Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

11887914_421706398031594_8793522401328404543_n.jpg


11889666_421706361364931_246354988763248536_n.jpg



11892227_421706301364937_8719282536885075909_n.jpg


11951143_421706478031586_5489110581185835480_n.jpg


11896013_421706548031579_4080802327592922626_n.jpg




11899987_421706428031591_2891750899293422322_n.jpg



11898583_421706241364943_8646198387736233079_n.jpg
 
Mbalizi ipi? Mkuu acha kujifariji. Ningeelewa kama ingekuwa chalinze vile lakini mbalizi upate watu 1000 wa kurudisha kadi na kupewa za kijani si kweli. Mbalizi watu wengine
 
Magufuli ninampenda bure!!! Kwani anachofanya ni kusaidia kueleza kero, karaha na maisha ya taabu tulinayoishi watanzania kwa miaka 50+ chini ya utawala huu wa CCM. Ninampenda sana Magufuli. Ninawashauri walioko katika timu yake ya kampeni wamwambie aongeze jambo mambo mawili katika hotuba zake:
1. Atueleze kwa nini serikali ya chama chake imeshindwa kushughulikia kero hizo kwa miaka yote hii? Atuambie wapi walipokosea watangulizi wake
2. Atupe mikakati mbadala anayoiona yeye kuwa inaweza kuwa mwarobaini.

Haitusaidii na haimsaidii yeye kutuambia kuwa kuna shida hii na ile (sote tunazijua hata teja mbwia unga wa mtaani anazifahamu fika. Amuulize hata mwanafunzi wa darasa la kwanza anazijua). Na hatuhitaji kutuambia nitaziondoa; "sitawangusha" . Tunataka atuambia ataziondoaje??

Mgombea mwenza wake Samia yeye ni tatizo na pengine hajui hata nachozungumza (mniwie radhi simkejeli mwanamke mwenzangu) ila nasema kile ninachokiona na kusikia akikizungumza.
Akiwa Same hospitalini ameonekana kushangaa hali ya uduni wa huduma za afya. Nikajiuliza huyu mama alikuwa nchi hii madaktari walipogoma? Je, aliwazi kushughulisha akili yake kufahamu kwa nini waligoma? Au hajui kwa kuwa huku ni bara na Zanzibar hali iko poa?
Jana akiwa Longido amezungumzia kero ya maji na kusema kuwa serikali yake imetenga bilioni kadhaa kwa ajili ya mradi huo kwa hiyo wakiingia madarakani watashughulikia. Hapa nikajiuliza maswali mawili:
1. Je, wananchi wale waliokuwa wanamsikia ni 'wapumbavu" kiasi cha kutohoji kama mmetenga hizo bilioni mnasubiri nini kutekeleza mradi huo? Kwa wasiofahamu Kuanzia Ngaramtoni (Arumeru) hadi Namanga kuna shida ya maji hadi watu huwa wanapigana huko (kaulize vijiji vya Kimnyaki, Olmotony, Emaoi, Mwandet, nk hata Olturmet yenye chanzo cha maji yaliyokwenda Monduli kuna shida balaa). Halafu kuna watu wana Bilioni kadhaa ambazo ni kodi za wamasai/ warusha hawa, wanasubiri uchaguzi ndio waseme mkituchagua tutawaleta maji!!!!

2. Nimejiuliza je, huyu mwanamama anafahamu juu ya sheria ya uchaguzi na mkataba wa maadili waliosaini hivi karibuni (chama chake kimesaini pia). Unawezaje kuahidi kwa fedha ambazo zimetengewa katika serikali ya sasa?
Ninashauri ile kamati/ timu ya kampeni angalieni hotuba mnazomuandikia huyu mama (maana yeye namuona akiwa na kablasha kubwa la kusoma).


Lugano E.J
 
Nimeshuhudia leo vijisanii vya chadomo vilivyokwenda kumsalimia Lowassa, hata kunyanyua mkono kusalamiana nao alishindwa kwa dharau na kunata, anaona watamchafua.

Sijaona mgombea urais mwenye majivuno kama huyu mamvi.

Hivi MUUZA NYUMBA amesema atajengea nyumba wafanyakazi wa serikali??????????
 
mwenye full updates za safari za magufuli kuanzia kesho wapi??
 
Hatimaye Mh John Pombe Magufuli apokelewa kwa shangwe na MAELFU ya wakazi wa Mbalizi, Mbeya.

Hata hivyo rais huyo mtarajiwa aliwahakikishia wakazi hao serikali yake itatoa kipaumbele katika kufufua viwanda, ikiwa ni kusaidia kutengeneza ajira nyingi kwa vijana. Aidha Mh Magufuli pia kasisitiza kuboresha miundo mbinu hususani ujenzi wa barabara za kisasa ambazo zitakuwa ni kitovu cha kuinua uchumi wa nchi hii na kuondoa umaskini.
Hata hivo katika mkutano huo zaidi ya wanchama 1000 wa CHADEMA wamerudisha kadi zao na kujiunga rasmi na CCM.
Wanachama hao wapya wameahidi kuachana na porojo, kubuluzwa, hatimaye kuchukua hatua mapema, wamempongeza sana Dr Magufuli kwa utendaji wake uliotukuka.

KAZI NI KAZI TU
Kajifunze matumizi ya "hata hivyo"
 
Naona Mbeya kila alipokuwa anapita vijana walikuwa wanamuonesha alama ya Chadema ya vidole viwili kuwa ccm hawana chao Mbeya. Yeye alivyozuzu akahisi anashangiliwa na Nyomi.
Kwi kwi kwi kwi.
 
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:

"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"

Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?

Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?

Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?

Je wananchi nyie hammshangai?

Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?

Mshangaeni! Chukueni hatua.

Hujitambui wewe ndama
 
Gharama za kuchapisha kadi ni zao muda wa kuzigawa ni wao na muda wa kuzipokea ni wao,pia fedha za kuwalipa hao wasanii ni zao.CHADEMA haijapoteza chochote.Watanzania tusidanganyike.saa ya ukombozi ni sasa.Tuchague UKAWA ,tuchague LOWASA.
 
acheni umbea mimi nilikuwa mbalizi na hawafiki elfu na pia wale ni makada wa ccm walikuwa wanaigiza ndo maana walikuwa wanazomewa
 
Back
Top Bottom