Mwe jamani sasa mbona unasema leo umgesema mapemaI used to like you but not anymore.👹👺
fVCK off
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwe jamani sasa mbona unasema leo umgesema mapemaI used to like you but not anymore.👹👺
fVCK off
Sasa nawaambukizaje makisudi wakati nawambia kabisa kuwa mie ninaoSawa we ushajitoa kafara its your life hakuna wa kukupangia hata ukitaka kunywa sumu ufe meza tu its your life shida yangu ni wewe kuambukiza wenzio ukimwi kwa makusudi.😠👺👹
Umesahau vyuoni kuna ule mradi maalumu wa kueneza umeme ili ARV ziendelee kuuzwa kwa sana kwa Wateja?Nyie mnao penda uterezi sehemu hatari kupata ukimwi kwa juju ni hizi.
1. Kwaya za walokole na walokole wanao kesha.
2. Singo maza wasio nyoosha maelezo yao kuhusi mzazi mwenzie iko wapi.
3. Makahaba wa Buguruni na sinza wengi wameathirika siku nyingi.
4. Wanachuo walio tokea mikoani angalieni wengi wanaambukuza bila kujua kwasbb ya axcitement ya mjini.
5.sexnetwork ndani workmates kazini hususani hizi kazi za field zenye trips hao watu wana laliana sana chungeni usikubali mkeo apangiwe hizo trips atakuletea ukimwi, komaa na kipato chako hicho kdgo.
Na hamna watu wako kwenye hatari ya maambukizi Kama watu walio kwenye serious relationship....Maana mnaaminiana,hakuna Tena condom baina yenu,kwa hiyo mmoja akichomoka akaleta kila mmoja anajifanya hajui umetokea wapi...ndio Maana unashangaa wale malaya hawana maambukizi Maana hamna mtu anamuamini kila akipiga nae anavaa protectionKwa hiyo kila mahusiano mapya mnapima? Mkiwa kwenye mahusiano mnatumia kinga au ni raw? Akichepuka na kuuleta hapo katikati? Aagr hili gonjwa labda tuache kungonoka, otherwise wote tupo kwenye risk.
Mtaa ni MET huo kuna balaa sana pale mzee,Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.
Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.
Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.
Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.
Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.
Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.
Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.
Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.
Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.
Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.
Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.
Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.
Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.
Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.
Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.
Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.
Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.
2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.
Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.
Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.
Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.
RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.
Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.
Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.
Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Bora tu kulewa🙆🙆🙆🙆,kuacha ni Bora watunyongeNasikia inalewesha hatari, basi tuache ngono kama ndio hivyo😜
Uzi wa "KULA TUNDA KIMASIHARA" ufutwe haraka sana kunusuru Taifa...[emoji57]Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
Acheni kuwatisha watu. Hapa duniani ni njia tu.Kuna wale members wa kula tunda Kimasikhara ujumbe huu uwafikie. UKIMWI upo na UNAUA
Hapo ndio tatizo lilipo, ukiaminiwa kumbe unapiga nje mwenzako anajua tuko wawili. Ila kuwa na mmoja tu nako mtihani sana jamani.Na hamna watu wako kwenye hatari ya maambukizi Kama watu walio kwenye serious relationship....Maana mnaaminiana,hakuna Tena condom baina yenu,kwa hiyo mmoja akichomoka akaleta kila mmoja anajifanya hajui umetokea wapi...ndio Maana unashangaa wale malaya hawana maambukizi Maana hamna mtu anamuamini kila akipiga nae anavaa protection
Vyovyote vile tutakufa tu, au sio😅😅Bora tu kulewa🙆🙆🙆🙆,kuacha ni Bora watunyonge
Da umefunga mjadala🤸....Kazi iendeleeVyovyote vile tutakufa tu, au sio😅😅
Nimesoma pale mwaka 2005, kila siku asubuhi ilikuwa ni lazima mtu azikwe. Hatukujua sababu za vifo ila kila siku udongo ulikuwa unapata nyama.Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.
Ni kanyigo ila Sina uhakika na hili jina... Hilo eneo lipo kama unaenda Karagwe unakata kulia kama unaenda Uganda. Nimebahatika kufika Hilo eneo, ila stori za wenyeji mpaka nilitetemeka ingawa maafa yalitokea kama miaka 30 iliyopita....Mkuu hicho kijiji kinaitwa je, au ni hearsay tu.
Verse 2Verse 1
Nasikia raha jinsi nilivo star
Ni zaidi ya Robert De Niro
Nini top in Dar
Najukikana dunia nzima
Na kila kona hua natajwa langu jina
Sio tu watu wazima hadi watoto
Majina mengi a.k.a moto
A.k.a umeme a.k.a miwaya
A.k.a ngoma nzito isiyo na dawa
Ayaaaaah
Lakini sina ubaya
Na sibagui nchi za Africa nchi za Ulaya
Ni wengi tu nshawaondoa duniani
Na wengi bado nawatesa vitandani
Acha idadi kubwa ambao wapo safarini
Sijali mtoto wa kishua au unapoa uswahilini
Si mshajua nachozungumzia nini?
(UKIMWI UKIMWI UKIMWI)
Yeah a.k.a mimi
Natesa sana napokuingia mwilini
Akina gono kaswende wote baba yao mimi
Amini mi ndo kubwa la maadui
Na leo nakuja kwako usizuge kama hunijui
Halaa
Mkuu tunapozungumzia ukimwi ishu hapa sio kufa, ila ishu ni kufa na ukimwi. Mtoa mada kana sentence anasema "kama hujawahi kumuona au kuuguza mgonjwa wa ukimwi huwezi kuelewa vizuri"Kwani hawatakufa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] bora wafe kutokana na utamu wa de libolo kuliko corona
Ata arv kuna stage ina gonga mwamba damu imechoka dawaSaivi ARV Zinaficha Mengi. Watu wameoza kabisa usilogwe kupiga kavu
Kuna mwalimu mmoja wa kike (RIP) tukiwa tunakaa kota, siku za mwisho mwisho wa uhai wake alitoka nje ya nyumba yake mida ya saa 2:30 usiku hana nguo mwilini, akawa anazungumza kwa sauti kubwa,"vijana njooni muone jinsi ninavyoteseka. Msiache tamaa ziwaponze, mtakufa. Mimi nitakufa sio muda mrefu, njooni mjionee ninavyoteseka". Alikaa kama miezi 2 hivi akaaga dunia akiwa kwao Mbeya. Hiyo ilikuwa mwaka 2009 hiviHalafu kuna watu wanaambiana waende kavu eti haya ni maisha tu sote tutakufa. Mungu atuepushe na huu ugonjwa umekaa pabaya
Hivi arv zinauzwa? Au serikali hununua kisha kuwagawia bure wananchi?Umesahau vyuoni kuna ule mradi maalumu wa kueneza umeme ili ARV ziendelee kuuzwa kwa sana kwa Wateja?
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app