Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.
Kama ni madesa hayupo aliyepewa madesa mengi na ya kutosha kuliko chama baba lao. Labda itakuwa ni kibri au labda ni ukiziwi tu uliopindukia.
Kwa mtanzania wa leo anahitaji mgombea wa namna gani? Hili liko wazi.
Kwamba ni mfanyakazi, mwanafunzi wa elimu ya juu, mkulima, mfanyabiashara, mstaafu au mtu wa wapi, jitajie mwenyewe uone matarajio yake yapi yamejibiwa.
Nyanja zote hizi zimeitisha kuhitaji uhuru, haki na ustawi. Wapi uhuru wala haki vimekuwa ni agenda kwa cha hiki? Wapi ustawi wa watu umekuwa na umuhimu wowote kwa chama hiki?
Kinyume chake pamoja na kuwa huu ni uchaguzi wa watu, huko mbogamboga vitisho na mashinikizo ya nani wakuchaguliwa vimeshamili. Ghiliba za kutumia hata ukabila kwenye mambo nyeti haya ya nchi vinazidi kushika kasi.
Chonde chonde. Uhuru, haki na maendeleo havina chama. Hivi ni vyetu. Hivi hatumwombi mtu.
Asipotupa kiroho safi, safari hii hatutakubali!
Kibri na ukiziwi dawa yake ni sanduku la kura.
Uamuzi wa kwenye sanduku la kura na uheshimiwe.