SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Vita ya Israel dhidi ya Iran imeanza kushika kasi kubwa huku mashambulizi yakiwa kwa upande mmoja zaidi na nguvu kubwa ikielekezwa kuifanya Iran kuwa kama Gaza ndani ya muda mfupi sana.

Bila kumumunya maneno, vita hii sio tu imelenga kuangamiza mipango ya kinyuklia ya Iran pia imedhamiria kuuondoa utawala wa sasa wa Iran na huenda ikatamatika kwa kumuua kama sio kumkamata Ayatollah.

Sioni namna yoyote ambayo Iran inaweza kustahimili kishindo cha hii vita, kwa kuwa;
1. Maeneo muhimu yote ya kijeshi ya Iran yametandikwa na mvua za mabomu.

2. Viongozi muhimu wa juu wa kijeshi wa Iran wanaendelea kuuwawa.

3. Anga lote la Iran lipo ndani ya udhibiti wa mamlaka ya Israel.

4. Mpaka sasa Iran hana mshirika kamili mkubwa wa kumsaidia katika hii vita. Sio nchi za kiarabu, Uturuki, Russia, China au Korea Kaskazini wote wako kimya, hawana msaada wa moja kwa moja kwa Iran.

5. Uwezo wa Iran kurusha makombora na kulenga maeneo muhimu ya Israel uko chini na umepunguzwa kwa zaidi ya 90%.
 
Russia vs Ukraine...
Hii vita ilikuwa ya kimkakati ili kumdhoofisha Russia asiweze kuingilia vita nyingine...
Hezbollah paa
Syria paa
Yemen paa
Iran kubaa
Hawa jamaa wapo mbali sana kifikra
Yani unavyoongea inaonesha hakuna unachojua mzee.
Hizbollah ilipoanza kutumia long range missiles US na France official walienda Beirut kuishinikiza serikali ya Lebanon wawashurutishe Hizbollah wasaini makubaliano ya kusitishwa vita na kuweka silaha chini.
Hizbollah ikafanya hivyo.

Yemeni juzi walirusha makombora Israel kama haujui ndio kisa Cha Israel kuzidiwa zaidi kwenye kudungua makombora.

Syria hapo kutokea anguko la Assad ilikua lazima na alishashauriwa a step down muda sana.

Russia huko amebeba maeneo yote yenye utajiri Ukraine na sasa anaelekea Kyiv.
Wewe unasema kadhoofishwa.
Na Bado ana uwezo wa kutoa silaha popote pale.

China imetangaza raia wake waondoke upesi sana Israel.
Tarajia mambo kuwa magumu zaidi.
 
Hizo propaganda na inatakiwa utumie ubongo kufikiri bro.
Tangu Ijumaa Israel ilitangaza kutawala anga la Iran,matokeo yake Iran ikarusha drone na makombora kuelekea Israel.
Muda mwingine tumieni akili msiwe kama chujio maji yanapita tu

Yani unavyoongea inaonesha hakuna unachojua mzee.
Hizbollah ilipoanza kutumia long range missiles US na France official walienda Beirut kuishinikiza serikali ya Lebanon wawashurutishe Hizbollah wasaini makubaliano ya kusitishwa vita na kuweka silaha chini.
Hizbollah ikafanya hivyo.

Yemeni juzi walirusha makombora Israel kama haujui ndio kisa Cha Israel kuzidiwa zaidi kwenye kudungua makombora.

Syria hapo kutokea anguko la Assad ilikua lazima na alishashauriwa a step down muda sana.

Russia huko amebeba maeneo yote yenye utajiri Ukraine na sasa anaelekea Kyiv.
Wewe unasema kadhoofishwa.
Na Bado ana uwezo wa kutoa silaha popote pale.

China imetangaza raia wake waondoke upesi sana Israel.
Tarajia mambo kuwa magumu zaidi.
Vijiweni mnadanganyana sana...angalia kipigo anachopokea Iran uko achana na story za vijiweni
 
Wazimu umempanda raisi Trump wa Marekani baada ya kushuhudia miji ya Israel ikipigwa bila kizuizi.Raisi huyo amelazimika kukatika mkutano wa G7 na kurudi nyumbani kushughulika na vita,

Tamko la aina hiyo pia limetolewa na Korea kusini wakiwataka raia wa Iran waondoke bila kutaja mamilioni hayo ya watu waelekee wapi.Hayo bila shaka ni matamko ya mtu aliyechanganyikia baada ya kupokea kipigo.

Maamuzi hayo na matamko yamekuja baada ya Netanyahu jana kwenda kukagua maeneo yaliyoshambuliwa na Iran ndani ya Tel Aviv na kutosadiki alichokiona.
Yanayokuja kutokea sio mazuri hata kidogo.
China imetangaza pia raia wake waondoke Tel Aviv upesi sana.
Naona vita inaenda kusambaa hapo mashariki ya kati.
 
Wazimu umempanda raisi Trump wa Marekani baada ya kushuhudia miji ya Israel ikipigwa bila kizuizi.Raisi huyo amelazimika kukatika mkutano wa G7 na kurudi nyumbani kushughulika na vita,

Tamko la aina hiyo pia limetolewa na Korea kusini wakiwataka raia wa Iran waondoke bila kutaja mamilioni hayo ya watu waelekee wapi.Hayo bila shaka ni matamko ya mtu aliyechanganyikia baada ya kupokea kipigo.

Maamuzi hayo na matamko yamekuja baada ya Netanyahu jana kwenda kukagua maeneo yaliyoshambuliwa na Iran ndani ya Tel Aviv na kutosadiki alichokiona.

😂😂😂🤣🤣

Vita imeshaisha?
 
Back
Top Bottom