Hapa ndipo kwenye rushwa
 
Hivi mkuu kuna charges au regulation tofauti hapa kwetu ukiagiza gari ambalo ni left hand?
 
TOYOTA COROLLA SEDAN Model ya 2000- 2006


KIMOMWE MOTORS (T) Ltd- Waagizaji Magari

Utangulizi
Gari hii ni zao au mwendelezo wa Corolla iliyodumu miaka ya 1995- 2000 (Corolla Limited).

Hii ilikuja kuendana na usasa haswa kwa kupatiwa injini yenye teknolojia pamoja na mwonekano unaovutia zaidi nje na ndani.

Injini
Corolla Sedan model tajwa inakuja na injini iitwayo 1NZ ambayo pia hupatikana kwenye Premio, IST, Vitz RS, Spacio, Rumion, Sienta, Ractis, Funcargo, Porte, Blade, Raum, Allex&Run X, Allion, Axio, Succeed, Probox, Fielder n.k


Sifa kuu ya injini hii ni matumizi madogo ya mafuta sababu ni injini ina teknolojia ya Vvti inayowezesha matumizi mazuri ya mafuta kwenye injini yenye Cc kubwa. inakadiriwa kwenda kati ya 16-18km kwa lita kutegemea na uzito wa body la gari husika.

Uimara na Utulivu

Ni moja ya sedan za Toyota ndogo yenye utulivu mzuri kwenye bara bara zote japo body lake ni tani 1 tu.

Vifaa na Mafundi
Vifaa na mafundi vinapatikana kila kona ya Tanzania kwa gharama nafuu.

Gharama
Kwa kuagiza, gari hii hugharim kati ya 12m mpaka 13m kutegemea na muuzaji na hali yake.

Maoni na Ushauri

Anayefikiria gari hii pia anaweza kuzifikiria Allion na Premio haswa kwa kua bei zinawiana huku Premio na Allion zikiwa na mwonekano wa ndani na nje unaovutia zaidi ya hii Corolla Sedan

Zaidi tembelea ofisi zetu za Dar au Mbeya au piga 0746 267740 au 0719 989 222.

 
Hii corrolla ina very beautiful and neat interiors. Halafu haili mafuta kabisa yani. Kwa wazee wa uber humu ndio mwake yani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Kinachofuata watu watapitishia gari Mombasa kukwepa usumbufu wa kubambikiwa matatizo ili mpigwe hela.
Hata ukipitisha mombasa ni lazima gari ikiingia Tz utaisajili TRA na kulipa ushuru. Ukimaliza hapo ndio unatakiwa clearance ya TBS ili upate release ya gari yako na kadi ndio ukaweke plate number.

Labda likipita mombasa likifika bongo uende kwenye mabucha ya magari ununue kadi then........ la sivyo lazima TBS wakague tu. Tena wamenunua mobile inspection machines nadhani ndio zitafungwa huko entry point za Holili, Namanga na Tunduma.
 
Hapa zitapita kutokea Mutukula na Rusumo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…