Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Hello
Shalom!
Naongea na wakomavu ambao wanahitaji chakula kigumu na si uji tena.

Uhai wa Mkristo uko katika maombi, mkristo ambaye haombi huyo ni mkavu, aidha amekufa kiroho au anakaribia kufa kiroho.

Hivyo ni wajibu wa kila mkristo kuhakikisha mito ya uzima ndani yake haikauki. Na kuifanya mito kuwa rejuvenating ni kuwa mwanamaombi.

Ila jambo kuu ni kuwa mwanamaombi katika roho.

Ni heri mtu anayeomba dakika 5 katika roho kuliko mtu anayekesha kwa ombi lakini anaomba kibinadamu.

Mtu ambaye anaomba kibinadamu ni kama bubu tu, anatumia nguvu nyingi na muda mwingine mpaka sauti inaanza kubadilika.

Kila Ijumaa Walokole wengi tunafanya mikesha kuliombea taifa lakini umaskini ndani ya taifa hauishi, ujinga hauishi, na matatizo sugu katika jamii bado yanaendelea.

Nini sababu?

Sababu kuu ni kwamba maombi yanafanyika katika mwili.

Kuomba katika roho kwa mujibu wa Mtume Paul ni kuomba katika lugha ya MBINGUNI (lugha za malaika, lugha za Kimungu) , lugha ambazo wakuu wa anga kama waliomzuia Gabriel kumpa majibu Nabii Daniel hawazijui

View attachment 2948811
What good is that MUNGU anatupa lugha ambazo pepo wachafu hawazijui au tuseme hawazisikii lakini bado tunang'ang'ania kuomba kwa Kiswahili na Kiingereza.

Mtu anayeweza kuomba katika roho lisaa limoja non stop huyo ana uwezo wa kushinda jaribu lolote lililo mbele yake.

View attachment 2948813

Na kama ataweza kuomba masaa 2 katika roho non stop mtu huyo ataweza kuuvuta muujiza wowote mbele yake.

NOTE: Yesu alikufa msalabani ili watu wote hasa wanaomwamini waokolewe na wataishi maisha mazuri MBINGUNI na si hapa duniani.

Kwahiyo mahitaji ya duniani Mungu anakupa kwa kipimo chake. Ingawa ni haki ya kila muamini kupata mahitaji yake muhimu lakini ni vyema akilini mwako ulitambue hili kuwa ujio wa Yesu na kifo chake ni kwaajili ya maisha yajayo (Eternal life).

USINENE wa kukariri au kwa kuiga, wapo wanaonena kwa kukariri na kuiga, ni wengi, wengine hunena kwa roho chafu.

Natamani nielezee hapa kunena kwa lugha kukoje, kuhutubu (kutabiri) kukoje.

Maana wengine huchanganya hivi vitu 2.

Kinachotakiwa kifasiriwe ni kuhutubu (kutabiri) sio kila mtu anaponena panahitajika mtafsiri.
Amen Mtumishi
Barikiwa sana 🌹
 
Mungu akubariki sana, hiki ulichoongea ni cha kweli, na wale waliobarikiwa kufikia level hizi ndio watakuwa mashuhuda hapa. Tanzania, au niseme dunia imejaa watu wanaoabudu dini badala ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli. Tunachotakiwa kukifanya ni kwamba, tukiimba tunatakiwa kuimba kwa Roho, tukiomba tuombe kwa Roho, na tukihubiri pia tuhubiri kwa Roho, kama haujajazwa na Roho hautaomba kwa Roho na hayo yote utafanya kimwili na hayana matunda kwako na kwa wengine.

Mungu hapatikani mwilini, anapatikana rohoni, na hata ukiwa unaomba unatakiwa kumfuata rohoni. ukimfuata huku mwilini kwa nguvu za kimwili (paza sauti yako hadi uchoke), kwa elimu yako hata kama ni ya theolojia, kwa elimu ya dunia hata kama wewe ni profesa, kwa hekima na ujuzi wa kupangilia maneno, huwezi kumpata. anayetupeleka Rohoni ni Roho Mtakatifu, mwili hauwezi kukupeleka kule. hivyo kama hujajazwa Roho na kama huneni, manake huwa huendi rohoni. na kanisa lolote ukienda ukiona hawahubiri hiki kitu, kimbia, hapo sio mahali salama.

Roho Mtakatifu ndio huwa anatupeleka kuleee rohoni mahali pa siri pake yeye Mungu, wengine wanaita kuingia chumbani, kufunga mlango na kuomba. pamoja na kwamba physically inaweza kuhusisha kuingia chumba cha majengo hayahaya, zima simu na kaa mahali pa utulivu, ila maana ya jumla ni ku shut up fikra zote na mazingira ya kimwili na kuelekeza fikra zako kwa Mungu na kumruhusu Roho Mtakatifu mwenyewe atumie kinywa chako kukusaidia kuomba, yeye anaomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ambako wewe huwezi, na anakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.

Pamoja na kwamba tunaweza kuomba kwa Roho na kuomba kwa akili pia, lakini kuomba hata dakika mbili tu kwa Roho kuna faida kubwa kuliko kuomba siku nzima kwa akili. bora niombe hata dakika moja tu kwa Roho kuliko kushika kitabu kilichoandikwa maombi ya kukariri na kutamka kwa usiku mzima. tone moja tu la Roho Mtakatifu linaleta badiliko kuliko kitabu cha maombi ya vita nitakachosoma na kutamka kwa akili zangu usiku mzima.

nilishapita sana kwenye hayo maisha, nanunua kitabu cha maombi ya vita, natamka hadi sauti inakauka usiku mzima ati nampiga shetani. siku Mungu aliponineemia ujazo wa Roho Mtakatifu, hata hauhitaji nguvu za akili za kimwili, nikiomba kwa kusoma kitabu nachoka sana na najilazimisha, ila nikianza kunena kwa lugha natamani nisimalize, furaha ya Roho Mtakatifu, raha ya Roho, amani ya ajabu ambayo haielezeki kwa maneno ya kibinadamu na imani na uhakika wa hali ya juu vinajaa moyoni, na unaondoka ukiwa na uhakika wa wokovu na yote uliyokuwa unayaomba.

na maombi ya Roho Mtakatifu (kunena kwa Roho) ndio maombi ambayo yana uhakika 100% kwamba yamefika kwa Mungu na yatajibiwa/yamejibiwa, kwasababu ni Mungu mwenyewe anakusaidia kuomba. haya mengine tunaenda kwa akili zetu, kwa elimu zetu, uwezo wa kupengilia maneno, hayajibiwi, kwasababu lazima tu utaomba kwa kufuata tamaa za miili yetu.

Kuna watu hapa duniani wamesoma theolojia miaka hata 7, wana uwezo mkubwa kupangilia speech, au kupangilia maneno ya kuomba, wakisimama kwenye makanisa yao ya dini, wakapangilia maombi, hakika utasema yamefika kwa Mungu,kumbe hamna kitu.

wapo wengine ambao, hawajui kuongea mbele za watu, hawajasoma kama kina Petro tu waliokuwa wavuvi, ila wakiomba au kuongea kwa Roho, nira za watu zinavunjwa, watu wanawekwa huru na Nguvu za Mungu zinajidhiririsha. ndugu zangu mnaofuata dini badala ya njia ya wokovu, mnapoteza muda wenu tu, ninyi mnaoabudu maria na wafu, ninyi mnaozikana nguvu za Mungu mkisema kunena kwa lugha hakuna umuhimu ndio maana hata viongozi wenu wote hakuna aliyewahi kunena, manake mnafundishwa na akili za watu hamfundishwi na Roho Mtakatifu kwasababu hayupo ndani ya wale wanaowafundisha. walitakiwa wajae Roho ili yeye awe anaongea kupitia wao kama vyombo tu, sio wao kuleta ujuzi wao wa kielimu. Kimbieni huko, hakuna Mungu huko, Mtafuteni Mungu na Nguvu zake, tafuteni kujazwa Roho Mtakatifu, ndio mapenzi ya Mungu.
 
Hujanijibu Mkuu Kunena kwa LUGHA mlitoa wapi?

Hata katika Filamu ya YESU sijaona Akisema Shakara "babababbaa la bosika la matembweleza salambaba"

Mmeitoa wapi hiyo staili?
Naomba nikuwekee mistari. nimechelewa sana kuiona hii threat.

Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya. (kusema kwa lugha mpya ndio kunena), na ni ishara kwamba umemwamini Yesu, kama huneni, wewe bado.

siku ya pentecoste, Petro alihubiri baada ya Roho Mtakatifu kushuka, watu waliokuwa hawaamini wakauliza tufanyeje? soma MATENDO 2: 37 - 39:

37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie

MATENDO 19:1 INASEMA: Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

WARUMI 8:26 - 27 INASEMA, 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

YUDA 1:20 INASEMA; Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.

MATENDO 10:44 INASEMA: 44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu.

NAOMBA KWA UCHACHE NIKUACHIE HAYO, Kunena kwa lugha ni kwa faida yako na ni muhimu kama wewe unajiita Mkristo. shida ni kwamba huwezi kunena bila kujazwa, na huwezi kujazwa bila kuokoka. Okokeni.

KIPAWA cha Roho Mtakatifu ni ahadi yetu,
 
Nitaweka kwa video nikikamilisha somo la Roho Mtakatifu na karama zake .
Somo nishaliandaa kwa mtindo wa kitabu lakini nawaza nifanye video.
Lengo ni kuwafungua watu fikra si kupata pesa. Kwakweli sihitaji pesa kwa njia ya Injili
Mtumishi wa Mungu, nashauri pia, ukipata nafasi, weka pia kwa maandishi kwenye pdf, watu wadownload hapa wakasomee polepole, na waweke kwenye hazina zao za mafunzo, na siku nyingine wawafundishe na wengine. Ubarikiwe.
 
LUGHA ni sauti zenye mpangilio na maana....

Sasa hizi mnazoongea nyie ni lugha gani? Zina maana gani?
1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

sasa, kama akili zako hazina matunda, huo mpangilio unautoa wapi? unapangilia saa ngapi, au haujui huu mstari?
 
Lugha unayonena, mnenaji unaielewa??
Unaelewa unachoomba??
Ukimaliza kuomba unakumbuka ulichoomba??
 
Hapa ndio mnapodanganywa, wachungaji na mapadre wenu kwasababu wamemkosa Roho, huwa wanahalalisha kutokunena kuonekane ndio sahihi kwasababu hawana jinsi. hawawezi kunena kwasababu hawana Roho, hawajajazwa, watanenaje sasa, na kuokoka hawajaokoka.

1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

sasa, kama akili zako hazina matunda, huo mpangilio unautoa wapi? unapangilia saa ngapi, au haujui huu mstari? anayenena ni Roho huku akili yako ikiwa haihusiki, unahitaji uielewe ili iweje sasa? utakachokijua tu ni uhakikisho rohoni kwamba huyo ni Roho Mtakatifu, uhakikisho ambao hauna mashaka, ambao ni yule tu aliewahi kunena kwa Roho wa kweli anajua ninachoongea, kama haujawahi hautaelewa hadi ujazwe.
 
Hello
Shalom!
Naongea na wakomavu ambao wanahitaji chakula kigumu na si uji tena.

Uhai wa Mkristo uko katika maombi, mkristo ambaye haombi huyo ni mkavu, aidha amekufa kiroho au anakaribia kufa kiroho.

Hivyo ni wajibu wa kila mkristo kuhakikisha mito ya uzima ndani yake haikauki. Na kuifanya mito kuwa rejuvenating ni kuwa mwanamaombi.

Ila jambo kuu ni kuwa mwanamaombi katika roho.

Ni heri mtu anayeomba dakika 5 katika roho kuliko mtu anayekesha kwa ombi lakini anaomba kibinadamu.

Mtu ambaye anaomba kibinadamu ni kama bubu tu, anatumia nguvu nyingi na muda mwingine mpaka sauti inaanza kubadilika.

Kila Ijumaa Walokole wengi tunafanya mikesha kuliombea taifa lakini umaskini ndani ya taifa hauishi, ujinga hauishi, na matatizo sugu katika jamii bado yanaendelea.

Nini sababu?

Sababu kuu ni kwamba maombi yanafanyika katika mwili.

Kuomba katika roho kwa mujibu wa Mtume Paul ni kuomba katika lugha ya MBINGUNI (lugha za malaika, lugha za Kimungu) , lugha ambazo wakuu wa anga kama waliomzuia Gabriel kumpa majibu Nabii Daniel hawazijui

View attachment 2948811
What good is that MUNGU anatupa lugha ambazo pepo wachafu hawazijui au tuseme hawazisikii lakini bado tunang'ang'ania kuomba kwa Kiswahili na Kiingereza.

Mtu anayeweza kuomba katika roho lisaa limoja non stop huyo ana uwezo wa kushinda jaribu lolote lililo mbele yake.

View attachment 2948813

Na kama ataweza kuomba masaa 2 katika roho non stop mtu huyo ataweza kuuvuta muujiza wowote mbele yake.

NOTE: Yesu alikufa msalabani ili watu wote hasa wanaomwamini waokolewe na wataishi maisha mazuri MBINGUNI na si hapa duniani.

Kwahiyo mahitaji ya duniani Mungu anakupa kwa kipimo chake. Ingawa ni haki ya kila muamini kupata mahitaji yake muhimu lakini ni vyema akilini mwako ulitambue hili kuwa ujio wa Yesu na kifo chake ni kwaajili ya maisha yajayo (Eternal life).

USINENE wa kukariri au kwa kuiga, wapo wanaonena kwa kukariri na kuiga, ni wengi, wengine hunena kwa roho chafu.

Natamani nielezee hapa kunena kwa lugha kukoje, kuhutubu (kutabiri) kukoje.

Maana wengine huchanganya hivi vitu 2.

Kinachotakiwa kifasiriwe ni kuhutubu (kutabiri) sio kila mtu anaponena panahitajika mtafsiri.
Ubarikiwe sana mtu wa Mungu
 
Hapa ndio mnapodanganywa, wachungaji na mapadre wenu kwasababu wamemkosa Roho, huwa wanahalalisha kutokunena kuonekane ndio sahihi kwasababu hawana jinsi. hawawezi kunena kwasababu hawana Roho, hawajajazwa, watanenaje sasa, na kuokoka hawajaokoka.

1Korinto 14:14 inasema; Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

sasa, kama akili zako hazina matunda, huo mpangilio unautoa wapi? unapangilia saa ngapi, au haujui huu mstari? anayenena ni Roho huku akili yako ikiwa haihusiki, unahitaji uielewe ili iweje sasa? utakachokijua tu ni uhakikisho rohoni kwamba huyo ni Roho Mtakatifu, uhakikisho ambao hauna mashaka, ambao ni yule tu aliewahi kunena kwa Roho wa kweli anajua ninachoongea, kama haujawahi hautaelewa hadi ujazwe.
Nimekuuliza vizuri unaleta mipasho, mapadri na wachungaji wametoka wapi hapo kwenye maswali yangu??

Enewei, sasa roho anaomba badala yako au imekaaje hiyo??
Mi nnachotaka kujua ni malengo ya kunena kwa lugha!!

Mfano mi huwa nasali kila asubuhi kwa kutubu, kushukuru na mwisho naomba mahitaji yangu kiroho na kimwili, na kiukweli majibu nayaona dhahiri kabisa.

Sasa kunena kwa lugha unakua unatubu, unashukuru au ni unafanya nn hasa??
 
Wanahitaji ukweli ili wafunguliwe.
Bahati mbaya huo ukweli hawautaki.
Mchungaji mmoja wa kkkt alikuwa anapinga ubatizo wa maji mengi kwa hoja mfu kabisa.
Kwakuwa yeye hakubatizwa kwa maji mengi na kwenye shule yao miaka yote 3 somo la ubatizo wa maji mengi wanalipiga chenga
 
Nimekuuliza vizuri unaleta mipasho, mapadri na wachungaji wametoka wapi hapo kwenye maswali yangu??

Enewei, sasa roho anaomba badala yako au imekaaje hiyo??
Mi nnachotaka kujua ni malengo ya kunena kwa lugha!!

Mfano mi huwa nasali kila asubuhi kwa kutubu, kushukuru na mwisho naomba mahitaji yangu kiroho na kimwili, na kiukweli majibu nayaona dhahiri kabisa.

Sasa kunena kwa lugha unakua unatubu, unashukuru au ni unafanya nn hasa??
Oh nashukuru kwa kuuliza vizuri. though hapo haikuwa mipasho, nilikuwa nafikisha ujume kwa wahusika.

Yesu kabla ya kupaa, aliahidi kwamba atatuletea msaidizi, Roho Mtakatifu kwanza ili atutie kwenye kweli yote, na kwamba bila yeye hatuwezi kufanya neno lolote lile. Waliomwamini walisubiri Yerusalem hadi siku ya Pentecost Roho yule aliyeahidiwa aliposhuka, na watu wakanena kwa Lugha kama ishara ya kujazwa, kwasababu Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. pamoja na kwamba wengi huwa wanaamini kumwabudu Mungu katika "roho" ni kumwabudu kimoyomoyo lakini msingi ni kwamba Unaopomwabudu, au unapomwendea Roho Mtakatifu anatakiwa kuhusika kukusogeza pale, hii ni Roho tu yake yeye mwenyewe kama mojawapo ya kiungo chake tu kinachokushika na kukusogeza kwenye kiti cha enzi. sawa na wewe unavyoweza kumshika mtoto na kumsogeza miguuni pako haimaanishi mikono yako iliyomsogeza na wewe uliyemsogeza ni vitu viwili, ni mwili ule ule. Mungu alitambua kwamba bila yeye kutusaidia kumwomba hatuwezi kuomba sawasawa na mapenzi yake kwasababu tumejaa tamaa za mwili/kidunia na hatujui yaliyo mbele yetu au yaliyotuzunguka. pia, tu wadhaifu, tunahitaji kusaidiwa kuomba.

sawa na upo nyumbani, mtoto anakuja kwako anakwambia baba nipe pesa. utamshika na kumsaidia kwamba, "tamke hivi, sema baba naomba pesa", ni kwamba Roho anatusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba ipasavyo.

WARUMI 8:26 - 27 INASEMA, 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

sasa kinachotokea, mtu akiokoka, anatakiwa kujazwa Roho Mtakatifu ili amsaidie katika maombi, na kumtia kwenye kweli yote ya maisha ya wokovu, ahadi hii ni kwa ajili ya wale watakaookoka tu (watakaomwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao), wale wanaoabudu dini na mapokeo yake hakika hii hawataipata. kama vile tu wayahudi waliokuwa wamekusanyika pale Yerusalem hawakujazwa, ila wale tu waliokuwa gorofani waliokuwa wamemwamini Yesu ndio walijazwa. Ukishajazwa Roho, utanena kwa lugha, ni muhimu na ni lazima. unaponena roho yako inakuwa inaomba kwa kusaidiwa na Roho wa Mungu, usiponena manake husaidiwi na Roho wa Mungu.

MATENDO 2: 37 - 39: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie

MATENDO 19:1 INASEMA: Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

mistari hapo juu utaona, kinachotakiwa ni kuokoka (kuamini na kutubu), na baada ya hapo unajazwa kwasababu hiyo ni ahadi Yesu aliahidi kwa wote watakaompokea. Kuomba tu kila siku bila kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu ni kujilisha upepo, hakuna matunda. unapoteza muda wako tu. Okoka, omba Mungu akujaze Roho Mtakatifu, yeye atakuongoza katika kila kitu iwe maombi, iwe kuhubiri, iwe maisha ya kawaida n.k.
 
Asante Mtumishi kwa andiko zuri. Lakini naomba nitofautiane na wewe kidogo kwa namna nzuri ya kuelimishana kuhusu neno. Ni kweli kabisa Maombi ndio muhimili na uti wa Mgongo wa Mwamini. Lakini sio sahihi kwamba kila Mwamini lazima anene kwa Lugha ndipo ambapo apate matokeo tarajiwa. Ingawa kunena kwa Lugha ni muhimu zaidi.

Kumbuka karama za Roho Mtakatifu ni nyingi mnoo na mojawapo ya hiyo Karama ni kunena kwa Lugha. Kuna karama zingine kama utabiri, uponyaji, n.k n.k na zote zatoka kwa roho mtakatifu. Kwa hivyo pia tujue kila Mtu na karama yake na sio kua sote ni muhimu tufanane Karama. Kuna watu ni wananeji wa Lugha ila hana karama ya uponyaji. Na mwingine ni Mtabiri ila hana karama ya unenaji. Kwa hivyo kila Mtu na Karama yake.

1Wakorintho 12-14.

Ingawa nakubaliana kabisa na wewe Mtumishi ya kwamba kunena kwa Lugha ni kama kuweka petrol kwenye Moto. Tubarikiwe
 
Nimekuuliza vizuri unaleta mipasho, mapadri na wachungaji wametoka wapi hapo kwenye maswali yangu??

Enewei, sasa roho anaomba badala yako au imekaaje hiyo??
Mi nnachotaka kujua ni malengo ya kunena kwa lugha!!

Mfano mi huwa nasali kila asubuhi kwa kutubu, kushukuru na mwisho naomba mahitaji yangu kiroho na kimwili, na kiukweli majibu nayaona dhahiri kabisa.

Sasa kunena kwa lugha unakua unatubu, unashukuru au ni unafanya nn hasa??
Anaposema akili Haina matunda ,maana ni kuwa,

Aombaye Kwa Roho mtakatifu, ni Roho anasema na Roho bila akili kuhusishwa.

Maana yake ni kuwa maneno na lugha utakayoongea katika Roho, utakielewa katika Roho,

Naamini Huwa unatoa ndoto, unaweza ona watu katika Roho na ukajua wanafanya nini na ukajua Nia Yao bila kuwahoji,

Ndipo sasa ujue, Roho ya mtu Haina limit, haifichwi chochote.

Anenaye Kwa lugha ni atumia lugha ya Mbinguni ambayo mapepo hawajui, ni Mungu anena kupitia kinywa chako akili hajielewi, ila Roho yajua yote katika Roho.
 
Asante Mtumishi kwa andiko zuri. Lakini naomba nitofautiane na wewe kidogo kwa namna nzuri ya kuelimishana kuhusu neno. Ni kweli kabisa Maombi ndio muhimili na uti wa Mgongo wa Mwamini. Lakini sio sahihi kwamba kila Mwamini lazima anene kwa Lugha ndipo ambapo apate matokeo tarajiwa. Ingawa kunena kwa Lugha ni muhimu zaidi.

Kumbuka karama za Roho Mtakatifu ni nyingi mnoo na mojawapo ya hiyo Karama ni kunena kwa Lugha. Kuna karama zingine kama utabiri, uponyaji, n.k n.k na zote zatoka kwa roho mtakatifu. Kwa hivyo pia tujue kila Mtu na karama yake na sio kua sote ni muhimu tufanane Karama. Kuna watu ni wananeji wa Lugha ila hana karama ya uponyaji. Na mwingine ni Mtabiri ila hana karama ya unenaji. Kwa hivyo kila Mtu na Karama yake.

1Wakorintho 12-14.

Ingawa nakubaliana kabisa na wewe Mtumishi ya kwamba kunena kwa Lugha ni kama kuweka petrol kwenye Moto. Tubarikiwe
Huu mstari huwa unauchukuliaje ndugu? Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya
 
Mkuu huo mstari unamaanisha unachokisema, lakini ili kuendelea kuelewa zaidi anachokisema alumn soma na mstari wa 18, utaona ishara nyingine pia kama za uponyaji, kushika nyoka n.k, zote ni karama na kila mtu anapewa kwa kadiri ya kipawa cha roho mtakatifu sawa na 1Kor 14

Mwisho kabisa Paulo anatukumbusha kuwa
1 Corinthians 14:15
[15]What is it then? I will pray with the spirit, and I will pray with the understanding also: I will sing with the spirit, and I will sing with the understanding also.
Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
 
kila mstari unatakiwa kuelewa ulitamkwa katika mazingira gani. paulo aliamua kuwaambia hivyo kwasababu watu walikuwa wakienda kanisani wananena tu kwa lugha, hivyo mgeni akija ambaye hajajazwa roho na asiyeweza kunena anakuwa haelewi kinachoendelea. na alikuwa anawaambia waongofu wapya. tofautisha na wewe umeenda chumbani kwako umefunga mlango, unasali, halafu useme kunena kwa Lugha ni karama ambayo unaweza usiwe nayo? wakati Neno la Mungu linasema sisi tu wadhaifu hatuwezi kuomba ipasavyo na Roho huwa anatusaidia udhaifu wetu kwani pale anapolia aba huwa anaugua vile tusivyoweza kufikia. kama ni karama ambayo sio lazima uwe nayo, niakuwaje paulo alipowakuta waliohubiriwa na Apolo wakaokoka, aliwauliza kama walijazwa Roho au la, na akaweka mikono ju yao wakaanza kunena kama ishara ya kujazwa.

shida ni kwamba kama haujawahi kujazwa, hakika yake utapinga kunena kwa lugha kwa nguvu zote kwasababu haujawahi kuipata hiyo experience, ila kama ulishawahi kujaza, utajua tunachosema. na kujazwa huku sio kujazwa tu mapepo na kuongea, ni kujazwa Roho mwenyewe kabisa, kwasababu shetani naye ana roho huwa anaweka mapandikizi kwenye madini huko watu wawe wananena wakifikiri ni Roho kumbe sio, matunda ya Roho yanakuwa hakuna na wao wenyewe hawana uhakika kama wana Mungu au la. Mungu akusaidie uelewe hili.
 
Back
Top Bottom