Special thread: Kutana na waagizaji wa magari kutoka Japan
Inabidi elimu ya kuhusu kuagiza magari itolewe kwa upana zaidi ili watu waelewe zaidi.
Kuanzia hatua za kuagiza,kulipia gari, gari kupakiwa melini, gari ukiwa melini,gari ikifika bandarini, tozo za bandarini na ushuru, utoaji wa gari..
 
Nataka nichangie kidogo kwenye kuagiza mtu anaweza akaagiza mwenyewe au kutumia mawakala kama Befoward au SBT.
Kwenye malipo watu wengi huwa hawana elimu sahihi ni kuwa kama wewe ni mteja wa benki ABC iliyopo hapa Tanzania na unataka kuagiza Toyota Carina na akaunti yako inakiasi fulani ambacho hakijatimia. Benki unayotumia huku ukitaka kulipia kule Japan na pesa yako haitoshi Benki wanauwezo wa kukuandikia Letter of Credit.

Letter of Credit ni barua inayoandikwa na benki unayotumia huku kwa benki ya huko Japan ambayo ni mshirika wake ili kukuwekea wewe dhamana na utapewa muda wa siku kadhaa ila gari itakuwa imepakiwa kuja huku.

Baada ya manunuzi kuna document muhimu kwa ajili ya gari ulilonunua
1.Commercial Invoice
Hii inaonyesha kiwango cha pesa uliyolipia na aina ya gari ulilonunua.

2.Bill of Lading
Hii ni document inayoandaliwa gari ikipakiwa melini kuonyesha nani ni mmliki wa gari na itatumika kupokelea gari na kutolea gari bandarini ili kupata Release Order na Get Pass ya Bandarini.

Pia kuna certification of origin,certificate of inspection.

Hiyo gari ikifika Bill of lading utapewa original na invoice.
 
Kuna gari kama Toyota Rush, Toyota IST, Toyota Raum, Toyota Cami, Toyota Vitz, Toyota, Fun Cargo, Passo, Nissan Note, Nissan March, Subaru Impreza, Pajero Mini, Premio, Terrious Kid, n.k

Mkuu mi nataka TOYOTA RUSH.. How much?
 
Asante Sana mkuu Kwa elimu Pana

Mimi nimeagiza Toyota rumion ya 2008 kupitia SBT Tanzania juzi tarehe 19/08 na baada ya kufanya malipo ya awali (CIF) nilitumiwa email Ile juzi na Jana pia nimepata email kutoka NBC bank kuwa pesa Yangu imeshatumwa....
Tc-v kiboko ya wote. Pesa ikitumwa inazuiwa mpaka mwenye gari Japan aipakie kwenye meli
 
Tc-v kiboko ya wote. Pesa ikitumwa inazuiwa mpaka mwenye gari Japan aipakie kwenye meli
Nilikuwa mwoga bure Tu kama ningejua ningeagiza gari kupitia tradecarview Ila ndiyo hivyo nimeshafanya biashara na SBT Japan pia bado mpaka Leo nasubir nimeambiwa kuanzia tar20 September itakuwa umefika bongo
 
Asante Sana mkuu Kwa elimu Pana

Mimi nimeagiza Toyota rumion ya 2008 kupitia SBT Tanzania juzi tarehe 19/08 na baada ya kufanya malipo ya awali (CIF) nilitumiwa email Ile juzi na Jana pia nimepata email kutoka NBC bank kuwa pesa Yangu imeshatumwa...
Punguza mizuka bwashee, SBT ni waaminifu balaa, hata wakichelewa relax

Bill of lading ile ni kama risiti ya makabidhiano ya gari yako kati ya meli inayobeba na hao sbt

Sasa wewe unatumiwa ile ili uweze kuitrack na kujua gari yako imepakiwa lini ili uanze kujiandaa na mchakato wa kuitoa bandari kavu.

NB. Mfano meli imetekwa au imezama, ( yenye gari yako) hapo ndo utaona umuhimu wa bill of lading coz lazima wewe utalipwa gari yako
 
Punguza mizuka bwashee, SBT ni waaminifu balaa, hata wakichelewa relax

Bill of lading ile ni kama risiti ya makabidhiano ya gari yako kati ya meli inayobeba na hao sbt...
Tatizo kubwa la SBT gari zao nyingi zimeenda km nyingi sana.

Magari mengi wameanza na km 100,000 na kuendelea. Au kukuta gari lenye km 150,000 ni kitu cha kawaida sana.
 
Tatizo kubwa la SBT gari zao nyingi zimeenda km nyingi sana.

Magari mengi wameanza na km 100,000 na kuendelea. Au kukuta gari lenye km 150,000 ni kitu cha kawaida sana.
Mbona hata hao Be foward wamechezea na odometer kwa sana.

Sbt magari yenye km nyingi ni ya bei rahisi, lkn yenye bei kidogo imechangamka km ni chache
 
Naomba kuuliza kua ukiagiza gari na ukafanya taratibu zotr kama inavo takiwa je itachukua muda gani kukufikia wewe mumliki
 
Mbona hata hao Be foward wamechezea na odometer kwa sana.

Sbt magari yenye km nyingi ni ya bei rahisi, lkn yenye bei kidogo imechangamka km ni chache
Odometer huwa inachezewa na muuzaji/mmiliki.

Kampuni kama be forward ni world wide na inaingiza revenue kubwa Sana japan,hizo biashara za kihuni zinafanywa na mtu mmoja mmoja Nyumbani kwake
 
Odometer huwa inachezewa na muuzaji/mmiliki.
Kampuni kama be forward ni world wide na inaingiza revenue kubwa Sana japan,hizo biashara za kihuni zinafanywa na mtu mmoja mmoja Nyumbani kwake
Ila kwa kule japan nadhani hiyo michezo hamna.

Itakuwa showroom za hapa bongo
 
Salam ndugu wadau.

Nissan Dualis katika mataifa mengine hujulikana kama Nissan Qashqai isipokua katika soko la Japan na Autralia. Gari hii ndogo ya juu juu ilianza kuundwa kuanzia mwaka 2006.

INJINI na MAFUTA

Kwa upande wa injini, zipo Nissan Dualis chache zenye injini ya Cc 1600 wakati injini inayofahamika zaidi ni MR20DE yenye Cc 2000 ambayo hii ni ya kisasa na hupatikana pia kwenye Nissan Xtrail kuanzia model ya 2007 (New Model). Injini hiyo ikiwa kwenye Dualis hukadiriwa kutumia mpaka kilomita 14 kwa lita iwapo kwenye barabara kuu.

Kuna Dualis zenye 2WD pekee na zipo zenye Option ya 2WD na 4WD.

UIMARA KATIKA MWENDO

Inaelezwa kua gari hii inapokua katika mwendo hua imetulia barabarani japo sio sana kwa wale waliozinyanyua juu kidogo.

VIPULI VYAKE

Wateja watu waliozitumia gari hizi kwa mda sasa wanaelezea kwamba vifaa au vipuli vyake vinakufa baada ya matumizi ya mda mrefu ikilinganishwa na gari za juu juu za Toyota. Upatikanaji wa vifaa vyake ni mkubwa kwa miji mikubwa kama Dar, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa, na Kilimanjaro...vifaa hivyo hupatikana kwa gharama za juu kiasi ingawa sifa yake ni kwamba hutabadirisha mara kwa mara.

ILI UFURAHIE GARI HII

Ili uweze kufahia vizuri gari hii inashauriwa kuhakikisha unatumia oil inayoshauriwa kwa Nissan, lakini pia kufanya service kila inapohitajika bila kupitisha kwa mda mrefu kama ilivyozoeleka kwa gari za Toyota.

Uzalishwaji kwa jina la Dualis ulidumu mpaka 2014, ambapo models mpya zilizotoka baada ya mda huo ziliitwa Nissan Qashqai badala ya Nissan Dualis.


GHARAMA ZA KUAGIZA GARI HIZI

Kwa wastani kuagiza gari hizi hugharim kuanzia 14.5m mpaka 15.8m kutegemea na muuzaji huko nje na mwaka husika wa gari ambao huamua ushuru kua juu au chini kidogo.

Pichani ni baadhi ya Nissan Dualis tulizokabidhi kwa wateja wetu hivi karibuni


WhatsApp Image 2020-09-12 at 14.44.08(1).jpeg
WhatsApp Image 2020-09-12 at 14.44.08(13).jpeg
Nissan Murano.jpg
 
'vifaa au vipuli vyake vinakufa baada ya matumizi ya mda mrefu ikilinganishwa na gari za juu juu za Toyota.'

Uongo ndio uko hapo,ni nani amenunua spare parts org za toyota na akaona kama vipuri vyake havikai muda mrefu kulinganisha na vya Nissan?
 
Back
Top Bottom