Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kinachoiponza ccm ni ubabe na kiburi, wao ubinafsi umewajaa hatari.wanatumia vyombo vya dola kubaki madarakani. Hakuna kitu kinachowakera watanzania ccm kujipendelea na kunyima haki za watu.Kwa mfano kutumia jeshi La polis na tume kukandamiza wapinzani wao.Watu wengi wanasema watainyima ccm kura kwa hayo.
 
Mtapika propaganda zoteee. Ila lisu wenu hatopata ata kula 1000. Mda utaongeaa. Mnatengeneza kiki hapa mwanza na geita halafu mnajicheka wenyeweee, mikutano yote ya mwanza na geitaaa tupoo hapooo hata yale makiki ya usikuuu na taa hata sisitulikuwemo kwenyee huo ukumbi. Hapa mwanza pia tupooo
 
Amini amini nakuambia, hakuna sera nono atakayonadi Magufuli imtakase gundu aliyojipaka wakati anatekeleza/sio tunatekeleza!
😅
👊 ✌️✌️✌️💥
 
Rudisha 20 alfu za watu bro, watu wakuelewe kama na wewe ni mshirika.
Elfu ishirini hazirudishwiiii, zaidi zinakiwa ziwe laki moja kwa kila mjasiliamali. Ilikuongeza pato la taifaa. Huyo mzeee wa kiiki, kama anawadanganya kwamba hamtolipa kodi kwaa ajili ya maendeleo, anawarubuniii,
 
Watu wameikataa CCM au wamemchoka Magufuli?
Watanzania wamewakataa wote kwa sababu wamewachoka wote. Kila anyesukumiziwa madaraka baada ya miaka mitano ni wa hovyo kuliko aliyemtangulia. Halafu walivo wapuuzi, wanang'ang'ania madaraka huku uwezo hawana na kwa miaka karibu 60 wameweza kulididimiza hili taifa lililojaaliwa kwa kila kitu. Safari hii tusifanye makosa, tuhakikishae genge hili linatoweka kabisa.
 
Huyu anaenda kushindishwa na tume sio umma, muda wote Yuko Live na TV na maredio, wenzake hawapewi hiyo favour.binafsi namchukia sana Jpm kwa kuvunja haki za watu tofauti na tulivyotarajia mwaka 2015 wakati anaingia madarakani.Binafsi nilimpa kura.
 
Wewe kunauwezekano Wazazi wako hawajawahi kukutana na kipigo cha Mgambo wa jiji na liwe jiji linaliongozwa na hao unaowasikiliza
Hao MGAMBO walikuwa wanatumwa na CUF? Kwa hiyo ili kuzuia ukatili wao hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kukamua wananchi 20000/- ambayo kuishika kwa pamoja na mtihani? Hao MGAMBO walikuwa wanajituma au kuna mamlaka ilikuwa inawatuma? Au hujui MGAMBO haohao ndo waliotumika kusaka wasio na vitambulisho vya 20000/- hadi kufikia Mama Ntilie mwenye watumishi 2 kulipa 60000/- yeye na Watumishi wake ili Mkuu wa Wilaya amalize vitambulisho maana ukipewa 10000 lazima uvimalize hata kama una wafanyabiashara wadogo 3000 tu. Msijisahaulishe kwamba baadhi ya Halmashauri watumishi walikatwa 20000 kwenye mishahara yao kulipia vitambulisho vya ujasiriamali!!!
 
anashinda kwa kukaa na tume badala ya kufanya campaign
 
Mimi ni mwana CCM Magufuli hata angegombea na mbwa ningempigia kura mbwa
Tumechoka kutawaliwa na dikteta
,, WE CAN'T BREATHE,,,
 
Ni ukweli usiopingika kwamba mitandao ya kijamii kama huu wa JamiiForums, twiter, fb na ile inayojadili mambo ya kisiasa hutumiwa kwa kiasi kikubwa na wasomi. Ktk mijadala mbalimbali iliyoibuliwa kuhusu wagombea wawili wanaochuana vikali imeonyesha dhahiri upande wa ccm umeelemewa kwa hoja za nguvu toka upande unaomuunga mkono Lissu

Hii ni ishara ya wazi kabisa kwamba wasomi wengi wanamuunga mkono Lissu mbali na wale wachache wanaoitetea ccm kwa ajili ya maslahi binafsi na kuonekana kabisa hawana hoja zenye ushawishi zaidi ya kejeli na matamko ya Magufuli mitano tena! Jamii ya wasomi imemkataa Magufuli na ccm yake!
 
Wadau salamu zangu kwenu!
Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Natambua unatambua ya kwamba mh. Magu kwenye uchaguzi huu kwake ungekuwa mdebwedo pasipo upinzani wa kumtisha.

Matokeo yake mambo yameenda tofauti na matarajio ya wengi kule CCM(Lumumba).

Sasa kwanini haya yametokea haraka sana awamu hii..!!!.!.?

Mambo ambayo naweza sema yamesababisha haya leo ni kama yafuatayo.
1> Bunge Kuongozwa kiushabiki zaidi pasipo kufuata haki kwa wote ili maslai mapana kwa taifa yatimie.

2>Viongozi kugeuka kuwa miungu watu( makonda,ole.... DC wa Hai kule moshi, Gambo,mh Job Ndugai, mh mtukufu magu, na wengine wengi)

3>Kuminya uhuru wa kupata habari.

4>Kuminya demokrasi ya vyama vya upinzani kufanya siasa miaka mitano ya utawala wake.

5>Mh mtukufu kutowajali raia wake( kwa mfano: wafanyakazi,kwa kutowaongezea mishahara yao kwa mujibu wa katiba yetu inavyo itaka).

6>Mh. Rais kutoa lugha kali kwa wa athirika wa majanga,kama vile matetemeko n.k

7>Watu wasijulikana wenye kutimiza mauaji ya raia na wengine wanatekwa na kuteswa chini ya utawala wa awamu hii.

8>....................
Haya ndiyo naweza kusema ni mambo ambayo yamesababisha hivi leo mgombea wa urais kupitia CCM kupata upinzani mkubwa
 
Huyu anaenda kushindishwa na tume sio umma, muda wote Yuko Live na TV na maredio, wenzake hawapewi hiyo favour.binafsi namchukia sana Jpm kwa kuvunja haki za watu tofauti na tulivyotarajia mwaka 2015 wakati anaingia madarakani.Binafsi nilimpa kura.
Huu ndio mwezi wa mwisho wa kuwa Raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…