Special thread: Kutana na waagizaji wa magari kutoka Japan
Huyu itakuwa alikutana na mbovu. Subaru siyo gari yenye sifa ya kusumbua labda kama mtu mwenyewe ndo aanze kuisumbua kabla haijamrudi
Ni kweli, subaru sio gari sumbufu. Kikubwa fanya service kwa kutumia recommended oils/fluids. Tatizo watu wengi hawazielewi hizi gari, mtu ananunua ma oil fake, unategemea nini. Mm bibafsi toyota zimenishinda, natumia subaru kwa mda mrefu tu, kwakweli ni gari nzuri sana. Kwa ss naona watu wengi wameanza kuzielewa hasa SH5/SG5.
 
Salam ndugu wadau. Hapa chini ni taarifa fupi ya kilichojiri katika Mkutano wa TBS na Wadau wa Magari

NB: Kimomwe Motors (T) Ltd ni Kampuni ya Kitanzania ya uagizaji magari inayoshirikiana na kampuni za nje zaidi ya 15.


MKUTANO WA WADAU WA MAGARI NA SHIRIKA LA VIWANGO (TBS) TAREHE 10/2/2021

WALIO HUDHURIA SHIRIKA LA VIWANGO (TBS)

1. DR. ATHUMANI Y. NGENYA(DIRECTOR GENERAL)
2. DAVID NDIBALEMA (DIRECTOR OF STANDARD DEVELEPMENT)
3. LAZARO MSASALAGA (DIRECTOR OF QUALITY MANAGEMENT)
4. VIOLA MATERN MASAKO (DIRECTOR OF HUMAN RESOURCE MANAGEMENT)
5. YONA AFRICA (STANDARD MANAGER)


WADAU WA MAGARI NA WENGINEO WALIO HUDHURIA


1. KAMPUNI ZA KUAGIZA MAGARI (45)
2. KAMPUNI CLEARING AND FORWADING (22)
3. WAANDISHI WA HABARI
4. GARAGE

MADA ILIHUSU MABADALIKO YA MFUMO WA UKAGUZI WA MAGARI KUTOKA NJE YA NCHI NA KUFANYIKIA HAPA NCHINI.

Mfumo ulio tumika hapo awali ulitambulika kama Pre- Shipment Verification of Conformity (PVOC) na mfumo tutakao tumia hapa nchini kwa sasa katika ukaguzi ni ule wa Destination Inspection (DI).

Serekali ilitoa maagizo kwa Shirika la Viwango (TBS) kuwa gari zote kwa sasa zinatakiwa kukaguliwa hapa nchini,na hii ni kutokana na maoni ya wadau mbalimbali waliokuwa wakihudhuria vikao kuomba ukaguzi wa magari ufanyike hapa nchini.

Kila nchi ina uwezo wa kuamua kufanya ukaguzi kwa namna wao wanavyoona inafaa, hivyo basi Shirika la Viwango (TBS) limeamua kufanya ukaguzi wa magari yote yatakayo kuwa yanaingia hapa nchini katika bandari ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 01/03/2021 ambapo ndio utakuwa ukomo wa mkataba wao na mawakala wao wanao husika na ukaguzi wa magari kwa nje ya nchi.

Hivyo basi gari zote zitakazo agizwa kuanzia tarehe 01/02/2021 hadi tarehe 28/2/2021 zitakaguliwa huko huko nje na si hapa nchini, isipokuwa gari zitakazo agizwa kuanzia tarehe 01/03/2021 ndizo zitakazo fanyiwa ukaguzi hapa nchini

Ili kuepuka usumbufu, hakikisha gari yako inakaguliwa katika hizo tarehe tajwa hapo juu kabla hujaisafirisha kwani endapo itakuja bila kukaguliwa basi utatozwa faini ambayo ni asilimia 30% (C&F) ya garama za mananuzi ya gari na kisha kukaguliwa hapa nchini. Magari yoye yanatakiwa kukidhi kiwango cha kitaifa (TZS698:2012)

Changamoto za PVOC
  • Ukosefu wa ufanisi kwani kuna usumbufu wakati wa mchakato mzima wa kulifikisha na kukagua gari kwenye kituo cha ukaguzi
  • Gharama kubwa za ukaguzi na upimaji wa bidhaa kwa utaratibu wa PVOC
  • Mawakala kutokuwa na ofisi za ukaguzi maeneo yote, hivyo kuchelewesha huduma za ukaguzi na upimaji.
  • Baadhi ya bidhaa zinazosafirishwa kuja hapa kuwa sio zilizopimwa
  • Ugumu wa kuwahudumia wajasiriamali wadogo wanaonunua bidhaa nyingi za aina mbalimbali ambazo thamani yake ni ndogo.
  • Upotevu wa fedha nje ya nchi kwani zingelipwa hapa zingeleta manufaa kwa maendeleo ya nchi.
  • Upotevu wa ajira kwa wananchi, na nchi kushindwa kujenga uwezo yaani miundombinu ya ukaguzi na wataalam wa ukaguzi
  • Mawakala kushindwa kufanya ukaguzi inavyostahili

Ukaguzi kuanza tarehe 01/03/2021
  • Magari yatashushwa kwa utaratibu wa kawaida kutoka kwenye meli na kuegeshwa kwenye eneo lililopangwa
  • Wakala wa forodha /muagizaji atafanya maombi ya ukaguzi wa gari katika mfumo wa TBS na kufanya malipo kabla ya ukaguzi
  • Wakala/muagizaji atafanya taratibu zote za kiforodha na kuzikamilisha
  • Ukaguzi wa gari utafanyika kama hatua ya mwisho ya utoaji wa gari bandarini.
  • Cheti cha ukaguzi pamoja na Cheti ha Ubora (CoR) vitatolewa katika mfumo uliotumika kuomba kufanya ukaguzi.
  • Cheti hicho kitatumika na mamlaka husika katika kuondosha gari bandarini.
  • Gari ambalo halitakidhi matakwa ya kiwango,litaruhusiwa kuondoshwa bandarini kwa masharti maalum na baada ya matengenezo litapimwa katika yadi ya UDA.
  • TBS imeagiza mitambo ya ukaguzi wa magari ambayo inatarajiwa kuanza kuwasili mapema mwezi wa pili kwa ajili ya kufungwa katika maeneo ya ukaguzi
  • Mitambo 11 itafungwa bandarini na mtambo mmoja utafungwa nje ya bandari (UDA) kwa ajili ya ukaguzi wa magari baada ya matengenezo.
  • Wataalam zaidi ya 45 wamesha andaliwa kwa ajili ya kuanza ukaguzi .

TPA imetenga maeneo katika yard zifuatazo

Ro-ro (seti 9 kwa magari madogo)
Copper yard (seti 1 kwa magari makubwa)
Lighter quay yard (seti 1 kwa magari makubwa)
Aidha,seti 1 itafungwa uda.


Hitimisho
  • Wito unatolewa kwa wadau wote kutoa ushirikiano kwa TBS ili kufanikisha utekelezaji wa ukaguzi hapa nchini.
  • Tunafahamu kuwa changamoto zitakuwepo hususani mwanzoni mwa utekelezaji
  • Kampuni za uagizaji tunapaswa kuzingatia ubora wa viwango wa gari wa tutakazokuwa tunaagizia wateja, kwani kampuni zitakazo bainika kuwa zinaagiza magari mabovu bila kuzingatia ubora zinaweza futiwa leseni.
  • Wateja wanashauriwa kutumia makampuni yaliyo sajiliwa na kutambulika na serekali na si kuagiza wao binafsi.
  • Gharama ndogo ndogo za matengenezo zitakuwa kwa mteja mfano: Tairi kama ni za kubadilisha, wheel balance, taa kama zinakuwa hazimuliki vizuri n.k
  • Sisi kama kampuni tutawajibika pale tu kuna kitu ambacho mteja ulikiona kwenye gari lako na hukukikuta au gari lako limekuja lina damege wakati linaagiza lilikuwa halina.
  • Sisi kama kampuni tutahakikisha gari za wateja wetu wote zinakuwa katika ubora kama ni changamoto basi ziwe hizi ndogo ndogo.

Ahsanteni kwa kuendelea kutukuza kwa namna mbali mbali ikiwemo mawazo na hata waliochagua kuagiza nasi. Tunatazamia kuendelea kuboresha huduma zetu siku hadi siku ili kutii kiu za wateja wetu.
 
KIMOMWEMOTORS ,

Tukiagizaga nje mara nyingi kwa gari ndogo ndogo gharama hua ni "Fixed Cost" ya $300/Gari. Sasa hapa je itakua vary kulingana na problems zitakavyokua detected au?
 
Gharama za ukaguzi zikoje
Gharama ni dola 140 boss
KIMOMWEMOTORS ,

Tukiagizaga nje mara nyingi kwa gari ndogo ndogo gharama hua ni "Fixed Cost" ya $300/Gari. Sasa hapa je itakua vary kulingana na problems zitakavyokua detected au?
gharama za ukaguzi kwa hapa nchini zitakua nafuu kidogo...ni dola 140 fixed boss.
Gharama za ukaguzi zikoje na muda gani zinachukua kukaguliwa?
inagharim dola 140 na zoezi husika halizidi masaa mawili.
 
Back
Top Bottom