Sitaki huruma yenu, lakini Wakuu maisha yananigonga vibaya sana!

Sitaki huruma yenu, lakini Wakuu maisha yananigonga vibaya sana!

Sikupi pole wewe mtoto wa kiume!
Jiongeze, tafuta sehemu kwenye mgahawa au wanapouza chips omba kibarua chakusaidia kumenya viazi au kuosha masufuria/vyombo. Wakikupa ujira wa msosi inatosha siku imekatika unaenda kupiga pindi. Huo ni mfano tu Kuna mishe ndogo ndogo zinaweza kukusaidia ukaishi kwa kushibisha tumbo.
 
Mkuu, nipo mwaka wa tatu, nalipiwa ada asilimia 17 na bodi, nyingine naongeza mm kutoka kwenye boom, Sina mpenzi mana najua hali ya nyumbani kwa Kwel maisha ya hapa Duce yamekuwa mwiba kwangu
Pole sana komaa dunia Haina huruma kwa watu wanyonge, kaza zungusha akili fikiria cha kufanya
 
Third year huwa pagumu sana!

Unaweza kosa nauli ya kuendea home,hasta semester ya mwisho Ile miezi miwili baada ya kuchukua boom la mwisho!
asikae idle sasa ajishugulishe kama anandugu aombe msaada huku na yeye anawaza cha kufanya maisha ya chuo ni challenge kama huna pesa najua. Kingine ni bora kiwa muwazi kwa ndugu na jamaa,, ukute anajikaza kisa yeye mwanaume, atapata stress mwishowe adisco
 
ndugu mwanahabari ww ni kalaxa sana huku unasema maisha yamekuchapa,kuna uzi mwungine nimeona unalalamika umejamba kwenye kikao cha kanisa na umebata Aibu kwa mwanamke unayempenda na haujui kama atakubali umuoe.
 
Tanzania ni nchi ya asali na maziwa na watu kutoka mataifa mengi duniani wanakimbilia kuja kuzitumia fursa zilizopo ambazo sisi hatuzioni.....mashamba yamejaa kibao,mazao mblmbl yanaoza sehemu mblmbl halafu mnakuja kulia kwenye mtandao
 
asikae idle sasa ajishugulishe kama anandugu aombe msaada huku na yeye anawaza cha kufanya maisha ya chuo ni challenge kama huna pesa najua. Kingine ni bora kiwa muwazi kwa ndugu na jamaa,, ukute anajikaza kisa yeye mwanaume, atapata stress mwishowe adisco
Ushauri mzuri, mimi nakumbuka miaka ya 2007-2010, nabakiza elfu 3 mfukoni! Sikuwa na kawaida ya kushirikisha ndugu, nilikuwa na rafiki yangu tulisoma naye sehemu, nilikuwa namwambia tu bro hapa mfukoni nina elfu 3, boom bado, atakwambia tu saa ngapi uende ucheki kwenye account unakuta elfu 50! Boom likitoka tu jambo la kwanza ni ku- refund. Mungu ampe maisha marefu huyo jamaa yangu.
 
Fanya usiku huu,twende buguruni kwa bosi kubwa,said salim bakhresa tukabebe viroba vya unga mpaka asubuhi uondoke na mavumba mengi,kesho ule milo mitatu boi.
 
What pains a man trains a man.

Ila nakuhakikishia humu hutopata chochote hata buku iliochakaa,kikubwa wewe ndo unatakiwa kujisaidia japo humu wapo maboss,wakuu mbalimbali.

No one is coming to save you it's only you.
 
Hayo ni mapito tu katika maisha.

Nakukumbusha uje uandike kitabu kuelezea mapito uliyopitia maishani Kwa manufaa ya umma.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom