Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

A H A D I Z A C C M.... kila uchaguzi ni zile zile tu.... sijui watanzania ni mataahila hatujui lolote au tumelogwa??????
 
makitoro hujui chochote kuhusu Mbalizi wewe na wala hujui Mbalizi ipo ktk Jimbo gani la uchaguzi!

Mbeya Vijijini ni UKAWA pickup saa 2 asubuhi!CHADEMA anzeni kufurahia ushindi wenu
 
Last edited by a moderator:
Wao wanashangilia kumnasa fisadi na Sumaye, sisi tunanyakua maelfu ya wanachama wao. Hapa Kazi Tu
 
Duh! Naona unajitoa ufahamu kwa makusudi
Lizaboni huko ni kwetu!Utanishinda uchambuzi ya Majimbo ya kwenu Ruvuma sio ya Mbeya!

Mbalali,Vwawa,Momba,Tunduma,Mbeya mjini na Mbeya vijijini haya 100% UKAWA

Busokela na Ileje haya yatabaki CCM

Lupa,Rungwe,Kyela na Songwe ni toss up yyt anaweza shinda
 
Last edited by a moderator:
Kaskazini inaendelea kutawala.Mnadanganywa na CCM oh, chadema ni ya kaskazini, wakati hata sasa kaskazini inanufaika sana kuliko kanda zingine kwa kupata huduma bora za kijamii kama vile elimu,afya na barabara. Watu wa kusini ndo wasikilizaji wa mipango ya maendeleo Tanzania.
 
Lizaboni huko ni kwetu!Utanishinda uchambuzi ya Majimbo ya kwenu Ruvuma sio ya Mbeya!

Mbalali,Vwawa,Momba,Tunduma,Mbeya mjini na Mbeya vijijini haya 100% UKAWA

Busokela na Ileje haya yatabaki CCM

Lupa,Rungwe,Kyela na Songwe ni toss up yyt anaweza shinda

Wacha ujinga wako wee Malfyale. Ukawa Mbeya haipo kama unavyojinadi. Hiyo Momba na Mbeya mjini nayo inarudi CCM
 
Last edited by a moderator:
Anapozungumzia kufufua viwanda atuambie nani aliviua ikiwa wenzake waliotangulia wameshiwa hata kudhibiti wanyama wetu yy atawezaje atueleze kwanza udhaifu wa watangulizi wake kisha atuambie atarekebisha

Hana muda wa kujadili alieviua atachelewa kufikia malengo.kama mtu akifa amekufa lakini maisha yanaendelea kwa waliobaki duniani.MAGUFULI ni safari ya kwenda mbele
 
Anaposema ataongeza ajira kwa vijana yupo sahihi na anaamini hivyo, uboreshaji tu wa miundo mbinu hususani barabara katika kipindi chote akiwa wizara ya ujenzi bado katengeneza ajira nyingi kwa vijana. Sasa anakuja na mikakati ya kufufua viwanda vya ndani ili kutengeneza ajira nyingi kwa vijana wote. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayemtaka kwa sasa Tanzania.

Kaleta wachina wajenge barabara na majengo wazawa hawawezi kujenga? Mkuu hayo nayaona kwa macho yangu
 
Wadau naomba tujiulize suala moja kuhusu mgombea wa CCM ambaye ni waziri wa ujenzi, wizara inayotuhusu sisi sana. Magufuli anasema nitaongeza ajira kwa vijana. Najiuliza amefanya juhudi gani kuinua wakandarasi wazawa? Anatoa takwimu kwamba kuna waandisi 15,000 wana kazi za maana. Anaweza kutuonyesha angalau wakandarasi wazawa 10 wanaoweza kufanya kazi kwenye nchi za East Africa Class one? Au hawa wanaoshinda whatsapp ? Kama ameshindwa kutengeneza wazawa contractors akiwa ujenzi wa kueleweka ataweza vipi nchi nzima? Bajeti ya wizara ya ujenzi ni kubwa kuliko wizara zote lakini pesa yote inarudi China. Sababu wachina wanaagiza kila kitu toka kwao. Tunachoambulia sisi ni pesa ya mchanga, hata kokoto wanapasua wao, wanakula kwenye migahawa yao kila kitu ni wao. Kwa nini hakuweka sera nzuri kwenye ujenzi? Uchumi lazima udumae hakuna mzunguko wa pesa kwa hawa watu kila kitu kinatoka kwao kuanzia nondo mpaka tooth pick. Hata wenye nyumba hawapati pesa maana wengi wanalala site. Wakipanga wanakaa nyumba moja watu hamsini kwenye nyumba moja. Unajivunia kuwa na waandisi wengi wasiokuwa na kazi. Na waliothubutu kujikakamua hawalipwi, wengine washauziwa mali zao na benki. Pesa inayozunguka kwenye barabara na miradi ya majengo toka mifuko ya jamii, NHC na taasisi ya serikali, kama kungekuwa na mipango madhubuti ya kuwaendeleza waandisi wazawa wangekuwa mbali sana sasa hivi. Sasa mtu kama huyu ameshindwa kuwa mlezi mzuri wa sekta moja anaweza nchi nzima. Tafakari.
We unazungumza utumbo tuu. Wenye proffession hii hatuzungumzi wewe utakuwa umelishwa maneno. Fanya tafiti kuhusu makandarasi kabla hujaja kutapika huku. Magufuli amejengea uwezo sana sekta hii pamoja na kujiamini ikiwa na kufanya kazi kiuadilifu na sio kisanii kama Lowasa.
Unazidi kututia machungu na hasa baada ya mgombea wetu Dr Slaa kukatwa bila sababu yoyote kwa hoja dhaifu eti za wafuasi wengi kumbe viongozi wamehongwa hela ili aweze kupitishwa kugombea.
Time is coming when all the puppets will be thrown away and leave our party safe. Dr Slaa be prepared to take over
 
Hii kitu ya miaka kumi ilopita ndo mnaileta leo jamani? Ngojeni 19215 ifike mjionee mambo
 
Back
Top Bottom