Special thread: Kutana na waagizaji wa magari kutoka Japan
'vifaa au vipuli vyake vinakufa baada ya matumizi ya mda mrefu ikilinganishwa na gari za juu juu za Toyota.'

Uongo ndio uko hapo,ni nani amenunua spare parts org za toyota na akaona kama vipuri vyake havikai muda mrefu kulinganisha na vya Nissan?
Boss tembelea garage uzungumze na mafundi wakueleze wateja wao wengi ambao ni sisi watanzania tunanunua spare za daraja lipi!! Hizo OG unazosema wanaonunua wengi ni mashirika au serikali. Gari kama Mazda, Nissan na Mitsubishi hawana spare za daraja la chini ndio sababu vifaa vyao vinakua juu kidogo kuliko Toyota mwenye daraja la chini, kati na juu....watanzania wengi tunakimbilia hizo za chini kabisa na matokeo yake vifaa havidumu
 
Mkuu Spare parts fake za Nissan umeziona ngapi mtaani?
 
Boss tembelea garage uzungumze na mafundi wakueleze wateja wao wengi ambao ni sisi watanzania tunanunua spare za daraja lipi!! Hizo OG unazosema wanaonunua wengi ni mashirika au serikali. Gari kama Mazda, Nissan na Mitsubishi hawana spare za daraja la chini ndio sababu vifaa vyao vinakua juu kidogo kuliko Toyota mwenye daraja la chini, kati na juu....watanzania wengi tunakimbilia hizo za chini kabisa na matokeo yake vifaa havidumu
Mkuu nikusahihishe kidogo...kwa sasa Nissan spea feki zipo za kumwaga kwa sababu na zwnyewe zimeanza kuwa nyingi mtaani...
Wiki iliyopita tu nimefunga shockup ya kichina kwenye nissan...nimeinunua 60k..

Kuna watu wa extrail nimeona wamefunga shockup za kichina pia..

Angalizo......Wamiliki wa magari ya Nissan wanaibiwa sana siku hizi wakidanganywa Nissan hazina spea feki..

Ninakiri zipo....hata ukitaka oil filter ya 3500 zipo...
People, watch out..

Sasa hivi Nissan zimekuwa affordable kuzi"maintain kwa watu wanaoishi miji mikubwa...

Nanunua ball joing ya Nissan 25k..[emoji119][emoji119][emoji119]..mchina huyu sometimes anatuokoa..
 
Mkuu Sorry,hv kodi ya TRA kwenye gari inapokuwa ni kubwa kuliko CIF kwa zaid ya 1M+,Je,mteja ana option yoyote ya kupata punguzo la kodi ya uagizaji wa gari kwendana na uzoefu wako?
 
Mkuu Sorry,hv kodi ya TRA kwenye gari inapokuwa ni kubwa kuliko CIF kwa zaid ya 1M+,Je,mteja ana option yoyote ya kupata punguzo la kodi ya uagizaji wa gari kwendana na uzoefu wako?
Ntatulia nikujibu baada ya kutafakali vizuri unachotaka kujua hapo juu...mda si mrefu sana ntarudi
 
'vifaa au vipuli vyake vinakufa baada ya matumizi ya mda mrefu ikilinganishwa na gari za juu juu za Toyota.'

Uongo ndio uko hapo,ni nani amenunua spare parts org za toyota na akaona kama vipuri vyake havikai muda mrefu kulinganisha na vya Nissan?
Hapo sasa ndio pa kujiuliza..Maana gari ya Toyota ikiwa imefanyiwa mainatanance kabla haijawa shipped ikija inakaa muda mrefu sana kabla ya mavifaa hayajaanza kusumbua. Sababu ubovu wa gari huanza na njia ikiwa rough na madimbwi.

Kama unakaa lami kwa lami kuna gari zinadunda hata miaka 2 we ni kubadili brake na kumwaga oil tu. Na ni gari za Toyota hizi hizi mnazozipondeaga.
 
Haya magari wabongo tunakosea sana, gari ishafanyiwa inspection Japan lakini ikishashuka kwenye meli mtu analipeleka Lumumba kufanya interior design, kufungua dashboard sijui kunyanyua juu, mwisho wa siku gari yako unaichukia balaa maana haina tena fleva zake, ukiendesha km 5 dashboard inawaka
 
Salam,

Hapo chini ni baadhi ya picha za Subaru Forester tulizoagiza na kuwakabidhi wateja wetu walioagiza nasi Kimomwe Motors (T) Ltd kupitia ofisi zetu za Dar na Mbeya

Model hii ya Forester yaani SG 5 ilianzia miaka ya 2002 ikaenda mpaka 2007.

Injini:
Injini yake ina Cc 2000 na nyingine 2500. Zipo zenye Turbo na ambazo hazina turbo. Mara nyingi unashauriwa kupata hii ya Cc 2000 isiyo na Turbo kwa kua hii ya kawaida ina matumizi madogo ya mafuta lakini pia nguvu yake bado ni kubwa na hivyo kuipa gari mwendo huku ukiepukana gharama za Turbo. Cc 2000 kwa wastani inaenda kilomita 12.2 kwa lita wakati Noah inaenda kilomita 10. 5 kwa lita.

Vifaa
Kwa sasa tofauti na zamani vifaa vimekua vingi kwa bei za wastani lakini pia uimara wa vifaa hivi ni mkubwa tofauti n Toyota

Utulivu
Iwapo kwenye mwendo gari hii imetulia sana tofauti na Rav 4 au Harrier au Nissan Extrail, na unaweza kukata nayo kona ikiwa hata kwenye speed 160.

Gharama
Kwa kuagiza nzuri yenye kilomita chini ya 100,000 itakugharim 12,800,000 mpaka 13,500,000

NB
Mafundi wengi bado hawawezi hii injini, hivyo ikianza changamoto unashauriwa utoe injini yote ufunge nyingine kwa 1,600,000.

Zaidi tupigie kupitia 0746 26 77 40 au 0719 989 222 au Tembelea ofisi zetu za Dar- Magomeni Mapipa na Mbeya- Mwanjelwa Soko Jipya.

32F30915-55B8-4F1F-8278-C215FD75434D.jpeg
2361F0DF-E99F-46FD-A601-0B956B7445C3.jpeg
611A569E-34D8-415A-B7FC-13953DD334C8.jpeg
C9356526-5773-4C2C-828D-6CCC30228EBB.jpeg
AA77E9EB-0BE0-4A70-BE4F-4675978C6B80.jpeg
 
Yenye turbo inakuwa na changamoto gani?Naomba kujua na recommended Oil
 
Kuna jamaa yangu wa bandari aliinunua mnadani bandarini Subaru. Imemsulubu sana, kila jmos garage.
Ok hii Subaru inaonyesha ni nzuri
 
Kuna jamaa yangu wa bandari aliinunua mnadani bandarini Subaru. Imemsulubu sana, kila jmos garage.
Ok hii Subaru inaonyesha ni nzuri

Huyu itakuwa alikutana na mbovu. Subaru siyo gari yenye sifa ya kusumbua labda kama mtu mwenyewe ndo aanze kuisumbua kabla haijamrudi
 
KIMOMWE MOTORS (T) Ltd waagizaji wa magari tunakufahamisha machache kwa ufupi

Injini na Mafuta
Gari hii inakuja na injini 2. Moja ina Cc 1500 na nyingine Cc 1800 zote zikiwa na mfumo wa Hybrid unaowezesha gari kutumia mafuta kidogo zaidi huku umeme ukitumika zaidi.

Injini ndogo ya Cc 1500 inaelezewa kwenda zaidi ya Kilomita 38 wakati injini ya Cc 1500 inaenda kilomita 34 kwa lita.

Utulivu/ Comfortability
Kwa ujumla gari hii ina utulivu wa wastani kama ilivyo kwa gari nyingine za Toyota za saizi yake na hiyo kuiwezesha kwenda mwendo mpaka 140 bjla kuyumba yumba na kwenye njia za vumbi pia ina utulivu wa wastani.

Ziada
Gari hii ina Camera angavu wakati unarudi nyuma, ina options kwenye usukani za kukuwezesha kupokea sim, kubadiri radio na kuzima na kuwasha AC

Vifaa

Vifaa vyake vinapatikana kwa gharama za wastani japo sio kwa wingi sana kwa sababu gari hizi hazijawa nyingi hapa Tanzania kutokana na bei yake hapo awali ilikua juu sana kuliko sasa.

Mafundi
Mafundi wa magari mengine ya Toyota ndio pia hutengeneza gari hizi hivyo mafundi wapo, kwa upande wa umeme kwa sasa mafundi wengi wa umeme wana vifaa vya muundo wa kompyuta inayowezesha kugundua tatizo na kulishughulikia.

Gharama
Kwa kuagiza gharama zote kwa sasa zinaanzia kwenye 13,800,000.

Zaidi tembelea ofisi zetu za Dar es Salaam- Magomeni Mapipa au Mbeya- Mwanjelwa Soko Jipya

Au piga 0746 267740 au 0719 989222.

8A985576-70B1-4C53-A273-53196DA5E1F7.jpeg
EE73F1B1-4941-4F5F-B6B3-1A80B2D307C1.jpeg
82DE0DCE-E712-464F-8290-C34904AF416C.jpeg
7BAA9BD1-C103-4DA2-A900-77B8C014E426.jpeg
AC8C752E-B843-44BB-9330-8F40AF5D1127.jpeg
EE8845F6-840B-47B4-A986-E91EA7D3A187.jpeg
59462720-D344-4C6F-9935-50F5CBC14B55.jpeg
4006D6B9-942C-4627-BCD9-7CB8B1AF50B2.jpeg
B271E605-8B01-45E1-937F-98AFDEA9922C.jpeg
13D70362-237B-4CD2-9411-47B9BEAD98D4.jpeg
24CC81E3-7B35-4C92-9B07-181346E2FB77.jpeg
 
Back
Top Bottom