Sisi wajaluo mila zetu zinamruhusu mwanaume kuoa wanawake mpaka watatu (3) waliozaliwa tumbo moja

Nakuelewa usemacho Infantry Soldier . Maana hata Yakobo (Israel) ambaye ni mtoto wa Isaka na mjukuu wa Ibrahim Baba wa Imani naye huyo Yakobo alioa wadada wawili Lea na Raheli watoto wa Baba mmoja Laban ambaye ni mjomba wake.

Sio kuoa tu bali aliwazalisha watoto Lea alizaa watano na Raheli akazaa wawili, kisha wengine watano wakazaliwa na vijakazi wa Lea na Raheli jumla wakaka watoto 12 ndio wakaitwa WANA WA ISRAEL hadi leo!
Sishangai kuona ipo hivyo kwa wajaluo ni watu kuwa na Positive Minds tu!
 
Sijasikia mila ya kabila la kitanzania inayokataza hiyo mila, labda ya marekani wanakokataza mke zaidi ya mmoja ila wanaruhusu ndoa jinsia moja. Hata katika Biblia nabii Yakobo alioa mtu na dada yake Bilhah and Zilpah na Mungu akambariki kuwa baba wa taifa la Israel
 
Itakuwa hakuna Wakristo huko!

Maana Biblia imekataza mambo hayo kabisa!
 
kumbe wewe ni mjaluo? ndo maana una akili.
Binadamu wote akili tunazo ila tunatofautiana viwango vya ujazo wa hizo akili zetu. Kwa mfano mwanasayansi Einstein ana akili nyingi sana kunizidi mimi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…