Hii ni sera ambayo watumishi hawajaisikia kutoka ccm, kwanini hawataki kuigusia, ina maaga sio muhimu kwa watumishiw ote wa umma?, je watumishi wana hali gani kutosikia sera hii kutoka ccm.
huelewi hata maana ya sera ,sera hutamka jumla kwenye utendaji ndio kunakuwa specific.mfano sera inaweza tamka lengo ni kuboresha maisha ya mtanzania unapoingia kwenye utekelezaji ndipo kila mhusika anatoholea hapo.
Mfano kwenye kipengele cha kuboresha maisha ya mtanzania mwajiri wa sekta ya umma au binafsi anatakiwa afanye nini kwa mfanyakazi wake kuboresha maisha? ndipo zinakuja nyongeza za mishahara,maruprupu nk
Unaenda wizara ya afya kwenye hicho kipengele cha kuboresha maisha ya mtanzania wao watafanya nini ndio unaona uboreshaji wa huduma za afya unaingia hapo
ukija wa wizara ya miundo mbinu inaenda hapo kwenye sera kuwa wao hicho kipengele cha kuboresha maisha ya mtanzania watafanya nini ndipo unaona uboreshaji wa miundo mbinu nk
Ndio maana ni lazima kila kiongozi wa serikali au taasisi ya umma kuwa na ilani na sera za chama tawala
Tatizo chadema mnadhani sera unatamka ohhh nitamlipia kila kijana wa kiume mahari na kila mtu nitampa kadi ya bima ya afya!!! hiyo ni katika level ya chini ya utendaji !!
Kutokana na ufinyu wako wa uelewa wa sera ndio maana umeuliza tu kuboresha mishahara ya watumishi wa umma huelewi kuwa wako na wa sekta binafsi!! unadhani kazi ya serikali ni kuboresha tu maslahi ya wafanyakazi wa umma!!!
Lisu ukimsikiliza hasa haongelei sera yuko kwenye low level ya kuongelea vitu vya chini sana sio vya kiupana kitaifa.Sera hujikita kwenye upana kitaifa mfano hata ukimpa kila mtu bima ya afya wakati hata panadol hakuna hicho kikadi kinamsaidia nini? ndio maana sera itatamka kuboresha maisha ya mtanzania hivyo ukiongelea hospitali sasa unaongea kuanzia uwepo wa miundo mbinu ya majengo,madaktari,maslahi yao,uwepo wa vitendea kazi,mazingira ya kazi ,uwepo wa madawa na ndio mwishoni huko unaongelea kugawa hivyo vikadi vyako vya bima ya afya.Ndio maana tunasema Huwezi tamka bima ya afya eti ni sera!!!! chadema ni zero kwenye utengenezaji sera ndio maana hata wewe huelewi unadhani kuongeza mshahara ni sera!!!