Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Hii sera ya majimbo ni moja ya sera mbovu kabisa. Sijui kwanini kila uchaguzi Chadema wanaibeba! Sijawahi kuikubali toka nawaunga mkono.
 
Akiwa Urambo JPM amewaonya watanzania kuwakataa wanaohubiri kuigawa nchi katika majimbo, sera hiyo ni hatari kwa mstakali wa umoja wa Taifa letu,amesema sera hiyo ni ubaguzi mtupu kwani majombo masikini yatabaki maskini.
MAENDELEO ni kodi zetu

Hazikusanywi kwa kadi za vyama vyetu

Tusipewe kwa rangi zetu

Kuchaguliwa/kuchagua ni haki yetu

Kodi ni pesa ya watanzania wote

Wasipochagua chama chako usiwachukie

Wasipokupenda, wakikukosoa, usiwakasirikie

Wanalipa kodi, wapewe maendeleo, Usiwafokee
 
.... mbona una-expose ujinga? Unakubali as of now Singida kwa Lissu ni malofa na maskini wa kutupwa; ni kwa sababu ya sera ya majimbo inayoongoza nchi kwa sasa ama?
Kama Sasa hivi malofa ikiongezewa hiyo sera ya majimbo ndio ulofa utazidi
 
Wasipochagua chama chako usiwachukie...
Mlipa Kodi anasena hataki maendeleo ya vitu na kachagua chama ambacho hakitaki maendeleo ya vitu kuwa huo ndio msimamo wao sera ya maendeleo ya vitu hawaitaki unawapelekea barabara au hospital au maendeleo ya vitu ya Nini?

Hakuna kupeleleka sababu wamekuonyesha wazi kuwa hawataki na Uzuri wagombea wao wote na Chadema wanawaeleza wazi hawawafichi kuwa labda wanna wa blackmail wanawaambia mchana kweupe with clear audible voice kuwa sera yetu Chadema hatutaki maendeleo ya vitu Sasa upeleke vitu vya Nini si kutafuta ugomvi usio na sababu

Wamesema hawataki wakachagua mbunge wa Chadema kuonyesha hawataki maendeleo ya vitu leave them alone Hakuna kupeleleka mradi wowote kuheshimu maamuzi Yao ya sera waliyoichagua
 
Wakuu habari za Leo, ninaimani kuwa mu wazima wa afya njema, tukiwa tunandelea na kampeni za uchaguzi kumekuwa na vituko toka kwa wagombea tofauti tofauti, kila mmoja na vituko vyake.

Kituko kilicho nisononesha ni cha huyu Mgombea Wa CHADEMA ndugu Tundu A.Lissu kutaka kuwaaminisha wafuasi wake kuwa unaarufu wake umepanda na kusifikia level za kina J.Magufuli hadi kufikia hatua ya kutaka mdahalo na JPM, maana yake haoni mwingine kwa wagombea urais zaidi 10,huku ni kuwapotosha wafuasi wake.

Kwanini nimesema hivyo, Lissu Mara kadhaa amekuwa akisisitiza kuwa anataka mdahalo na mgombea wa urais kupitia chama tawala cha CCM, swali la kujiuliza hapa ni kuwa kwanini Lissu alazimishe mdahalo na Magufuli tu, je katika uchaguzi huu washindani ni wawili tu?,je hawaoni akina B. Membe, Prof. Lipumba nk?

Ukweli ni kwamba Lissu ana wadharau sana Watanzania amefikia level za kujiona yuko juu ya Watanzania wote ,na elimu na uelewa alionao ni wajuu hakuna mtanzania wa kumliko.

Kitendo cha Mh. Lissu kuwadanganya na kuwaaminisha wafuasi wake kuwa kwa sasa amekomaa kisiasa na anao uwezo wa kufanya midahalo na kina Magufuli ni kitendo cha kilaghai kinacholenga kuwaaminisha wafuasi wake kuwa tofauti na Magufuli hakuna mwingine wa kuweza kujadiliana naye, kwanini asitake midahalo na kina Membe?

Hii inadhihirisha kuwa mtu huyu akipewa madaraka ni hatari sana na ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa hawezi kushirikiana na watu wanyonge, na ni kweli hili tumeliona maana kampeni zake muda mwingi zinazungumzia habari za ulaya na mabeberu tu, Ulaya kwenyewe katika akiwa mgonjwa na kaka miaka miwili, je angekulia ulaya na kusomea ulaya si angefikia hatua ya kututemea mate?

Shime Watanzania agopeni sana mtu anayeishi kwa kuigiza maisha huyu ni hatari sana, akipewa madaraka mtu huyu rafiki zake watakuwa ni watu wenye vipato vya juu hali ambayo itapelekea kuongezeka kwa pengo kati ya masikini na tajiri na kupelekea chuki na mafarakano miongoni mwa Watanzania.

Say NO for Tundu A. Lissu
View attachment 1576065
 
Kagera state tuonane hapa tuna jambo letu.. senata Rutashobya na Gavana wetu Muganyizi watakua na maongezi nasi
 
Akiwa Urambo JPM amewaonya watanzania kuwakataa wanaohubiri kuigawa nchi katika majimbo, sera hiyo ni hatari kwa mstakali wa umoja wa Taifa letu,amesema sera hiyo ni ubaguzi mtupu kwani majombo masikini yatabaki maskini.
Huyo hana uwezo bana anachojua ni kufoka
 
Lete matokeo yao ya O-LEVEL N A-LEVEL achana n ya chuo maana mmoja Hadi leo hajui maana alifanyiwa pepa[emoji3]
 
Mi sioni kama anakosea kuwaaminisha wafuasi bali anachofanya Lissu ni kujishushia hadhi yeye mwenyewe kwa sababu ukindoa polisi na vyombo vya dola, JPM is just a piece of trash mbele ya Lissu!

Wanachofanana TL na JPM ni kimoja tu: Wote ni Wagombea wa Urais, PERIOD!!

Lakini kwa upande mwingine TL anaamua tu kujilinganisha na JPM kwa sababu tu anafahamu JPM bado ni rais, na kwa mtu muungwana, hawezi kueleza mbele za umma daraja stahiki la JPM.
 
Akiwa Urambo JPM amewaonya watanzania kuwakataa wanaohubiri kuigawa nchi katika majimbo, sera hiyo ni hatari kwa mstakali wa umoja wa Taifa letu,amesema sera hiyo ni ubaguzi mtupu kwani majombo masikini yatabaki maskini.
Huyu jamaa yaani siasa zake ni za fear mongering....

Madikteta ni mawatu fulani hivi akili ni rare commodity kwao....

Hajui hata maana ya dhana nzima ya majimbo,hajui...

Aende SA,USA au hata hapo Kenya aone...dhana ni kurudisha madaraka kwa wananchi na mikoa yao...

Ni simple tu,ni kama Mkuu wa Mkoa asiteuliwe na Rais achaguliwe na watu wa mkoa husika,simple!

Eti yeye hilo anaita mifarakano,yaani unaangalia majibu yake unaishia kumuonea huruma....He will never get it...

Kila anachojibu amekiona threat kwake,kisingekua threat asingemjibu Lissu on this....

Mpaka kura hapo October,huyu jamaa anaongea sijui vitu gani maana watu washajua level zake,ni kuleeee,chini kule!
 
Babu yenu hakujiandaa kuwa rais alisokomezwa tu, Tundu lissu rais mtarajiwa kumfananisha na mnyampara wa mabarabara kwa kweli unakuwa humtendei haki lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…