Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Ndugu sitamgazi biashara, kama jambo hauko interest pita kimyakimya.
Unaweza kujiona una hekima kumbe uangamivu uko mlangoni kwako.
Sasa umekuja kifundisha nini kama unaanza kuwa mkali.... Nieleweshe Mtumishi zile Lugha zinatokeaga wapi? Na zina maana gan
 
Msingi wetu hauko katika filamu ya Yesu. Ile ni ya waigizaji tu waliigiza kama njia ya kutafuta pesa.
Soma Maandiko hayo ndipo tulikotoa kunena kwa lugha.
Ni maagizo ya Yesu mwenyewe.
Maagizo ya YESU?
Naomba Andiko mtumishi nijifunze hilo.... Yesu kawaambia wanafunzi wake wanene kwa Lugja
 
Nitoe siri iliyo kuu kuliko zote, mara muombapo msiropokeropoke,
Siri ya pili, kuomba katika lugha sahihi, binafsi natumia lugha halisi, ya zama hizo, lugha yake yeye, lugha aliyoiongea yeye, huu ni mfano wa Sala ya BABA YETU,
""ABBA NAWASHABAH SHAMAYIIM QADASH HAYAH SHAM KA AHAYAH MALAK NAWASHABAH SHAMAYIIM...... ""
Aramaic the language of heavenly!
 
Hello
Shalom!
Naongea na wakomavu ambao wanahitaji chakula kigumu na si uji tena.

Uhai wa Mkristo uko katika maombi, mkristo ambaye haombi huyo ni mkavu, aidha amekufa kiroho au anakaribia kufa kiroho.

Hivyo ni wajibu wa kila mkristo kuhakikisha mito ya uzima ndani yake haikauki. Na kuifanya mito kuwa rejuvenating ni kuwa mwanamaombi.

Ila jambo kuu ni kuwa mwanamaombi katika roho.

Ni heri mtu anayeomba dakika 5 katika roho kuliko mtu anayekesha kwa ombi lakini anaomba kibinadamu.

Mtu ambaye anaomba kibinadamu ni kama bubu tu, anatumia nguvu nyingi na muda mwingine mpaka sauti inaanza kubadilika.

Kila Ijumaa Walokole wengi tunafanya mikesha kuliombea taifa lakini umaskini ndani ya taifa hauishi, ujinga hauishi, na matatizo sugu katika jamii bado yanaendelea.

Nini sababu?

Sababu kuu ni kwamba maombi yanafanyika katika mwili.

Kuomba katika roho kwa mujibu wa Mtume Paul ni kuomba katika lugha ya MBINGUNI (lugha za malaika, lugha za Kimungu) , lugha ambazo wakuu wa anga kama waliomzuia Gabriel kumpa majibu Nabii Daniel hawazijui

View attachment 2948811
What good is that MUNGU anatupa lugha ambazo pepo wachafu hawazijui au tuseme hawazisikii lakini bado tunang'ang'ania kuomba kwa Kiswahili na Kiingereza.

Mtu anayeweza kuomba katika roho lisaa limoja non stop huyo ana uwezo wa kushinda jaribu lolote lililo mbele yake.

View attachment 2948813

Na kama ataweza kuomba masaa 2 katika roho non stop mtu huyo ataweza kuuvuta muujiza wowote mbele yake.

NOTE: Yesu alikufa msalabani ili watu wote hasa wanaomwamini waokolewe na wataishi maisha mazuri MBINGUNI na si hapa duniani.

Kwahiyo mahitaji ya duniani Mungu anakupa kwa kipimo chake. Ingawa ni haki ya kila muamini kupata mahitaji yake muhimu lakini ni vyema akilini mwako ulitambue hili kuwa ujio wa Yesu na kifo chake ni kwaajili ya maisha yajayo (Eternal life).

USINENE wa kukariri au kwa kuiga, wapo wanaonena kwa kukariri na kuiga, ni wengi, wengine hunena kwa roho chafu.

Natamani nielezee hapa kunena kwa lugha kukoje, kuhutubu (kutabiri) kukoje.

Maana wengine huchanganya hivi vitu 2.

Kinachotakiwa kifasiriwe ni kuhutubu (kutabiri) sio kila mtu anaponena panahitajika mtafsiri.
mtumishi
-Kama ataweza kuomba masaa 2 katika roho non stop mtu huyo ataweza kuuvuta muujiza wowote mbele yake?

Mawazo yangu chariti
kuomba katika roho kwa masaa mawili mfululizo hakuna mahusiano na matokea
kinacholeta matokeo
maombi+hazina yako+imani+fuata hatua zote za maombi ikiwepo na toba=na muujiza lakini sio muujiza wowote itategemea sana hazina yako mbinguni

mtumishi
-Uhai wa Mkristo uko katika maombi, mkristo ambaye haombi huyo ni mkavu, aidha amekufa kiroho au anakaribia kufa kiroho?

Mawazo yangu chariti
tunafahamu maombi ni upanga wa roho yaani silaha lakini imani ndio ngao au kinga uhai wa mkristo unashikiliwa na maombi? mbona yesu aliomba lakini walimsulibisha uhai wa mkristo ni imani buana mtumishi yesu imani ndio ilikua uhai wake alikua anaimani atatoboa hata nini kimkute

mtumishi
-Kuomba katika roho kwa mujibu wa Mtume Paul ni kuomba katika lugha ya MBINGUNI (lugha za malaika, lugha za Kimungu) , lugha ambazo wakuu wa anga kama waliomzuia Gabriel kumpa majibu Nabii Daniel hawazijui

Mawazo yangu chariti
mtumishi hujamwelewa vizuri mtume paulo
kuomba katika roho lengo ni kumpiga chenga shetani kwa namna yoyote sio kumficha lugha tu, hata kuomba mbele yake mara nyingi ni kosa imeandikwa sehemu nyingi kwenye biblia kwanini yesu alikua anajitenga peke yake kwenda kuomba, ukienda mbali linakuja swala la kufunga ile unajitenga na watu kweli kweli, hufungi kijanja janja kama kanisa la leo na dini nyingine wafanyavyo ili kuwafurahisha walimwengu

nadhani sijakukwaza mtumishi.
 
Yes alikuwaga na ROHO MAKATIFU Ila hakuwahi kuomba kwa KUNENA nyie mmeitoa wapi bhandugu?

Au ndio mashetani ya kigalatia yanapandishwa hivyo

Nauliza tu
Siku ya pentekoste mitume alinena kwa lugha gan? Walizitoa wapi hizo lugha?
 
Dini ya kweli ni upendo. Na kushika amri zake Mwenyezi Mungu mpende Mungu wako kwa moyo wako na akili zako zote.
Mpende jirani yako kama unavyo jipenda.
 
Mungu akubariki sana, hiki ulichoongea ni cha kweli, na wale waliobarikiwa kufikia level hizi ndio watakuwa mashuhuda hapa. Tanzania, au niseme dunia imejaa watu wanaoabudu dini badala ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli. Tunachotakiwa kukifanya ni kwamba, tukiimba tunatakiwa kuimba kwa Roho, tukiomba tuombe kwa Roho, na tukihubiri pia tuhubiri kwa Roho, kama haujajazwa na Roho hautaomba kwa Roho na hayo yote utafanya kimwili na hayana matunda kwako na kwa wengine.

Mungu hapatikani mwilini, anapatikana rohoni, na hata ukiwa unaomba unatakiwa kumfuata rohoni. ukimfuata huku mwilini kwa nguvu za kimwili (paza sauti yako hadi uchoke), kwa elimu yako hata kama ni ya theolojia, kwa elimu ya dunia hata kama wewe ni profesa, kwa hekima na ujuzi wa kupangilia maneno, huwezi kumpata. anayetupeleka Rohoni ni Roho Mtakatifu, mwili hauwezi kukupeleka kule. hivyo kama hujajazwa Roho na kama huneni, manake huwa huendi rohoni. na kanisa lolote ukienda ukiona hawahubiri hiki kitu, kimbia, hapo sio mahali salama.

Roho Mtakatifu ndio huwa anatupeleka kuleee rohoni mahali pa siri pake yeye Mungu, wengine wanaita kuingia chumbani, kufunga mlango na kuomba. pamoja na kwamba physically inaweza kuhusisha kuingia chumba cha majengo hayahaya, zima simu na kaa mahali pa utulivu, ila maana ya jumla ni ku shut up fikra zote na mazingira ya kimwili na kuelekeza fikra zako kwa Mungu na kumruhusu Roho Mtakatifu mwenyewe atumie kinywa chako kukusaidia kuomba, yeye anaomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa ambako wewe huwezi, na anakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.

Pamoja na kwamba tunaweza kuomba kwa Roho na kuomba kwa akili pia, lakini kuomba hata dakika mbili tu kwa Roho kuna faida kubwa kuliko kuomba siku nzima kwa akili. bora niombe hata dakika moja tu kwa Roho kuliko kushika kitabu kilichoandikwa maombi ya kukariri na kutamka kwa usiku mzima. tone moja tu la Roho Mtakatifu linaleta badiliko kuliko kitabu cha maombi ya vita nitakachosoma na kutamka kwa akili zangu usiku mzima.

nilishapita sana kwenye hayo maisha, nanunua kitabu cha maombi ya vita, natamka hadi sauti inakauka usiku mzima ati nampiga shetani. siku Mungu aliponineemia ujazo wa Roho Mtakatifu, hata hauhitaji nguvu za akili za kimwili, nikiomba kwa kusoma kitabu nachoka sana na najilazimisha, ila nikianza kunena kwa lugha natamani nisimalize, furaha ya Roho Mtakatifu, raha ya Roho, amani ya ajabu ambayo haielezeki kwa maneno ya kibinadamu na imani na uhakika wa hali ya juu vinajaa moyoni, na unaondoka ukiwa na uhakika wa wokovu na yote uliyokuwa unayaomba.

na maombi ya Roho Mtakatifu (kunena kwa Roho) ndio maombi ambayo yana uhakika 100% kwamba yamefika kwa Mungu na yatajibiwa/yamejibiwa, kwasababu ni Mungu mwenyewe anakusaidia kuomba. haya mengine tunaenda kwa akili zetu, kwa elimu zetu, uwezo wa kupengilia maneno, hayajibiwi, kwasababu lazima tu utaomba kwa kufuata tamaa za miili yetu.

Kuna watu hapa duniani wamesoma theolojia miaka hata 7, wana uwezo mkubwa kupangilia speech, au kupangilia maneno ya kuomba, wakisimama kwenye makanisa yao ya dini, wakapangilia maombi, hakika utasema yamefika kwa Mungu,kumbe hamna kitu.

wapo wengine ambao, hawajui kuongea mbele za watu, hawajasoma kama kina Petro tu waliokuwa wavuvi, ila wakiomba au kuongea kwa Roho, nira za watu zinavunjwa, watu wanawekwa huru na Nguvu za Mungu zinajidhiririsha. ndugu zangu mnaofuata dini badala ya njia ya wokovu, mnapoteza muda wenu tu, ninyi mnaoabudu maria na wafu, ninyi mnaozikana nguvu za Mungu mkisema kunena kwa lugha hakuna umuhimu ndio maana hata viongozi wenu wote hakuna aliyewahi kunena, manake mnafundishwa na akili za watu hamfundishwi na Roho Mtakatifu kwasababu hayupo ndani ya wale wanaowafundisha. walitakiwa wajae Roho ili yeye awe anaongea kupitia wao kama vyombo tu, sio wao kuleta ujuzi wao wa kielimu. Kimbieni huko, hakuna Mungu huko, Mtafuteni Mungu na Nguvu zake, tafuteni kujazwa Roho Mtakatifu, ndio mapenzi ya Mungu.
Barikiwa sana
 
Dini ya kweli ni upendo. Na kushika amri zake Mwenyezi Mungu mpende Mungu wako kwa moyo wako na akili zako zote.
Mpende jirani yako kama unavyo jipenda.
Na mtu wa tatu tuliyeagizwa tuwapende ni adui zetu
 
Msingi wetu hauko katika filamu ya Yesu. Ile ni ya waigizaji tu waliigiza kama njia ya kutafuta pesa.
Soma Maandiko hayo ndipo tulikotoa kunena kwa lugha.
Ni maagizo ya Yesu mwenyewe.
Waigizaji wa filamu ya Yesu walifanikiwa vitu viwili Vikuu.KUPOTOSHA kwamba Yesu alifanana na yule wa igizo pia WALIPIGA hela nyingi sana kutokana na mauzo ya filamu.
 
Huu mstari huwa unauchukuliaje ndugu? Marko 16:17 imeandikwa, Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa Jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya
Basi Mkuu tusije leta pengine ubishani kwenye neno la Mungu. Sote ni wa Mungu. Asante kwa neno
 
Basi Mkuu tusije leta pengine ubishani kwenye neno la Mungu. Sote ni wa Mungu. Asante kwa neno
sote sio wa Mungu, kuna uwezekano mkubwa wewe sio wa Mungu ndio maana huutaki huu mstari. hutaki kujazwa Roho Mtakatifu, unaamini ni kipawa wanapewa wachache tu wakati mstari huo Yesu anasema ni ahadi kwa kila atakayemwamini, wote watapewa. hata wale wa siku ya pentecost walijazwa WOTE, Roho hakumwagwa kwa wachache tu kwamba ni karama NO, wote walijazwa Roho Mtakatifu na wote walisema kwa lugha mpya. nakushauri tafuta hiki kipawa. Petro alipoulizwa tufanyeje aliwaambia tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina lake Yesu mpate uondoleo la dhambi nanyi mtapata kipawa cha Roho Mtakatifu.meaning, unatakiwa kuokoka, hapo ulipo hujaokoka ndio maana huyajui haya, uondolewe dhambi zako nawe utapata hiki kipawa, ni ahadi yako, ni haki yako ukija kuokoka. USIPOKUWA NA ROHO MTAKATIFU WEWE SIO WA MUNGU.

WARUMI 8: 12 INASEMA, Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

kwahiyo wengi wanaabudu dini na mapokeo ya dini, wanakataa kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema bila huyo hamwezi kufanya neno lolote. angelikuwa anamaanisha ni kitu ambacho mmoja anaweza kupokea na mwingine hawezi, asingeongea akimmaanisha mmoja mmoja namna hii. kwanza alisema atakayemwamini atampokea ni ahadi yake, pili alisema bila huyo ninyi mnayemwamini hamuwezi kufanya neno lolote. na hapo warumi inaonyesha wazi, usipokuwa naye, manake kama hujajazwa, wewe sio wake, na kunena ni ishara ya kujazwa.
 
Hiki unachoeleza na mafungu uliyotumia haviendani kabisa. Mafungu yanasema uombe kwa roho na ufahamu(akili)[understanding] wewe unaongea kuhusu eti mashetani hayajui lugha.

Jambo lingine ambalo hujui techniques hizo ambayo Christian science inafundisha ni Visualization kitu ambacho si kweli bali kuongizwa na spirit guide usiyemjua ambaye hutamka maneno ambayo hata wee unayeomba hujui.
Mwisho ni uelewa kuwa Maombi hayamtawali Mungu bali Yeye hujibu kwa kanuni moja kuu nayo ANAKUPENDA na KUKUJALI hivyo maombi yako yatajibiwa kulingana na hayo.
 
Hiki unachoeleza na mafungu uliyotumia haviendani kabisa. Mafungu yanasema uombe kwa roho na ufahamu(akili)[understanding] wewe unaongea kuhusu eti mashetani hayajui lugha.

Jambo lingine ambalo hujui techniques hizo ambayo Christian science inafundisha ni Visualization kitu ambacho si kweli bali kuongizwa na spirit guide usiyemjua ambaye hutamka maneno ambayo hata wee unayeomba hujui.
Mwisho ni uelewa kuwa Maombi hayamtawali Mungu bali Yeye hujibu kwa kanuni moja kuu nayo ANAKUPENDA na KUKUJALI hivyo maombi yako yatajibiwa kulingana na hayo.
unaelewa nini maana ya "kuomba kwa roho" na unaelewa nini maana ya "kuomba kwa akili". labda tuanzie hapo.
 
Nenda mstari wa 8

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Matendo ya Mitume 2:8

Lengo la kunena kwa lugha nyingine ni kupeleka ujumbe kwa watu wasio wa lugha yako ambao wanatakiwa waupate
KWa akili zako timamu unadhani ile filamu ni uhalisia wa Yesu?
Fuata biblia ilisema nini na sio filam
 
Nenda mstari wa 8

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?
Matendo ya Mitume 2:8

Lengo la kunena kwa lugha nyingine ni kupeleka ujumbe kwa watu wasio wa lugha yako ambao wanatakiwa waupate
hiki mlichokaririshwa baada ya kuona mmeshindwa kumpata Roho, wapi wameandika kwenye Biblia? Roho Mtakatifu hata leo hii hunena kwako kwa lugha ile yeye atakayoiamua kutumia, iwe ya mbinguni au ya duniani, iwe ya malaika au ya kidunia.

pia, ukisoma Matendo 19:3, Paulo alifika akaona waongofu walihubiriwa na apolo, akawauliza walibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema wa Yohana, akawauliza kama walijazwa Roho, wakasema hawajawahi hata kumsikia, akawabatiza kwa Ubatizo wa Yesu, na akaweka mikono juu yao, wakajazwa Roho wakaanza kunena kwa lugha. hapo walikuwa wanamtafsiria nani kwa akili yako?

pia, huwa mnahalalisha kutokunena, kwasababu paulo alisema awepo mtafsiri. hamjui mazingira yepi aliongelea hilo. ni kwamba, palikuwepo waongofu wapya ambao walifurahia mno kipawa hiki, wakawa wakikutana ibadani wananena tu hawahubiri Neno, ndio paulo akawa anawafundisha kwamba msinene muda wote, awepo mtafsiri pia kwa wengine waliowatembelea hapo. hakumaanisha kwamba msinene.

siri ipo hapa, kwamba, tunaposema mnene kwa lugha, hatumaanishi muda wooote muwe mnanena tu msiombe hata kwa maneno ya akili,ndio maana Paulo alisema nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili pia, akimaanisha, nitanena kwa lugha na nitaomba kwa akili/maneno ya kawaida pia. AJABU YAKE NI KWAMBA, ninyi na wachungaji wenu na mapadre wenu hadi maaskofu wenu, hata walau mara moja tu kunena kwa lugha hamjawahi, mmechagua kuomba kwa akili peke yake. kwanini basi kama mmeamua kulipinga hili, msiombe walau kama Paulo? muombe kwa lugha, na muombe kwa akili pia? imekuwaje hamuwezi kuomba kwa lugha? ni kwasababu hamna Roho na mmemkataa. Paulo alisema ananena kwa lugha kuliko wote? kwanini hakuwa anaomba kwa akili peke yake? mlishawahi kutafakari hili?
 
Back
Top Bottom