Siwezi kusahau haya manyanyaso ya mama wa kambo

Kusamehe mtu aliyetengeneza donda moyoni si kazi ya muda mfupi ndugu yangu.

Anahitaji mtu sahihi wa kumweleza na mengine mengi aliyoyapitia.ninaimani siku akijaribu kufanya hivyo atalia sana basi na hapo ndio utakuwa wakati wake sahihi kwa kulia sana bila kubembelezwa anyamaze kulia,taratibu ataanza kupata ahueni mazungumzo ya kusamehe yataanzia hapo na kidogo kidogo atajikuta anaachilia vitu.

Hakika Mungu amtie nguvu aise vinginevyo itaathiri baadhi ya vitu😌
 
 
Hii sikubaliani nayo kwa maana mimi sikuwa na huo ukaribu wa kutisha mzee
 
Asante sana mkuu ngoja nianze kutafuta mwanasaikolojia
 
Mimi huyu baba angu alikuwa kashikwa akili na mkewe kabisa, yaani unamwambia anasikitika tu na hafanyi kitu, anaona kabisa matusi kama hayo tunatukanwa lakini hafnyi kitu
Katika viumbe ambavyo tunapaswa kuviombea sana basi ni Mwanaume.Awe baba,kaka,mtoto,mjomba..hawa viumbe wanapitaga kwenye mambo mengi na magumu na kwa bahati mbaya sana si viumbe rahisi wa kusema yanayowasibu💔.

Mwanaume yeyote akitekwa ufahamu amekwisha.msamehe baba yako.Tuwaombee mno
 
Mwanzoni umesema mambo yalienda sawa ila yalikuja kubadilika ulipobalehe na kuanza kuwa na tabia za ukaidi kwahy tatizo ni wewe
Mwanadamu kwa asili ni mbinafsi sana.hakuna mtu asiyejua kuwa wakati wa balehe kuna vitabia huwa vinaibuka ninauhakika angekuwa mwanae kuna adhabu na maneno makali asingemtamkia mwanae.

Kwa upande wako Binti Sayuni03 hii stori unayotupa leo ipo siku itakufikisha sehemu ambayo ilikuwa ni lazima upitie hayo mateso ili ufike ulipokusudiwa.

Praise the Lord..
 
Nadhani wewe ndio umeanza hizo shida, angalia sifa ulizomwaga hapo juu, kwahiyo tabia zako ndio zilimbadilisha mama wa watu, akaona akicheka na nyani atavuna mabua. Na hakuna mahali umesema kuwa wewe ulikuwa mtoto mtiifu, bali kiburi, jeuri mbavyo mpaka leo unavyo
 
Siyo kweli mkuu, mimi siyo muandishi mzuri hivyo mengine sijaandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…