Dada aliolewa na miaka 21 alipomaliza form six si unajua zamani unakuta mtu anamaliza shule ya msingi anapambana na vibarua anakuja kuendelea na shule baadae.
So kipindi anaolewa wala hakuwa mtoto.
Unavyosema ndoa ni watu wawili wanaosaidiana kutimiza ndoto ndo unaona matusi yote haya kwenye hii thread yameletwa na huyo mpuuzi alieanzisha mada. Kuna sehemu anasema eti mwanamke ana uwezo gani wa kukusaidia, eti mwanamke hatakiwi kufanya chochote. Na ndo dada yangu alivyokua anapelekwa na mumewe, na tulikua tunatukanwa ukoo mzima hadi mama yangu anatukanwa kwamba sisi ni maskini hatuna kitu eti yeye shemeji anamfuga dada yetu hana pa kwenda anafanya kumsaidia tu. Leo uje useme mwanamke mpambanaji ni feminist pumbavu kabisa. ndo maana natamani sana kumjua mleta mada huyu
The unpaid Seller unaweza kuta ye ndo mwanaume nnaemuongelea hapa maana ana itikadi za kipumbavu sana. Kila nikikumbuka dada yangu alivyoteswa kwakuwa tu hakuwa na kipato wala shughuli yoyote alinyanyasika sana kidogo tumzike maaana aliwahi kupigwa hadi akaingia kwenye coma miezi kibao. Niliomba likizo shule ili nimhudumie mama na dada kwa pamoja. Pesa hakuna. Janaume limekaa huko eti liseme mwanamke hatakiwi kuwa na chochote atakua mjeuri eti atakua feminist. Wanaume wote wenye itikadi za design hii ni wapumbavu na wanyanyasaji wa wake zao shenzi kabisa. Nikikumbuka yale maumivu ya dada najikuta nawachukia sana wenye tabia za kitesi na itikadi za kijibwa. Mwanamke usikubali kukaa nyumbani eti mume anakuletea kila kitu wakibadilika hao watakutesa ufe.