Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Hii nchi utadhani serikali ilishakufa
Mkuu,
Alhamis wiki iliyopita nilipanda kimotco mida ya Saa nane kasoro mchana, (nadhani ile inayotoka arusha), kutoka Dodoma kuelekea Iringa, abiria wenzangu walikalia mabegi yao kwenye kile kikorido cha kupita, wengine walikalia zile "arm rest", na wengine kusimama kabisa, pia yule kondakta alikuwa anaenda siti za nyuma anawaomba wakae watu watatu katika siti zilizotengenezwa kwa ajili ya kukaa watu wawili tu(muundo wa siti za basi hilo ni 2 by 2(2*2)). Na Bado njiani waliendelea kuchukua raia/abiria.Wakati wa kukata tiketi ukiuliza siti zipo wanakwambia zipo za kutosha.

Katika "Traffic Stops" zote kutoka dodoma mpaka ninafika iringa hakuna polisi alieingia ndani ya basi. Mwana usalama pekee alieingia ndani ni afisa wa uhamiaji pale mtera basi.

Haya mambo yapo na yanaendelea.
 
Na nyie abiria mnachukua hatua gani?
Etiee nyie abiaria mnachukua hatua gan.. ??unazungumzia Tanzania ipi Hii ya vi wonder au?? Askar asimamishe gari aingie ndan na asichukue hatua au asimamishe na asiingie ndaniii??
 
Back
Top Bottom