Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,729
- 2,851
Wewe umekosa uhuru gani?Mheshimiwa Dr. Magufuli Rais wa Tanzania tunaomba majibu yako juu ya hoja za wapinzani kuwa umeminya Uhuru na haki za Watanzania kwa maslahi yako binafsi na chama chako CCM. Chaguzi zilizopita wapinzani waliomba kura kwa wananchi kwa kuwaahidi maendeleo na kuahidi kupigana na ufisadi uliofanywa na viongozi wa CCM, lakini mwaka huu wapinzani wanaahidi maendeleo na kuwaahidi Uhuru na haki .
Hata makaburu wa south Africa walileta maendeleo ya juu sana, Mimi binafsi nimesoma A- level shule iliyojengwa na Wazungu, na O-level pia nimesoma shule iliyojengwa na Wazungu pia. Wakoloni pia walileta maendeleo kwa kiasi chao. Lakini akina Nyerere walidai Uhuru.
Jibu la maendeleo hayana chama halitutoshi sisi tunaojua historia. Sisi ambao tumesoma historia na kufaulu vizuri A- level tunajua jinsi Waingereza walileta maendeleo America lakini Waamerika hawajaruhusu US. liwe koloni la kudumu la Uingereza.
Tunaomba majibu ili wananchi wajue kuwa Uhuru na haki vipo kila mahali na zile za wapinzani ni kelele mfu .