Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Huo muda wa mdahalo unatumiwa kwa kampeni nyingine zenye tija zaidi.

Mdahalo wanafanya wagombea ambao hawajawahi kuingia ikulu.

Ule wa 1995 ulifanyika wakati wagombea wote hawajulikani kwa ukaribu kwa wananchi.

Leo Magufuli anajulikana anasimamia nini na ana maono gani.
Anasimamia wizi wa KOROSHO
Ukatili na mauji ya wapinzani?
Kwa hiyo trump hajulikani kwa wamarekani? Mbona anashiriki MIDAHALO? huu upimbi utaisha lini hapo lumumba
 
Jukwaa kubwa la ccm ni kwa ajili ya wasanii kufanyia show, otherwise kama ni kampeni mbona Meko anafanya tu akiwa kwenye roof ya gari hiyo nayo mbona huiongelei?
Mikutano ya siasa hatuendi kama Chadema unakuta hata kijukwaa cha kuhutubia Lisu anasimama juu ya meza ya kuuzia mitumnba.Angalia vijukwaa alivyotumia Lisu bagamoyo na morogoro ni mgombea uraisi kusimama vijukwaa kama vya Lisu au Membe


Unahangaika na quality ya sound systems kisha mgombea anakuja kuongea pumba tu, mngejikita kwenye quality ya sera zenu sio majukwaa.

Watu hawahitaji majukwaa, hamuelewi ndio maana mmekazana na SGR, Ndege na Flyovers wakati wananchi wanashindia mlo mmoja.
Sisi quality ni muhimu kwetu mkutano uwe highly organuzed logistics zote yakiwemo majukwaa sound system nk Akienda akute kila kitu classic
 
Anasimamia wizi wa KOROSHO
Ukatili na mauji ya wapinzani?
Kwa hiyo trump hajulikani kwa wamarekani? Mbona anashiriki MIDAHALO? huu upimbi utaisha lini hapo lumumba
Trump anaongoza Marekani na Magu anaongoza TZ.

Trump alishiriki mdahalo mmoja tu na Hillary Clinton. Mwaka huu anafanya mikutano ya hadhara na ile sio midahalo.
 
Ratiba ta Magufuli bado mleta mada angalia ratiba ya tume ya wagombea. Kampeni huendishi tu unaenda kwa ratiba ya tume
 
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
Mbona Lissu alipopumzika hamkusema haya msemayo!? Au ndiyo kule kukosa HOJA na kungoja kudandia MATUKIO!? Leteni HOJA jamani..!
 
Trump anaongoza Marekani na Magu anaongoza TZ.

Trump alishiriki mdahalo mmoja tu na Hillary Clinton. Mwaka huu anafanya mikutano ya hadhara na ile sio midahalo.
Kwenye mikutano wasanii wanaenda kufanya nn? Hawa kina zuchu? Kwann wagombea wengine hawapewi airtime ya kutosha? Kwann magari ya ikulu yabandikwe karatasi za Ccm? Kwann mgombea wa CCM alipora KOROSHO za wana mtwara?
 
Tatizo la Magufuli kwa miaka 5 alifanya kampeni peke yake akadhani upinzani umekufa, Kwa hiyo anapoona nyomi leo kwa Lissu kesho kwa Zitto haamini.
 
Sasa inakuwaje yule aliyekaa hospitali miaka mitatu anaonekana ngangari zaidi kuliko yule aliyekaa kwenye kiyoyozi Ikulu miaka mitano?
Mmoja anapiga chaka kwa chaka kwa njia ya barabara..kijiji kwa kijiji na anapiga mikutano na kukutana na voters.

Mwingine ye anatumia ndege tu..dar to bagamoyo anataka kupanda chopa..mikutano yako anapiga kwenye miji..yaani kwa mfano dar nzima alipiga mikutano mitatu..tuseme mkonwa temeke, mkoa wa ilala na mkobwa kinondoni..mbeya akapiga mmoja, mwanza akapiga mmoja.

Yeye anashuka kwenye ndege, anaenda hotelini, kisha uwanjani kwenye mkutano..kisha hotelini tena then kwenye ndege..kamaliza huyo.
 
Amepuuza vilio vya watanzania kuhusu biashara zao kudorora, vijana kukosa ajira na kutoyakemea matukio ya utekaji, mauaji, matusi ya Musiba kwa wazee wastaafu na mengine mengi.

Alifanya maamuzi mengi kibabe. Mfano kukataza mikutano ya siasa, kukataza bunge kuwa live, n.k kwa kisingizio kuwa watanzania wachape kazi. Lakini yeye kutwa kucha yuko mubashara hata kwa mambo yasiyo na umuhimu.

Laiti kama Magufuli angekuwa msikivu, mnyenyekevu na mpenda watu, uchaguzi huu ungekuwa rahisi kwake.
Hakujawahi kutokea uchaguzi RAHISI NA MWEPESI kwa CCM kama huu wa 2020. Hii ni kwa sababu wanaharakati hawana hoja za kuwaambia wapiga kura isipokuwa MATUSI NA PERSONAL ATTACKS tu ambavyo vinafanya uchaguzi huu kuwa utelezi kwa CCM.
 
Aliyepora KOROSHO zetu naye anataka tumchagie ili aendelee KUTUPORA????
 
Back
Top Bottom