Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

Somo la mali kwa wanandoa kwa kilichotokea kwa Achraf Hakimi na mkewe

-wewe ulipata division ngapi shuleni?
-cpa inasaidia kwenye uchambuzi, ndio maana wewe ulikuwa hujui maneno haya "when granting or subsequent to the grant of decree of divorce " haya maneno umeyashindwa kuyajua maana yake,
  • hakuna sheria ya kumuhudumia former husband/wife, wakati nimekupa kifungu Cha 115, soma na 120, au huelewi?
  • kama Mimi maandishi yangu ni ya kijinga mbona maswali yangu yote umeyashindwa inamaanisha labda ww ni mjinga zaidi?
-ndiyo nimekufundisha Kwa sababu nilikuuliza swali, la Tools of statutory interpretation ukashindwa na ukaomba nizitaje nikataja, Sasa hapo Mimi na wewe Nani mjinga zaidi?

Wewe ni mjinga Kwa sababu hizo tools zako nimeshakutajia lakini Kwa vile uelewa wako Mdogo hujaona hata principle moja ya statutory interpretation. Ni wale mnaokariri vitu ndio maana unataka nikutajie kama mtoto wa darasa la Kwanza.

Nilikuuliza swali unafikiri ni Kwa nini Busara inatumika kwenye sheria? Lakini Kwa vile Akili yako ni ndogo hujajua jibu la swali hilo ni sehemu ya hizo Principles of Statutory interpretation.

Nakuambia kama ungekuwa Wakili hizi kesi ungeshindwa Kwa sababu umekariri sheria kama Kasuku.
Nilikuambia sheria ni zaidi ya zilivyoandikwa
 
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense.
Duuu! Ndugu mahakama inaangalia umiliki
 
Wewe ni mjinga Kwa sababu hizo tools zako nimeshakutajia lakini Kwa vile uelewa wako Mdogo hujaona hata principle moja ya statutory interpretation. Ni wale mnaokariri vitu ndio maana unataka nikutajie kama mtoto wa darasa la Kwanza.

Nilikuuliza swali unafikiri ni Kwa nini Busara inatumika kwenye sheria? Lakini Kwa vile Akili yako ni ndogo hujajua jibu la swali hilo ni sehemu ya hizo Principles of Statutory interpretation.

Nakuambia kama ungekuwa Wakili hizi kesi ungeshindwa Kwa sababu umekariri sheria kama Kasuku.
Nilikuambia sheria ni zaidi ya zilivyoandikwa
  • twende taratibu, umenitajia tools ngapi? , Na Mimi nimetaja tools ngapi?, Na je ulitaja baada ya Mimi kuanza kuzitaja, ulianza kuzitaja wewe?, Mimi ndiye niliyeanza kwa kukuuliza swali kuwa, unazijua principles of statutory interpretation, ukasema huzijui Mimi nikaja nikakutajia kitu kinaitwa literal rule na intention of the legislature au umesahau? Na ndiyo na wewe ukaenda ukaGoogle ukaleta principle of mischief ambayo kimsingi ni marudio ya hoja yangu, au umesahau, infact ulikuwa hujui statutory interpretation, Kwa sababu hata sheria ya tafsiri ya sheria ulikuwa huijui, ungekuwa unaijua ungeweza kuzitaja Principles of statutory interpretation haraka, bila kusubiri Mimi nianze kutaja,na kuchambua,
  • kwani Mimi Toka awali nilikuwa nanukuu kifungu kikitumia lugha gani? si kifungu kimesema the Court may, na nikakwambia hiyo ni discretion kwa kuangalia mazingira Fulani Fulani au umesahau, au Kati ya Mimi na wewe nani ambaye aliyeleta hoja ya discretion? unakumbuka mwanzoni msimamo wako ulikuwaje kuhusu maintenance Kwa former wife?
-mimi na wewe nani amekariri sheria?, Wewe unayeelewa mbona ulishindwa kujua tools of statutory interpretation?, Mbona ulikuwa hujui Sababu za kuvunja ndoa zote?, Mbona ulikuwa hujui kifungu Cha 115, na 120 vinasemaje?, Kama wewe unajua sheria mbona haya maneno yamekushinda " when granting or subsequent to the grant of decree of divorce" nimekuuliza zaidi ya Mara tano umeshindwa? hii tafsiri yake nini? Kama unaelewa sheria si ungetoa tafsiri ya hicho kifungu
 
😂😂😂
Sasa unakubali alafu muda huohuo inakataa.
Kama Mahakama zinaangalia utamaduni kama Sheria ilivyotoa hiyo discretion power Kwa Hakimu au judge ndio nikakuambia huwezi kumhudumia Mtalaka, wapi hauelewi?

Kama ingekuwa ni sheria inayohusu amri ingesema Shall, lakini Kwa vile inahusu busara ya Mahakama kumaanisha wataangalia mazingira ya wenye kesi, na unaposema mazingira unagusa mpaka Mila na desturi, moja Kwa moja ushasema Mtalaka hahudumiwi Kwa maana Mila na tamaduni zetu waafrika hakunaga kitu kama hicho.

Ndio maana nilipokuwa assesment ya kunitakia angalau kesi moja kusapoti hoja yako umeshindwa mpaka saa hii
-sheria imesema the court may order when granting or subsequent to the grant of decree of divorce? hayo maneno umeyaelewa? Mahakama inaweza, Kwa kuangalia mazingira Fulani Fulani, Sasa hapo kipi Huelewi? inaangalia mazingira Fulani Fulani ndiyo itoe hiyo amri, na Mimi tangu awali ndiyo ulikuwa msimamo wangu wa Kisheria,
-kama hicho kitu hakipo au hakiruhusiwi, Kisheria sheria ingesema "The court shall not order grant order when granting or subsequent to the grant of decree of divorce" , sheria ingepiga marufuku expressly, Kwa kuwa hicho kitu Cha maintenance kinawezekana kwenye mazingira Fulani Fulani basi mahakama inaweza, na ndio maana kifungu Cha 120 kimesema matunzo yatakoma pale tu former husband/ wife anapoolewa, umeelewa?
- Unapotaka nikuwekee Kesi hapo ndio unapoonyesha hujui sheria, Iko hivi Kama kitu kimeshasemwa na sheria,na sheria Iko expressly haina haja kwenda kwenye caselaw
 
Nafikiri Mahakama imeweka hicho kifungu kama mtego Kwa mwenza ambaye aidha alivunja sheria Fulani za kiwajibu na kimajukumu kimakusudi.
Na pia imelenga kutoa msaada Kwa mwenza ambaye anaweza kuwa kwenye hali ngumu iwe kimazingara, kiuchumi, au kiafya.

Hata hivyo sheria hiyo ni ngumu kufanya kazi Kutokana na sababu kuwa MTU akiachwa wengi wao huingia katika mahusiano mengine, na hapa ndipo Watu hawatakubali kuhudumia mtalaka( mwanaume au Mwanamke) ambaye yupo katika mahusiano na MTU mwingine hata kama hajafunga naye Ndoa.

Ingawaje sheria Vifungu vya Chini vinaeleza kwenye Duration of Maintenance Ipo katika namna mbili, mosi, aidha Kwa kifo (,Mtalaka anapokufa, lakini sababu ya pili, ni Akiolewa au kuoa tena, basi huo ndio utakuwa mwisho wa kumhudumia.

Sasa kama sababu inayoweza kuvunja ndoa ni Adultery, basi sababu hiyohiyo inaweza mpelekea Mtalaka asihudumiwe Baada ya kuachana.

Huwezi hudumia mwenza anayelala na MTU mwingine. Hiyo sheria ya hivyo haipo
Hivi kwa ulichoandika hapa ni kwamba umekubaliana na kile alichokuwa akikisema Balensiaga kwamba mtalaka anaweza kuhudumiwa au? Binafsi sikujua kwamba wewe ni mbishi wa kiwango hicho.
 
Nilikuambia Mimi ni mtaalamu wa Lugha lakini sio haimaanishi mtaalamu wa Lugha ya kisheria.

Mtalaka ni Mwanamke aliyewahi kuolewa akaachika au kuachwa.
Zamani alikuwa ni MKE lakini sasa sio MKE na Hana Haki za Mke.

Sifahamu Mkuu, Ila Kwa faida ya wengine eleza Kwa ufupi ni nini, alafu hakikisha iwe inahusiana na tunachojadili.
-hapa ulikiri kuwa hufaamu principles of statutory interpretation?! Si umeona? Umekiri kabisa Kwa kuandika "sifahamu mkuu"
 
  • kutoa istilahi kwenye sheria ni kiashiria kuwa unajua sheria, na ukikosea tu neno Moja kulitafsiri hapo unakuwa unapoteza maana halisi ya kifungu Cha sheria, ndiyo maana hapo awali nikakwambia maneno 'The Court may' maana yake hiyo ni hiyari au ni Mapenzi ya Mahakama, ingesema 'the court shall' maana yake Hilo jambo ni Lazima, na nikakupa na Sheria kabisa inaitwa The statutory interpretation Act, ukiingia huko ndiyo utakuta maana ya hayo maneno madogo madogo ambayo wewe unataka kuyapuuza wakati yana Umuhimu mkubwa kwenye statutory interpretation, ni Mimi ndiye nimekufundisha maana ya hayo maneno ulikuwa hujui, kama Mimi nitapoteza Kesi basi wewe hoja zako zote hazitaingizwa kwenye kumbukumbu za mahakama kabisa, Kwa sababu hazina authority i.e kifungu Cha sheria au Kitabu chochote Cha Kisheria i.e book of authority,
  • kumbe Hata principles za statutory interpretation huzijui, umeonyesha hujui hata unachosimamia Ili utafsiri sheria huwa zinatumika principles, Intention of the legislature nk, itabidi ujiulize kuwa Kwa Nini Bunge limesema hivi when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce Kwa Nini Bunge litunge hiki kifungu Cha sheria i e s.115 of sheria ya Ndoa, hiyo inaitwa intention of the legislature, kumbe hata principles of statutory interpretation huzijui,na ndio maana huelewi unachoambiwa, ukiongeza na kutokujua Lugha ya Kisheria.
  • kama wewe ni mtaalam wa Lugha mbona haya maneno yamekushinda _ when granting or subsequent to the grant of a decree of divorce_ ? Nimekuuliza zaidi ya Mara tatu, lakini umeshindwa Kujibu na umekubali kule juu.
-
- hapa ndiyo nilianza kutaja majibu Kuhusu principles of statutory interpretation!, Umeona? Sasa Mimi na wewe nani mjinga?
 
Hakuna Sheria ya kutunza MWANAMKE uliyeachana naye.

Alafu wanandoa wakiachana neno MKE na Mume linaondoka automatically. Ndoa ndio inamfanya MTU kuitwa Mume au MKE.

Wanao tunzwa ni Watoto tena wenye umri Fulani
- hapa ulisema hakuna sheria ya kumtunza Mwanamke uliye achana naye, huu ndiyo ulikuwa msimamo wako, lakini nikaja nikakupa kifungu Cha 115, na 120 kinachosema ukomo wa maintenance?
 
Hakuna sheria yoyote Duniani ya Aina Hiyo.

Kama Ipo hata nchi yoyote iweke hapa.

Anayehudumiwa ni MKE wa Ndoa, mkishaachana hakuna kitu kama hicho,
Hapa ulisema hivi, "Mkishaachana hakuna kitu Kama hicho" wakati kifungu Cha 115 miongoni mwa mambo kinasema "when granting or subsequent to the grant of decree of divorce ", kifungu Cha 120 kinahusu ukomo wa maintenance,
Msimamo wako ulikuwa 'mkishaachana hakuna kitu Kama hicho "
 
  • umejiona usivyojua Sheria 😀
  • ndio maana Sheria ikatumia maneno ' the court may order ', ikamaanisha sio lazima ni hiyari ya Mahakama, s
-kwenye kutafsiri sheria tunasoma kifungu Cha sheria kwa ujumla wake, Kwa sababu huwezi kusema kutenganisha tafsiri ya kisheria kwenye kifungu kimoja Cha sheria chenye subsections nyingi
- hapa nikaanza kukufundisha matumizi ya maneno "the court may"
 
Bwana Bashir Yakub ukaona ile ni fursa ili uwapige pesa wabongo wajinga sio?! 😃😃😃

Fanya kazi kwa bidii upate pesa yako ya halali, wacha utapeli utapeli... sasa kuweka namba yako hapo maana yake ni nini?!
 
Ndio maana nikasema sheria huzijui, unaposema mazingira Fulani Fulani ambayo sheria haijayataja unamaanisha ndio hiyo Discretion ya Mahakama?😀😀

Hakuna kitu kama hicho.
Sio jukumu la mwanaume au Mwanamke kujua Hali ya Mtalaka wake, Ila ni jukumu lake kuangalia Hali ya Watoto wao.
Unazungumzia mawazo ya kijiweni tena ya Mwaka 47 Huko.

Hiyo shall au may au discretion ninaweza kutokujua maana yake katika Muktadha wa sheria.
Bahati nzuri ni mtaalamu wa Lugha hivyo najua kila neno linaweza kuwa na maana Fulani kulingana na Muktadha. Hivyo upo sahihi.
Hapa ukasema hivi, "hiyo shall au may au discretion ninaweza kutokujua maana yake katika muktadha wa Sheria" hapa ulikiri Kuwa maneno shall, may na discretion yanaweza yakawa yanakushinda! Umekiri kuwa hujui Sasa hapa Mimi na ww nani mjinga?
 
Bwana Bashir Yakub ukaona ile ni fursa ili uwapige pesa wabongo wajinga sio?! 😃😃😃

Fanya kazi kwa bidii upate pesa yako ya halali, wacha utapeli utapeli... sasa kuweka namba yako hapo maana yake ni nini?!
Awapige pesa, kuwa na adabu huyo ni Wakili, na kazi ya uwakili ni kazi yenye heshima kabisa, na ndio maana Uwakili unapewa/ unaapishwa na Jaji Mkuu, kama Rais anavyoapishwa na Jaji Mkuu
 
Hichohicho kifungu cha 115 hujakisoma chote, hujakielewa, umesoma 115 kifungu kidogo cha cha Kwanza Roman d,e,f. Umeacha kifungu kidogo cha pili na cha tatu.
Ndio nikakuambia soma hiyo sheria kuanzia 115, kisha 116, mpaka 120, ndio utajua kuwa hiyo sheria inasema nini na inalenga nini?

Nimeshakuambia sheria ni Lugha, sasa kama Lugha inakupiga chenga huwezi sema unajua sheria. Waulize waliosomea hizo sheria wakuambie.

Nikakueleza kuwa hiyo sheria nusunusu uliyoitoa inayomtaka ATI mwanaume kumhudumia Mtalaka wake(Mwanamke aliyewahi kumuoa) inaendelea section ya 2 ambapo pia inatamka kuwa mamlaka itaweza kumshinikiza Mwanamke kumhudumia mumewe au Mtalaka wake wa kiume ikiwa hiyo mwanaume hajiwezi iwe jumlajumla au namna fulani.

Nikakuambia hilo Jambo haliwezekaniki, zingatia sheria Mahakamani pia zinaangalia utamaduni wa jamii walizotoka Watu. Sasa wewe unasoma Vifungu kama Kasuku, hauelewi unapoambiwa kitu kuwa Jambo Fulani haliwezekaniki, hasa katika jamii zetu za kiafrika.

Huwezi mhudumia Mtalaka, na kama utamhudumia itatokana na adhabu ya Mahakama kama ulitenda kosa Wakati WA Ndoa. Na ikiwa ni hivyo, huwezi iita hiyo ni Huduma bali itakuwa NI adhabu.

Ni Sawa na umpige MTU aumie alafu Mahakama iamuru umtunze MTU huyo mpaka apone.
Inawezekana vipi sheria kutungwa huku ikiwa imebeba vitu ambavyo haviwezekani kama unavyodai?
 
SOMO LA MALI KWA WANANDOA KWA KILICHOTOKEA KWA ACHRAF HAKIMI NA MKEWE.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Mke wa ACHRAF HAKIMI ameshindwa kupewa mali yoyote baada ya ndoa yao kuvunjika kwasababu Hakimi aliziandika mali zote jina la mama yake mzazi.

Je jambo hili linawezekana kwa Sheria za Tanzania ?.

Ndio linawezekana , ni hivi :-

Kwa wanandoa kuna mali za aina 2;-

1. Mali zilizopatikana kabla ya ndoa.
2. Mali zilizopatikana wakati wa ndoa.

MALI ZILIZOPATIKANA KABLA YA NDOA.

Hizi ni mali ambazo mtu anakuwa nazo kabla hajaoa ama kuolewa. Yumkini akiingia kwenye ndoa anaingia nazo.

Hata hivyo Sheria ya ndoa inasema mali hizi zinahesabika si za ndoa kwa maana ya kuwa huyo mwenye nazo ni zake peke yake bila mwenza wake. Ndoa ikivunjika haziwezi kugawiwa.

Pamoja na hayo, mali hizo pia zinaweza kubadilika na kuwa za ndoa ikiwa mambo mawili yatafanyika.

KWANZA, ikiwa mwenza mwenye hizo mali ataingia makubaliano na mwenza wake kuwa ziwe za ndoa basi zitakuwa za ndoa na itakapovunjika basi zitagawiwa

PILI, iwapo mali umeingia nayo kwenye ndoa lakini kipindi cha ndoa imeendelezwa.

Mfano, Umeingia kwenye ndoa na kiwanja chako lakini kipindi cha ndoa ndo kimejengwa, AU kilikuwa kimejengwa lakini ni pagala tu, kipindi cha ndoa ndo mmemalizia na kuwa nyumba kamili.

Hapa ndoa ikivunjika mtagawana na hautasema alinikuta na Pagala langu au kiwanja changu. Kitendo cha kuendeleza mkiwa wote kinampa haki mwingine na kuwa mali ya wote.

Lakini kama mali ameingia nayo kwenye ndoa na hakuna maendelezo yoyote yaliyofanyika kipindi cha ndoa basi hiyo mali haiwezi kugawiwa ndoa ikivunjika na inabaki mali ya mwenza huyo pekee.

MALI ZILIZOPATIKANA WAKATI WA NDOA.

Hizi huhesabika moja kwa moja kuwa ni za wanandoa wote mpaka isemwe vinginevyo.

Na haijalishi zipo kwenye jina la mke au mme, madhali zilipatikana kipindi cha ndoa basi zinahesabika ni za wanandoa na zinastahili kugawiwa ndoa inapovunjika.

Hata hivyo, ili ziweze kugawiwa ni lazima kila mwanandoa athibitishe mchango wake katika upatikanaji wa hizo mali.

Tafsiri ya mchango ni pamoja na pesa, vifaa, lakini hata kazi za nyumban nao ni mchango katika kupatikana kwa mali.

Mke au mme anayebaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za nyumbani anahesabika amechangia kwa kile kinachopatikana kutoka kwa yule aliyeingia mtaani kutafuta.

Kwahiyo wakati wa kuthibitisha mchango hayo yote yanazingatiwa.

JE MGAWANYO WA MALI NI NUSU KWA NUSU.

Hapana, mgawanyo mali za ndoa inapovunjika sio lazima kuwa nusu kwa nusu. Inaweza kuwa 20%/80%, 70%/30%, 90%/10%, nk nk. Kwa ufupi hakuna kiwango maalum, hata kukosa kabisa kupo.

Kikubwa ni kuwa utapata fungu lako kutokana kiwango cha mchango wako kama tulivyoona hapo juu. Na kama huna mchango kabisa basi waweza kutoka kapa pia.

MALI AMBAZO ZIKO KWENYE MAJINA YA WATOTO.

Mali hizi hamuwezi kuzigawa ndoa inapovunjika. Hii ni kwasababu kitendo cha kuandika majina ya watoto ni sawa na kuwa mlikubaliana kuwapa zawadi watoto.

Ukitoa zawadi maana yake maslahi(ownership interest) yenu katika hiyo mali yalishahama kwenda kwa watoto kwa njia ya zawadi nanyi hamna maslahi tena katika hiyo mali.

MALI ZILIZOANDIKWA MAJINA YA WATU WENGINE.

Mali ambayo haina jina la mke au mme sio rahisi kuigawa ndoa inapovunjika.

Huyu HACHRAF HAKIMI aliandika majina ya mama yake. Mali ya namna hii ni vigumu kuigawa kama mali ya ndoa kwasababu inaonekana inamilikiwa na mtu mwingine.

Kwa msingi huu huwezi kugawa mali ambayo haihusiki. Wengine huandika majina ya ndugu zao, marafiki nk.

Ndio, akifanya hivi basi ni vigumu hiyo mali kuigawa ndoa ikivunjika hata kama una uhakika wa 100% kuwa ni yenu.

Hii ni kwasababu ushahidi wa nani mmiliki wa mali ni nyaraka au usajili. Nyaraka na usajili unaonesha mtu mwingine ni vigumu useme hii mali ni yetu.

MALI INAYOBADILISHWA UMILIKI.

Kama mali imeanza ikiwa ni ya ndoa halaf ikabadilishwa majina hiyo unaweza kuidai na ikagawiwa.

Wapo wanandoa wakiona mambo yameanza kubadilika basi ama huanza kubadili majina ya mali au huuza.

Ikiwa tarehe zitaonesha mali ilibadilishwa au kuuzwa kipindi cha ndoa na ni mali ya wanandoa,na mwenza hakuwa ameridhia, basi ubadilishwaji huo ama uuzaji huo ni batili na hiyo mali itarudishwa kwenye mali za wanandoa ili igawiwe.

WANANDOA WANAWEZA KUFANYA NINI KUHUSU MALI.

KWANZA, yafaa ikiwa mtakubaliana basi mali iwe na majina ya wote mke na mme. Iwe ni gari, kiwanja, nyumba,akaunti benki, nk. Sheria inaruhusu.

Hii husaidia sana hata kipindi cha kifo ambapo mjane au mgane hawezi kusumbuliwa.

PILI, mnaweza kuwa na makubaliano kuhusu kila mali,kuanzia zile ambazo mlikuwa nazo kabla hamjaoana, mpaka zile mtakazopata wakati wa ndoa. Mtakubaliana ipi iwe ya pamoja na ipi iwe ya mmoja.

Japo hili ni gumu kwa maisha yetu sababu ukilianzisha hili utaambiwa HUNA MAPENZI YA KWELI.

TATU, muwe na utaratibu wa kucheki mara kwa mara hadhi(status ) ya mali. Pitia pitia huko Ardhi, TRA, Serikali ya mtaa ujue. Msilale sana.

Huenda ukagundua kitu mapema kabla mambo hayajaharibika.

NNE, msajili/andika mali kwa majina ya watoto, maana yake muwape zawadi watoto. Hata kama mnatumia nyie lakini ikijulikana ni za watoto.

Ila lazima iwe imesajiliwa na sio kusema tu kwa mdomo kuwa hizi ni mali ni za watoto.

Ukisema mali ni za watoto na hakuna usajili rasmi hiyo hukataliwa sababu watoto hawana mali bali mali ni za wazazi na majina zitakuwa zinasoma wazazi.

TANO, kama hamuwezi kufanya lolote mapema kati ya hayo manne juu basi mmoja awe tayari kupoteza au msubiri mahakama iwaamue.

REJEA ya maandiko haya ni :-

Sheria ya ndoa R:E 2019 hasa vifungu vya 58,59,,60, na114.

NA

Shauri la Bi Hawa Mohammed vs Ally Sefu(Rufaa Na.9/1983) TZCA 12.
Asante sana.
Kwanza naomba kufahamu ikiwa mali imeuzwa ndani ya ndoa na fedha iliyotokana na mauzo hayo haitakuwepo wakati wa kugawana mali?

Pili,je, inawezekana kuandikisha mali kwa majina ya watoto kabla ya kufikisha umri wa miaka 18?
 
Waelekeze mkuu! Nashangaa wabongo walivyomkazania hiyo kijana, kutwa ma-post ya hakimi. Na hawa wanaoshabikia huu upuuzi ni vijana wasio na pesa. 🤔
  • Wakili, umezungumzia Kuhusu kuandikisha Mali Kwa majina ya wengine eg Mama Ake Hakimi, na kusema kuwa Hana Mali yoyote (Hakimi), hiyo mahakama iliyoamua Hilo shauri ilitakiwa ijiulize inawezekana vipi mtu mwenye kipato Cha zaidi ya Bilioni 2 asiwe na Mali yoyote? Tuseme alikuwa anatumia zote? Mahakama ilitakiwa ijiulize Mama Hakimi ameweza vipi kumiliki ukwasi wa kutisha i.e hizo Mali kama Nyumba? , Mama Hakimi analipwa Bilioni ngapi , Hadi aweze kumiliki hizo Mali?, Mahakama ilitakiwa itoe amri kwa Hakimi atoe matunzo Kwa mke wake
  • Hapo Hakimi ametumia false pretense
 
Back
Top Bottom