Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

😭😭😭hii ndiyo hali nayopitia kwa sasa, nahitaji mshauri kweli
 
Sad,sahau....usiwe Kama Mimi niliweka kinyongo na kikaja kunitesa mwenyewe...Kupitia njia ngumu ni sehemu ya maisha
Hakika namshukuru Mungu nimepitia huko nimejifunza kupambana na kusimama mwenyewe maana hakuna ndugu yeyote aliyekuwa nami kipindi hicho japo walikuwa wanajua yote hayo
 
Kama ulikuwa unafanya maujinga kakitia viboko kwa ajili ya kukutia adabu alikuwa anafanya viziri sema kuanza kukutukana matusi ya nguoni lilikuwa ni tatizo, mlezi au mzazi hutakiwi kumtamkia mtoto wake tusi hata kwa bahati mbaya.
Ni hapo sasa mkuu, alikuwa anakosea na kwenda mbali zaidi hadi kuniambia nina laana hii huwa inanitesa kwani kuna muda nafanya vitu, kama haviendi hadi nawazaga au ni kweli nilivyoambiwa nina laanq😭😭
 
Unavyoongea hivyo ni kama tumekuwa wote, aya endelea kunielezea
Si ninavyo kuelezea bali jinsi ulivyo jielezea ww, au sio ww uliye leta mada ya kujutia maisha yako ya nyuma?
Na kwenye maelezo yako sio ww ulie sema kuwa mama yako wa kambo alikuwa vizuri mpaka pale ulipo anza tabia za ajabu?
Hata ww una upande wa pili iwapo mtu atavuka mipaka yako ya uvumilivu.

Kama ww unavyo jutia makosa yako ya nyuma na hutaki kuhukumiwa kwa uliyo yafanya huko nyuma, hivyo hivyo huna haki ya kumuhukumu mama yako wa kambo kwa mama yako wa kambo kwa mambo ya nyuma msamehe maisha yaende mbele.
 
Hayo maisha mabaya nilipitia kwasababu yake, nilishamsamehe
 
Kiukweli nilikuwa nikimchukia baba yangu, lakini sioni faida ya kufanya, nimeamua tu niache hayo maana kuna leo na kesho, nyie “”single faza jaribuni kuoa au kuishi na wanawake watakaowapenda watoto wenu, siyo unaishi na mwanamke unajua kabisa hampendi mwanao ila kwasababu wewe anakupenda unaganda nae hii siyo sawa””

Single Daddy ni muhimu sana kuzingatia 👆.


Anyways, kama ningekuwa mwanaume basi ningetumia njia nyingi sana kumfahamu vizuri mwanamke anaenda kuishi na watoto ambao hajawazaa yeye.wababa/wamama jaribuni kuwasikiliza watoto wenu wanaoishi na mama/baba wa kambo wanakuwaga na mengi yakuzungumza.
 
Mimi huyu baba angu alikuwa kashikwa akili na mkewe kabisa, yaani unamwambia anasikitika tu na hafanyi kitu, anaona kabisa matusi kama hayo tunatukanwa lakini hafnyi kitu
 
Ni hapo sasa mkuu, alikuwa anakosea na kwenda mbali zaidi hadi kuniambia nina laana hii huwa inanitesa kwani kuna muda nafanya vitu, kama haviendi hadi nawazaga au ni kweli nilivyoambiwa nina laanq😭😭
Yaa maneno ya mzazi huwa yana umba hutakiwi kumtamkia laana mtoto hata kama atakuwa amekosea, mtoto akikosea inatakiwa kumtia bakora kumrudisha kwenye mstaari na sio kumtamkia maneno ya ajabu.
 
Mengi ya aliyofanya hata mama yako mzazi angefanya. Bond ya binti na baba yake huwa inakuwa kubwa kiasi cha kuanza kutiliwa shaka na mama. Wanawake wengi wanakuwa na wivu na huu uhusiano wa binti na baba yake.

Kama umeolewa na una mtoto wa kike hili utalishuhudia wazi. Akivunja ungo na kuota vimatiti uhusiano wa karibu haufi. Na binti anaongeza kiburi zaidi. Utaomba chochote utapewa na kupewa muda zaidi kuliko yeye. Hapo ndio utaanza kuona wivu wa mama kuelekea binti yake na kuanza kukuhisi unaliwa. Sio mama wa kambo tu hata mama mzazi
 
Yaa maneno ya mzazi huwa yana umba hutakiwi kumtamkia laana mtoto hata kama atakuwa amekosea, mtoto akikosea inatakiwa kumtia bakora kumrudisha kwenye mstaari na sio kumtamkia maneno ya ajabu.
Hakika mkuu maneno siyo mabaya hayafai kumtamkia mtoto
 
Mtoa mada anajifunga mwenyewe halafu anataka ahurumiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…