Oh nashukuru kwa kuuliza vizuri. though hapo haikuwa mipasho, nilikuwa nafikisha ujume kwa wahusika.
Yesu kabla ya kupaa, aliahidi kwamba atatuletea msaidizi, Roho Mtakatifu kwanza ili atutie kwenye kweli yote, na kwamba bila yeye hatuwezi kufanya neno lolote lile. Waliomwamini walisubiri Yerusalem hadi siku ya Pentecost Roho yule aliyeahidiwa aliposhuka, na watu wakanena kwa Lugha kama ishara ya kujazwa, kwasababu Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. pamoja na kwamba wengi huwa wanaamini kumwabudu Mungu katika "roho" ni kumwabudu kimoyomoyo lakini msingi ni kwamba Unaopomwabudu, au unapomwendea Roho Mtakatifu anatakiwa kuhusika kukusogeza pale, hii ni Roho tu yake yeye mwenyewe kama mojawapo ya kiungo chake tu kinachokushika na kukusogeza kwenye kiti cha enzi. sawa na wewe unavyoweza kumshika mtoto na kumsogeza miguuni pako haimaanishi mikono yako iliyomsogeza na wewe uliyemsogeza ni vitu viwili, ni mwili ule ule. Mungu alitambua kwamba bila yeye kutusaidia kumwomba hatuwezi kuomba sawasawa na mapenzi yake kwasababu tumejaa tamaa za mwili/kidunia na hatujui yaliyo mbele yetu au yaliyotuzunguka. pia, tu wadhaifu, tunahitaji kusaidiwa kuomba.
sawa na upo nyumbani, mtoto anakuja kwako anakwambia baba nipe pesa. utamshika na kumsaidia kwamba, "tamke hivi, sema baba naomba pesa", ni kwamba Roho anatusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba ipasavyo.
WARUMI 8:26 - 27 INASEMA, 26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
sasa kinachotokea, mtu akiokoka, anatakiwa kujazwa Roho Mtakatifu ili amsaidie katika maombi, na kumtia kwenye kweli yote ya maisha ya wokovu, ahadi hii ni kwa ajili ya wale watakaookoka tu (watakaomwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao), wale wanaoabudu dini na mapokeo yake hakika hii hawataipata. kama vile tu wayahudi waliokuwa wamekusanyika pale Yerusalem hawakujazwa, ila wale tu waliokuwa gorofani waliokuwa wamemwamini Yesu ndio walijazwa. Ukishajazwa Roho, utanena kwa lugha, ni muhimu na ni lazima. unaponena roho yako inakuwa inaomba kwa kusaidiwa na Roho wa Mungu, usiponena manake husaidiwi na Roho wa Mungu.
MATENDO 2: 37 - 39: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie
MATENDO 19:1 INASEMA: Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
mistari hapo juu utaona, kinachotakiwa ni kuokoka (kuamini na kutubu), na baada ya hapo unajazwa kwasababu hiyo ni ahadi Yesu aliahidi kwa wote watakaompokea. Kuomba tu kila siku bila kuwa na uhusiano na Roho Mtakatifu ni kujilisha upepo, hakuna matunda. unapoteza muda wako tu. Okoka, omba Mungu akujaze Roho Mtakatifu, yeye atakuongoza katika kila kitu iwe maombi, iwe kuhubiri, iwe maisha ya kawaida n.k.