Inaelekea hujamuelewa Mgombea wetu Urais wa Chauma.
Kifupi anajaribu kuhimiza lishe bora kwa Watanzania huku mkazo ukitiliwa kwa wanafunzi wanaoshinda shuleni muda mrefu bila kupata chakula mchana. Kwa waliosoma zamani wanakumbuka mchana wanafunzi waliweza kupatiwa msosi shuleni, mwanafunzi mwenye njaa hawezi kuwa active darasani.
Lishe bora kwa Watanzania ni muhimu maana itasaidia kuondoa tatizo la udumavu wa miili na akili, unaweza ukawa unakula lakini unajaza tumbo tu na si lishe bora unayokula. Kupitia lishe bora hata shahawa zitokazo kwa mwanaume huwa bora, mshika mimba naye anakuwa strong, kiumbe kitokacho nacho kinakuwa bora.
Chagua Rungwe, chagua Chauma upate lishe bora kwa maendeleo ya familia yako na Taifa letu, tumuunge mkono kwa Mzee wetu ameona jambo muhimu saana.