SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia


Kwa hii impact, hata mende hawezi choropoka hapo.

View: https://x.com/jacksonhinklle/status/1935558964810494379
 

Your browser is not able to display this video.

Kuna jamaa alikua ana post movies na video games humu ,hamna defence system ya israel yenye speed hivi .avheni ku post wallpapers😅😅
 
Us akiingia vitan ujue iran ni mshindi kwa Israel
Wacha wapambane wenyewe tuone mwisho wao
Mbona hadi sasa US kashaingia vitani silaha nyingi wanazotumia Israel na mifumo ya ulinzi kama Thaad na Arrow 3 ni mifumo ya marekani, ila Iran anaitandika Israel hivyo hivyo, USA alichokiona ni kuwa Israel anaenda kuzidiwa kwahiyo na yeye anataka aokoe jahazi.

Iran ni tishio makombora anarusha kwa masafa marefu kabla hayajafika Israel yanaanza kutunguliwa huko Jordan lakini bado yanapenya kwenda kuipiga Israel hivyohivyo wa Iran ni hatari hasara anayoipata Israel kwa sasa ni kubwa sana ambayo haijatarajiwa
 
Hakuna nuclear facility ya Iran iliyoshambuliwa picha za satellite zinazonyesha iko salama, na kufikika kwake ni ngumu ndo maana USA anataka aingie na yeye kujaribu ila Israel kashindwa, unatuma drone ikashambulie Nuclear facilities utawezea wapi? Drones za Israel zimeishia kutunguliwa
 
Vita haina mwezi lakini Israel imechakaa vibaya, ikifika miezi miei miwili itakuwa Gaza..
Ila Hadi Sasa Iran akishindwa NDIYE aliyeonyesha uwezo mkubwa wa Kijeshi.

Mtu unarusha bomu 2000 kilometer kwenda kulenga kasehemu kadogo huko bila kukosea target ni tofauti na ndege kupita nakushambulia eneo ambalo linaonekana.

Hawa jamaa wangeachwa bila vikwazo wangetisha. Ndio maana mababu ZAO wakina Koreshi au Cyrus walitawala middle east yote
 
US anataka kutumia B-2 bomber ambazo zinaweza kubeba heavy bunke buster, lakini psipo hiyo ni kujisumbua...
 
sidhani kama Israeli alitarajia direct hits za hizi ballistic na hypersonic za Iran.

Ninachoona kuna hatari Houthis wakapewa decoys na drones nyingi wazirushe kuzioverwhelm hizi ADs maana tayari udhaifu wake umeshaonekana.
 
Hii vita Israel hatoki, ndio maana Trump anapiga kelele kuingilia ugomvi, wapo katika sintofahamu, taarifa za kijasusi ni kwamba muda mchache ujao , Israel itashindwa kabisa kuzuia mapigo... halisi nzuri.. Iran inatambua hilo na ndio maana wanawachezea.. wanarusha missiles sometimes kuwamalizia interceptors Israel... makusudi.. lengo si kulipua..

Ndio maana irone dome wanasema zimechoka sasa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…