Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.
Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.
Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.
Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.
Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.
Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.
Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.
View attachment 1567050