatufanya tupate hofu juu ya utiifu wao kwetu kama waume zao,hivyo tunaishi nao Kwa kujihami Sana na kutoaminiana kunaongezeka.
Sasa nini kifanyike........
Nadhani wanawake pamoja na kujitegemea kiuchumi na kuwa na elimu kubwa,ifike kipindi mtambue kuwa pamoja na yote hayo bado wanaume watabakia kuwa wanaume Tu, unaporudi nyumbani Kwa mumeo hata huko ofisini wewe ni CEO Fulani basi Acha cheo ofisini kwako na nyumbani uwe mke mtiifu Kwa mumeo na mama WA watoto wako.
Na hata kama kuna mambo ambayo wewe na Mr wako hayapo Sawa basi ongea nae Kwa upole na heshima kubwa kama mke,hapo mtaenda Sawa kwani wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Hakuna mwanaume mkorofi kama atapewa heshima yake na kupewa hadhi yake,nadhani bahati mbaya Sana wanawake wengi wanajisahau juu ya hili.
Na wanaume pia tuache hofu na dhana mbaya juu ya wanawake kama wako submissive kwetu na wanatusikiliza,huenda siku moja moja wanaweza teleza lakini tusisahau kuwakumbusha kuwa wanaume watabakia kuwa wanaume,naamini tukiwakumbusha haya Kwa mapenzi na mahaba watatuelewa na kubadilika.
Kutoka kwangu
ETUGRUL BEY
Ni hayo Tu!