Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Lissu shikilia hapo hapo!Huenda kesho mtu huyu akaahidi kuyapa kipaumbele maendeleo ya watu!
 
Amesha copy na kupaste leo ndo anajua inawezekana je alikuwa wapi siku zote hizo
 
Atazingua huyu. Apigwe chini tu. Aliongopa kwamba kila Kijiji kitapata mil. 50 mpk leo tunapewa swaga.

Aliwaahidi walimu kuwapatia kompyuta kila mmoja. Hili haliongelewi tena.
 
Leo Rais Magufuli amedema bima ya afya ipo inakuja muda sio mrefu kuanzia Sasa.

Amesema inawezekana watu kupewa bima na kila mmoja kuipata
View attachment 1563145
Zilizopo hivi Sasa,ubora was huduma unaporomoka kwa Kasi ya 5G badala ya kuimarika kwa wenye nazo,kweli itawezekana katika mazingira ya Sasa,kupatikana kwa Kila mmoja? Mimi yangu macho,ila pia Kama kweli ,kwanini iwe wakati huu,na sii kabla ya wakati huu?
 
Ni kweli kabisa,huwezi kuweka kipaumbele ununuzi wa ndege kwa nchi kama Tanzania ukaacha kilimo ambacho 70 kinawagusa watanzania!

Lissu ni miongoni mwa watanzania wachache wenye uwezo wa kupanda ndege,na hapa ndipo unapaswa kuona akili kubwa ya Lissu!Hajifikirii yeye bali watanzania wenye hali mbaya!Masuala ya ndege yangeachiwa sekta binafsi na serikali ikabaki kuwa na ndege chache tu!

Tulichoshindwa ni kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia mashirika kuleta route za ndege zao hapa nchini kwetu!
Nawashangaa wengi mnaonesha hiyo picha ya Lissu na kudhani mmepata hoja kumbe mnaonekana mapopoma tu!
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Kama ni madesa hayupo aliyepewa madesa mengi na ya kutosha kuliko chama baba lao. Labda itakuwa ni kibri au labda ni ukiziwi tu uliopindukia.

Kwa mtanzania wa leo anahitaji mgombea wa namna gani? Hili liko wazi.

Kwamba ni mfanyakazi, mwanafunzi wa elimu ya juu, mkulima, mfanyabiashara, mstaafu au mtu wa wapi, jitajie mwenyewe uone matarajio yake yapi yamejibiwa.

Nyanja zote hizi zimeitisha kuhitaji uhuru, haki na ustawi. Wapi uhuru wala haki vimekuwa ni agenda kwa cha hiki? Wapi ustawi wa watu umekuwa na umuhimu wowote kwa chama hiki?

Kinyume chake pamoja na kuwa huu ni uchaguzi wa watu, huko mbogamboga vitisho na mashinikizo ya nani wakuchaguliwa vimeshamili. Ghiliba za kutumia hata ukabila kwenye mambo nyeti haya ya nchi vinazidi kushika kasi.

Chonde chonde. Uhuru, haki na maendeleo havina chama. Hivi ni vyetu. Hivi hatumwombi mtu.

Asipotupa kiroho safi, safari hii hatutakubali!

Kibri na ukiziwi dawa yake ni sanduku la kura.

Uamuzi wa kwenye sanduku la kura na uheshimiwe.
 
Kwani mmenyimwa na nyie kuweka wasanii? kwani ccm peke yake ndio wanaweka wasanii kwenye majukwaa? ACT mpaka NEY wa Mitego yupo, tafuteni sera ingine hii ishachacha

Magufuli ana followers 910K twitter, Tundu Lissu ana 100K, mpaka apo tumefunga mada
Mkuu, hiyo serikali yako ya WATEKA NYARA, kubambikia kesi zisizo na dhamana na kucharaza mvua za risasi raia wema MCHANA KWEUPE haikubaliki kwa sasa.
 
Akiwa ktk kampeni zake ktk wilaya ya Kigamboni Mkoani DSM Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM Samia Suluhu amesema kuwa baada ya uchaguzi mkuu kwisha itakuwa zamu ya wilaya ya ubungo na kigamboni kutembelewa na miradi ya DMDP.

lakini haswa ktk wilaya ya UBUNGO haswa pembezoni ktk jimbo la kibamba, kiluvya n.k amabo hapana lami hata nusu km.
mradi wa DMDP umeboresha sana mji wa dsm, ila kama wilaya ya ubungo haswa jimbo la kiluvya/kibamba linapaswa litazamwe zaidi ktk maendeleo hayo.
 
Ni kweli kabisa,huwezi kuweka kipaumbele ununuzi wa ndege kwa nchi kama Tanzania ukaacha kilimo ambacho 70 kinawagusa watanzania!

Lissu ni miongoni mwa watanzania wachache wenye uwezo wa kupanda ndege,na hapa ndipo unapaswa kuona akili kubwa ya Lissu!Hajifikirii yeye bali watanzania wenye hali mbaya!Masuala ya ndege yangeachiwa sekta binafsi na serikali ikabaki kuwa na ndege chache tu!

Tulichoshindwa ni kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuvutia mashirika kuleta route za ndege zao hapa nchini kwetu!
Nawashangaa wengi mnaonesha hiyo picha ya Lissu na kudhani mmepata hoja kumbe mnaonekana mapopoma tu!

si unaona akili zenu sasa, kwamba sisi tanzania kazi yetu kuwanufaisha pilots wa nchi zingine si ndio? hawa wa kwetu wafanye nn? opportunity ipo, watalii wapo, tuuze izo ajira kwa wengine si ndio?? uko timam kichwan?
 
Back
Top Bottom