Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Kam Sera yako ni Hakimi Kucheat sasa Naludisha Swali kwako, una uhakka Mke wa Hakimi alkuwa Hacheat ?

Suala la Pili Hawa wanawake wa sasaivi ukijifanya Mkweli sana kwny mambo yako utaumia.

Nadhan Kam Hakimi asingekuwa ametumia akili kubwa kam aliyotumia ,..... Leo hii yamkini Post yako ingekuwa ni Kuwalaumu Wanawake na Kuwashauri vijana kuchagua mwanamke Sahihi.

Ila kwasababu karata imegeuka leo mnaona Hakimi kakosea sana, inshort Bro naona saiv Upo kweny Penzi zito sana maan nyuzi zako kadhaa za nyuma sku hzi unawatukuza sana Wanawake ila hivi viumbe Hiyo Formula ya Hakimi ndo Inapaswa iwe Njia ya kujilinda na Ushetani wao. HONGERA HAKIMI

UZI TAYARI
 
Mi nadhan umeandika porojo la kutosha:;
Hivi wewe ni dini gani mpaka umpende mkeo zaidi kuliko mama yako aliyekuzaa?

Sisi waislam dini yetu imetuusia tumpende mama mara 3 zaidi ya baba mara 1, uyo mke ata hakutajwa kabisa katika hiyo khadithi

Kama Hakimi alikuwa mtu mbaya katika hili sakata ni kwa nini mwanamke baada ya kudai talaka alifungua kesi Mahkaman kudai kugawana mali? Kwa nini kwa wema wake alionao baada ya kwisha kudai talaka hakusubiri uungwana kutoka kwa Hakimi ambaye amemzalia watoto?

Ndio, kwa sababu ugavi wa mali ni issue nyengine na talaka ni kitu chengine

Kwa msingi huu ni wazi huyu mwanamke She went for it., lengo lake na tamaa zake ata sikuachwa lakini ni mali na utajiri wa Hakimi ambao ni wazi ulikuwa unamdedemkia mate,

Wanawake kama hawa hata bongo wapo tele kila siki tunasikia wamewaua waumw zao wapate mali, izo kesi zipo tele hazina idadi.,

Lazima uelewe wanawake ni maumbile yao kutaka mali na utajiri wakat hawapendi kujituma, they are after their husband, they demand alot, sio Africa tu ni kote ulimwenguni
 
Ww jamaa mbona siku hizi una andika chenga.
Yaani nimpende mke ambaye tumekutana ukubwani na ambaye kesho ataniacha na kwenda kwa mwanaume mwingine kuliko mama yangu aliye nizaa ,kunishomesha na kunipa maarifa?

Mke na mama kila mtu atapedwa kwa nafasi yake lakini mama ana nafasi zaidi ya mara kumi mbele mke wangu.

Katika ulimwengu huu hakuna kitu chenye thamani kama mama na baba yako chochote utakacho kifanya hilo unatakiwa kulitambua.
Wazazi wana thamani kuliko hata watoto wako.
 
Andiko lako ni batili lote kwa kesi ya Emanuel ebou na sakata la bill gate yaani mpaka wanaume kweli wanaona hakimi kamuonea binti kwani kumpenda mama kuliko mke kuna shida gani,
Je unaijua historia ya hakimi na mama yake mpaka kaamua kufanya hivyo.

Wanaume tunasafari ndefu sana ndio maana tunakufa mapema.
 
Mdau leo kazingua sana hili andiko halina uhalisia wowote.
 
Unaweza ukawa sawa kiasi ila si sahihi mnoo.Halafu,huyo muomba talaka si binti kwa umri wake.Ni vema ukamtambulisha vema.
 

Kitendo cha Mwenza kutompenda MKE au Mume wake huo tayari ni Utapeli.
Kama kuna mtu unampenda kuliko Mkeo ya Mumeo basi jua unatenda isivyohaki na ndoa haikuhusu.

Ndio maana wadau WA kataa ndoa wanahoja kwani ndoa zenye fikra za namna hiyo ni Utapeli, dhulma na upigaji.

Hata MKE Kam hampendi mumewe, au kuna MTU anampenda kuliko mumewe basi huyo NI tapeli na ndoa haimfai.
 
Aache sifa za kutaka kugawana mali za Mwanamke, anaweza pigwa na kitu cha ncha kali ndio ikawa kwaheri.
 
"Mwanangu hakuniambia kuhusu uhamisho wa pesa" - Mama wa Hakimi afichua

Kujibu uvumi kwamba utajiri wa mwanawe umehamishiwa kwenye jina lake, mama wa Achraf Hakimi, Saida Mouh, amesema hakuwa na habari ya uhamisho kama huo lakini amesisitiza kwamba ikiwa mwanawe hajafanya hivyo, hataweza kuachana na Hiba Abouk.

Mouh aliiambia vyombo vya habari vya Morocco kwamba Hakimi hakuwa amemweleza chochote kuhusu hali hiyo, na kwamba "ikiwa amechukua hatua yoyote ya kujilinda, sina habari nayo."

Mama wa Hakimi aliendelea kusema, "Kuna tatizo gani ikiwa habari ni kweli? Ikiwa mwanangu hafanyi hivyo, hataweza kuachana na mwanamke huyo [Hiba Abouk]."

Kulingana na ripoti za hivi karibuni, Abouk hatapata chochote kutoka kwa utajiri na mali ya Hakimi kwa sababu kila kitu kimeripotiwa kwenye jina la mama wa mchezaji huyo wa soka kutoka Morocco.

Makala ya habari ya Kihispania Marca iliripoti siku ya Ijumaa, Aprili 14 kwamba Abouk alikuwa akihitaji nusu ya mali na utajiri wa Hakimi lakini aligundua kwamba hana kitu chochote kwa jina lake.

Kulingana na chanzo hicho hicho, mama wa Hakimi amekuwa akipokea mshahara wake kwenye akaunti yake ya benki kwa muda fulani, na yeye ndiye mnufaika pekee wa mapato na utajiri wake.

Haki ya kucheza kimataifa wa Morocco na beki wa kulia wa PSG pamoja na mwigizaji wa Kihispania-Tunisia Hiba Abouk walitalikiana mwezi uliopita.

Hakimi ni mmoja wa wachezaji ghali zaidi barani Afrika na anachukuliwa kama mmoja wa mabeki bora wa kulia duniani. Mnamo mwaka 2022, Kituo cha Kimataifa cha Masomo ya Michezo (CIES) kilimtaja mchezaji huyo kutoka Morocco kwenye orodha yake ya wachezaji 100 ghali zaidi kwa thamani yake ya uhamisho iliyokadiriwa.

Data iliyochapishwa mnamo 2022 na tovuti ya habari za soka ya GiveMeSport ilionyesha kwamba beki wa kulia wa PSG ni mchezaji wa soka wa Afrika anayelipwa vizuri zaidi wa sita, akipata zaidi ya dola za Marekani 215,000 kwa wiki.
 
Duuh! Naona bado sakata linaendelea.

Kwa hali hii tutayasikia mengi kuliko tulivyotarajia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…