Siri ambayo waombaji wengi wa Kikristo hawajaijua. Chukua hii uone matokeo katika maombi yako

Asante Dr...
Na ndio maana tunasisitiziwa sana kumuomba roho mtakatifu atusaidie kutuongoza,Kwa kuwa wengi hatujui kuomba,twaomba vibaya ila Kwa msaada wa Roho mtakatifu tunaweza kuongozwa vyema
Warumi 8:26
Vivyohivyo, Roho mtakatifu hutusaidia katika udhaifu wetu,Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo.Bali roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa
 
Kama mbinguni kuna maisha mazuri, Kufa nenda kwenye hayo maisha mazuri.

Kwa nini uombe kuishi maisha marefu duniani?

Kufa.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
na kwakweli kwa fungu hilo la neno,
tunakumbushwa kuweka nia na dhamira zetu bayana dhidi ya vitu tunavyoviomba kwa Mungu tutavitumia nanma gani?

Tutavitumia kwa anasa na kua kero au usumbufu kwa wengine? ama tutavitumia na vikawa msaada na Baraka kwa wengine 🐒

Tuombee vizuri,
ni vema kuweka wazi nia, dhamira na matumizi mujarabu ya unachokiomba kwa Mungu 🐒
 
Kufa hamtaki mnapiga porojo za maisha mazuri mbinguni.

Kama mbinguni kuna maisha mazuri, kufa nenda kwenye hayo maisha mazuri.

Kwa nini uombe maisha marefu duniani ilhali unajua mbinguni kuna maisha mazuri?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Roho Mtakatifu asaidie kuhuisha roho na nafsi zetu, nakufanya maskio ya rohoni mwetu yawe tayari kutambua na kuskia vema, sauti ya wito wa Mungu, katika maisha, kazi na majukumu yetu 🐒
 
Barikiwa Kwa Neno Ila Kwa navyofaham kunena kwa lugha hiyo Ni Karama ambayo Sio wote wamepewa
 
Ni kama u
Ni kama umeniacha njiani ndugu, uzi mzuri lakini haujakamilika kwa upande wangu.
 
Roho Mtakatifu asaidie kuhuisha roho na nafsi zetu, nakufanya maskio ya rohoni mwetu yawe tayari kutambua na kuskia vema, sauti ya wito wa Mungu, katika maisha, kazi na majukumu yetu 🐒
Amina...Kuna nyakati Huwa nasikia kufariki sana kiroho,yaani napoa kabisa,Siwezi kabisa kuzungumza na Baba,ila nikimwita roho aisee anahuisha,utasikia vile Kuna chem hem ndani yako inataka tu kuomba,unafufuka....Hakika ni msaidizi mwema
 
Yes alikuwaga na ROHO MAKATIFU Ila hakuwahi kuomba kwa KUNENA nyie mmeitoa wapi bhandugu?

Au ndio mashetani ya kigalatia yanapandishwa hivyo

Nauliza tu
Yesu baada ya kufufuka alieashukia mitume. Akawajaza Roho Mtakatifu kila mtu akanena kwa lugha. Ndiyo mwanzo wa kunena.
 
We mjomba, hakuna kiumbe chochote m inguni na duniani kinachoweza kumzuia Mungu asisikie maombi yako au kujua dhambi zako.
Mungu hasikii maombi ya wenye dhambi. Husomi maandiko?

Ni kumpigia tu kelele!!
 
Yesu baada ya kufufuka alieashukia mitume. Akawajaza Roho Mtakatifu kila mtu akanena kwa lugha. Ndiyo mwanzo wa kunena.
Mwingine Huyu hapa hajui lolote katika IMANI wala KITABU chake

YESU alishukia wapi 😁😁😁
Yaani wewe hata biblia hujui kabisa?


Sijakudhihaki ila wewe kweli HUJUI kabisaaaaaa!


Kama unajua Leta ANDIKO kuwa huyo YESU alishuka kuwaambia wanene kwa Lugha
 
(Yohana 14:26)
 
Mkuu wewe Ni mwanatheolojia??
Mkuu unajua/Umejifunza Lugha ya kiebrania,Kigiriki,Kiaramaic au Hata kilatini??

Kama ndiyo Mkuu Samahani kama nitakukosea kwa nitakachokisema, Rudi Tena kasome grammar Sana sana kwa Lugha hizi Tatu inaonekana zinakuchangnya Arabic,Aramaic na Hebrew..

Ukimuona Mtu aliyesoma Theolojia Bado anasumbuliwa na Maneno aliyotamka Yesu asijue ni lugha gani mtilie mashaka sana..
Yesu aliongea Simple aramaic sana hapo..

Sasa Twende kwenye kujifunza ili watu wasipotoshwe na maneno yako

Je ni mara ya Kwanza yesu aliongea Kwa lugha ya Aramaic na Sehemu hiyo ikaacha kutafasiriwa au ikatafasiriwa pamoja na kuacha lugha asili?

hapana,

Yesu alikuwa anaongea lugha ya Aramaic na Kiebrania, Lugha ya aramaic ilikuwa ni lugha official kwa ajili ya mazungumzo na mawasiliano ila lugha ya kiebrania ilikuwa ni lugha ya kiofisi na lugha rasmi kwa wayahudi wote..

Alipomfufua yule mtu aliye kufa alimuambia talitha Kumi..(Hii ni kiaramu)..

Marko 5:41
"Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka."


Concern Yako ya kwanza ni watu kushangaa pale msalabani baada ya yeye Kusema Eloh eloh...


Kama nilivyosema Mwanzo kuwa Lugha iliyokuwa inaongewa na Wayahudi kama lugha ya mawasiliano.ilikuwa ni kiaramu kwa wakati huo
Na kwa bahati mbaya Utawala wa kipindi hicho ulikuwa ni utawala wa Kirumi kwahyo Warumi wengi hawakujua Kiaramu wala kiyahudi, Unless uwe katika jamii za wayahudi..

Na ikumbukwe waliomsulubisha yesu hawakuwa wayahudi kwa hiyo Siwezi kushangaa wao kusema anamwita eliya kwa sababu hawakujua anaongea nini hawakuwa familia na Lugha ya kiaramu..

Concern ya Pili ni neno lenyewe Eloi Eloi Lama sabakhtan..
Ulivochambua hili Neno kwenye Post yako Hapo Juu ndo kulifanya nitilie shaka uelewa wako wa Ligha ya tatu Kigiriki,Kiebrania,Kiarabu..

Ngoja tuandika Neno halisia kwa Lugha ya kiaramu..

"ܐܠܗܐ ܐܠܗܐ ܠܡܢܐ ܫܒܩܬܢܝ

(Eloi, Eloi, lama sabakhtani)

Kwa lugha ya Kigiriki..

"Ἐλωΐ, Ἐλωΐ, λεμὰ σαβαχθανί;"
Concern yako kuwa kwanini Kwenye Kigiriki hawakutumia Kappa (k) wakatumia Chi (χ)
Neno "ܫܒܩܬܢܝ" au kwa Kigiriki σαβαχθανί linatamkwa "shabakhtani" na maana yake ni "Umeniacha mimi".

limetkna na mzizi wa Lugha ya Kiaramu "shbq" ambayo humaanisha "kuaondoka" ,"Kuacha" au "kutelekeza,"

na hiyo suffix ya -tani" Inamaansiha second person singular pronoun ambayo ni "you." So, kwa pamoja itatamkwa "shabakhtani" Tafsiri Yake mbona umeniacha..
Herufi za Kiaramu iliyotumika kama Kh ni ni herufi ya kiaramu Qop ( ܨ ) ambayo ni sawa na Herufi ya Kiarabu Qaf (ق) na ni sawa na Herufi ya Kiebrania Qaf ("ק" )
katika Lugha hizo tajwa hapo juu matamshi ya K,Kh, q yote yana herufi zake..

tatizo linaanza kwenye Lugha za magharibi kama Greek, English na latin hakuna tofauti mwa herifu

Sasa Qaf/Qof hutambulishwa kwa. Qi au chi (χ) kwa ligha ya Kigiriki na kappa hutambulishwa kwa k..
Asili ya Sabakhthani ni Qaf kwa lugha ya Kiaramu kama umeniacha ..

Ila ukiweka Kappa inapoteza maana Yake..

Kwahyo wengi huikosea kuitamka kutokana na lugha yake kupotea kwenye maandishi..

By the way ni Kiaramu na sio lugha ya Kiroho....

Sijui kama umenielewa
 
Nani kakudanganya umaskini unatolewa na maombi,omba mpka ubinuke hakuna matokeo yoyote utakayo pata usipo badili fikra na kuchukua hatua .




First Law (Law of Inertia): An object at rest stays at rest, and an object in motion stays in motion with the same speed and in the same direction unless acted upon by an external force.
 
Msingi wetu hauko katika filamu ya Yesu. Ile ni ya waigizaji tu waliigiza kama njia ya kutafuta pesa.
Soma Maandiko hayo ndipo tulikotoa kunena kwa lugha.
Ni maagizo ya Yesu mwenyewe.
Mitume walionena kwa lugha linachukuliwa na wajasilia dini kama sanaa ya maigizo kuvuta masikio ya hadhira.

Haujajibu kwa mantiki post #6 maana halisi ya neno 'kunena kwa lugha'.

Sisi wenye imani za kadiri, tunaamini kuwa baraka ya lugha waliyojaliwa mitume wakati wa kujazwa Roho mtakatifu iliwasaidia kuwafikia mataifa mbali mbali kwa lugha zao na kuanza kulihubiri neno la bwana kwa urahisi zaidi kuliko wangelifika maeneo hayo na kuanza kutafuta wakalimani.

Kwa nini nyie mnayapotosha maandishi yaliyo wazi kwa tafsiri zenu za mifukoni?

Historia zinaeleza wazi kuwa kila mtume alichukua uelekeo wake katika kazi ya kuhubiri injili kwa msaada wa lugha zao hizo mpya za mataifa mbali mbali walizoshushiwa na Roho mtakatifu.

Sasa nyie kupandisha mori mfano wa kupandisha mashetani na kutamka maneno yasiyo na maana katika tafsiri, mnaita kunena kwa lugha!

Nena kwa lugha itakayoeleweka kwa waumini wote wanaosikiliza mafundisho yako ili ueleweke kwa usahihi.
 
Hujawahi kutembea katika roho au hujawahi kutembea na watu wanaotembea na MUNGU.
Kuna Wainjilisti wengi tu mpaka sasa wanaweza kuhubiri lugha yoyote mahali popote.
Nyie mnaishia kuwatazama matapeli wa kwenye tv na shuhuda zao za uongo ilhali ni wazinzi wakubwa na mioyoni mwao hakuna Mungu.
•Kuna Karama ya lugha hii ndio inampa mtu uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali za kibinadamu lakini anakuwa katika Roho.
•Kuna karama ya kutafsiri lugha, hii karama inampa mtu uwezo wa kutafsiri lugha za Kimungu (za kimbingu) kwenda katika lugha za wanadamu.
Hizi karama zote zipo na zinafanya kazi kwa watu mbalimbali leo.
Kama hujaona au hujawahi kupata huwezi kuamini
 
Tatizo lako unaongea mambo ambayo hayawezi kueleweka na mtu.

Kutokukuelewa unachoongea hakumfanyi mtu kutokuwa na roho wa Mungu ama roho wa wokovu ndani yake.

Kwa sababu wewe hauna hakimiliki ama mamlaka kwenye imani za watu wengine wamwaminio Mwenyezi Mungu.

Hauwezi kunena lugha ya rohoni ambayo jamii inayokuzunguka ibakie ikikushangaa na isiielewe tafsiri yake.

Hata wale mitume uliosema, walinena kwa lugha ngeni za kibinadamu za mataifa waliyokusudia kwenda kupeleka injili.

Na walipofika huko, lugha hizo ziliwasaidia kuongea na wenyeji wao moja kwa moja bila msaada wa wakalimani katika kuneza neno la bwana.

Hakuna maana nyingine ya kunena kwa lugha zaidi ya hii iliyoandikwa kwenye biblia chanzo chake kikiwa ni mitume kushukiwa na roho mtakatifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…