kidawisee
Senior Member
- Feb 27, 2020
- 143
- 212
- Thread starter
- #161
Asanteeee,hapo pa kusema tumeshariki unanijua,Asante kwa maneno ya busara,natamani niamishie aya maneno mdomoni nisitoe neno hata moja.Mpenzi (mtaje kwa jina lake),
Kuna jambo linanitatiza sana. Na kwa hili naomba nikueleze yanayonisibu.
Kwanza, tambua ya kuwa nakupenda na hakika nakupenda mno. Hilo halina shaka yeyote na wewe walifahamu vema. Naamini ya kuwa hata wewe unanipenda.
Pili, naamini ya kuwa misuko suko ya hapa na pale hayatahitimisha mapenzi yetu kama kweli yanatoka miyoyoni mwetu. Tumeshajenga msingi, kinachofuata ni ukuta imara wa kutukinga.
Tatu, najua fika ya kuwa mapenzi (kulalana) ni nguzo moja imara katika kuimarisha mahusiano. Na tumeshafanya hivyo mara kadhaa. Unanijua nje ndani.
Lakini, hivi karibuni nimeanza kupitia misukosuko fulani (itaje). Na nimeoteshwa pia ndoto juu ya misukosuko hii (mhadithie ilivyokuwa). Na katika kutafuta suluhisho la changamoto hii, nimeelezwa kuwa usinzi ndiyo mlango unapotokea. Na nikijaribu kufikiri naona kama kweli kwa kuwa kabla ya hapo haikuwa hivi.
Kwa hiyo, ikikupendeza naomba tuendelee kuwa wapenzi bila ya kushiriki tendo la ndoa mpaka pale ambapo tutafunga ndoa. Narudia nia yangu siyo kukunyima tendo kwa sababu ni kwa manufaa yetu sote. Na ingekuwa hivyo nisingekubali tangu hapo mwanzo.
.......
Kaa tulia mpe akujibu. Mtapata muafaka na utaendelea na maisha.