Special thread: Kutana na waagizaji wa magari kutoka Japan
Ukaguzi kuanza tarehe 01/03/2021
  • Magari yatashushwa kwa utaratibu wa kawaida kutoka kwenye meli na kuegeshwa kwenye eneo lililopangwa
  • Wakala wa forodha /muagizaji atafanya maombi ya ukaguzi wa gari katika mfumo wa TBS na kufanya malipo kabla ya ukaguzi
  • Wakala/muagizaji atafanya taratibu zote za kiforodha na kuzikamilisha
  • Ukaguzi wa gari utafanyika kama hatua ya mwisho ya utoaji wa gari bandarini.
  • Cheti cha ukaguzi pamoja na Cheti ha Ubora (CoR) vitatolewa katika mfumo uliotumika kuomba kufanya ukaguzi.
  • Cheti hicho kitatumika na mamlaka husika katika kuondosha gari bandarini.
  • Gari ambalo halitakidhi matakwa ya kiwango,litaruhusiwa kuondoshwa bandarini kwa masharti maalum na baada ya matengenezo litapimwa katika yadi ya UDA.
  • TBS imeagiza mitambo ya ukaguzi wa magari ambayo inatarajiwa kuanza kuwasili mapema mwezi wa pili kwa ajili ya kufungwa katika maeneo ya ukaguzi
  • Mitambo 11 itafungwa bandarini na mtambo mmoja utafungwa nje ya bandari (UDA) kwa ajili ya ukaguzi wa magari baada ya matengenezo.
  • Wataalam zaidi ya 45 wamesha andaliwa kwa ajili ya kuanza ukaguzi .
Hapa ndipo kwenye rushwa
 
Point kubwa sana niliyotegemea isingekosa ni upande wa uscan. Tz tunatumia right hand ila kuna nchi tofaut zenye left hand ambayo ni changamoto kwa hapa tz. So Japani wanadrive right hand site tofaut na most of European countries (except UK, ireland etc) na USA.

Swala la inspection ilo lipo kila nchi. Hata japani magar yao yanakuja mabovu tu hasa yale ya bei ndogo.

Gar ya mwingereza nayo gharama kwa mtz ni wachache wa kuafford ndyomaana tunakomaa na za kijapan.
Hivi mkuu kuna charges au regulation tofauti hapa kwetu ukiagiza gari ambalo ni left hand?
 
TOYOTA COROLLA SEDAN Model ya 2000- 2006


KIMOMWE MOTORS (T) Ltd- Waagizaji Magari

Utangulizi
Gari hii ni zao au mwendelezo wa Corolla iliyodumu miaka ya 1995- 2000 (Corolla Limited).

Hii ilikuja kuendana na usasa haswa kwa kupatiwa injini yenye teknolojia pamoja na mwonekano unaovutia zaidi nje na ndani.

Injini
Corolla Sedan model tajwa inakuja na injini iitwayo 1NZ ambayo pia hupatikana kwenye Premio, IST, Vitz RS, Spacio, Rumion, Sienta, Ractis, Funcargo, Porte, Blade, Raum, Allex&Run X, Allion, Axio, Succeed, Probox, Fielder n.k


Sifa kuu ya injini hii ni matumizi madogo ya mafuta sababu ni injini ina teknolojia ya Vvti inayowezesha matumizi mazuri ya mafuta kwenye injini yenye Cc kubwa. inakadiriwa kwenda kati ya 16-18km kwa lita kutegemea na uzito wa body la gari husika.

Uimara na Utulivu

Ni moja ya sedan za Toyota ndogo yenye utulivu mzuri kwenye bara bara zote japo body lake ni tani 1 tu.

Vifaa na Mafundi
Vifaa na mafundi vinapatikana kila kona ya Tanzania kwa gharama nafuu.

Gharama
Kwa kuagiza, gari hii hugharim kati ya 12m mpaka 13m kutegemea na muuzaji na hali yake.

Maoni na Ushauri

Anayefikiria gari hii pia anaweza kuzifikiria Allion na Premio haswa kwa kua bei zinawiana huku Premio na Allion zikiwa na mwonekano wa ndani na nje unaovutia zaidi ya hii Corolla Sedan

Zaidi tembelea ofisi zetu za Dar au Mbeya au piga 0746 267740 au 0719 989 222.

PhotoGrid_Plus_1613980659196.jpg
IMG-20210221-WA0003.jpg
IMG-20210221-WA0002.jpg
IMG-20210221-WA0007.jpg
IMG-20210221-WA0005.jpg
 
Hii corrolla ina very beautiful and neat interiors. Halafu haili mafuta kabisa yani. Kwa wazee wa uber humu ndio mwake yani 😂😂😂
 
  • Wateja wanashauriwa kutumia makampuni yaliyo sajiliwa na kutambulika na serekali na si kuagiza wao binafsi.
  • Gharama ndogo ndogo za matengenezo zitakuwa kwa mteja mfano: Tairi kama ni za kubadilisha, wheel balance, taa kama zinakuwa hazimuliki vizuri n.k
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kinachofuata watu watapitishia gari Mombasa kukwepa usumbufu wa kubambikiwa matatizo ili mpigwe hela.
Hata ukipitisha mombasa ni lazima gari ikiingia Tz utaisajili TRA na kulipa ushuru. Ukimaliza hapo ndio unatakiwa clearance ya TBS ili upate release ya gari yako na kadi ndio ukaweke plate number.

Labda likipita mombasa likifika bongo uende kwenye mabucha ya magari ununue kadi then........ la sivyo lazima TBS wakague tu. Tena wamenunua mobile inspection machines nadhani ndio zitafungwa huko entry point za Holili, Namanga na Tunduma.
 
Hata ukipitisha mombasa ni lazima gari ikiingia Tz utaisajili TRA na kulipa ushuru. Ukimaliza hapo ndio unatakiwa clearance ya TBS ili upate release ya gari yako na kadi ndio ukaweke plate number.

Labda likipita mombasa likifika bongo uende kwenye mabucha ya magari ununue kadi then........ la sivyo lazima TBS wakague tu. Tena wamenunua mobile inspection machines nadhani ndio zitafungwa huko entry point za Holili, Namanga na Tunduma.
Hapa zitapita kutokea Mutukula na Rusumo.
 
Back
Top Bottom