Sitaki huruma yenu, lakini Wakuu maisha yananigonga vibaya sana!

Sitaki huruma yenu, lakini Wakuu maisha yananigonga vibaya sana!

Maisha yamenitenda ubaya sana. Mwezi ya nne sasa nakula mlo mmoja tu Kwa siku(Wakati wa usiku).

Ee Mungu unae watajirisha wengine naomba nikumbuke.
Mm bado kijana mdogo mwenye ndoto nyingi sana, Mungu nikumbuke.

Nimekonda, hadi mwezangu wanadhani naumwa, na pepesuka hali mbaya sana. Venue sielewi lekcha anachofundisha njaa inataka kuniua.

Kama kazi na madili na fanya lakini still mambo magumu.

Kama ndio nipo chuo, na Hali ipo hivi je nikimaliza?
Acha ujinga.
UDOM pale 1500/- niliitumia siku 6.
Half cake moja 250 na maji ya ku -download mida ya saa 5 asubuhi kila siku. Siku boom lilipotoka nikakaa sawa.

Ndio,ukifikiria sana kuhusu unayopitia masomo hayawezi kupanda lkn ni vizuri kukubaliana na hiyo hali utasoma vizuri tu.
 
Mkuu, nipo mwaka wa tatu, nalipiwa ada asilimia 17 na bodi, nyingine naongeza mm kutoka kwenye boom, Sina mpenzi mana najua hali ya nyumbani kwa Kwel maisha ya hapa Duce yamekuwa mwiba kwangu
Kuwa mpole ili ufanye vizuri UE yako ya mwisho.
Itakuwa hatari zaidi uki supp, carry dakika za jioni.
 
Sikupi pole wewe mtoto wa kiume!
Jiongeze, tafuta sehemu kwenye mgahawa au wanapouza chips omba kibarua chakusaidia kumenya viazi au kuosha masufuria/vyombo. Wakikupa ujira wa msosi inatosha siku imekatika unaenda kupiga pindi. Huo ni mfano tu Kuna mishe ndogo ndogo zinaweza kukusaidia ukaishi kwa kushibisha tumbo.
Sio rahisi kama ulivyoandika mjinga wewe.
 
Acha ujinga.
UDOM pale 1500/- niliitumia siku 6.
Half cake moja 250 na maji ya ku -download mida ya saa 5 asubuhi kila siku. Siku boom lilipotoka nikakaa sawa.

Ndio,ukifikiria sana kuhusu unayopitia masomo hayawezi kupanda lkn ni vizuri kukubaliana na hiyo hali utasoma vizuri tu.
Ulitisha sana sahivi keki 400
 
Maisha yamenitenda ubaya sana. Mwezi ya nne sasa nakula mlo mmoja tu Kwa siku(Wakati wa usiku).

Ee Mungu unae watajirisha wengine naomba nikumbuke.
Mm bado kijana mdogo mwenye ndoto nyingi sana, Mungu nikumbuke.

Nimekonda, hadi mwezangu wanadhani naumwa, na pepesuka hali mbaya sana. Venue sielewi lekcha anachofundisha njaa inataka kuniua.

Kama kazi na madili na fanya lakini still mambo magumu.

Kama ndio nipo chuo, na Hali ipo hivi je nikimaliza?
Tenga muda wako wa ziada fanya vibarua, umesema upo chuo jaribu dili za uwinga unaongea na wauza nguo wanakupa mzigo unapitisha hostel kwa washkaji na mademu pia jaribu kuomba msaada kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao unaona wanaweza kukusaidia humu utaishia kupewa pole tu ambazo hazisaidii chochote.
 
Hili wazo liliishia wapi?
Sio makosa yake kaka....ni wishes tu za watoto wa chuo.
 
Hivi hii hali ngumu ya maisha ya chuo mbona wengi lialia ni jinsia ya kiume? Jinsia ya kike wote wanapata boom 💯 au? Wao wanawezaje au mkipata hela wanawakamua mpaka zikiisha wanawabwaga?
Kwaiyo haujui jinsia ke wana-survive vipi mjini njaa zikiwapiga au unatu-enjoy tu? Kama ulikua haujui basi jibu ni kwamba wanafanya umalaya
 
Shukuru Mungu angalau wewe unakula mlo mmoja kwa siku. Wengine wana kula mlo mmoja kila baada ya siku tatu.

Ulipangiwa utaishi hivyo unavyoishi Pindi tu tangu ulipozaliwa.
Daah
 
Umeshatafuna boom kwenye betting wewe...

Pole sana dogo..
Kuna jamaa aliwahi kupitiwa na Qnet, mwingine alidanganywa kuhusu scholarship akatoa hela ya boom karibia yote kipindi tupo Chuo. Kilichofuata sasa..

Huyo aliyepitiwa na Qnet baada ya kujua kazulumiwa akaanza kuunga unga kwa kukopa ili alipe madeni maana wakati analipa Qnet hela yake aliikopa akijua itarudi mapema ili alipe hayo madeni. Alisuffer sana

Huyo wa Scholarship alipogundua kazulumiwa, alichanganyikiwa akaamua kuondoka chuo arudi nyumbani, yaani aliamua aache chuo kwani aliachwa mtupu huku muda wa boom lingine ukiwa bado mrefu hadi litoke. Tulipogundua dhmira ya jamaa wakati tayari kashafika kwao Songea tukajikita kumpa nasaha ili arudi kuja kuendelea na chuo bahati nzuri alituelewa akaamua kurudi, akaja kuunga unga hela ya msosi hadi boom lilipotoka ndio mambo yakatengamaa.

Ki ukweli Chuo kuna mambo mengi sana yanayotia stress na kuvuruga future za watu
 
Wewe utakuwa first year, mkifika chuo mnajisahau mnahonga na kula bata. Kingine kuwa na bajet unapopata hela ya kujikimu, usijihusishe na mambo mengi yasiyo ua msingi fanya kilichokupeleka chuo, hayo mengine yape nafasi kidogo
Naona unatoa uzoefu wako kijana wangu 😂
 
Umebetia boom na kushinda wavuvi na kidimbwi kushangaa maslay queen wale dragons 🤣🤣🤣
 
Wewe utakuwa first year, mkifika chuo mnajisahau mnahonga na kula bata. Kingine kuwa na bajet unapopata hela ya kujikimu, usijihusishe na mambo mengi yasiyo ua msingi fanya kilichokupeleka chuo, hayo mengine yape nafasi kidogo
Umepiga kwenye mshono mkuu.Jamaa achukue huu ushauri wako aufanyie kazi naamini utamsaidia sana
 
Back
Top Bottom