Tetesi: SirJeff Khagolla (Alias Ontario) amedakwa Mafinga kwa kosa la Uhujumu Uchumi

Jamaa kadakwa kizembe sana aisee nakumbuka alishwahi kutapeli wajinga Sasa ni zamu yake kutapeliwa mahakamani anahamishiwa kisutu leo vijana fanyeni kazi halali acheni wizi na utapeli maana nyakati hizi sio za ujanjaujanja huyu Kawa wa mfano
Tuliza akili uandike habari ieleweke. Huyo mtu ni nani, amekamatwa katika mazingira gani, hilo kosa la uhujumu uchumi amekamatwa na vielelezo gani vilivyopelekea awe na kosa hilo, huko Mafinga alikuwa anafanya nini? Unapotoa taarifa hakikisha unaeleweka
 
Ni tapeli Fulani hivi alikua anapiga pesa za wajinga maana tanzania wajinga wanazaliwa Kila siku
Inavyoonekana umewahi kutapeliwa na huyo mtu, majibu yako yamejaa hasira na ghadhabu ndani yake. Kama ulitapeliwa pasipokushikiwa bundika wala siraha yoyote jipige ngumi kifuani halafu useme hautatapeliwa tena lakini sio kumuombea mwenzako mabaya
 
Wengi wanamuona tapeli kwasababu ya yale mafunzo yake ya forex miaka ile. Aliwakusanya wengi, wakalipa ada, wakaweka mitaji na mwisho wa siku wakaambulia patupu. Wao wakaona wametapeliwa

Wanachosahau ni kwamba mafanikio huwa hayapatikani kirahisi rahisi kama walivyotegemea na mbaya zaidi mafanikio huwa si ya kila mtu! Mnaweza kupewa mchongo mkiwa watu 20 lakini wakajikuta wanafanikiwa watu wawili tu kati yenu walioweza kuchanganya vizuri akili zao na fursa waliyokutana nayo. Hao 18 waliofeli haimaanishi wametapeliwa, pengine halikuwa fungu lao kufanikiwa kwa njia ile

Wengi wanaomuita tapeli akiwemo mleta mada ni ama ni aina ya wale watu wanaotaka mafanikio ya haraka haraka au wale watu wasiojiweza kutumia maarifa na akili walizopewa na Mungu kufanikisha ndoto zao
 
Sio tapeli ni Trader mmoja mkubwa sana na pair yake ya GBPJPY
Huyu kesi yake ni ngumu sana ,alikusanya pesa kwa watu akishirikiana na Capital market broker wa south ambaye hakuwa broker halali ..kinyume chake alikuwa anachezesha kama upatu ,hapa ukitaka nitakufafanulia ,yaani alikuwa anapata faida baada ya kuwaingiza watu watapeliwe na huyo broker ...

Kumbuka broker wa Kipind hicho hakuwa amesajiliwa huko sauth hata hapa bongo so ni kosa ,sio kutrade forex bali ni kuwauza kwa broker tapeli.

Nakukumbusha ,ishu za pesa zina taratibu zake ..Kesi za kukusanya pesa isipokuwa kwa kufundisha watu ,kama huduma za mentorship ila kushiriki moja kwa moja kuwapeleka watu kwenye uwekezaji ni kosa ,ikiwa huo uwekzaji haufuati taratibu wa BOT ..
...
 
Maelfu ya watu, wengine 20 hadi walikufa wakikanyaga mafuta katika huo utapeli wake huko Moshi.
Imani yao ndiyo ilipelekea yale maafa, sidhani kama Mwamposa directly anahusika na uzuzu wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…