Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Hakika kazi zilizosimamiwa na Dk. Magufuli kwa maendeleo yaliyofanywa nchini ndani ya miaka mitano ni kubwa sana.Ilani ya CCM ya uchaguzi 2015-2020 imetekelezwa ipasavyo kwa kishindo.

Tusibeze maendeleo haya. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni huyu mzee.
Sawa
 
NDIYO ANGEMUUNGA MKONO MAGUFULI - Ni ingeshindikana asingewapa uongozi Chadema. Kama ambavyo alirudia rudia mpaka CCM ipasuke ndio upinzani utakuwepo nchi hii....

Kwa sasa system hiyo haipo na itachukua karne zijazo kwani kwa sasa chama tawala kinazidi kuimarika kupitia Mwenyekiti wetu JPM ambaye pia ni Rais wa Nchi yetu.

Tunamuombea kwa Mungu ili aendelee kuimarisha CCM ili iwe imara zaidi na hayo unayoyatamani yasitokee kabisa.
 
Mkuu Magufuli nakukumbusha kutekeleza ahadi yako.

Ulisema mwaka huu Uchaguzi utakua huru na wa haki.

Ahadi Ni Deni,
Na kutimiza ahazi Ni uungwana.

Hata hivyo Uhuru na Haki sio tu siku ya kupiga kura,Bali Ni mchakato mzima wa Uchaguzi,yaani kuanzia
Kujiandikisha,
Kupiga kampeni,
Kupiga kura,
Kuhesabu kura,
Kutangaza matokeo,
Na
Kukubali matokeo.
Simamia ahadi yako Mkuu.
 
Kwa sasa system hiyo haipo na itachukua karne zijazo kwani kwa sasa chama tawala kinazidi kuimarika kupitia Mwenyekiti wetu JPM ambaye pia ni Rais wa Nchi yetu.
Tunamuombea kwa Mungu ili aendelee kuimarisha CCM ili iwe imara zaidi na hayo unayoyatamani yasitokee kabisa.

Hayo siyatamani mimi, ni mfumo tuu wa kuendesha serikali za wanadamu duniani.
Ni kama tuu kampuni inajiendesha vizuri sana lakini bado itakuwa na Bodi ya wakurugenzi. Na haiwezi kuondoka hali hiyo ili kuleta utengamano.

Katika uongozi ilikuja kuonekana kuwa siyo kila siku wapiga kura wanakuwa sahihi na pia sio kila siku viongozi wanakuwa sahihi.

CCM itapewa muda wa kuimarisha uchumi na hali ya watanzania na ikifika hapo CCM kama alivyo sema Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM, na hapo ndio chama chako itabidi kipasuliwe tuu.
 
Kwa hiyo baada ya miaka 5 kama bado hajamaliza miradi (kumbuka ataanzisha mingine), tutengue katiba ili tumpe mitano tena au tuondoe ukomo? Naona umejifunga goli tu.

Kuweka ukomo ni kunyima wapiga kura haki yao ya uchaguzi. Tunatakiwa tumchague yeyote tunaemtaka na ikiwa miaka 30 sawa tuu, na kama hatumtaki tunampiga chini.

Kuweka ukomo wa mihula miwili ni udikteta wa katiba na lazima uangaliwe upya.
 
Enzi zake hakuwa mkandamizaji ?

Sisi wadogo kiumri huwa tunaambiwa Magufuli anafanana sana na Nyerere, sema tu magufuli hana speech sensible kama za nyerere

Ndio ni kweli kabisa anafana na Nyerere lakini sio kwa kila kitu. Sisi wazee wako tumepinda kwa kuwa baada ya Nyerere kwa muda mrefu tumekuwa na viongozi wanaofanana lakini wakitofautiana sana na Nyerere, na hawafanani na Magufuli.

Tunacho pambana nacho kipindi cha Magufuli ni mabadiliko ya mifumo ya kuendesha maisha ambayo hatuyategemea, lakini tutayazoea tuu.
 
Miaka yote tangu 1995 Viongozi wa Dini wamekuwa ni waangalizi wa uchaguzi.Utawala huu wa mkono wa Chuma umewatupilia mbali.

Jiwe aanze kuhama ikulu mapema.
Amekataliwa kila kona.
Watanzania wengi hatumtaki.
Wewe ndio humtaki,ila sio watanzania wote. Mbowe na genge lake nani anawataka?. Vibaraka wa beberu nani anashida na nyie?.

Mpo ki maslahi yenu zaidi, hamna nafasi kwenye uchaguzi huu kuanzia watendaji wa vijiji mpaka u Rais. Kafanyeni upuuzi wenu huko Ubelgiji sio hapa kwa mama Tanzania. Tanzania live long, God bless JPM.
 
Back
Top Bottom