Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Uchaguzi 2020 SPECIAL THREAD: Taarifa za Kampeni na Sera za Mgombea Urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda

Rungwe anajua WaTz wanachotaka ni zile three basic needs,food...shelter & clothes basi iii
 
Mzee anatoa points ila uwasilishaji wake wengi hawaelewi. Inaonyesha atawekeza sana kwenye mahitaji muhimu ya binadam kabla ya miundombinu na mengineyo.
 
Wala hana akili mbovu. Anajua vizuri anachofanya. He is just having fun.

Anajua reality ya Watanzania walivyo na reality ya tume ya uchaguzi.
Akili mbovu haimaanishi kua hajielewi...I meant he is fun to the fullest.....afu akishindwaga utaskia...huu uchaguz wamenionea ilikua nipite maana nilipigiwa kura nyingi tu,🤣🤣🤣🙌🙌🙌🙌
 
Hashim Rungwe Spunda aliwahi kusema kwamba.
Ana uhakika alishinda uchaguzi mkuu kwa ugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, lakini aliibiwa kura nyingi sana na ushahidi anao kwasababu alipokea sim nyingi za pole maradufu kuliko idadi ya kura alizopata.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
🤣🤣🤣 Mimi huyu mzee ananiachaga hoi Sana.....yani bila uyu uchaguz unakua hauna amsha...ana vitu vya pekee amusing sana
 
Hashim Rungwe Spunda aliwahi kusema kwamba.
Ana uhakika alishinda uchaguzi mkuu kwa ugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, lakini aliibiwa kura nyingi sana na ushahidi anao kwasababu alipokea sim nyingi za pole maradufu kuliko idadi ya kura alizopata.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji1787]
 
Ndugu Hashim Rungwe, mgombea wa urais kupitia chama cha CHAUMA afika studio za clouds FM na ma hot-pot makubwa ya ubwa na mboga, ikiwa ni sehemu ya sera zake. Na watangazaji wote kwa pamoja wakanza kuufinya ubwabwa kwa pamoja na mgombea huyo wa urais huku mahojiano yanaendelea.
 
Hiii wajameni,

Hivi huu utani tumeshindwa kabisa kuuchorea mipaka?

Mgombea Urais kabisaaaaa, mbona asikemewe au kuondolewa mapema tu kwenye kinyang’anyiro!

Hivi taasisi ya Urais tunaichukuliaje, ni kweli watu hawana uwezo wa kumudu milo mitatu.

Lakini hii kutembea na mahando ya ubwabwa na kula hadharani ni kuonesha ufahari, kuwasimanga na kuwatamanisha wananchi!

Rungwe hautokuwa ukiwagawia misosi watu wote, waambie tu utawasaidiaje wamudu milo ya kiafya.

Hapa njaa inaniuma hadi nimeshindwa kuandika, ngoja kwanza.

Hii mizaha si vichekesho, tuikemee na kuipinga.

Rungwe.jpg
 
Rungwe ndio mwanasiasa pekee Tz anayependwa na kila mtu.
2025 twende na rungwe[emoji23]

Hata mimi huwa namuelewa sana huyu jamaa! Siyo yule anayewaza kununua madege tu huku tukishindia daily mihogo ya kukaanga na maji.

Watu washibe kwanza halafu kila kitu kitajiset chenyewe.
Shikamoo Hashimu Rungwe Spunda! Waamshe hawa Watawala wetu jeuri, wachoyo, wabinafsi, waongo, wakatili, wajivuni, na waliolewa madaraka kiasi cha kudhani wanawatawala ng'ombe badala ya binadamu wenzao.
 
Back
Top Bottom