SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Hivi Israeli hawezi kupambana mwenyewe mpaka hawa superpower?..

Maana yake Iran hawezekani mpaka hawa jamaa?..
Kama Israeli vita kwake ni nyepesi kwanini wasimuache aimalize mwenyewe? ? Kuna nini mpaka waje muda huu.
Huo ukanda ni mgumu!

Kwa namna yoyote ikiwa washirika wa Israel wakiingia mashariki ya kati yote inachafuka.

Nchi zote za kiarabu hapo zitakuwa kwenye vita.

Kwa namna hiyo usidhani China na Russia zitakuwa kimya.

Ndege ya kubeba mizigo ya kijeshi ya China imefanya safari mara 2 kuelekea Iran tangu mtifuane wake na Israel.
 
Ilitua kiwanja kipi?
 
Trump ametweet kua tayar wamecontrol anga la Irani
Trump unamuona ana maana?

Kamsemea vibaya Tucker kuhusu hii vita.

Kamsemea vibaya Macron baada ya kusema Trump ameondoka mapema ili kuangalia namna gani ya kuweza kuitisha Iran kwenye meza ya mazungumzo ili wasitishe mapigano.

Trump kamsema vibaya Macron kuhusu hili.

Huyo ni msema hovyo!
 
Acha porojo. Wamejilalia kivipi wakati Israel kutwa kucha wanashambulia bila kupumzika
Wanashambulia bila kupumzika huku Waajemi wakiwa wanaendelea na shughuli zao mchana na usiku wanajilalia zao hawana presha kama nguchiro wa Israel walivyo kwenye mahandaki mchana na usiku πŸ˜‚πŸ˜‚.

Mida ya Muajemi ni mapema Alfajiri anaamsha madude hadi yalipopangiwa kupiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…